Seminari
Kitengo cha 29: Siku ya 4, Etheri 3


Kitengo cha 29: Siku ya 4

Etheri 3

Utangulizi

Bwana alimuuliza kaka ya Yaredi, “ Ungetaka nifanye nini ili muwe na mwangaza kwenye mashua yenu?” (Etheri 2:23). Katika kujibu, kaka ya Yaredi alitayarisha kwa makini mawe 16 na akaomba kwa unyenyekevu kwamba Bwana ayaguse “ili yaangaze kwenye giza” (Etheri 3:4). Kwa sababu ya imani kuu ya kaka ya Yaredi, aliona kidole cha Mwokozi, Mwokozi alipokuwa akigusa mawe. Bwana kisha akajionyesha kwa kaka ya Yaredi na kumwamuru aandike kile alichokuwa ameona na kusikia.

Etheri 3:1–20

Bwana anagusa mawe ili kutoa mwangaza kwa mashua ya Wayaredi, na kujionyesha kwa kaka ya Yaredi.

Ni baadhi ya mifano gani ya kile wewe na vijana wengine huombea kwa dhati? Chagua moja ya vitu hivi, na ukiandike hapa:

Unaposoma mfano wa kaka ya Yaredi katikaEtheri 3, tafuta umaizi ambao ungekusaidia wewe ama rafiki kupokea usaidizi kutoka kwa Bwana.

Fikiria kuhusu ombi la kaka ya Yaredi kwake Bwana kuhusu kutoa mwangaza kwa mashua na jibu la Bwana kwake. Rejel Etheri 2:22–3:1. Kisha andika maelezo mafupi kwa kila moja ya picha hizi zinazoelezea kile kaka ya Yaredi alifanya kama wajibu wake ili kusuluhisha shida ya kutokuwa na mwangaza.

Picha
mwanaume na moto na ala

Picha
mwanaume akipanda mlima

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kuhusu kile kinachokufurahisha kuhusu juhudi za kaka ya Yaredi kusuluhisha shida ya kuwa na mwangaza katika mashua. Hata ingawa kaka ya Yaredi alitia bidii sana, zingatia jinsi mawe yake yaliyoyeyuka yangefaa kwa kutoa mwangaza bila usaidizi wa Bwana.

Soma Etheri 3:2–5, na kisha ufanye yafuatayo:

  • Tambua ama weka alama vishazi vinavyoonyesha kwamba kaka ya Yaredi alikuwa mnyenyekevu na alitambua kumtegemea kwake Mungu. Inaweza kusaidia kujua kwamba kishazi “maumbile yetu yamekuwa maovu siku zote” kinarejea hali yetu ya dhambi duniani. Kwa sababu ya Kuanguka kwa Adamu, tumetengwa kimwili kutoka kwa Mungu. Tuna pia uelekeo kwa dhambi Bila usaidizi mitakatifu, hatungeweza kamwe kurudi kwa uwepo wa Mungu.

  • Tambua kile kaka ya Yaredi alimuuliza Bwana afanye.

  • Tambua ama alamisha kile kaka ya Yaredi alishuhudia alijua kuhusu Mungu.

Picha
Kaka ya Yaredi Aona Kidole cha Bwana
  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni ushahidi gani unaweza kupata katika Etheri 3:1–5 kwamba kaka ya Yaredi alikuwa na imani kwamba Bwana angeweza kumsaidia kutatua shida yake?

    2. Mfano huu unawezaje kukusaidia kutambua tegemeo lako kwake Bwana unapoomba usaidizi Wake?

Soma kauli ifuatayo kutoka kwa Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, inayohimiza imani ya kaka ya Yaredi: ‘ Hakika Mungu, pamoja na msomaji, anahisi kitu fulani cha kuvutia katika umaasumu wa kitoto na ari ya imani ya mtu huyu. ‘Tazama, Ee Bwana, unaweza kufanya hivi’ [Etheri 3:5]. Pengine hakuna mstari moja ya imani yenye nguvu zaidi iliyo zungumziwa na mtu katika maandiko. Walakini nabii akiwa hana uhakika kuhusu uwezo wake mwenyewe, yeye hana shaka kuhusu nguvu za Mungu” (“Rending the Veil of Unbelief,” in Nurturing Faith through the Book of Mormon: The 24th Annual Sidney B. Sperry Symposium [1995], 12).

Soma Etheri 3:6, na ufikirie vile ingekuwa kuwa katika hali iliyoelezwa katika mstari huu.

Soma Etheri 3:9, ukitafuta ni kwa nini Bwana alikuwa tayari kushika mawe na kwa nini kaka ya Yaredi aliweza kuona kidole cha Bwana.

Kamilisha kauli ya msingi ifuatayo kulingana na kile umejifunza hadi sasa katika Etheri 3: Tunapomwita Bwana kwa unyenyekevu, atatujibu kulingana na [yetu] na mapenzi Yake.

  1. Jibu swali moja au yote mawili yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Reje kwa kile ulichoandika mwanzoni mwa somo hili kuhusu kile wewe ama vijana wengine huombea. Mtu anawezaje kuonyesha imani katika Bwana anapotafuta usaidizi wa Bwana na mwongozo katika hali hiyo.

    2. Umepitia nini maishani mwako kilichokuelekeza kujua ukweli wa kanuni kwamba tunapomwita Bwana kwa unyenyekevu, atatujibu kulingana na imani yetu na mapenzi Yake?

Chukua muda na tathmini kimya kiwango cha imani yako kwa Bwana. Soma Etheri 3:9–12, na utafute na ualamishe ushahidi wa imani ambayo kaka ya Yaredi alikuwa nayo katika Bwana.

Rejea Etheri 3:11, na ufikirie kuhusu kama una imani ya kutosha katika Bwana kujitolea kuamini na kufuata kile atakachokufunulia hata kabla akifunue.

Picha
Mzee Jeffrey R. Holland

Soma kauli ifuatayo kutoka kwa Mzee Jeffrey R. Holland, na upige mstari kile tunalazimika kufanya ili kuonyesha imani kama kaka ya Yaredi: Imani ya msingi hukuzwa na matukio katika siku zilizopita—na yanayojulikana, ambayo yanatoa msingi wa imani. Lakini imani ya uokovu mara nyingi ni lazima ielekezwe kwa matukio katika siku za usoni—yale ambayo hayajulikani, yanayotoa fursa ya miujiza. Imani kama ile ya kaka ya Yaredi hutangulia miujiza na maarifa, Ilimbidi aamini kabla Mungu azungumze. Ilimbidi atende kabla uwezo wa kukamilisha kitendo hicho ufahamike. Ilimbidi ajitolee kwa tukio lote kikamilifu mapema kabla ya hata kitengo cha kwanza cha utekelezi wake. Imani ni kukubali bila pingamizi— na mapema kabla—ya hali yoyote Mungu angehitaji katika siku zijazo hivi karibuni na usoni” (Christ and the New Covenant: The Messianic Message of the Book of Mormon [1997], 18–19).

Fikiria kuhusu yale ambayo kaka ya Yaredi alipitia, kuanzia kwenye Mnara wa Babeli. Ni matukio gani huenda yakasaidia kuongeza imani yake katika Bwana? Unafikiria matukio haya yalimtayarishaje kuonyesha “imani kubwa vile” (Etheri 3:9) kwa wakati huo.

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni tukio gani maishani mwako lililoongeza imani yako katika Bwana?

    2. Tukio hilo lilikutayarisha vipi kuonyesha imani kubwa zaidi katika siku za usoni?

Soma Etheri 3:13–20, na utafute baraka kaka ya Yaredi alipokea kwa sababu ya imani yake. Kaka ya Yaredi alijifunza nini kuhusu Mwokozi kutoka kwa tukio hili la ajabu? Kanuni ingine muhimu unayoweza kujifunza kutoka kwa Etheri 3 ni hii: Tunapoweka imani yetu katika Bwana, tutakuwa karibu zaidi Naye.Unaweza taka kuandika kanuni hii katika maandiko yako karibu na Etheri 3:11–20.

Mzee Jeffrey R. Holland alitoa maoni juu ya Etheri 3:15–16 na mkanganyiko unaoweza kuepuka kutokana na tukio hilo:

“Suala linalohitaji kuzungumziwa kwa kifupi linatokana na msemo wa Bwana ‘Hakujakuwa na mtu aliyekuja kwangu kabla yako mwenye na imani kubwa vile umefanya; kwani kama hungekuwa hivyo hungeona kidole changu.’ Na baadaye, ‘Kamwe sijajionyesha kwa binadamu ambaye nilimuumba, kwani binadamu hajaamini kwangu vile umefanya.’ [Etheri 3:9, 15.]

“Uwezekano wa mkanganyiko hapa unakuja na ufahamu kwamba wengi (na pengine wote) wa manabii wakuu walioishi kabla ya kaka ya Yaredi walikuwa wamemwona Mungu. Basi, vipi, tunaeleza tangazo la Bwana? …

“Suala hili limejadiliwa sana na waandishi wa Watakatifu wa Siku za Mwisho, na kuna maelezo machache yanayowezekana, yoyote — ama yote —yanayoweza kutoa ufahamu juu ya ukweli mkubwa wa kifungu hiki. Hata hivyo, bila ufunuo wa ziada au ufafanuzi juu ya suala hilo, dhana yote hiyo ni duni na pungufu. …

“Baadhi wanaamini kwamba Bwana alimaanisha hakuwahi kujionyesha kwa binadamu kwa kiwango hicho ama hivyo. Nadharia hii inapendekeza kwamba maonyesho ya kiungu kwa manabii wa awali hayakuwa na ukamilifu, kama ule, kwamba kamwe pazia haikufunuliwa kutoa ufunuo wa kikamilifu wa asili na utu wa Kristo. …

“Maelezo ya mwisho—na katika suala la imani ya kaka ya Yaredi ya kuvutia zaidi—ni kwamba Kristo alikuwa anamwambia kaka ya Yaredi, “Kamwe sijajionyesha kwa binadamu kwa njia hii, bila hiari yangu, ikisababishwa pekee yake na imani ya anayenitazama.’ Kama desturi, manabii hualikwakatika uwepo wa Bwana, huelekezwa kuingia mbele yake na yeye na tu kwa idhini yake. Ndugu wa Yaredi, kwa upande mwingine, inaonekana kuwa alijipitisha mwenyewe kupitia pazia, si kama mgeni asiyekaribishwa lakini pengine kihalisi kama mmoja asiyealikwa. Alisema Yehova, ‘ Hakujakuwa na mtu aliyekuja kwangu kabla na imani kubwa vile umefanya; kwani kama hungekuwa hivyo hungeona kidole changu. Hakujakuwa na mtu aliyeamini kama ulivyoamini.’ Ni wazi kuwa Bwana mwenyewe alikuwa analinganisha imani isiyokuwa ya kawaida na ono hili lisilokuwa la kawaida. Kama ono lenyewe halikuwa la kipekee, basi lazima iwe ilikuwa imani na jinsi ono lilipatikana iliokuwa tofauti kabisa. Njia pekee imani hiyo ingeweza kuwa ya ajabu sana ilikuwa uwezo wake wa kumchukua nabii, akiwa hajaalikwa, ambapo wengine walikuwa wameweza kwenda tu na aliko la Mungu (Christ and the New Covenant, 20–23).

Etheri 3:21–28

Bwana amwamuru kaka ya Yaredi aandike mambo aliyoona na kufunga kumbukumbu yake

Soma Etheri 3:25–26, na utambue nini kingine Bwana alimuonyesha kaka ya Yaredi. Kama ilivyoandikwa katika Etheri 3:21–24, 27–28, Bwana alimuamuru kaka ya Yaredi aandike vitu alivyoonyeshwa katika ono na kuvifunga. Bwana pia alieleza kwamba angetayarisha njia ya maandiko ya kaka ya Yaredi kutafsiriwa katika siku za usoni. Njia moja unabii huu ulitimia ilikuwa wakati Nabii Joseph Smith alitafsiri kitabu cha Etheri kutoka kwa mabamba ya dhahabu kama sehemu ya Kitabu cha Mormoni na kufanya rekodi ya Wayaredi kupatikana kwa kila mtu kusoma.

Tafakari jinsi unaweza kutumia kile umejifunza leo na kile unaweza kufanya ili kuonyesha imani yako katika Bwana. Unapoonyesha imani yako katika Yesu Kristo, Mungu atamimina baraka juu yako, kama alivyomfanyia kaka ya Yaredi.

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Etheri 3 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningetaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha