Seminari
Kitengo cha 11: Siku ya 4, Mosia 5–6


Kitengo cha 11: Siku ya 4

Mosia 5–6

Utangulizi

Mosia 5Inahitimisha hotuba ya Mfalme Benyamini kwa watu wake ambayo ilianza katikaMosia 2. Kama matokeo ya imani yao katika maneno ya Mfalme Benyamini, watu walipata mabadiliko makubwa ya moyo. Waliingia katika agano na Mungu na kujichukulia juu yao wenyewe jina la Yesu Kristo. Kama ilivyoandikwa katika Mosia 6, Mfalme Benyamini alihamisha uwezo wake wa utawala juu ya ufalme wake kwa mwanawe Mosia, na Mosia alitawala kwa haki, akifuata mfano wa baba yake.

Mosia 5:1–4

Watu wa Mfalme Benyamini walipata mabadiliko makubwa

Fikiria kuhusu maswali yafuatayo: Je, umeshawahi kutamani ungeweza kubadili kitu fulani kuhusu wewe mwenyewe ? Ulifanya nini kuhusu hicho?

Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alielezea haja ya kila mmoja wetu kupata mabadiliko makubwa katika maisha yetu: “Kiini cha injili ya Yesu Kristo kinahitaji mabadiliko ya kimsingi na ya kudumu katika hasili yetu yenyewe inayowezeshwa kupitia utegemezi wetu wa ‘fadhili, na rehema, na neema za Masiya Mtakatifu’ (2 Nefi 2:8). Tunapochagua kumfuata Bwana, tunachagua kubadilishwa—kuzaliwa upya kiroho” (“Ye Must Be Born Again,” Ensign or Liahona, May 2007, 20).

Unaweza kutaka kuandika kishazi kifuatacho katika maandiko yako karibu na Mosia 5:2: “Tunapochagua kumfuata Bwana, tunachagua kubadilika.”

Ni kwa njia gani unafikiria tunachagua kubadilika wakati tunapochagua kumfuata Yesu Kristo?

Rejea muhtasari wa sura ya Mosia 3 na Mosia 4 ili kukumbuka lengo muhimu la hotuba ya Mfalme Benyamini. Katika hitimisho la mahubiri yake, Mfalme Benyamini aliwauliza watu kama wanaamini maneno aliyokuwa amewafunza kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo (ona Mosia 5:1). Soma Mosia 5:2–4, na utafute kile kilichobadilika katika mioyo ya watu baada ya kusikiliza maneno ya mfalme wao. Unaposoma, itasaidia kujua kwamba “silika”(Mosia 5:2) linahusu mitazamo, hamu, au mwenendo.

Picha
Mzee David A. Bednar

Soma kauli ifuatayo kutoka kwa Mzee David A. Bednar: “Injili ya Yesu Kristo inajumuisha zaidi kuliko kuepuka, kushinda, na kutakaswa kutoka kwa dhambi na ushawishi mbaya katika maisha yetu; pia inahitaji kufanya vyema, kuwa mwema, na kuboreka. … Kuwa na mioyo yetu iliyobadilishwa na Roho Mtakatifu kiasi kwamba ‘hatuna tamaa ya kutenda maovu tena, lakini kutenda mema daima’ (Mosia 5:2), kama walivyofanya watu wa Mfalme Benjamini, ni uwajibikaji wa agano tulilokubali. Mabadiliko haya makubwa si jambo la matokeo ya kushughulika sana au kukuza nidhamu kuu ya kibinafsi. Badala yake, ni matokeo ya mabadiliko ya kimsingi katika hamu zetu, nia zetu, na asili yetu inayowezeshwa kupitia Upatanisho wa Kristo Bwana. Madhumuni yetu ya kiroho ni kushinda vyote dhambi na hamu ya kutenda dhambi” (“Clean Hands and a Pure Heart,” Ensign, Nov. 2007, 81–82).

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, jibu maswali yafuatayo:

    1. Unafikiria inamaanisha nini kupata “mabadiliko makuu” katika moyo wako? (Mosia 5:2).

    2. Tunapochagua kumfuata Yesu Kristo, kwa nini tunahitaji kubadilisha silika zetu na si tu tabia yetu.

    3. Kwa nini unafikiria Upatanisho wa Yesu Kristo ni muhimu kwa mabadiliko kutokea ndani yetu?

Jifunze Mosia 5:2, 4, ukitafuta kile watu walifanya ambacho kiliruhusu mabadiliko makuu kutokea ndani yao. Unaweza kuweka alama vitu hivi katika maandiko yako. Kumbuka kwamba maneno ya Mfalme Benyamini yalikuwa ni kuhusu uwezo wa Upatanisho wa Yesu Kristo, na watu walikuwa na imani kuu katika maneno haya.

Mojawapo wa kanuni tunazojifunza kutoka kwa aya hizi ni: Tunapofanya imani katika Yesu Kristo na kupokea Roho Mtakatifu, tunaweza kupata mabadiliko makuu ya moyo.

  1. Kulingana na mafunzo yako ya Mosia 5:1–4 na kanuni iliyopo hapo juu, andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kile unaweza kufanya kutumia imani zaidi katika Mwokozi. Ni vitu gani mahususi unavyoweza kufanya, kuanzia leo, kufanya imani zaidi ili kwamba uweze kuhimiza na kudumisha mabadiliko makuu ya moyo katika maisha yako?

Mosia 5:5–15

Watu wa Mfalme Benyamini wanaingia katika agano na Mungu na kupewa jina jipya

Baada ya watu wa Mfalme Benyamini kupata mabadiliko makuu ya moyo, walitamani kuingia katika agano na Bwana. Tambua maneno au vishazi katika Mosia 5:5 ambayo vinaonyesha kiwango cha azimio watu wa Mfalme Benyamini walihisi juu ya kufanya na kuweka agano hili.

Tunapofanya maagano na Mungu, Yeye huamua masharti ya maagano, na sisi tunayakubali masharti hayo. Kisha Mungu anatuahidi baraka fulani kwa utiifu wetu (ona M&M 82:10). Kufanya maagano ni njia moja wapo ya kumwonyesha Bwana sisi ni waaminifu katika hamu zetu za kumhudumia Yeye.

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni vishazi gani katika Mosia 5:5 vinavyokukumbusha ahadi tunazofanya upya kila wakati tuposhiriki sakramenti?

    2. Unafikiria kufanya na kuweka maagano kunakusaidia vipi kudumisha “mabadiliko ya moyo” makuu?

Rejea tena kwa Mosia 1:11–12. Mojawapo wa madhumuni ya Mfalme Benyamini katika kuwakusanya watu wake ilikuwa ni kuwapa jina. Soma Mosia 5:6–7, na uweke alama jina Mfalme Benyamini aliwapatia watu wake baada ya wao kufanya agano lao na Bwana.

Aya hizi zinafunza kanuni hii: Tunajichukulia juu yetu wenyewe jina la Yesu Kristo kupitia maagano matakatifu. Soma Mosia 5:8–14, na utafute kwa nini ni muhimu kwetu sisi kujichukulia juu yetu wenyewe jina la Yesu Kristo.

Ni baadhi ya baraka zipi za kuwa na jina la Yesu Kristo kuandikwa katika mioyo yetu?

Ni nini kinaweza kusababisha jina “kufutwa” kutoka kwenye moyo wako au moyo wa mtu mwingine?

Soma Mosia 5:15, na utafute ahadi Bwana anawawekea wale wanaoweka maagano yao.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika jinsi unavyohisi unapofikiria kuhusu kuwa jina la Yesu Kristo limeandikwa katika moyo wako. Andika sababu moja au zaidi kwa nini unataka kuweka jina hili na kamwe usilipoteze.

Mosia 6:1–7

Mosia inaanza enzi yake kama mfalme

Soma Mosia 6:3, na utambue kile Mfalme Benyamini alifanya kabla ya kuruhusu umati uondoke.

Mfalme Benyamini alifanya nini ili kuwasaidia watu wake kukumbuka maagano waliyofanya?

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika jinsi viongozi wa ukuhani na walimu wanakusaidia wewe kuweka maagano yako.

Mfalme Benyamini alikufa miaka mitatu baada ya yeye kutoa mahubiri yake. Soma Mosia 6:6–7, na utafute jinsi Mfalme Mosia alifuata mfano wa baba yake kama kiongozi mwema.

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Mosia 5–6 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha