Seminari
Kitengo 23: Siku ya 1, Helamani 10


Kitengo 23: Siku ya 1

Helamani 10

Utangulizi

Baada ya kesi kukamilika kwa mauaji ya jaji mkuu (ona Helamani 7–9), Nefi alianza kurudi nyumbani kwake mwenyewe. Alitafakari kile Bwana alikuwa amemwonyesha na pia kuwa na wasiwasi kuhusu uovu wa watu. Katika wakati wa Nefi wa kuvunjika moyo, Bwana aliongea naye na kumbariki milele na uwezo wa kuunganisha. Bwana aliagiza Nefi kuendelea kuhubiri toba kwa watu, agizo ambayo Nefi alitii mara moja.

Helamani 10:1–11

Nephi anapokea uwezo wa kuunganisha

Fikiria juu ya wakati ulipojaribu uwezavyo kufanya yaliyo sahihi lakini majibu uliopokea kutoka kwa wengine au matokeo uliopokea yalikuwa tofauti kuliko ulivyotarajia. Katika Helamani 10 utasoma jinsi Bwana alibariki Nefi alipoendelea kuwa mwaminifu katika mazingira magumu.

Baada ya kuondolewa mashtaka ya mauaji ya jaji mkuu, Nefi aligundua kuwa watu hawakujibu katika imani na kutubu baada ya kushuhudia matukio makubwa ya yaliyoelezwa katikaHelamani 9. Nefi alianza kurudi nyumbani akihisi kuvunjika moyo. Soma Helamani 10:1–3, na uangalie kile Nefi alitafakari akielekea nyumbani. Unaweza kutaka kuweka alama kila wakati neno kutafakari linapotajwa katika mistari hizi. Kutafakari kunamaanisha kuwaza na kufikiri kwa undani, mara nyingi juu ya maandiko au mambo mengine ya Mungu. Ikiunganishwa pamoja na maombi, kutafakari mambo ya Mungu kunaweza kuleta ufunuo na ufahamu zaidi.

Fikiria juu ya maswali yafuatayo:

  • Nefi alikuwa akitafakari juu ya nini?

  • Kwa nini alikuwa akihisi “kuhuzunishwa,” au huzuni?

  • Ni nini kilichotokea alipokuwa akitafakari?

Kanuni iliyoonyeshwa katika Helamani 10:1–3 ni: Kutafakari mambo ya Bwana hutuandaa kuupokea ufunuo. Mifano mingine katika maandiko pia inaonyesha kanuni hii: Nefi alitafakari juu ya mambo ambayo baba yake, Lehi, alikuwa akifundisha na kujifunza ukweli wake (ona 1 Nefi 10:17; 11:1); kijana Joseph Smith “alitafakari tena na tena” juu ya Yakobo 1:5 na ukweli ukafunuliwa (ona Joseph Smith—Historia 1:11–19); na Rais Joseph F. Smith alitafakari na kuwaza juu ya maandiko yanayohusiana na ukombozi wa wafu na ukweli ukafunuliwa kwake (ona M&M 138:1–6, 11).

Ufunuo mwingi watu hupokea wanapotafakari mambo ya Bwana, hata hivyo, haiji kupitia kwa njia ya kusikia sauti, kuona maono, au njia nyingine ya ajabu kama hayo. Mzee David A. Bednar wa Akidi ya wale Mitume Kumi na Wawili alielezea:

Mzee David A. Bednar

“Ufunuo hutolewa katika njia mbalimbali, ikiwemo, kwa mfano, ndoto, maono, na mazungumzo na wajumbe wa mbinguni, na uongozi. Ufunuo mwingine hupokelewa mara moja na kwa nguvu, mwingine yanatambuliwa hatua kwa hatua na kwa ustadi. …

 Mara nyingi zaidi, ufunuo huja katika kiwango kidogo kwa muda na hutolewa kulingana na matakwa yetu, ustahiki, na maandalizi. Mawasiliano kama hayo kutoka kwa Baba wa Mbinguni hatua kwa hatua na kwa upole ‘yatatonatona juu ya[nafsi zetu] kama umande utokao mbinguni’(M&M 121:45). Muundo huu wa ufunuo huonekana kuwa ya kawaida zaidi kuliko nadra na ni dhahiri katika matukio ya Nefi jinsi alivyojaribu njia kadhaa tofauti kabla ya kufanikiwa kupata bamba za shaba kutoka kwa Labani (ona 1 Nefi 3–4). …

 Kweli za msingi za injili rejeshwa hazikutolewa zote mara moja kwa Nabii Joseph Smith katika Kisitu Kitakatifu. Tunu hizi zenye thamani kuu zilifunuliwa kadri hali ilivyostahili na kadri muda ulivyostahili.

“Rais Joseph F. Smith alielezea jinsi muundo huu wa ufunuo wa yaliyotokea katika maisha yake: ‘Kama kijana mara nyingi ningemwomba Bwana kunionyesha baadhi ya mambo ya kushangaza, ili niweze kupokea ushuhuda. Lakini Bwana alificha maajabu kutoka kwangu, na akanionyesha ukweli, mstari juu ya mstari … , mpaka alinifanya kujua ukweli kutoka kwenye utosi wa kichwa changu hadi kwenye nyayo za miguu yangu, na mpaka shaka na hofu yatolewe kutoka kwangu. (in Conference Report, Apr. 1900, 40–41).

“Sisi kama waumini wa Kanisa hujaribu kusisitiza sana juu ya maonyesho makubwa na ya ajabu ya kiroho kiasi kwamba tunaweza kushindwa kufahamu na hata tunaweza kupuuza njia ya kawaida ambayo Roho Mtakatifu hutimiza kazi yake” (“The Spirit of Revelation,” Ensign or Liahona, May 2011, 88).

  1. ikoni ya shajaraAndika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kuhusu wakati ulihisi ulipokea ufunuo binafsi. Ni hali zipi zilizosababisha kuletwa kwa ufunuo? Jinsi gani kutafakari kulikusaidia kupokea ufunuo? (Kumbuka kuwa ufunuo unaweza kuja katika njia nyingi. Inaweza kuhusisha wakati ghafla au polepole wa kutaalamika na uelewa au hisia za amani na uhakika.)

msichana katika msitu

Tenga muda wa kutafakari mara kwa mara katika maisha yako, kama vile wakati wa mikutano za kanisa, kabla na baada ya sala ya binafsi na kujifunza maandiko, baada ya kuangalia au kusikiliza mkutano mkuu, wakati wa kufunga, au wakati wa kuheshimu Sabato.

Fikiria ulikuwa na kitu chenye thamani kuu kwako na ulitaka kuiacha chini ya ulinzi wa mtu mwingine. Ni nani utakayeamini kuutunza? Ni kwa nini ungemchagua mtu huyo? Ni nini ambayo mtu huyo amefanya ili kupata imani yako?

Soma Helamani 10:4–5, na uangalie ni kwa nini Bwana aliamini Nefi. Bila kusita kunamaanisha “bila kuchoka.” Tafakari mifano ya watu unaowajua wanaonekana kumtumikia Bwana bila kusita pasipojalisha hali ilivyo.

Majibu ya Bwana kwa Nefi katika Helamani 10:4 inafundisha kanuni: Bwana anatuamini na baraka na majukumu tunapoweka mapenzi Yake mbele yetu.

  1. ikoni ya shajaraJibu moja au zaidi ya maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni kwa njia gani unaweza kujua mapenzi ya Bwana kuhusu maisha yako?

    2. Umefanya nini katika maisha yako hivi karibuni kuonyesha Bwana kwamba mapenzi Yake ni muhimu zaidi kuliko mapenzi yako mwenyewe na kwamba ndicho unahitaji kufuata wakati wote?

    3. Ni eneo gani moja ya maisha yako ambayo unaweza kutafuta vyema na kufuata mapenzi ya Bwana badala ya yako mwenyewe?

Soma Helamani 10:5–7, na utambue baraka na ahadi ambazo Bwana alimpa Nefi kwa kuwa mwaminifu. Andika baraka na ahadi karibu na mstari sambamba:

Mstari 5:

Mstari 6:

Mstari 7:

Baraka zilizotambuliwa katika Helamani 10:7 ni mafundisho ya msingi ya injili ya Yesu Kristo: Uwezo wa kuunganisha hufunga na hufungua duniani na mbinguni. Je, unajua watu wengine katika maandiko ambao walipewa uwezo huu wa kuunganisha? Unaweza kutaka-kurejeaHelamani 10:7 kwa maandiko yafuatayo: 1 Wafalme 17 (Eliya); Mathayo 16:15–19 (Petro); Mafundisho na Maagano 132:46 (Joseph Smith).

Hekalu la Bern Switzerland

Soma Mafundisho na Maagano 128:9 , na utambue kile Nabii Joseph Smith alifundisha juu ya uwezo wa kuunganisha.

Funguo hizo hizo za uwezo wa kuunganisha zimeshikiliwa leo na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Kama vile Bwana aliweza kuamini Nefi, Bwana pia anajua Rais wa Kanisa hatatumia uwezo huu kwa njia yoyote kinyume na mapenzi Yake. Mamlaka hii ya kuunganisha imepewa wamiliki wengine wa ukuhani wanaostahili duniani kote, kuwezesha maagizo ya ukuhani kufunganishwa duniani na mbinguni.

Fikiria juu ya taarifa ifuatayo na Mzee Bruce R. McConkie wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kuhusu umuhimu wa uwezo huu wa kuunganisha:

Mzee Bruce R. McConkie

“Mambo yote yasiyoidhinishwa kwa uwezo huu yana mwisho watu wanapokufa. Isipokuwa ubatizo uwe na idhinisho hii ya kudumu, haitaruhusu mtu kwa ufalme wa selestia; isipokuwa agano la milele la ndoa lifungwe kwa mamlaka hii, haitawapeleka wahusika kuokolewa katika mbinguni kuu ndani ya ulimwengu wa selestia.

“Mambo yote yanaweza kupata nguvu ya kudumu na uhalali kwa sababu ya uwezo wa kuunganisha” (Mormon Doctrine, 2nd ed. [1966], 683).

  1. ikoni ya shajaraJibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Kulingana na Mzee McConkie, ni nini kinatokea ikiwa agizo haijaidhinishwa kwa mamlaka sahihi?

    2. Jinsi gani uwezo wa kuunganisha umebadilisha maisha yako, na ni kwa jinsi gani ungeitaka kubariki maisha yako katika siku zijazo?

Soma thibitisho lifuatalo la na Mzee Russell M. Nelson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kwamba uwezo wa kuunganisha wa Mungu umerejeshwa: “Mahekalu, ibada, maagano, karama, na miunganisho, yamerejeshwa, tu kama ilivyotabiriwa. Maagizo ya hekalu huleta upatanisho na Bwana na hufunganisha familia pamoja milele. Utii kwa maagano matakatifu yaliyofanywa katika mahekalu inatustahilisha kwa uzima wa milele —zawadi kubwa ya Mungu kwa mwanadamu” (“Prepare for the Blessings of the Temple,” Ensign, Oct. 2010, 42).

Kulingana na Mzee Nelson, ni nini kinatustahilisha kupokea baraka zilizo ahidiwa za uwezo wa kuunganisha?

Helamani 10:12–19

Nefi anatii amri ya Bwana ya kuhubiri toba kwa watu

Umewahi kuulizwa kufanya kitu na mzazi, mwajiri, au kiongozi na kuchelewa kufanya hivyo au kushindwa kufanya kile kilichoulizwa? Fikiria ni ujumbe gani unatuma wakati unapochelewa kutenda kwa kile unachoulizwa.

Soma Helamani 10:11–12, na uangalie jinsi Nefi alivyoitikia amri ya Bwana kwake kuhubiri toba kwa watu. Tunaonyesha Bwana nini tunapoitika mara moja na kwa haraka kwa shauri Lake, na amri?

  1. ikoni ya shajaraSoma Helamani 10:13–18. Kisha, katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika sentesi chache kuhusu yale unayojifunza kutoka kwa mfano wa Nefi wa kuitikia amri ya Bwana. Andika njia moja unaweza kuweka hii katika maisha yako.

Uaminifu wa Nefi ulionyesha kwamba Bwana angeweza kumwamini, na alibarikiwa na uwezo mwingi na ulinzi.

ikoni ya umahiri wa maandiko
Rejeo la Umahiri wa Maandiko

Kwa rejeo umahiri wa maandiko, soma1 Nefi 3:7; 2 Nefi 2:27; 2 Nefi 31:19–20; na Mosia 2:17. Fikiria jinsi mistari hizi za umahiri wa maandiko zinahusika na Nefi na utumishi wake katikaHelamani 10.

Tafuta njia za kuweka mapenzi ya Bwana kabla yako mwenyewe na kutii kwa haraka. Unapomtumikia Bwana kwa uaminifu jinsi Nefi alivyofanya, atakuamini na kukubariki.

  1. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Helamani 10na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: