Kitengo 27: Siku ya 3
3 Nefi 27
Utangulizi
Mapema katika huduma yao, baada ya siku ya pili ya kutokea kwa Mwokozi Aliyefufuka miongoni mwao, wale mitume kumi na wawili Wanefi walikutana pamoja katika maombi yenye nguvu na kufunga. Yesu Kristo tena aliwatokea na kujibu swali lao kuhusu kile jina la Kanisa linapaswa kuwa. Mwokozi Aliwafundisha kwamba Upatanisho ni kiini cha injili Yake na kwamba kupitia kwa Upatanisho tutaweza kusimama bila doa mbele Yake tunapotubu, kubatizwa, na kuvumilia hadi mwisho. Aidha, aliwaamuru wanafunzi Wake wawe kama Yeye.
3 Nefi 27:1–12
Bwana anawafundisha wanafunzi kumi na wawili kwamba Kanisa Lake linapaswa kupewa jina Lake
Fikiria kwamba ulitaka kuanzisha klabu mpya au timu ya michezo. Amua ni aina gani ya klabu au timu ungetaka kujenga, na kisha chagua jina la shirika lako. Andika majina yote na aina ya shirika uliochagua:
Fikiria kuhusu mashirika kadha unazojua kuhusu na kile majina yao yanamaanisha kuhusu madhumuni yao na watu wanaoshiriki nao.
Wanafunzi kumi na wawili Wanefi waliendelea kufundisha na kuwabatiza watu. Katika tukio moja walikuwa wameungana pamoja katika kufunga na kuomba wakati Yesu alipowatembelea tena (ona 3 Nefi 27:1–2). Soma 3 Nefi 27:3–7, ukiangalia swali ambalo wanafunzi waliuliza na jibu la Mwokozi. Unaweza kutaka kuwekea alama sababu ambazo Yesu Kristo alitoa kwa kuita Kanisa katika jina Lake.
Tafuta 3 Nefi 27:8–10, na uwekee alama kile Mwokozi alifundisha kuwa ishara za Kanisa Lake la kweli. Kamilisha kishazi kifuatacho katika mwongozo wako ili kuonyesha makala kadhaa muhimu ya Kanisa la kweli:
Kanisa la kweli la Yesu Kristo ni .
Fikiria ni kwa nini ni muhimu kwamba Kanisa la kweli la Yesu Kristo haibebi tu jina Lake bali pia limejengwa juu ya injili Yake (ona 3 Nefi 27:8–10). Mwokozi aliahidi Wanefi kwamba kama Kanisa limejengwa juu ya injili Yake, basi Baba wa Mbinguni ataonyesha kazi Zake ndani yake (ona 3 Nefi 27:10). Tafakari jinsi wewe binafsi umeona Baba wa Mbinguni Akionyesha kazi Zake katika Kanisa.
-
Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika Kuwa mshiriki wa Kanisa la kweli la Yesu Kristo ni muhimu kwangu kwa sababu … Kisha andika aya fupi inayoeleza mawazo yako juu ya kishazi. Jaribu kujumuisha sababu nyingi uwezavyo kutoka kwa kile ulichojifunza ulipokuwa ukisoma3 Nefi 27:1–12.
3 Nefi 27:13–22
Yesu Kristo anafafanua injili Yake na anafundisha kile tunapaswa kufanya ili kusimama bila hatia mbele Zake
Fikiria juu ya wakati ulipopatikana ukifanya kitu ulichojua kuwa ni kibaya. Kumbuka jinsi ulivyojisikia wakati ukweli kuhusu kile ulifanya kilipojulikana. Tafakari maswali yafuatayo: Ungejisikiaje kusimama mbele ya Bwana kuhukumiwa kama bado kulikuwa na baadhi ya matendo mabaya ambayo bado haujatubu? Ungejisikiaje kusimama mbele ya Bwana ili kuhukumiwa kama hakungalikuwa na njia ya kutubu kwa dhambi yoyote uliyotenda wakati wa maisha yako?
Baada ya kufundisha Wanefi kwamba Kanisa Lake lazima lijengwe juu ya injili Yake, Mwokozi aliendelea kuwafundisha maana ya injili Yake. Neno injili maana halisi ni “habari njema” Kupitia kwa Injili bado kuna habari njema kwa sisi sote ikiwa tutatenda dhambi.
-
Soma 3 Nephi 27:13–16, 19, na uangalie vipengele vya injili ambavyo ni habari njema kwetu sote. Msingi wa Injili ya Yesu Kristo ni kwamba Alifanya mapenzi ya Baba Yake katika kutimiza Upatanisho.Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Mwokozi Alishuhudia kwa wanafunzi Wake kwamba Alikuja ulimwenguni ili kufanya mapenzi ya Baba Yake. Kwa mujibu wa 3 Nefi 27:14, mapenzi ya Baba wa Mbinguni ilikuwa gani kwa Mwanawe Mtakatifu?
-
Kwa sababu Mwokozi alitimiza mapenzi ya Baba Yake, ni nini kinapatikana kwa wanadamu wote? (ona hasa 3 Nefi 27:19).
-
-
Ili kukusaidia kufahamu ukuu wa habari hii njema, soma moja au zaidi ya vifungu vifuatavyo vya maandiko na uandike maelezo mafupi katika shajara yako ya kujifunza maandiko kuhusu ni kwa nini Upatanisho wa Yesu Kristo ni habari njema vile:2 Nefi 9:8–10; Alma 34:14–16; Helamani 14:15–18.
Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alishuhudia ni kwa nini Injili ni habari njema kwa watu wote: ‘Habari njema’ ilikuwa kwamba kifo na kuzimu vinaweza kutorokwa, kwamba makosa na dhambi vinaweza kushindwa, kwamba kulikuwa na matumaini, kwamba kulikuwa na usaidizi, kwamba kisichoweza kutatuliwa kilitatuliwa, kwamba adui alikuwa ameshindwa. Habari njema ilikuwa kwamba kaburi la kila mtu siku moja itakuwa tupu, kwamba nafsi ya kila mtu inaweza kuwa safi tena, kwamba kila mtoto wa Mungu anaweza tena kurudi kwa Baba ambaye aliwapa uhai” (“Missionary Work and the Atonement,” Ensign, Mar. 2001, 8, 10).
Je, umewahi kusikia mtu akisema kwamba tunahitaji “kuishi injili”? Wakati mtu anapotualika “kuishi injili,” wao kwa kawaida hutualika kuishi kulingana na kanuni na kupokea ibada ambazo hualika uwezo wa Upatanisho wa Yesu Kristo katika maisha yetu ili tuweze kuokolewa. Tafuta 3 Nefi 27:20–21 ukiangalia kile tunapaswa kufanya ili kupokea baraka zote za Upatanisho na kujiandaa kwa ajili ya hukumu.
-
Andika Kama tuta ,basi tutakuwa na uwezo wa kusimama bila madoa mbele ya Yesu Kristo katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Kamilisha kishazi hiki kwa kuandika kanuni ya injili kutoka 3 Nefi 27:20–21 ambayo ni lazima tufuate ili kusimama bila doa mbele ya Bwana. (Unaweza kutambua kanuni kadhaa kwa sehemu ya “kama” ya taarifa kuu.) Kisha jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Naweza kufanya nini katika maisha yangu sasa hivi ili “kuishi injili” kikamilifu zaidi ili niweze kuona uwezo wa Upatanisho na kusimama mbele ya Mungu bila doa, siku ya mwisho?
Tafakari vile itakavyokuwa siku moja kusimama mbele ya Yesu Kristo ukijua kwamba umefanywa msafi kupitia kwa Upatanisho Wake kwa utii wa kanuni, amri, na maagizo ya injili Yake.
3 Nefi 27:23–33
Yesu Kristo anafundisha wanafunzi Wake kuwa kama Yeye Alivyo
Kama ilivyoandikwa katika mwisho wa 3 Nefi 27, Yesu Kristo alitoa maelekezo kwa wanafunzi Wake kumi na wawili na kuwafundisha kuhusu wajibu wao kama viongozi na waamuzi wa watu wao. Soma 3 Nefi 27:27, na uangalie amri Aliowapa wanafunzi ili kuwasaidia kutimiza majukumu yao kwa haki. Chukua muda na ufikirie juu ya maswali yafuatayo:
-
Mbona itakuwa ni muhimu kwa wale ambao wahukumu wengine kuwa kama Mwokozi?
-
Rejea nyuma kwa 3 Nefi 27:21, ni nini Mwokozi Aliamuru wafuasi kufanya?
-
Kuna uhusiano gani kati ya kufanya kazi ya Mwokozi na kuwa kama Yeye?
Soma tena 3 Nefi 27:21, 27, na uweke alama katika maandiko yako maneno na vishazi vinavyoonyesha kwamba Bwana anatarajia wanafunzi Wake kuiga matendo Yake na kuwa kama Alivyo.
-
Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko ili kukusaidia kutumia mafundisho ya Mwokozi ili kuwa zaidi kama Yeye:
-
Ni nafasi zipi nilikuwa nazo jana za kuwa kama Mwokozi?
-
Jinsi gani naweza kuwa zaidi kama Mwokozi leo?
-
Ni matendo gani ya Mwokozi naweza kufanya kesho katika shule au nyumbani?
-
Rais Ezra Taft Benson alifundisha kwamba wale wanaojitahidi kuwa kama Yesu Kristo hufikia ukuu wa kweli: “Mtu huyo ni mkubwa zaidi na mwenye baraka zaidi na furaha ambaye maisha yake yanakaribia mfano wa Kristo. Hii haina uhusiano na mali ya dunia, utajiri, mamlaka, au heshima. Jaribio pekee la kweli la ukuu, kubarikiwa, furaha, ndivyo jinsi maisha inavyoweza kuwa kama Mwalimu, Yesu Kristo. Yeye ndiye njia ya kweli, ukweli kamili, na uzima tele” (“Jesus Christ—Gifts and Expectations,” Ensign, Dec. 1988, 2).
-
Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
Nimejifunza 3 Nefi 27 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).
Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: