Seminari
Yaromu


Utangulizi wa Yaromu

Kwa nini Ujifunze Kitabu Hiki?

Unapojifunza kitabu cha Yaromu, utaona kwamba Mungu anaweka ahadi Yake na kuwabariki wale ambao wanatii amri Zake. Pia utajifunza kuhusu juhudi za wafalme Wanefi, manabii, walimu, na makuhani wa siku za Yaromu za kuwasaidia watu watubu na kuepuka maangamizo.

Nani Aliandika Kitabu Hiki?

Yaromu mwana wa Enoshi ndiye aliandika kitabu hiki. Kama vile baba yake—na kama babu yake Yakobo na babu mkuu Lehi—Yaromu alikuwa na roho ya unabii na ufunuo (ona Yaromu 1:2). Wakati alikamilisha kumbukumbu yake, alikabidhi mabamba madogo ya Nefi kwa mwanawe Omni.

Kiliandikwa Lini na wapi?

Kitabu cha Yaromu kinahusika na takriban miaka 59, kutoka miaka 420 Kabla Kristo hadi miaka 361 Kabla Kristo (ona Enoshi 1:25; Yaromu 1:13). Kiliandikwa katika nchi ya Nefi.