Seminari
Kitengo cha 7: Siku ya 1, 2 Nefi 11–16


Kitengo cha 7: Siku ya 1

2 Nefi 11–16

Utangulizi

Nabii Isaya aliishi takriban miaka 100 kabla ya wakati wa Nefi. (Isaya alianza kutoa unabii wakati fulani kabla ya miaka 740 Kabla Kristo na aliendelea kutoa unabii kwa zaidi ya miaka 40, mpaka miaka 701 Kabla Kristo; ona Bible Dictionary, “Isaiah.”) Katika njia nyingi, Nefi anaweza kuwa alikuwa amepata hisia sawa sawa za upendezwaji na upendo kwa Isaya ambao sisi tunao leo kwa Nabii Joseph Smith. Sisi tunajua kutoka kwa maandishi ya Nefi kwamba yeye “alifurahia” katika maneno ya Isaya (ona 2 Nefi 11:2). Kama ilivyoandikwa katika 2 Nefi 12–16, Nefi alinukuu kutoka kwa maandishi ya Isaya, ambayo yalipatikana katika mabamba ya shaba. Maandishi haya yalieleza kiburi cha Israeli ya kale na uovu na hukumu ambazo zilizowasuburi. Isaya pia alisimulia ono lake la Bwana, ambalo kwalo yeye alitakaswa dhambi zake.

2 Nefi 11:1–8

Nefi anafurahia katika ushuhuda wa Isaya juu ya Yesu Kristo

Fikiria kuhusu wakati ulipendezwa na ushuhuda wa mtu fulani juu ya Mwokozi Soma 2 Nefi 11:2–3, na utambue ni uzoefu gani Nefi, Yakobo, na Isaya ambao kila moja wao alikuwa nao na Yesu Kristo.

Bwana huita manabii kutoa ushuhuda juu Yake. Kwa kujifunza shuhuda za mashahidi wa Yesu Kristo, tunaweza kuimarisha imani yetu katika Yesu Kristo na kufurahia katika Yeye.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika fikra zako kuhusu kwa nini unafikiria ni muhimu kuwa na ushahidi wa Yesu Kristo kutoka kwa manabii wengi.

Tafuta mara nne Nefi alisema “nafsi yangu inafurahia” katika 2 Nefi 11:4–6. Unaweza kutaka kuweka alama haya katika maandiko yako.

“Kufurahia” katika kitu fulani kunaonyesha kwamba mtu anapata furaha kubwa katika hicho kitu na kwamba hicho kitu kinamletea shangwe kuu.

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kauli tatu au zaidi za “nafsi yangu inafurahia” ambazo zinawakilisha misingi ya injili ambayo wewe unazifurahia. Elezea kwa nini kila moja ya hizi hukuletea shangwe…

Soma 2 Nefi 11:8, na uandike kile Nefi alitumainia kingekuwa matokeo ya kujifunza kwako maandishi ya Isaya.

2 Nefi 12:1–5

Isaya alitoa unabii kwamba hekalu litajengwa katika siku za mwisho

Fikiria mlima mkubwa. Je! Unaweza kufikiria mifano yoyote ambayo inaweza kulinganisha kati ya mlima na hekalu?

Soma 2 Nefi 12:2–3, 5, ukitafuta kile Mungu aliahidi kutengeneza katika siku za mwisho. Neno “mlima wa nyumba ya Bwana” humaanisha hekalu la Bwana. Kulingana na vifungu hivi, ni baraka gani zitakazokuja kutoka kwa nyumba ya Bwana katika siku za mwisho?

Picha
Minara ya Hekalu la Salt Lake

Unaweza kutaka kuandika katika maandiko yako kitu kama hiki: Mungu ametengeneza mahekalu ili kutufunza sisi njia Zake na kutusaidia sisi kutembea katika mapito Yake (ona 2 Nefi 12:3).

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Hekalu hutusaidia vipi kutembea katika njia ya Bwana?

    2. Unaweza kujitayarisha vipi mwenyewe kuingia hekaluni?

2 Nefi 12–15

Somo hili halitatoa misaada kwa utondoti kwa uelewa wa 2 Nefi 12–15. Hata hivyo, unaposoma na kutafakari sura hizi katika kusoma kwako kwa kibinafsi Kitabu cha Mormoni, tafuta matokeo ya kiburi na dhambi. Simulizi, au maelezo yafuatayo, pia yatakusaidia katika kusoma kwako:

2 Nefi 12:6–18. Angalia kwa makiniarejeo yote ya kuabudu sanamu, pamoja na maneno na mifano ambayo inaonyesha kiburi—kwa mfano, kujikweza, maringo, majivuno, kujiinua juu, na juu sana. Hii itakusaidia kuelewa kwa nini hukumu kali namna hiyo inawangojea watu hawa.

2 Nefi 12:9–11. “Mtu wa kawaida” (mstari wa 9) humaanisha mtu wa chini au hafifu. Wote “mtu wa kawaida” na “mtu mkuu,” kama wao wana kiburi, watanyenyekezwa katika Ujio wa Pili wa Yesu Kristo (ona mstari wa 11).

2 Nefi 12:12–13.“Siku ya Bwana” ni kishazi ambacho kinalenga wakati wa hukumu. Ujio wa Pili wa Kristo utakuwa “siku ya Bwana” wakati waovu wataangamizwa.

2 Nefi 13–14. Katika 2 Nefi 13 ni muendelezo wa mazungumzo ya Isaya ya kile kitakachotokea ikiwa Waisraeli wataendelea katika uovu wao. Isaya aliwaita wanawake Waisraeli “mabinti wa Sayuni” (mstari wa 16), kupendekeza kwamba wao ni watoto wa agano. Isaya aliwafananisha wao na mwanamke mwenye kiburi ambaye amelaaniwa na Bwana, na mapambo ya vito vyake vyote na marembesho ya kimwili yanachukuliwa (ona 2 Nefi 13:16–26). Na tofauti, 2 Nefi 14 inajumuisha maelezo ya Isaya ya nini kitatokea ikiwa mabinti wa Sayuni watajinyenyekeza wenyewe, watatubu, na kumgeukia Bwana. Kama unaweza kupata toleo la WSW la Biblia, tumia tanbihi ya Isaya 3 kukusaidia kuelewa 2 Nefi 13:16–26.

Picha
Isaya

2 Nefi 15:8–22. Neno ole linalenga hali ya huzuni wa kina. Isaya alilitumia mara sita katika vifungu hivi anapotambua dhambi za Waisraeli. Isaya alijua kwamba kama Waisraeli hawatatubu, matokeo ya dhambi zao yatawaletea huzuni ya kina—hususani wakati wa hukumu. Kama Isaya angekuwa nabii duniani leo, angeona dhambi za aina hiyo hiyo ambazo aliziona miongoni mwa Waisraeli?

  1. Soma 2 Nefi 15:20. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko baadhi ya njia ambazo watu leo wanaita vitu vyema viovu, au vitu viovu vyema.

2 Nefi 16:1–8

Isaya anaitwa kuhudumu kama nabii

Maandishi ya Isaya yana ufasaha katika ishara. Ishara ni njia moja Bwana hutufunza kuhusu kanuni za injili. Kama ilivyoandikwa katika 2 Nefi 16, Isaya anaelezea uzoefu wake wa kumwona Bwana. Unaposoma 2 Nefi 16, kumbuka ishara zifuatazo na maana yake inayowezekana kuwa.

Maserafi: Malaika ambao wanaishi katika uwepo wa Mungu. Nabii Joseph Smith alifunza kwamba “malaika wa Mungu hana mabawa kamwe” (Historia ya Kanisa, 3:392). Mabawa ya malaika ni ishara ya uwezo wao wa kwenda na kutenda.

Moshi: Inaweza kuashiria uwepo wa Bwana (ona Ufunuo wa Yohana 15:8).

Midomo michafu: Kutosahili

Makaa ya moto (moto): Nguvu ya kusafisha, kama vile nguvu za kutakasa za Roho Mtakatifu.

Altari: Kihalisi, altari ilikuwa ni mahali ambapo dhabihu zilitolewa. Inaweza hapo kumaanisha dhabihu iliyofanywa na Yesu Kristo kwa niaba yetu—Upatanisho.

  1. Soma 2 Nefi 16:1–7, na uandike katika shajara yako ya kujifunza maandiko majibu yako kwa maswali yafuatayo:

    1. Ni nini mmoja wa maserafi alisema kuhusu Bwana wa Majeshi?

    2. Unafikiri Isaya alimaanisha nini aliposema, “Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu? Ni nini kilichomfanya yeye ghafula kuhisi hivi? (3 Nefi 27:19 inaweza kutoa mapendekezo.)

    3. Ni nini kilitokea na kubadilisha hisia za Isaya za kutosahili?

    4. Je! Uzoefu huu ungemtayarisha Isaya vipi kuenenda miongoni mwa watu na kuwafunza toba?

Mojawapo Rejea kweli kuu zilizofunzwa katika wito wa Isaya ni kwamba tunaweza kutakaswa kutostahili kwetu kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo. Tafakari kuhusu wakati ulipohisi nguvu za utakazo za Upatanisho katika maisha yako.

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya chini ya kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza 2 Nefi 11–16 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha