Seminari
Kitengo 3: Siku 2, 1 Nefi 8


Kitengo 3: Siku ya 2

1 Nefi 8

Utangulizi

Katika 1 Nefi 8 tunasoma kuhusu ono la Lehi la mti wa uzima. Alihisi furaha kuu alipokuwa akila tunda la mti, ambalo linaashiria baraka za Upatanisho. Kisha akaonyeshwa baadhi ya makundi ya watu walioitikia kwa njia tofauti tofauti kwa mti na tunda lake. Ili kukusaidia kujiandaa kwa somo hili, unaweza kutaka kuomba au kusoma maneno kwa “Fimbo ya Chuma” (Wimbo, no. 274). Unaposoma kifungu hiki, tafakari jinsi Upatanisho umekuletea furaha kuu na kile unapaswa kufanya sasa na katika siku zijazo ili kupokea baraka zake zote. Fikiria kuhusu vizuizi unavyohitaji kuepukana navyo ili kudai baraka hizi.

1 Nefi 8:1–18

Lehi anakula tunda la mti wa uzima na kualika familia yake kufanya vivyo hivyo.

Fikiria kuhusu nyakati katika maisha yako ulipohisi upendo wa Bwana kwako binafsi. Fikiria jinsi chaguzi unazofanya zinaathiri kuwa kwako kwa karibu na Bwana na uwezo wako wa kuhisi upendo Wake. Unapojifunza 1 Nefi 8, tafuta kile hukufundisha kufanya na kile unapaswa kuepukana nacho ili kusogea karibu na Bwana na kuhisi upendo Wake kwa wingi sana katika maisha yako.

Soma 1 Nefi 8:2, na utambue kile Lehi aliona alipokuwa nyikani. Soma 1 Nefi 8:5–12, ukitafuta kinachoonekana kuwa picha kuu au sehemu kitovu ya ndoto ya Lehi.

Picha
Ndoto ya Lehi ya Mti wa Uzima

Baada ya kutambua picha kuu, orodhesha mengine ya maneno na vishazi ambavyo Lehi alitumia kueleza matunda katika 1 Nefi 8:10–11.

Bwana kila mara hutumia vyombo vya kawaida kama ishara za kutusaidia kuelewa kweli za milele. Ili kukusaidia kutambua kile mti na tunda katika ndoto ya Lehi iliashiria, soma taarifa ifuatayo kutoka kwa Mzee Neal A. Maxwell wa Akidi ya Wale Mitume Kumi na Wawili: “Mti wa uzima ni upendo wa Mungu (ona 1 Nefi 11:25). Upendo wa Mungu kwa watoto Wake unaonyeshwa kwa kina katika kipawa Chake cha Yesu kama Mkombozi wetu: ‘Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee’(Yohana 3:16). Kupata upendo wa Mungu ni kupata Upatanisho na ukombozi wa Yesu [uhuru kutoka kizuizini au dhambi] na shangwe inayopatikana” (“Lessons from Laman and Lemuel,” Ensign, Nov. 1999, 8).

Ili kukusaidia kuelewa kanuni ya injili inayoelezwa katika 1 Nefi 8:10–12, piga mstari chini ya kile Lehi alifanya na tunda katika maandiko yako katika1 Nefi 8:11, na upige mstari chini ya matokeo katika 1 Nefi 8:12. Fikiria kuhusu njia ambazo unaweza “kushiriki” Upatanisho kama vile Lehi “alivyokula” lile tunda.

Uzoefu wa Lehi unaonyesha kwamba kuja kwa Yesu Kristo na kushiriki Upatanisho wake huleta furaha na shangwe.

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Upatanisho wa Mwokozi ulikuletea furaha na shangwe katika maisha yako lini?

Tafakari kwa nini sisi, kama Lehi, tunapaswa kutamani kwamba familia yetu na marafiki wetu wapate baraka za Upatananisho baada ya sisi kupata uzoefu wake. Soma 1 Nefi 8:3–4, 13–18, na utafute jinsi wanafamilia wa Lehi walivyofanya kwa mwaliko wa Lehi wa kushiriki lile tunda la mti wa uzima.

Hatuwezi kuamua ikiwa wengine watachagua kushiriki upendo wa Mungu. Hata hivyo, kama Lehi, tunaweza kuwaalika na kuwahimiza. Fikiria jinsi unaweza kualika na kuhimiza mtu mwengine unayemjua kuja kwa Kristo na kupokea baraka za Upatanisho Wake…

1 Nefi 8:19–35

Lehi anaona ufanisi wa wengine na kushindwa kwa wengine wanaposonga kufikia mti wa uzima na kushiriki lile tunda.

Baadaye katika 1 Nefi hutasoma kuhusu jinsi Nefi alionyeshwa pia ono la mti wa uzima. Aliandika maana ya baadhi ya ishara na picha katika ono hilo Tumia chati ifuatayo ili kutambua ishara na ufafanuzi wake. Pekua maandiko yako ili kukamilisha zoezi ifuatayo. Tayari umesoma na kujifunza ufafanuzi wa ishara mbili za kwanza.

Ishara kutoka katika Ndoto ya Lehi

Ufafanuzi wa Ishara Uliotolewa kwa Nefi

Mti (ona 1 Nefi 8:10; unaitwa mti wa uzima katika 1 Nefi 15:22)

Upendo wa Mungu (ona 1 Nefi 11:25)

Tunda la mti (ona 1 Nefi 8:10–12)

Zawadi kubwa zaidi ya zawadi za Mungu—baraka ya Upatanisho wa Yesu Kristo (ona 1 Nefi 15:36)

Mto wa maji (chafu) (ona 1 Nefi 8:13)

(ona 1 Nefi 12:16; 15:27)

Fimbo ya chuma (ona 1 Nefi 8:19)

(ona 1 Nefi 11:25; 15:23–24)

Ukungu wa giza (ona 1 Nefi 8:23)

(ona 1 Nefi 12:17)

Jengo kubwa na pana (ona 1 Nefi 8:26)

(ona1 Nefi 11:36; 12:18)

Itakuwa muhimu kuweka alama katika maandiko yako kwa kuandika ufafanuzi wa kila ishara (majibu katika safu ya pili ya chati juu) kando ya mstari au mistari ambapo ishara imetajwa (mistari katika safu ya kwanza ya chati)

Unaposoma dondoo ifuatayo kutoka kwa Rais Boyd K. Packer wa Akidi ya Wale Mitume Kumi na Wawili, piga mstari chini ya kile alisema kuhusu kwa nini ni muhimu kwetu kujifunza ndoto ya Lehi:

“Unaweza kufikiria kwamba ndoto ya Lehi au ono halina maana maalumu kwako, lakini linayo. Wewe upo ndani yake; sisi sote tupo ndani yake. …

Ndoto au ono la Lehi lina ndani yake kila kitu ambacho Mtakatifu wa Siku za Mwisho anahitaji kuelewa majaribu ya maisha (Finding Ourselves in Lehi’s Dream, Ensign, Aug. 2010, 22).

Unapojifunza salio la 1 Nefi 8, fikiria jinsi kile unachojifunza kinaweza kukusaidia “kuelewa majaribu ya maisha.” Soma 1 Nefi 8:21–33 ukitafuta jinsi mto, ukungu wa giza, na jengo kubwa na pana lilivyowazuia watu katika ndoto ya Lehi kuweza kula au kufurahia tunda la mti wa uzima. Unaweza kutaka kuweka alama katika maandiko yako maneno muhimu na vishazi vinavyotaja vikwazo hivi na madhara yaliyokuwa nayo kwa watu.

Vikwazo hivi Lehi alivyoviona vinaweza kuwa nini katika maisha yetu leo? Piga mstari chini ya vikwazo vifuatavyo ambavyo umeona vinazuia mtu kuja kwa Mwokozi na kuhisi furaha: ngono, kutafuta utambuzi au sifa ya wengine, uraibu, uchoyo, tamaa, kuwa na wivu kwa wengine, kukosa kuomba na kujifunza maandiko, matumizi mabaya ya burudani ya elektroni, kushiriki kupita kiasi katika shughuli yoyote au michezo, uwongo, na kufuata chochote ambacho mtu mwingine anafanya. Fikiria kuhusu mifano mengine ya siku hizi ya vikwazo hizi.

Kanuni ifuatayo ni njia moja ya kufupisha kile ambacho unaweza kijifunza kutokana na vikwazo katika 1 Nefi 8:21–33: Kiburi, malimwengu, na kuingia katika majaribu kunaweza kukuzuia kupokea baraka za Upatanisho.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika muhtasari ufuatao na hisia zako kuhusu ukweli wake na njia unavyoweza kutumika katika maisha yako.

Tafakari jinsi uchafu wa ulimwengu, majaribu ya Shetani, na kiburi cha ulimwengu unaweza kuzuia au kuchelewesha ukuaji wako wa kiroho.

Pekua 1 Nefi 8:21–33 tena. Wakati huu tafuta majibu kwa maswali yafuatayo:

  • Jinsi gani fimbo ya chuma (neno la Mungu—ambayo inajumuisha maandiko, maneno yenye maongozi ya manabii na viongozi wengine wa Kanisa, na ufunuo wa kibinafsi) ni muhimu kwa wale waliokula lile tunda kwa ufanisi?

  • Ni maneno gani katika 1 Nefi 8:30yanaonyesha kile tunapaswa kufanya ili neno la Mungu lituongoze salama kwenye mti wa uzima?

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko jinsi neno la Mungu linaweza kutuongoza na kutuweka salama kutokana na majaribu.

Mistari hii inafundisha kanuni zifuatazo za injili: Kama tutashikilia kwa nguvu neno la Mungu, litatusaidia sisi kushinda majaribu na ushawishi wa malimwengu. Kushikilia kwa nguvu neno la Mungu, hutusaidia kuwa karibu na Bwana na kupokea baraka za Upatanisho

  1. Ili kukusaidia kuona ushahidi wa kanuni hizi katika maisha yako, jibu moja au yote ya maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni wakati gani neno la Mungu lilikuongoza wewe au lilikusaidia kushinda majaribu, kiburi, au malimwengu?

    2. Ni lini neno la Mungu lilikusaidia kuja karibu na Mwokozi?

Lehi aliwasihi familia yake “kwa huruma zote za mzazi mwenye upendo, kwamba wasikilize maneno yake” (1 Nefi 8:37). Aliwataka kuhisi shangwe na baraka za Upatanisho wa Yesu Kristo kama alivyofanya.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika lengo lako la kuboresha kujifunza kwako kwa neno la Mungu.

Unapofuata na kushikilia kwa nguvu neno la Mungu, unaweza kushinda vikwazo ambavyo vinaweza kukuzuia kushiriki Upatanisho na kupokea shangwe kamili.

  1. Andika yafuatayo mwisho wa kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza1 Nefi 8 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha