Seminari
Kitengo cha 29: Siku ya 2, Mormoni 9


Kitengo cha 29: Siku ya 2

Mormoni 9

Utangulizi

Moroni alihitimisha kumbukumbu ya babake kwa kuwaita wale ambao hawaamini katika Yesu Kristo kumgeukia Mungu kupitia toba. Alifundisha kwamba Mungu ni Mungu wa miujiza ambaye habadiliki. Alifundisha pia kwamba miujiza hukoma tu wakati watu wanapowacha kuwa na imani. Aliwahimiza wanadamu wote waombe kwake Baba katika jina la Yesu Kristo ili wapokee vile vitu wanavyohitaji.

Mormoni 9:1–6

Mormoni anawaita wale ambao hawaamini katika Yesu Kristo watubu

Fikiria kile ambacho ungewazia ama kuhisi ikiwa ungeweza kuingia katika uwepo wa Mungu leo. Unafikiria watu waovu wangehisi vipi katika uwepo Wake? Soma Mormoni 9:1–5, na ugundue kwamba Mormoni alieleza kile ambacho hatimaye kingetendeka wakati watu ambao wanachagua kutoamini katika Yesu Kristo hatimaye wanaletwa katika uwepo wa Mungu.

Rais Joseph Fielding Smith alieleza kwamba watu wengi huamini kimakosa kwamba watajisikia vyema katika uwepo wa Mungu hata ikiwa hawajatubu dhambi zao:

Picha
Rais Joseph Fielding Smith

“Hapawezi kuwa na wokovu bila toba. Mtu hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu katika dhambi zake. Lingekuwa jambo lisilosahihi kwa mtu kuja katika uwepo wa Baba na kuishi katika uwepo wa Mungu katika dhambi zake. …

“Ninafikiri kuna watu wengi katika dunia, wengi wao pengine katika Kanisa—angalau baadhi katika Kanisa—walio na dhana kuwa wanaweza kupitia maisha haya wakifanya watakavyo, wakivunja amri za Bwana na hatimaye watakwenda katika uwepo wake. Wanafikiri watatubu, labda katika dunia ya kiroho.

“Wanapaswa wasome maneno haya ya Mormoni: “Mnadhani kwamba mtaishi na Yeye [Kristo] chini ya ufahamu wa makosa yenu? Mnadhani kwamba mgekuwa na furaha kuishi na kile Kiumbe kitakatifu, wakati nafsi zenu zina msukosuko na ufahamu wa makosa kwamba daima mmetusi sheria zake?

“Tazama, ninawaambia kwamba mtakuwa na taabu sana kuishi na Mungu aliye mtakatifu na wa haki, chini ya ufahamu wa uchafu wenu mbele yake, kuliko kuishi na nafsi zilizolaaniwa katika jehanamu. Kwani tazama, wakati mtaletwa kuona uchi wenu mbele ya Mungu, na pia utukufu wa Mungu, na utakatifu wa Yesu Kristo, itawasha ulimi wa moto usiozimika juu yenu” [Mormoni 9:3–5]” (Doctrines of Salvation, comp. Bruce R. McConkie, 3 vols. [1954–56], 2:195–96).

  1. Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Kwa nini unafikiri ni vibaya kungoja kutubu katika maisha haya, ukiamini unaweza kutubu katika maisha yajayo? (Unaweza kuamua utumie kile umejifunza kutoka kwa Mormoni 9:1–5; Alma 12:14; na Alma 34:32–34 katika jibu lako.)

Soma Mormoni 9:6, na utafute kile “wasioamini” lazima wafanye ili kuepuka mateso Moroni alielezea. Zingatia kutia alama maneno katika Mormoni 9:6 ambayo yanaelezea hali ya watu ambao wanamgeukia Mungu na kumwomba msamaha. Kutoka kwa mstari huu tunajifunza: Tukitubu na kumwita Mungu, tutakuwa bila waa tutakapo kuja katika uwepo Wake.Unaweza kuamua uandike kanuni hii katika maandiko yako ama shajara yako ya kujifunza maandiko.

  1. Katika shajara yako ya maandiko, andika sentensi chache kuhusu jinsi unadhani huenda ukahisi katika uwepo wa Mungu ikiwa ungejua ulikuwa umefanywa kuwa msafi na bila waa kupitia Upatanisho wa Mwokozi.

Kupitia toba na kuishi kwa haki, unaweza kujitayarisha kuwa na faraja katika uwepo wa Mungu. Tafakari jambo la muhimu zaidi unalohisi unaweza kufanya sasa ili kujitayarisha kukutana na Mungu.

Mormoni 9:7–20

Moroni atangaza kwamba Mungu hufanya miujiza na kujibu maombi ya wenye haki

Picha
Kristo Akimponya Kipofu

Je, umewahi kushuhudia ama kupokea miujiza? Andika maelezo yako ya neno muujiza:

Tafuta neno muujiza katika Kamusi ya Bibilia ama Mwongozo kwa Maandiko ili kufafanua ama kuongezea kwa maelezo yako. Kwa nini unadhani baadhi ya watu siku hizi hawaamini miujiza?

Kama ilivyoandikwa katika Mormoni 9:7–8, Moroni aliwaandikia watu katika siku za mwisho ambao wangekana kwamba Mungu yu hai, kwamba Yeye hupeana ufunuo, na kwamba Yeye humwaga karama kwa waaminifu. Moroni alifundisha kwa uwezo mkuu kwamba kuna Mungu na kwamba Yeye ni yule yule “jana, leo na milele” (Mormoni 9:9). Anaendelea kufanya miujiza miongoni mwa watu waaminifu katika karne zote. Soma Mormoni 9:9–11, 15–19, na utambue kile Moroni alifundisha kuhusu uhalisi wa Mungu ili aweze kuwasaidia watu kuamini kwamba Mungu bado hufanya miujiza.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kile umejifunza kutoka kwa Mormoni 9:9–11, 15–19 kuhusu asili ya Mungu. Pia andika jibu lako la swali hili: Mistari hii inafundisha nini kuhusu kutaka kwa Mungu na uwezo wa kufanya miujiza katika maisha ya watu siku hizi?

Soma Mormoni 9:20, na utafute sababu kwa nini baadhi ya watu huenda wasipokee miujiza.

Maneno ya Moroni yaliyoandikwa katika Mormoni 9:9–19 yanafundisha kanuni hii: Kwa sababu Mungu habadiliki, Atatoa miujiza kulingana na imani ya watoto Wake. Unaweza kuamua uandike kanuni hii kando ya Mormoni 9:19–20 katika maandiko yako.

Tunaweza kupokea nguvu za kimiujiza za Mungu kwa njia nyingi katika maisha yetu. Baada ya kurejea baadhi ya miujiza kuu iliyoelezwa katika maandiko, Dada Sydney S Reynolds, aliyehudumu katika urais mkuu wa Watoto, alifundisha:

“Ikiwa na umuhimu sawa na hii ‘miujiza mikuu’ ni ile ‘miujiza ya kibinafsi’ midogo inayofundisha kila mmoja wetu kuwa na imani katika Bwana. Hii huja tunapofahamu na kufuata ushawishi wa Roho katika maisha yetu. …

“Nina amini kwamba kila mmoja wetu anaweza kutoa ushahidi kwa miujiza hii midogo. Tunawajua watoto wanaoomba msaada ili kupata kitu kilichopotea na wanakipata. Tunawafahamu vijana wanaopata ujasiri kusimama kama mashahidi wa Mungu na kuhisi Mkono wake wa usaidizi. Tunawafahamu marafiki wanaolipa zaka kutoka kwa pesa zao zote kisha, kupitia mujiza, hujipata wanaweza kulipa karo zao au pesa za kukodi nyumba au kwa jinsi fulani kupata chakula kwa ajili ya familia zao. Tunaweza kushiriki matukio ya maombi yaliyojibiwa na baraka za ukuhani zilizopatiana ujasiri, kuleta faraja au kurejesha siha. Miujiza hii ya kila siku inatujulisha kwa mkono wa Bwana maishani mwetu” (“A God of Miracles,” Ensign, Mei 2001, 12).

  1. Andika katika shajara yako ya maandiko kuhusu tukio ulilokuwa nalo ama moja ambalo unalojua kuhusu linalodhihirisha Mungu bado ni Mungu wa miujiza leo.

Mormoni 9:21–37

Moroni afundisha kuhusu sala na kuhusu lengo la kumbukumbu ya Wanefi.

Picha
msichana akiomba

Je, unaweza kukumbuka wakati ulihisi kwamba Baba wa Mbinguni alikupatia usaidizi uliohitaji kwa sababu ulikuwa umeomba? Soma Mormoni 9:21, na utafute kile Moroni alifundisha kuhusu kuomba kwake Baba wa Mbinguni kwa ajili ya usaidizi.

Soma kauli ifuatayo, na utafute inamaanisha nini kuomba katika jina la Kristo: “Tunaomba katika jina la Kristo wakati mawazo yetu ni mawazo ya Kristo, na matakwa yetu ni matakwa ya Kristo —wakati maneno yake yanapokaa ndani yetu (( Yohana 15:7). Kisha tunaomba vitu ambavyo Mungu anaweza kutupatia. Maombi mengi hubaki bila kujibiwa kwa sababu hayako katika jina la Kristo hata kidogo, na hayawakilishi kwa njia yoyote akili yake, lakini hutokana na uchoyo wa moyo wa binadamu” (Bible Dictionary, “Prayer”).

Zingatia maombi yako kulingana na yale uliyosoma punde. Unaweza kufanya nini ili kuomba kikamilifu zaidi katika jina la Yesu Kristo?

Ili kutoa mfano wa watu walioamini katika Mwokozi na walioweza kufanya miujiza, Moroni alinukuu kile Yesu Kristo aliwafundisha wafuasi Wake Wanefi. Kama ilivyoandikwa katikaMormoni 9:22–25, Mwokozi aliwaamurisha wafuasi Wake waende kote duniani na wahubiri injili, na akaahidi kwamba “ishara [ya ajabu] itafuatana nao ambao huamini” (Mormoni 9:24). Moroni kisha aliendelea mafundisho yake kuhusu sala.

  1. Soma Mormoni 9:27–29, na utambue kile Moroni alifundisha kuhusu jinsi tunapaswa tuombe kwa imani. Andika vitu umetambua katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Kisha andika sentensi chache ukieleza jinsi unaweza kutumia mafundisho haya kuboresha maombi yako mwenyewe.

Unaweza kuamua uandike kanuni ifuatayo katika maandiko yako karibu na Mormoni 9:27: Tukiomba kwa imani kwake Baba wa Mbinguni katika jina la Yesu Kristo, atatupatia baraka zitakazotusaidia kushughulikia uokovu wetu.

Moroni alipohitimisha maneno yake, alielezea wasi wasi kwamba baadhi ya watu katika siku za mwisho wangekataa Kitabu cha Mormoni kwa sababu ya mapungufu ya wale waliokiandika (ona Mormoni 9:30–34). Soma Mormoni 9:35–37, na utafute kile Moroni alitangaza kuhusu madhumuni ya Kitabu cha Mormoni.

Zingatia jinsi kuja kwa Kitabu cha Mormoni ni ushahidi wa ziada kwamba Mungu ni Mungu wa miujiza na kwamba Yeye hujibu maombi.

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimesoma Mormoni 9 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningetaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha