Seminari
Kitengo cha 10: Siku ya 3, Enoshi


Kitengo cha 10: Siku ya 3

Enoshi

Utangulizi

Baada ya kutafakari juu ya maneno ya baba yake, Enoshi aliomba na kupokea ondoleo la dhambi zake. Kisha aliomba kwa ustawi wa kiroho wa Wanefi na Walamani na kutumia maisha yake akifanya kazi wa ajili ya wokovu wao.

Enoshi 1:1–8

Baada ya kutafakari juu ya maneno ya baba yake, Enoshi aliomba na kupokea ondoleo la dhambi zake.

Soma Enoshi 1:1, 3, na uangalie ushawishi Yakobo alikuwa nao juu ya Enoshi. Ingawa Enoshi alikuwa mwana na mjukuu wa manabii, bado yeye alihitaji uzoefu wa nguvu za Upatanisho wa Yesu Kristo kwake mwenyewe.

Fikiria wakati ulihisi unaona njaa sana. Weka mviringo maneno hapo chini ambayo yanaelezea kile unahisi wakati unaona njaa:

  • tupu

  • udhaifu

  • kutotosheka

  • kufa njaa

  • uchungu

  • wasi wasi

  • kutamani

Angazia kishazi “nafsi yangu ikapata njaa” katika Enoshi 1:4. Unafikiri kishazi hiki kina maana gani?

Kishazi “nafsi yangu ikapata njaa” kinaweza kujumuisha hisia kama vile utupu wa kiroho au uchungu, au hamu ya kujazwa kiroho. Enoshi aliandika kuhusu wakati ulipopata uzoefu wa hii njaa ya kiroho. Aliandika kwamba maneno ya baba yake “yakapenya ndani ya moyo [wake]” (Enoshi 1:3). Alipotafakari juu ya maneno hayo, alipata hamu ambazo zilimfanya yeye kutenda kwa imani. Matendo yake ya uaminifu yalileta mabadiliko katika maisha yake na baraka kutoka kwa Bwana.

Enoshi Akiomba
  1. ikoni ya shajaraAnza mfululizo wa mazoezi ili kukusaidia kuelewa uzoefu wa Enoshi na kuulinganisha na maisha yako kwa kugawa ukurasa mzima kwa shajara yako ya kujifunza maandiko katika sehemu sita na kuweka kitambulisho kwenye kila sehemu kama ifuatavyo:

Kile Enoshi alitamani:

Kile ninachotamani:

Kile Enoshi alifanya:

Kile ninahitaji kufanya:

Kile Enoshi alipata uzoefu juu yake:

Uzoefu wangu:

  1. ikoni ya shajaraSoma Enoshi 1:2–3, na utafute vishazi katika kila aya ambavyo vinaonyesha kile Enoshi alitamani kuwa nacho katika maisha yake. Andika vishazi hivi katika sehemu iliyoalamishwa “Kile Enoshi alitamani” katika chati ya shajara yako ya kujifunza maandiko.

Hamu ya Enoshi ya ondoleo la dhambi zake hutusaidia kuelewa kile alimaanisha katika Enoshi 1:4 alipoandika, “Nafsi yangu ikapata njaa.” Kama ziada ya kupata njaa ya msamaha, Enoshi pia alitamani “uzima wa milele, na shangwe ya watakatifu” (Enoshi 1:3). Alitaka kuhisi furaha ambayo huja kutokana na kuwa mstahiki kuwa pamoja na Bwana na wengine ambao ni wenye haki.

  1. ikoni ya shajaraFikiria kama una baadhi ya hisia kama hizo za njaa ya kiroho ambazo Enoshi alielezea. Katika chati ya shajara yako ya kujifunza maandiko, katika sehemu iliyoalamishwa “Kile ninachotamani.” Andika kuhusu baadhi ya hamu za kiroho ambazo wewe una njaa kwazo katika maisha yako.

Hamu za Enoshi zilisababisha aifanyie kazi imani yake na kutenda. Katika Enoshi 1:2, tambua na uweke alama neno Enoshi alilolitumia kuelezea juhudi alizofanya. Kumbuka kwamba Enoshi hakushindana na Mungu bali alienda mbele za Mungu katika maombi. Kushindana kama huku kunajumuisha masumbuko ya kiakili na kiroho ili kumwonyesha Baba wa Mbinguni uaminifu wa hamu zetu na utayari wetu wa kutubu na kufanya mabadiliko yanayohitajika katika maisha yetu. Katika Enoshi 1:4, Enoshi aliandika baadhi ya utondoti unaoelezea kushindana kwake.

  1. ikoni ya shajaraSoma Enoshi 1:4, na uweke alama vitu Enoshi alifanya ili kuonyesha alikuwa mwaminifu alipotafuta ondoleo la dhambi zake. Orodhesha kile unatambua chini ya “Kile Enoshi alifanya” katika chati ya shajara yako ya kujifunza maandiko.

Neno kulilia katika Enoshi 1:4 humaanisha kuomba kwa unyenyekevu na kwa hamu kuu. Maombi yetu yanaweza kuwa yasiwe marefu kama ya Enoshi, lakini yanahitaji kuwa ya uaminifu.

  1. ikoni ya shajaraKatika chati ya shajara yako ya kujifunza maandiko, chini ya “Kile ninahitaji kufanya,” andika mawazo yako kuhusu jinsi unaweza kumwonyesha Bwana uaminifu wako unapoomba na kutafuta baraka Zake za kiroho.

  2. ikoni ya shajaraJuhudi za Enoshi za uaminifu na dhati zilileta baraka kuu katika maisha yake. Soma Enoshi 1:5–8, na uweka alama kile Enoshi alipata uzoefu wake. Orodhesha hivi katika sehemu ya “Kile Enoshi alipata uzoefu wake” ya chati ya shajara yako ya kujifunza maandiko. Unaposoma aya ya 5 na 6, angalia jinsi Enoshi alijua alikuwa amesamehewa. Sauti iliyotajwa katika aya ya 5 ilikuwa sauti ambayo ilikuja katika akili ya Enoshi (ona Enoshi 1:10).

Enoshi 1:7–8 anafunza kwamba tunapofanya imani katika Yesu Kristo, dhambi zetu zinaweza kusamehewa na tunaweza kuwa wazima. Hamu yetu ya kuboreka, maombi yetu ya uaminifu, na juhudi zetu za kutubu ni njia tunazoweza kuonyesha imani katika Yesu Kristo.

Rais Dieter F. Uchtdorf wa Urais wa Kwanza alielezea jinsi hatia yetu inaweza kufagiliwa mbali tunapofanya imani katika Yesu Kristo na kutubu dhambi zetu.

Rais Dieter F. Uchtdorf

“Mara tunapotubu kikweli, Kristo ataondoa mzigo wa hatia ya dhambi zetu. Tunaweza kujua wenyewe kwamba tumesamehewa na kutakaswa. Roho Mtakatifu atathibitisha haya kwetu; Yeye ni Mtakasaji. Hamna ushuhuda mwingine wa msamaha unaoweza kuwa mkuu zaidi ya huu. …

“[Bwana] alitangaza, ‘Tazama, yule ambaye ametubu dhambi zake, huyu anasamehewa, na Mimi, Bwana, sizikumbuki tena’ (M&M 58:42).

“Shetani atajaribu kutufanya sisi tuamini kwamba dhambi zetu haziwezi kusamehewa kwa sababu sisi tunaweza kuzikumbuka. Shetani ni muongo; yeye hujaribu kutia mawaa kuona kwetu na kutuelekeza mbali kutoka kwenye mapito ya toba na msamaha. Mungu hakuahidi kwamba sisi hatungezikumbuka dhambi zetu. Kukumbuka kutatusaidia sisi kuepuka kufanya makosa yale yale tena. Lakini kama tutakaa wakweli na waaminifu, kumbukumbu ya dhambi zetu italainishwa baada ya muda. Hii itakuwa sehemu ya mchakato wa uponyaji na utakaso unaohitajika ” Ensign au Liahona, May 2007, 101).

Ili kukusaidia wewe kutumia maneno ya Rais Uchtdorf, tafakari maswali yafuatayo: Ni lini ulihisi kwamba Bwana amekusamehe dhambi zako? Ulijua vipi umesamehewa? Umeshahisi msamaha wa Bwana hivi majuzi?

  1. ikoni ya shajaraBaada ya kutafakari maswali hayo hapo juu, andika katika sehemu ya “Uzoefu wangu” katika chati ya shajara yako ya kujifunza maandiko uzoefu wako pamoja na hisia za msamaha. Au unaweza kuandika kuhusu kile unatumania kupata uzoefu wake unapofanya imani katika Yesu Kristo.

Enoshi 1:9–27

Enoshi anawaombea Wanefi na Walamani na anafanya kazi pamoja wa wengine kwa wokovu wao

duara za kati moja

Mchoro huu unaonyesha maombi ya Enoshi. Alijiombea mwenyewe kwanza na kisha akapanua maombi yake kujumuisha wengine. Soma Enoshi 1:9–10, na uweke alama katika maandiko yako ni nani Enoshi aliombea mara ya pili. Soma Enoshi 1:11–14, na uweke alama ni nani Enoshi aliombea mara ya tatu.

  1. ikoni ya shajaraJibu swali kifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Kulingana na maelezo ya Enoshi ya nia ya Walamani katika Enoshi 1:14, ni nini kinachokupendeza kuhusu maombi yake kwa wao?

Tunajifunza kutoka kwa mfano wa Enoshi kwamba tunapopata uzoefu wa baraka za Upatanisho wa Yesu Kristo, tutatafuta kuwasaidia wengine kupokea wokovu. Ili kukusaidia kukumbuka ukweli huu, unaweza kutaka kuandika yote au sehemu ya kauli ifuatayo kutoka kwa Rais Howard W. Hunter pembezoni mwa maandiko yako.

Rais Howard W. Hunter

“Wakati wowote tunapopata baraka za Upatanisho katika maisha yetu, hatuwezi kujizuia bali tutajali ustawi wa ndugu zetu. …

“Kiashiria kikuu cha uongofu wa kibinafsi wa mtu ni hamu ya kushiriki injili na wengine” (The Teachings of Howard W. Hunter, ed. Clyde J. Williams [1997], 248–49).

Soma Enoshi 1:19–20, 26, na uweke alama maneno au vishazi ambavyo vinaonyesha uaminifu wa hamu za Enoshi kwa Wanefi na Walamani baada ya yeye kuwaombea wao.

Soma Enoshi 1:27, na utafute ushahidi wa furaha Enoshi alipata kwa juhudi zake na hakikisho la uzima wa milele yeye alilopokea.

  1. ikoni ya shajaraIli kukusaidia kutumia kile umejifunza katika somo hili, kwa maombi amua njia moja au zaidi unazoweza kufuata mfano wa Enoshi. Chagua kauli moja hapo chini, na uikamilishe katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Kama Enoshi, mimi natamani kupokea ondoleo la dhambi zangu. Nitamwonyesha Bwana mimi ni mwaminifu katika hamu hii kwa …

    2. Kama Enoshi, mimi natamani kuwasaidia wanafamilia yangu na marafiki kuja kwa Yesu Kristo. Mtu mmoja nitakayetafuta kumsaidia ni (jina la mtu). Nitatafuta kumsaidia mtu huyu kwa …

    3. Enoshi aliwaombea Walamani, ambao wangedhaniwa kuwa maadui zake. Kama Enoshi, mimi nitaka kuonyesha upendo wa Bwana kwa wale ambao si wapole kwangu. Njia moja nitafanya hivyo ni …

Tafuta kukamilisha kile umeandika katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Unapofanya imani katika Upatanisho wa Yesu Kristo na kutubu, unaweza kupata msamaha, shangwe, na ongezeko la hamu ya kuwasaidia wengine.

  1. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Enoshi 1na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu: