Seminari
Kitengo cha 17: Siku ya 3, Alma 21–22


Kitengo cha 17: Siku ya 3

Alma 21–22

Utangulizi

Haruni, mmoja wa ndugu za Amoni, alijaribu kuwafundisha Waamaleki na Waamuloni kuhusu Yesu Kristo na Upatanisho, lakini watu walimkataa. Yeye na wenzake wengine waliishia gerezani katika nchi ya Midoni. Walibakia waaminifu wakati wao wa mashaka. Baada ya Amoni na Mfalme Lamoni kupata uhuru wao, Haruni alimfundisha babake Lamoni jinsi ya “kuzaliwa kwa Mungu” (Alma 22:15). Mfalme alijifunza kwamba kwa kutubu dhambi zake, angeweza kuja kumjua Mungu na hatimaye kupokea uzima wa milele. Uaminifu wa Haruni na ndugu zake uliwasaidia Walamani kuja kumfahamu Mungu na njia Yake ya ukombozi.

wamisionari gerezani

Alma 21:1–23

Haruni na ndugu zake wahubiri injili licha ya majaribio na kifungo

Fikiria juu ya wakati ulipokuwa ukijaribu kwa nguvu kutii amri na bado ulikabiliawa na matatizo. Kisha tafakari maswali yafuatayo: Ulifanya nini ili kuwa mwaminifu licha ya majaribio yaliyokukabili? Unapokumbuka kuhusu uzoefu huo, unahisi Bwana alikubariki vipi kwa wakati huo?

Wakati Amoni alikuwa akifundisha Mfalme Lamoni na watu wake (ona Alma 17–19), Haruni na wenzake walipatwa na mashaka makubwa walipojaribu kufundisha katika sehemu mbalimbali za nchi. Kwa muhtasari wa majaribio ambayo Haruni na wenzake walipitia wakiwa gerezani, somaAlma 20:28–30. Kisha soma vifungu kutoka Alma 21:1–17 vilivyotambuliwa katika shughuli hapa chini. Angalia jinsi Haruni na ndugu zake walipitia majaribio yao.

  1. ikoni ya shajaraNakili chati ifuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko, ukiacha nafasi kwa maoni yako baada ya kila andiko:

    Changamoto au Ugumu

    Jinsi Haruni na Wenzake Walivyojibu

    Alma 21:3

    Alma 21:4

    Alma 21:5–6, 8

    Alma 21:7, 9

    Alma 21:10–11

    Alma 21:11–12

    Alma 21:13–14

    Alma 21:15

    Baada ya kusoma kila kifungu cha maandiko, katika safu ya kushoto ya chati, andika changamoto au matatizo ambayo Haruni na wenzake walipitia. Katika safu ya kulia, andika jinsi Haruni na wenzake walijibu. Kisha jibu maswali yafuatayo:

    1. Kwa nini unafikiri ingekuwa rahisi kwao kukata tamaa, kupoteza matumaini, na kurudi nyumbani mahali pa urafiki miongoni mwa Wanefi?

    2. Tunawezaje, kama washiriki wamisionari, kufaidika kwa kusoma maelezo haya?

Soma Alma 21:16–17, na uangalie jinsi Bwana aliwasaidia Haruni na ndugu zake kufanya kazi Yake walipovumilia kwa imani. Kupitia kwa Haruni na ndugu zake, tunajifunza kanuni hii: Tukivumilia kwa uaminifu kupitia majaribio yetu, Bwana atatusaidia kufanya kazi Yake. Unaweza kutaka kuandika kanuni hii katika maandiko yako au shajara ya kujifunza maandiko.

Fikiria ni aina gani ya kazi Mungu anayo kwako ya kufanya sasa na katika siku za baadaye na ni changamoto gani unaweza kukabiliana nazo kwa kujaribu kukamilisha kazi hii. Soma maelezo yafuatayo kutoka kwa Rais Thomas S. Monson, aliyefundisha kwamba tunaweza kuwa na majaribio tunapojitahidi kufanya kazi ya Bwana:

Rais Thomas S. Monson

“Ili kufikia, kufundisha, kugusa nafsi zenye thamani ambazo Baba yetu ametayarisha kwa ujumbe Wake ni kazi kubwa sana. Mafanikio ni nadra sana. Kwa kawaida unatanguliwa na machozi, majaribio, uaminifu, na ushuhuda . …

“… Watumishi wa Mungu hupata faraja kutoka kwa hakikisho la Bwana: ‘Mimi ni pamoja nanyi siku zote (Mathayo 28:20). Ahadi hii ya ajabu inakuimarisha. … Inakufariji wakati ule wa kukata tamaa, ambayo huja kwa wote” (“Tears, Trials, Trust, Testimony,” Ensign, May 1987, 43).

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kuhusu uzoefu ulipokuwa unavumilia kwa uaminifu kupitia majaribio. Au unaweza kuandika kuhusu jinsi unapanga kuwa mwaminifu katika changamoto ya sasa, kwa kutumia kanuni katika somo hili. Pia, andika kuhusu hali chache za baadaye unapofikiri unahitaji kuvumilia kupitia majaribio unapofanya kazi ya Bwana.

Soma Alma 21:18–23 ili kuona kile Amoni alifanya baada ya kuwasaidia Haruni na ndugu zake kuachiliwa kutoka gerezani. Angalia jinsi maisha ya Walamani yalivyobadilika kwa sababu Amoni aliwafundisha injili.

Fikiria jinsi Injili ya Yesu Kristo imebadilisha maisha ya mtu unayemjua. Tafakari jinsi unavyoweza kushiriki injili na mtu unayemjua, au fikiria juu ya mtu anayeweza kuvutiwa na mfano wa Haruni na ndugu zake. Fikiria kushiriki na huyo mtu yale uliyojifunza kutoka kwa mfano wa Haruni na ndugu zake walipovumilia kwa uaminifu katika kazi ya Bwana.

Alma 22

Babake Lamoni, ambaye ni mfalme juu ya nchi yote, anaamini injili kama ilivyofundishwa na Haruni.

Kumbuka tukio la Amoni na babake Lamoni, ambalo lilichambuliwa katika somo lililopita. Soma tena ombi maalum la mfalme kwa Amoni, kilichoandikwa katika Alma 20:27. Unaposoma Alma 22:1–3, angalia jinsi mfalme aliitikia ziara ya Haruni.

Soma Alma 22:4–6, na utambue kilichomsumbua babake Mfalme Lamoni. Pekua Alma 22:7–14 upate kweli ambazo Haruni alifundisha babake Lamoni.

Tafakari juu ya maswali yafuatayo (inaweza kuwa na manufaa kukumbuka majadiliano sawa kuhusu Mfalme Lamoni katikaAlma 17–18):

  • Kwa nini mfalme alifaa kuamini katika Mungu ili kuelewa toba?

  • Ni kwa jinsi gani kujua kuhusu Kuanguka kulimsaidia mfalme kuelewa toba?

  1. ikoni ya shajaraJibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Kwa nini ni muhimu kuelewa Kuanguka kwa Adamu na Upatanisho wa Yesu Kristo ili kuelewa toba?

Pekua Alma 22:15, ukiangalia kile ambacho babake Mfalme Lamoni alikuwa tayari kuachana nacho ili kupokea furaha na uzima wa milele, na ufikirie kuweka alama katika maandiko yako.

  1. ikoni ya shajaraJibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Kwa nini unafikiri mtazamo ambao babake Mfalme Lamoni alikuwa nao ni muhimu kwa kila mtu anayetaka kuja kumjua Mungu?

Soma Alma 22:16 ili kuona jinsi Haruni alijibu swali la mfalme kuhusu jinsi ya kupokea uzima wa milele. (Fikiria kuweka alama kweli muhimu unaona zikifundishwa katika mstari huu.) Ni kwa jinsi gani kukubali na kuishi kweli ambazo Haruni alifundisha kunaongoza mtu kupokea uzima wa milele?

Soma Alma 22:17–18, ukiangalia jinsi mfalme alijibu maelekezo ya Haruni. Tafakari swali lifuatalo: Tunaweza kujifunza nini kuhusu kuzaliwa kwa Mungu kutoka kwa babake Mfalme Lamoni?

Unaweza kutaka kuweka alama kishazi hiki katika Alma 22:18: “Nitaacha dhambi zangu zote ili nikujue wewe” Tafakari ukweli ufuatao, na ukiandike katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Lazima tuwe tayari kuziacha dhambi zetu zote ili tubadilishwe kiroho na kuzaliwa kwa Mungu.

Mzee Dallin H. Oaks

Soma maelezo yafuatayo ya Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Wale Mitume Kumi na Wawili: “Injili ya Yesu Kristo hutupatia changamoto tubadilike. ‘Tubuni’ ni ujumbe wake wa mara kwa mara, na kutubu inamaana kuachana na matendo yetu yote —binafsi, familia, kabila, na kitaifa—ambayo ni kinyume na amri za Mungu. Madhumuni ya injili ni kubadilisha viumbe vya kawaida na kuwa raia wa selestia, na hiyo inahitaji mabadiliko (“Repentance and Change,” Ensign or Liahona, Nov. 2003, 37).

Tafakari kile unahitaji kufanya katika maisha yako sasa ili kubadilishwa kiroho.

Soma Alma 22:19–22 ili kuona ni matukio gani yalifuata sala ya mfalme. Soma Alma 22:23–27, ukiangalia ili kuona kile babake Lamoni alifanya kwa sababu alikuwa amepokea mabadiliko ya moyo na alikuwa amepokea Roho wa Bwana kwa ajili yake mwenyewe.

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kile ulichojifunza kuhusu kuzaliwa tena kwa kujifunza kuhusu babake Mfalme Lamoni. Eleza jinsi unafikiri mfano wake ungeweza kuwasaidia vijana leo kufanya mabadiliko katika maisha yao ili kuwasaidia kuzaliwa kwa Mungu.

  2. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    NimejifunzaAlma 21–22 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: