Kitengo cha 7: Siku ya 2
2 Nefi 17–20
Utangulizi
Katika 2 Nefi 17–20, Nefi aliandika kwamba Isaya alijaribu kumshawishi mfalme wa Yuda na watu wake kuaamini katika Bwana badala ya ushirikiano wa dunia. Ukitumia aina na vivuli—vya ishara au mawasilisho ambayo yanafunza na kushuhudia juu ya kweli kuu— Isaya alitoa unabii kuhusu matukio ya siku yake mwenyewe, kuzaliwa kwa Yesu Kristo, na maangamizo ya waovu katika Ujio wa Pili wa Bwana.
2 Nefi 17–18
Ufalme wa Yuda ulibarikiwa ulipoweka matumaini yao katika Yesu Kristo
Ili kukusaidia kujitayarisha kwa somo la leo, fikiria wakati ulipokabiliwa na hali ya kuogofya. Je! Unaweza kukumbuka kile ulichofanya kwanza? Unapojifunza 2 Nefi 17–18, jaribu kutambua ushauri wa Isaya kwa wale ambao walijikuta katika hali ngumu au ya kuogofya.
Kwa kujifunza kwako kwa 2 Nefi 17–18, utahitaji kujua kuhusu mataifa madogo matatu ya Shamu, Israeli, na Yuda, vilevile Himaya ya Ashuri kubwa sana, ambayo ilijaribu kuteka mataifa haya madogo. Rejea ramani ifuatayo na chati inayoambatana nayo.
Taifa |
Shamu |
Israeli (Efraimu) |
Yuda |
Mfalme |
Resini |
Peka |
Ahazi |
Mji mkuu |
Dameski |
Samaria |
Yerusalemu |
Soma 2 Nefi 17:1–2, na urejee kwenye ramani. “Shamu ina mwungano na Efraimu” inamaanisha kwamba nchi zilifanya ushirikiano au mkataba. Jaribu kutathimini nani alikuwa anashambulia nani. Tahadhari kwamba kishazi “nyumba ya Daudi” katika kifungu cha 2 kinalenga Ahazi na watu wa Yuda.
Falme za Israeli na Shamu zilitaka kuteka ufalme wa Yuda na kushurutisha Yuda kuingia katika ushirikiano na wao dhidi ya Himaya ya Ashuru yenye nguvu. Ashuru ilikuwa inatishia kuteka eneo lote la ulimwengu wakati huo. Israeli na Shamu waliamini kwamba kwa kuteka Yuda, wangekuwa na watu wengi zaidi na mali zaidi za kupigana Waashuru ambao walikuwa wanasonga mbele (ona 2 Nefi 17:5–6). Mfalme Ahazi alifikiria kufanya ushirikiano huu na Israeli na Shamu.
Fikiria kile ungefanya kama wewe ungekuwa Mfalme Ahazi. Upande mmoja, Ashuru ilikuwa inatishia kushambulia watu wako. Upande mwingine, Shamu na Israeli zinatishia kushambulia kama wewe hautajiunga na ushirikiano na wao kupigana dhidi ya Ashuru. Isaya aliishi katika ufalme wa Yuda, na Bwana alimtuma kwa Ahazi na ujumbe. Unafikiria ungehisi vipi kuhusu ujumbe kutoka kwa nabii kama wewe ungekuwa Mfalme Ahazi?
-
Soma 2 Nefi 17:3–8, na uweke mstari chini ya ujumbe wa Bwana kwa Ahazi na watu wake, kama ulivyotolewa kupitia kwa nabii Isaya. (Neno “mikia ya miwili ya mwenge itakayo moshi” katika msitari wa 4 inalenga mwenge ambao mwale wake umepoa, ishara ya hizi falme mbili zikuvunjika na kutekwa.) Fikiria ulisikia Isaya akisema haya kwa Ahazi. Baadaye, rafiki anakuuliza kile Isaya alisema. Andika sentensi mbili au tatu katika shajara yako ya kujifunza maandiko ukielezea jinsi unaweza kumjibu rafiki yako.
Isaya alijaribu kumsaidia mfalme na watu wake kumtegemea Bwana kwa usaidizi, badala ya kutumainia katika ushirikiano wa kisiasa usiothabiti.
-
Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Kwa nini ni muhimu kwetu kumgeukia Bwana wakati tunahitaji msaada badala ya kutegemea tu watu wengine kutusaidia?
-
Ni baadhi ya njia zipi ambazo kwazo vijana wanaweza kujaribiwa kuweka uhusiano wao na watu wengine mbele ya uhusiano wao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?
-
Bwana alisema angempatia Ahazi na ufalme wa Yuda ishara ya kwamba Yeye angewalinda wao na kwamba hawangehitaji kutegemea ushirikiano wa kilimwengu. Soma 2 Nefi 17:14 ili kutambua ishara. Zungushia neno Imanueli katika mstari huu. Karibu na mstari huu andika “Mathayo 1:22–23.” Soma Mathayo 1:22–23 ili kugundua maana ya jina Imanueli.
Ishara ambayo inamaanisha “Mungu pamoja nasi” ingemsaidia vipi Ahazi wakati huu? Je! Unabii wa Isaya kama huo pia ungekuwa unalenga vipi kuzaliwa kwa Yesu Kristo karne nyingi baadaye?
Kwa uelewa zaidi wa ishara za mtoto akizaliwa, fikiria maelezo yafutayo ya Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili: “Kuna nguvu nyingi au sambamba kwa unabii huu, kama vile ilivyo na wingi wa maandishi ya Isaya. Maana ya moja kwa moja sana inaweza labda kulenga mke wa Isaya, mwanamke halisi na mwema ambaye alimpata mwana karibu na wakati huu [ona 2 Nefi 18:3], mtoto akiwa aina na kivuli kikuu, baadaye kutimizwa kwa unabii ambao ungefanyika katika kuzaliwa kwa Yesu Kristo” (Christ and the New Covenant [1997], 79).
Isaya alitoa unabii kwamba kabla ya mtoto kukua, Ashuru ingeteka majeshi ya wote Israeli (Efraimu) na Shamu (ona 2 Nefi 17:15–25). Ishara inayomaanisha “Mungu pamoja nasi” ilidhamiriwa kumhakikishia Mfalme Ahazi kwamba Mungu atakuwa pamoja nasi wakati tunaweka matumaini katika Yeye, hata nyakati za ugumu na kuogofya. Fikiria kuandika kanuni hii katika maandiko yako.
Soma 2 Nefi 18:6–8, na uweke mstari kishazi “maji ya Shiloa.” Maji ya Shiloa yaliashiria kwa Isaya ushawishi, mtulivu, imara, wa kuhimili na nguvu za Mungu ambazo zinahitajika kuwa sehemu ya maisha ya kisiasa ya taifa (ona 2 Nefi 18:6). Isaya alitumia mfano wa maji ya Shiloa kama kinyume kwa sababu ya watu wa Israeli na watu wa Yuda walimkataa Masiya—“maji ya Shiloa” au mtulivu, mpole, imara, nguvu za kuhimili za Mungu. Kwa hivyo, kama alivyotoa unabii Isaya, mfalme wa Ashuru na ushawishi mbaya na nguvu angamizi za jeshi la uvamizi lake—yaliwakilishwa na “maji ya mto, yenye nguvu na mengi”— yaliteka Shamu na Israeli.
Isaya, kama mshairi, alitumia mitiririko miwili bali ya mito ya maji miwili tofauti kabisa kuelezea kile kitatokea Yuda. Jeshi la Ashuru kisha likaja Yuda—ilikiwakilishwa na neno nchi. Lakini jeshi halikuteka Yerusalemu—iliwakilishwa na kauli “atafurika na kwenda juu, atafika hata kwenye shingo.”
Soma 2 Nefi 18:9–12, na utambue ni mara ngapi Bwana alishauri Yuda isijiunge na Shamu na Israeli. Kama ilivyoandikwa katika 2 Nefi 18:13, ni wapi Bwana, kupitia Isaya, alishauri Yuda aende kwa msaada badala yake?
Kufikia wakati Waashuru waliteka Yuda na kutishia Yerusalemu, ufalme wa Yuda ulikuwa na mfalme mpya. Jina lake likuwa Hezekia. Alitumainia katika Bwana na nabii Isaya. Hatimaye askari 185,000 Waashuru walichinjwa katika kambi yao na malaika wa Bwana (ona 2 Wafalme 19:35; Isaya 37:36).
-
Jibu moja au zaidi ya maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Je, ni hatari gani zilizopo kwa kuweka imani yetu katika nguvu na vishawishi vya ulimwengu badala ya kwa Bwana? (Unaweza kutaka kufikiria juu ya hali ambazo zinaweza kukujaribu ufanye maamuzi kwa sababu ya woga.)
-
Ni lini umemgeukia Bwana kwa nguvu wakati awali ulipojaribiwa kugeukia vyanzo vingine? Ulijifunza nini kutokana na uzoefu huo?
-
Chini ya Mfalme Hezekia, watu wa Yuda walinusurika maangamizo kwa sababu walifuata ushauri wa Isaya kutoka kwa Bwana. Je! Kufuata manabii wa kisasa kunaweza kukulinda vipi dhidi ya madhara ya kiroho?
-
2 Nefi 19:1–7
Isaya anaongea Kimasiya
Je! Umeshakaa muda mrefu bila kuona jua au kusikia joto lake? Kama hujapata, fikiria kwamba ulipata kivuli juu yako wakati wote, bila kupata mwanga na joto la jua (kama vile kuwa katika chumba chenye giza wakati wote). Isaya alitumia ishara kama hiyo ili kuonyesha hali ya kiroho ya watu ambao wanaishi bila nuru ya Yesu Kristo.
Kuna nchi mbili zilizotajwa katika 2 Nefi 19:1–2. Soma mistari hii, na uweke alama majina ya hizo nchi mbili.
Katika karne nyingi kabla ya wakati wa Isaya kuandika mistari hii , vita vingi vilikuwa vimepiganwa katika jaribio la kudhibiti eneo linalojulikana sasa kama Nchi Takatifu. Wengine waliliita eneo hili “nchi ya kivuli cha mauti” kwa sababu wengi sana walipoteza maisha yao hapo katika mapigano. Wakati wa nyakati za Agano Jipya, Nazareti, Kapenaumu, Naini, na Kana zilikuwa katika maeneo yaliyojulikana rasmi kama nchi za Zabuloni na Naftali. Hii ilikuwa miji ambayo Yesu Kristo alitumia wakati Wake mwingi, akihudumia watu zaidi ya miaka 500 baadaye. Inajulikana siku hizi kama eneo la Galilaya.
Weka alama katika 2 Nefi 19:2 kile Isaya alisema watu wa eneo hili hatimaye wangeona.
Katika kauli ya Isaya kwamba wale ambao “walitembea katika giza” na kuishi katika “nchi ya kivuli cha mauti” walikuwa “wameona nuru kuu” ulikuwa ni unabii kuhusu huduma ya maisha ya duniani ya Yesu Kristo katika sehemu hii ya ulimwengu. Watu ambao waliishi katika eneo la Galilaya walikuwa wanatembea katika giza la kiroho, lakini wakati Yesu Kristo aliishi na kuhuhudumu miongoni mwao, waliona “nuru kuu.”
-
Soma 2 Nefi 19:6–7, na ufikirie ni jina gani la Mwokozi katika mstari wa 6 ambalo lingekuwa na maana sana kwa watu wa Yuda, ukiangalia hali zao. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika jinsi moja au zaidi ya haya majina yanavyoelezea jinsi walivyohisi kumhusu Mwokozi.
2 Nefi 19–20
Isaya anaeleza maangamizo ya waovu katika Ujio wa Pili
Unabii wa Isaya wa maangamizo ya Ashuru ulioandikwa katika 2 Nefi 20, pia ni unabii wa maangamizo ya waovu wakati wa Ujio wa Pili. Unaposoma sura hii, kumbuka kwamba jinsi Hezekia alitumaini katika ushauri wa Isaya kutoka kwa Bwana na akabarikiwa, kama unaweka imani yako katika Bwana, hautakuwa na haja ya kuogopa hukumu ambazo zitakuja juu ya wakazi wa dunia katika wakati unaotangulia Ujio wa Pili.
Ni sentensi gani ilirudiwa katika 2 Nefi 19:12, 17, 21 na 2 Nefi 20:4? Unaweza kutaka kuweka alama haya katika maandiko yako. Andika sentensi katika shajara yako, na uweke mstari chini ya neno hasira na neno mkono. Chini ya neno hasira, andika hukumu, na chini ya neno mkono, andika rehema. Soma sentensi kwa sauti, ukibadilisha maneno hukumu na rehema. ( “Pamoja na hayo yote [hukumu] yake haikugeukia mbali, lakini [rehema] yake imenyoshwa hata sasa.”)
-
Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Je! Sentensi katika zoezi la kujifunza hapo linaeleza vipi jinsi Bwana anavyojibu mataifa, familia, au watu ambao watamkataa Yeye?
-
Je! Unaweza kutumia vipi kweli zifuatazo katika maisha yako? Yesu Kristo ni Mungu wa hukumu na rehema. Rehema yake imeenyooshwa kwa wale wanaotubu na kuweka amri Zake.)
-
-
Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kuhusu wakati ulipokuwa mtiifu kwa amri fulani na kuhisi rehema ya Mungu.
-
Andika yafuatayo katika sehemu ya chini ya kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
Nimejifunza2 Nefi 17–20 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).
Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu: