Seminari
Kitengo cha 13: Siku ya 4, Mosia 25


Kitengo cha 13: Siku ya 4

Mosia 25

Utangulizi

Kama ilivyoandikwa katika Mosia 25, watu wa Limhi na wafuasi wa Alma walisafiri hadi Zarahemla kuungana kwa usalama chini ya utawala wa Mfalme Mosia. Makundi haya ya Wanefi yalipokuja pamoja, yalitambua wema wa Mungu na nguvu Zake za kuwakomboa. Pia walianzisha Kanisa lililoungana. Unapojifunza somo hili, unaweza kufaidika kutokana na kufikiria kuhusu jinsi wewe ulivyoona wema wa Mungu katika maisha yako na baraka za kuwa wa Kanisa la Yesu Kristo la kweli.

Mosia 25:1–13

Wale waliokusanyika katika Zarahemla wanaunganika na kujulikana kama Wanefi.

Soma hadithi ifuatayo kuhusu msichana ambaye alilindwa kwa sababu ya kumsikiliza Roho wakati alipokuwa katika matembezi marefu pamoja na kikundi cha Wasichana:

“Tilipokuwa njiani tukirudi, mimi nilikuwa katika kundi la waenda pole pole, wasichana watano na kiongozi wetu. Walikuwa na shughuli nyingi sana wakipiga picha, kwa hivyo niliamua kutangulia. Nilipokuwa nikiteremka kilima nilimsikia ng’ombe [ambaye alisikika kama alikuwa anakufa]. Sauti ya onyo, hali thabiti na kimya, ikasema “Rudi nyuma.’ Mimi karibu niipuuze, lakini ikaja tena. Wakati huu nilisikiliza na nikarudi kwenye kundi lile. Tulipoanza kuteremka, tukawaona dume wawili weusi wakubwa wakitembea upesi na kwa hasira wakipanda kilima. Yule mkubwa alianza kuparura mchangani akitukazia macho sisi. Tuliingia uoga wa kuchachawisha, lakini kiongozi wetu wa ukuhani alimvuta mawazo, na tuliweza kupanda ua kwenda kwenye usalama.

Tulipokuwa tunaingia kambini tena, nilitambua kwamba kama singesikiliza onyo kutoka kwa Roho, ningejeruhiwa vibaya sana au hata kuuawa. Nilijua kwamba Baba wa Mbinguni ananijali mimi kibinafsi na alikuwa ameniweka salama. Mimi nina shukrani sana kwa Bwana kwa onyo hilo. Uzoefu huu uliimarisha ushuhuda wangu na kunipatia upendo mkubwa sana kwa Bwana” (Marissa W., “Turn Back,” New Era, Nov. 2010, 47).

Je! Kusikia au kusoma kuhusu uzoefu wa watu wengine ambao unaonyesha wema na nguvu za Mungu katika maisha yao kunasaidia vipi kukuimarisha wewe?

Picha
mchoro wa safari

Watu wa Limhi na watu wa Alma waliopoungana na watu katika Zarahemla, Mfalme Mosia alifanya kumbukumu zao zisomwe kwa watu wote (ona Mosia 25:1–6). Pekua Mosia 25:7 upate jinsi watu wa Mfalme Mosia walijibu walipokuwa wanasikiliza taarifa za vile Mungu aliwatendea watu hawa.

  1. Kwa kila moja ya aya hizi nne katika Mosia 25:8–11, andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko mjibizo wa watu waliposikia matukio ya ndugu zao. Kwa mfano, katika Mosia 25:8, walipowaona wale ambao walikombolewa kutoka kwa utumwa wa Walamani, watu “walikuwa wamejazwa na shangwe kuu.”

    1. Mosia 25:8

    2. Mosia 25:9

    3. Mosia 25:10

    4. Mosiah 25:11

Fikiria kuandika kanuni ifuatayo pembezoni mwa maandiko yako karibu na Mosia 25:8–11: Kwa kujifunza kumbukumbu za matendo ya Mungu na wengine, tunaweza kuhisi shangwe na shukrani kwa wema wa Mungu.

Fikiria vyanzo viwezekanavyo kutoka kwavyo unaweza kujifunza juu wengine ambao walipata kuona wema wa Mungu. Hii inaweza kujumuisha maandiko, historia ya Kanisa, magazeti ya Kanisa, hotuba za mkutano mkuu, kumbukumbu za historia ya familia yako mwenyewe, mikutano ya ushuhuda, na Shule ya Jumapili na madarasa ya ukuhani au Wasichana. Fikiria wakati ulipojifunza kuhusu wema wa Mungu kutoka katika vyanzo hivi. Kisha tafakari majibu yako kwa maswali yafuatayo:

  • Je! Nimewahi kupata uzoefu ambapo kujifunza wema wa Mungu kwa wengine kulinisaidia kuhisi shangwe au shukrani?

  • Nini kinaweza kuwa baadhi ya athari za muda mrefu kama kila mara ningejifunza uzoefu wa wema wa Mungu katika mahusiano Yake na wengine— iwe ni katika maandiko au vyanzo vingine?

Katika wiki inayokuja, fikiria kutafuta mojawapo ya vyanzo ulivyofikiria vya hadithi ya wema wa Mungu ambavyo vinakujaza wewe na mshangao, mastaajabu, shangwe, au shukrani. Unaweza kuandika kuhusu kile wewe umejifunza na jinsi kimekuathiri katika shajara yako ya kibinafsi. Pia unaweza kutumia hadithi hii katika jioni ya familia nyumbani kufundisha familia yako kuhusu wema wa Mungu, au unaweza kushiriki hadithi hii na darasa lako la seminari au na rafiki.

Mosia 25:14–24

Alma alianzisha makanisa ya Mungu katika nchi yote ya Wanefi

Baada ya Mosia kumaliza kusema na kusoma kumbukumbu za watu, Alma aliongea na wao. Soma Mosia 25:14–16, na utambue kile Alma alifunza. Andika majibu ya maswali yafuatayo katika kitabu cha kiada:

  • Ni kwa jinsi gani kile Alma alifunza ni muhtasari unaofaa wa uzoefu wa watu wa Limhi pamoja na wafuasi wa Alma?

  • Kwa nini unafikiria maneno ya Alma yangekuwa na umuhimu kwa watu kuusikia baada ya kusikia historia ya watu wa Zenifu?

Kabla ya kusoma zaidi katika Mosia 25, fikiria kuhusu wakati ulipohudhuria kata au tawi la Watakatifu wa Siku za Mwisho lingine lisilo tawi au kata yako ya nyumbani. Fikiria kuhusu mifanano uliyogundua kati ya kata au tawi la nyumbani na lile wewe ulitembelea.

Soma Mosia 25:17–22, na utafute jinsi Kanisa lilivyotawaliwa miongoni mwa Wanefi katika siku za Alma. Rejeo la “makanisa” katika Mosia 25:21 ni sawa sawa na njia tunayoita kata na matawi katika Kanisa siku hizi. Kama vile katika siku za Alma, Mungu huwaita viongozi kuongoza Kanisa Lake siku hizi.

Picha
mkutano wa sakramenti

Katika Mosia 23:16 ulijifunza kwamba Alma “alikuwa kuhani wao mkuu” na “mwanzilishi wa Kanisa lao”(Mosia 23:16) Rais Joseph Fielding Smith alielezea hivi: “Sehemu kubwa ya Wanefi, chini ya Mfalme Mosia wa pili, ilikuwa bado salama katika nchi ya Zarahemla. Rejeo linasema kwamba Alma alikuwa mwanzilishi wa kanisa lao lina rejeo tu kwa wakimbizi ambao walikuwa wametoroka kutoka nchi ya Wanefi ya urithi wa kwanza. Hatimaye walipata njia yao kurudi kwenye sehemu kuu ya Kanisa na Alma alikuwa amesimikwa kama kuhani mkuu juu ya Kanisa katika nchi zote zilizomilikiwa na Wanefi” (Answers to Gospel Questions, comp. Joseph Fielding Smith Jr., 5 vols. [1957–66], 3:39-40).

  1. Andika majibu mafupi kwa maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni kwa njia gani Kanisa la Wanefi linafanana na Kanisa leo?

    2. Kwa nini unafikiria ni muhimu kwamba viongozi waliitwa na Alma, ambaye alikuwa na mamlaka kutoka kwa Mungu?

    3. Kwa nini ni muhimu kwa viongozi kufunza kweli hizo hizo kwa washiriki wote wa Kanisa kote ulimwenguni?

Unaposoma Mosia 25:23–24, tafuta vishazi ambavyo vinaelezea wale ambao walijiunga na Kanisa la Kristo ambavyo pia vinawaelezea washiriki wa Kanisa la Bwana leo. Kanuni moja tunayojifunza kutoka kwa aya hizi ni: Tunapojichukulia juu yetu jina la Yesu Kristo na kuishi vilivyo, Bwana atatumwagia Roho Yake juu yetu.

  1. Andika majibu kwa maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni kwa njia gani vishazi katika Mosia 25:23–24 ambavyo vinaelezea washiriki Wanefi wa Kanisa pia vinatumika na washiriki wa Kanisa leo?

    2. Ni kwa jinsi gani kukumbuka kwamba wewe umejichukulia juu yako jina la Yesu Kristo kunaweza kuleta tofauti katika fikra zako na chaguo za kila siku unazofanya?

Fahamu katika Mosia 25:24 kwamba “Bwana aliwateremshia Roho wake” watu Wake. ‎ Mzee Joseph B. Wirthlin wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisisitiza thamani ya kipawa cha Roho Mtakatifu kwa waumini wa Kanisa:

Picha
Mzee Joseph B. Wirthlin

“Kipawa cha Roho Mtakatifu, ambacho ni haki ya kupokea Roho Mtakatifu kama mwenzi wa daima, kinapatikana tu kwa masharti ya imani katika Kristo, toba, ubatizo kwa uzamisho, na kuwekelewa mikono na watumishi walioidhinishwa waliotawazwa kwa Ukuhani wa Melkizedeki. Ni kipawa chenye thamani kubwa kinachopatikana tu kwa waumini wastahiki wa Kanisa la Mungu.

 Ni chanzo cha ushuhuda na vipawa vya kiroho. Kinaelimisha akili, hujaza nafsi zetu kwa shangwe, hutufunza sisi vitu vyote, na hutuletea elimu iliyosahaulika katika kukumbuka zetu. Roho Mtakatifu pia ‘atatuonyesha [sisi] vitu vyote ambavyo [sisi] tunastahili kutenda’ [2 Nephi 32:5]” (“The Unspeakable Gift,” Ensign or Liahona, May 2003, 26).

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni kwa njia gani ushirika wako katika Kanisa la Yesu Kristo unakusaidia wewe kuhisi Roho?

    2. Unaweza kufanya nini ili kuongeza uaminifu wako na matendo mema ili kwamba uweze kuhisi kuwa karibu zaidi na Roho?

Tafuta nafasi ya kushiriki na mtu jinsi kipawa cha Roho Mtakatifu kimebariki maisha yako. Baraka ulizopokea kupitia Roho Mtakatifu zinaweza kuongezeka unapojitahidi kuwa mwenye kustahili wenzi Wake.

  1. Andika yafuatayo mwisho wa kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Mosia 25 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha