Seminari
Maneno ya Mormoni


Utangulizi wa Maneno ya Mormoni

Kwa nini Ujifunze Kitabu Hiki?

Katika kujifunza Maneno ya Mormoni, unaweza kuongeza imani yako kwamba “Bwana anajua vitu vyote” (Maneno ya Mormoni 1:7) na kwamba anawaongoza watumishi Wake ili kuleta azma zake. Katika usimulizi wa kihistoria, kitabu hiki kinatumika kama daraja kati ya mabamba madogo ya Nefi (1 Nefi–Omni) na ufupisho wa Mormoni wa mabamba makubwa ya Nefi (Mosia–4 Nefi). Maneno ya Mormoni yanaweza kukusaidia kuelewa vyema ni kumbukumbu gani Mormoni alifupisha alipokuwa anatengeneza Kitabu cha Mormoni. Pia kinakujulisha imani na mafanikio ya Mfalme Benyamini.

Nani Aliandika Kitabu Hiki?

Mormoni ndiye aliandika kitabu hiki. Alikuwa nabii, mweka kumbukumbu, na mfupishaji na mtunzi wa sehemu nyingi za Kitabu cha Mormoni. Kitabu cha Mormoni kimeitwa kwa jina lake. Alikuwa pia jemadari Mnefi na baba mwema. Nabii Moroni alikuwa mwanawe.

Kiliandikwa Lini na Wapi?

Mormoni aliandika kitabu hiki karibu miaka 385, Baada ya Kristo baada ya “kushuhudia maangamizi yote ya watu wake, Wanefi” (Maneno ya Mormoni 1:1). Mormoni hakuandika mahali alipokuwa wakati akiandika kitabu hiki.

Chapisha