Seminari
Kitengo 26: Siku ya 2, 3 Nefi 18


Kitengo 26: Siku ya 2

3 Nefi 18

Utangulizi

Yesu Kristo alipohitimisha siku ya kwanza ya huduma Yake kati ya Wanefi, Alitoa sakramenti na kuwaamuru watu kuomba daima kwa Baba na kueneza ushirika kwa watu wote. Mwokozi aliahidi baraka kubwa kwa wale ambao wanashika amri hizi. Baadaye aliwapa wanafunzi Wake Wanefi kumi na wawili maagizo kuhusu huduma zao katika Kanisa. Kabla ya kupaa mbinguni, Aliwapa uwezo wa kutoa karama ya Roho Mtakatifu.

3 Nefi 18:1–14

Yesu Kristo anatoa sakramenti kwa Wanefi

Soma hadithi ifuatayo na Mzee Gerald N. Lund, aliyehudumu kama mjumbe wa Sabini, na ufikiri jinsi ingekuwa kwa mtu katika hadithi hii:

“Wakati mwingine uliopita kulikuwa na makala ya kuvutia kuhusu upandaji wa mlima [wenye] hadithi inayotoa jibu ajabu kwa swali, ‘Tunaweza kufanya nini kama watumishi wasiokuwa na faida kwa Kristo kwa kile alichotufanyia?’

“Makala ilikuwa juu ya mtu aitwaye Czenkusch anayesimamia shule ya kupanda. Czenkusch alikuwa akimwelezea aliyehoji mfumo salama wa kupanda mlima. Huu ndio mfumo ambao wapandaji hujilinda kutokana na maporomoko. Mpandaji mmoja hufikia eneo salama na kushika kamba kwa niaba ya mpandaji mwingine, kwa kawaida kuzunguka mwili wake mwenyewe. ‘Nimekufunga,’ maana yake, ‘Nimekushika wewe. Kama kitu kitatokea, nitakuzuia kuanguka.’ Ni sehemu muhimu ya kupanda mlima. Sasa ona kile kilichofuatia katika makala: ‘Kujifunga kwa kamba kumemletea Czenkusch nyakati zake bora na mbaya katika upandaji. Czenkusch aliwahi kuanguka kutoka kwenye gema refu, na kuchomoa visaidizi vitatu vya kimitambo na kutoa mtambo wa usalama kwenye mwamba. Alisimamishwa, kichwa chini, futi 10 kutoka ardhini wakati mtambo wake wa usalama ulipozuia kule kuanguka kwa nguvu za mikono yake iliyonyooshwa. “Usiokoe maisha yangu,” asema Czenkusch. “Utajibu vipi mtu kama huyo? Mpe kamba iliotumika kupanda kama zawadi ya Krismasi? La, unamkumbuka yeye. Unamkumbuka daima ”’ [Eric G. Anderson, , “The Vertical Wilderness,” Private Practice, Nov. 1979, 21; mkazo umeongezwa]” (“The Grace and Mercy of Jesus Christ,” katika Jesus Christ: Son of God, Savior, ed. Paul H. Peterson, Gary L. Hatch, and Laura D. Card [2002], 48).

Soma 3 Nefi 18:1–11,, na uangalia kile Yesu Kristo aliomba Wanefi kufanya ili kumkumbuka Yeye. Unaweza kutaka kuwekea alama maneno ukumbusho na ukumbusho katika mistari 7 na 11. Kwa nini unafikiri ni muhimu kukumbuka daima dhabihu ya upatanisho wa Mwokozi kwa ajili yako? Utatendaje tofauti unapomkumbuka Mwokozi?

Amri ya Mwokozi ya kukumbuka mwili wake na damu ingekuwa na maana hasa kwa watu kwa sababu walikuwa wameona majeraha katika mwili wake muda mfupi tu kabla. Ingawa hujaona majeraha katika mwili wa Mwokozi, kama vile watu wa Kitabu cha Mormoni walivyofanya, unaweza kukumbuka dhabihu ya upatanisho Wake unaposhiriki sakramenti.

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, jibu swali lifuatalo: Jinsi gani kukumbuka dhabihu ya Mwokozi wakati wa sakramenti imekusaidia kuhisi shukrani Kwake?

Maneno ya Yesu Kristo yaliyoandikwa katika 3 Nefi 18:7–11 yanafundisha kanuni zifuatazo: Tunaposhiriki sakramenti, tunashuhudia kwa Baba kwamba tuko tayari kufanya yote Ametuamrisha. Tunaposhiriki sakramenti, tunashuhudia kwa Baba kwamba tutamkumbuka Yesu Kristo daima. Chambua 3 Nefi 18:7–11, na uwekee alama maneno au vishazi vinavyofundisha kanuni hizi. Unaposoma mstari 11, fikiri jinsi ungejisikia ikiwa Mwokozi angesema maneno hayo kwako.

  1. ikoni ya shajaraChagua mawili ya maswali yafuatayo yakujibu katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni vipengele gani vya maisha ya Mwokozi na huduma unaweza kukumbuka wakati wa ibada ya sakramenti?

    2. Unaweza kufanya nini ili daima kumbuka Mwokozi wakati wa wiki nzima?

    3. Ukijitahidi kwa dhati kukumbuka Mwokozi wakati wa sakramenti, hii inaweza kukuathiri kivipi wakati wa wiki ifuatayo?

Tambua kanuni nyingine inayofundishwa katika 3 Nefi 18:7, 11kwa kukamilisha taarifa ifuatayo kwa kishazi kinachoelezea kile Mwokozi aliahidi wale wanaoshiriki sakramenti na kumkumbuka Yeye. Tunaposhiriki sakramenti na kumkumbuka Mwokozi daima, tuta.

mkate na maji
  1. ikoni ya shajaraLinganisha 3 Nefi 18:12–14 na Helamani 5:12. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika jinsi kushiriki sakramenti kila wiki kunaweza kukusaidia kufanya Yesu Kristo msingi ambao unaweza kujenga maisha yako.

  2. ikoni ya shajaraIli kukusaidia kukumbuka Mwokozi zaidi, andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kila siku kwa wiki ijayo kile ulifanya kukumbuka Mwokozi siku hiyo. Unaweza kujumuisha yale ulifikiria kuhusu wakati wa sakramenti au jinsi kukumbuka Mwokozi kulihawishi mawazo yako, maneno, na matendo.

3 Nefi 18:15–25

Yesu alifundisha Wanefi kuomba daima kwa Baba na kukutana pamoja kila mara

Baada ya Yesu Kristo kutoa sakramenti kwa Wanefi, Aliwafundisha kanuni muhimu kuhusu maombi. Moja wapo ya kanuni Alizofundisha ni: Ikiwa tutakuwa waangalifu na kuomba daima kwa Baba, tunaweza kupinga majaribu ya Shetani. Tunapokuwa waangalifu, tunakuwa macho kiroho, waangalifu, au kujihadhari.

Soma 3 Nefi 18:15–21, na uwekee alama maneno au vishazi vinavyofundisha kanuni iliyo onyeshwa hapo juu. Kwa nini unafikiri kwamba kuangalia na kuomba ni muhimu kwa kupinga majaribu?

Tambua kwamba 3 Nefi 18:15, 20–21 ni marejeo ya maandiko. Fikiria kuwekea alama mistari hizi katika maandiko yako.

  1. ikoni ya shajaraSoma na ufikiri juu ya maswali yafuatayo, na kisha ujibu maswali mawili au zaidi katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Jinsi gani kuomba kumekusaidia kupinga majaribu ya Shetani?

    2. Unaweza kufanya nini ili kuboresha maombi yako binafsi?

    3. Ni baraka gani umeona kwa kuomba pamoja na familia yako? (ona 3 Nefi 18:21).

    4. Unaweza kufanya nini ili kusaidia familia yako kukuwa na maombi thabiti na ya maana ya familia?

Tunapoomba kwa Baba wa Mbinguni na kumkaribia Mwokozi wetu Yesu Kristo, mara nyingi tunataka kuwasaidia wengine kusogea karibu na Yeye pia. Fikiria juu ya mtu ambaye ungependa kusaidia kusogea karibu na Mwokozi. Soma 3 Nefi 18:22–24, na uangalie kanuni ifuatayo katika mistari: Tunapohudumia wengine, tunaweza kuwasaidia kuja kwa Kristo.

Kama ilivyoandikwa katika 3 Nefi 18:24, Mwokozi alifundisha kwamba tunapaswa kila mmoja kuinua juu nuru yetu ili iangae juu ya dunia. Pia alisema kwamba Yeye ndiye mwangaza ambao tutainua. Mzee Robert D. Hales wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha kwamba tunapaswa kuinua juu mwangaza wa Mwokozi kwa kushika amri Zake na kufuata mfano Wake:

Mzee Robert D. Hales

“Tunapaswa kuwa kama Mwokozi Anapotuamuru ‘Njooni, mnifuate.’ Je, si itampendeza Yesu kama tutaacha nuru yetu kuangaza kwamba wale wanaotufuata watakuwa wanamfuata Mwokozi? Kuna wale wanaotafuta nuru[ambao] watapita kwa furaha kupitia lango la ubatizo kwenye njia iliyosonga na nyembamba iendayo kwenye uzima wa milele (ona 2 Nefi 31). Je, utakuwa na ile nuru ambayo itawaongoza kwenye hifadhi salama? …

“Je, umewahi kukoma kufiri kwamba labda wewe ndiwe nuru iliotumwa na Baba wa Mbinguni kuongoza mwingine nyumbani salama au kuwa nguzo kutoka mbali wa kuonyesha njia ya kurudi kwenye njia iliyosonga na nyembamba iendayo uzima wa milele? Nuru yako ni nguzo na kamwe haipaswi kukoma kuwaka au kupotosha wale wanaotafuta njia ya kwenda nyumbani. …

 Yesu Kristo ndiye mwangaza ambao tumepewa ili tuweze kufuata na kujua pa kwenda. [Naomba] kwamba kila mmoja wetu aweze kuchagua haki [ili tuweze] kuinua na kuimarisha walio karibu nasi” (“That Ye May Be Children of Light” [Church Educational System fireside for young adults, Nov. 3, 1996], 6–7).

Kuwaombea wengine, kuwakaribisha kuhudhuria mikutano ya Kanisa, na kuweka mfano wa Kristo ni njia tunazoweza kuhudumia wengine. Tafakari jinsi ulivyojisikia ulipofuata mfano wa Yesu Kristo na kusaidia mtu mwingine kuja karibu na Mwokozi. Utafanya nini leo au wiki hii kufanya nuru yako iangaze ili wale wanaokufuata waweze pia kumfuata Mwokozi?

3 Nefi 18:26–39

Mwokozi anafundisha wanafunzi Wake kueneza ushirika kwa watu wote

Baada ya Mwokozi kuanzisha sakramenti na kufundisha Wanefi kuhusu maombi, Aligeukia wanafunzi kumi na wawili Aliowachagua na kuwafundisha jinsi ya kuongoza na kuelekeza maswala ya Kanisa (ona 3 Nefi 18:26–39). Ona katika 3 Nefi 18:26 kwamba Mwokozi aliacha kuzungumza na umati na kugeukia viongozi “ambao alikuwa amewachagua.” Ujumbe wake katika mistari 28–29 ilitolewa kwa wale viongozi wa ukuhani kama onyo dhidi ya kuruhusu wale wasiostahili kushiriki sakramenti.

Washiriki wa kanisa wanapaswa kuzingatia ustahiki wao wenyewe kushiriki sakramenti na kuacha wajibu wa kuamua ustahiki wa wengine wa kushiriki sakramenti kwa wale ambao Bwana amewaita kufanya maamuzi kama hayo, kama vile askofu au rais wa kigingi. Soma 3 Nefi 18:32, ukiangalia jinsi Mwokozi alivyowafundisha wanafunzi kuhudumia wale waliokuwa wamepotea mbali na imani. Fikiria jinsi unavyoweza “kuendelea kuhudumia” rafiki, mwanafamilia, au mtu katika Kata yako au tawi ambaye amepotea kutoka katika imani.

ikoni ya umahiri wa maandiko
Umahiri wa Maandiko—3 Nefi 18:15, 20–21

Fikiria kutumia dakika chache kukariri3 Nefi 18:15, 20–21. Andika mistari mitatu kwenye kipande cha karatasi, na kisha ujifunze kuyasema. Baada ya kuyasoma mara chache, anza kufuta au kuondoa sehemu mbalimbali za mistari wakati ukiendelea kusema mistari. Unaweza kutaka kurudia utaratibu huu mpaka maneno yote yafutiliwe au kuondolewa.

Unapokariri mistari hizi, fikiria juu ya kile Mwokozi alikuwa akifundisha. Kama ilivyoandikwa katika 3 Nefi 18:15, Yesu Kristo alifundisha Wanefi jinsi kuhimili majaribu ya shetani. Tazama nguvu inayotokana na maombi. Kupitia kwa maombi tunaweza kupewa nguvu ya kupinga majaribu.

Kama ilivyoandikwa katika 3 Nefi 18:20–21, Yesu Kristo alifundisha kwamba tunapoomba kwa imani, Baba hujibu maombi yetu daima, lakini Hujibu kulingana na mpango Wake kwa ajili ya watoto Wake na kile Anajua ni haki kwetu. Rudia mstari 20 kwa sauti: “Na chochote mtakachomwomba Baba katika jina langu, ambacho ni haki, mkiamini kwamba mtapata, tazama mtapewa.” Unafikiri kishazi “ambacho ni haki” kinamaanisha nini katika fungu hili? (Unaweza kutaja Yakobo 4:3.)

Rais Gordon B. Hinckley

Rais Gordon B. Hinckley alishiriki ushuhuda huu: “Mungu, Baba yetu wa milele, Anaishi. Yeye ni Muumba na Mtawala wa ulimwengu na bado Yeye ni Baba yetu. Yeye ni Mwenyezi na ni juu ya yote. Anaweza kufikiwa katika maombi. Je, Yeye husikia maombi ya mtoto? Bila shaka Anasikia. Je, Yeye huijibu? Bila shaka Anajibu. Si kila mara tunavyotaka, lakini Anajibu. Anasikia na Kujibu” (Teachings of Gordon B. Hinckley [1997], 468).

Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha: “[Katika3 Nefi 18:20] Mwokozi anatukumbusha kwamba imani, bila kujali ilivyo na nguvu, haiwezi kuzalisha matokeo kinyume na mapenzi ya yule mwenye nguvu hio. Matumizi ya imani katika Bwana Yesu Kristo daima iko chini ya utaratibu wa mbinguni, kwa wema na mapenzi na hekima na wakati wa Bwana. Hiyo ndio kwa sababu hatuwezi kuwa na imani ya kweli katika Bwana bila pia kuwa na imani kamili katika mapenzi ya Bwana na katika wakati wa Bwana” (“Faith in the Lord Jesus Christ,” Ensign, May 1994, 100).

  1. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza 3 Nefi 18 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: