Seminari
Kitengo cha18: Siku ya 2, Alma 30


Kitengo cha 18: Siku ya 2

Alma 30

Utangulizi

Kufuatia vita vya kutisha na Walamani, amani iliingia nchini Zarahemla. Katikati ya kipindi hiki cha amani, mtu aitwaye Korihori alianza kuhubiri kwamba hakutakuwa na Kristo. Mafundisho yake ya uongo yaliwaongoza wale waliomwamini kutenda dhambi. Alizungumza dhidi ya viongozi wa Kanisa, akidai walikuwa wakifundisha “desturi za upuzi” (Alma 30:27). Korihori aliletewa mbele ya Alma, aliyemfundisha ya kwamba mambo yote yanashuhudia Kristo. Hatimaye, Korihori alikiri wazi kwamba matendo yake yaliongozwa na ibilisi.

Alma 30:1–29

Korihori, mpinga Kristo, anayafanyia mzaha mafundisho ya Kristo.

Fikiria kwamba mtu alikutayarishia chakula. Kilionekana na kunukia ladha tamu, lakini ulipokila, ukawa mgonjwa sana. Hebu fikiria kwa muda jinsi mafundisho ya uongo yanaweza kuwa sawa na kupewa chakula kinachoonekana tamu lakini kina sumu kisiri.

Hapo awali mlijifunza kuhusu mpinga Kristo Sheremu (ona Yakobo 7) na Nehori (ona Alma 1). Kumbuka kwamba, maana moja wa mpinga-Kristo ni “mtu yeyote au kitu chochote ambacho kinaiga mpango wa kweli wa injili wa wokovu na ambayo inapinga hadharani au kupinga Kristo faraghani” (Guide to the Scriptures, “Antichrist,” scriptures.lds.org). Leo utajifunza kuhusu mtu mwingine ambaye alikuwa adui wa Kristo na ambaye mafundisho yake ya uongo yaliwadanganya wengine na kuwapeleka kwa dhambi. Wengi katika ulimwengu leo wanatumia ubishi sawa na wa Korihori dhidi ya wale wanaoonyesha imani katika Mungu.

Korihori alianza kuhubiri miongoni mwa Wanefi. Soma Alma 30:6, 12, na uangalie vishazi vinavyoonyesha Korihori alikuwa mpinga Kristo.

Read Alma 30:12–18, na ulinganishe mafundisho ya uongo ya Korihori na matokeo yao.

Baadhi ya Mafundisho ya uongo ya Korihori, Mpinga Kristo

Tafsiri Ziwezekanazo na Matokeo ya Mafundisho ya Uongo

  1. Alma 30:13–14

  1. Isipokuwa uwe na ushahidi wa kuonekana wa kweli za dini, hupaswi kuamini katika Yesu Kristo au injili Yake. Hakuna kitu kama ufunuo wa binafsi kwa njia ya Roho Mtakatifu.

  1. Alma 30:15

  1. Hakuna kitu kama dhambi. Hakuna kiwango ulimwenguni wa kile ambacho ni sahihi au kibaya.

  1. Alma 30:16

  1. Watu hufanikiwa kwa juhudi zao wenyewe, peke yake. Hakuna haja ya Mungu katika mambo ya mtu.

  1. Alma 30:17 (“every man fared …”)

  1. Maneno ya manabii na maandiko si ya kweli, hivyo hupaswi kuamini unabii wao.

  1. Alma 30:17 (“whatsoever a man did …”)

  1. Hakuna kitu kama ondoleo la dhambi. Hakuna haja ya kutafuta msaada kupitia kwa Upatanisho kwa sababu hakuna kitu kama Upatanisho.

  1. Alma 30:18

  1. Hakuna maisha baada ya kifo, hivyo hakuna haja ya kuwa na wasiwasi juu ya hukumu baada ya maisha haya.

(Majibu kwa zoezi hili la kuoanisha yanapatikana mwisho wa somo hili.)

Alma 30:18 inafundisha kanuni: Shetani anatumia mafundisho ya uongo kutushawishi tutende dhambi

Rais Boyd K. Packer, Rais wa Akidi ya Wale Mitume Kumi na Wawili, alifundisha:

Rais Boyd K. Packer

“Tabia yetu haidhibitiwi kabisa na tamaa za kimwili. Tabia huanza na imani pia.

“Imani huzaliwa kutoka kwa falsafa, au mafundisho. Mafundisho yanaweza kuwa ya kiroho au ya kidunia, ya kujenga au haribifu, kweli au uongo. …

“Mafundisho ya kweli, yakieleweka, hubadilisha mitazamo na tabia” (“Little Children,” Ensign, Nov. 1986, 17).

  1. ikoni ya shajaraChagua mafundisho mawili au zaidi ya uongo ya Korihori yaliyotajwa katika chati ya zoezi ya kuoanisha. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika mafundisho ya kweli ni yapi na ueleze jinsi kujua ukweli huathiri mitazamo na tabia yako.

Baada ya mafanikio yake katika nchi ya Zarahemla, Korihori alienda katika nchi ya Yershoni kuhubiria watu wa Amoni. Soma Alma 30:19–20, na utambue kama walikubali mafundisho yake ya uongo.

Watu wa Amoni “walikuwa werevu kuliko wengi wa Wanefi” na “walilazimisha kwamba atolewe nje ya nchi” (Alma 30:20–21). Kutokana na yale ambayo umejifunza kuhusu watu wa Amoni, kwa nini unafikiri hawakuamini mafundisho ya uongo ya Korihori?

Alma 30:21–29 inaelezea jinsi Korihori alienda katika nchi ya Gideoni, “na pale hakufaulu sana” (Alma 30:21). Baadhi ya mabishano ya Korihori dhidi ya Kanisa na mafundisho yake yanapatikana katika Alma 30:24, 27, mawili ambayo ni: (1) wale ambao wanaamini katika Mungu wako katika utumwa na (2) dini huondoa uhuru. Mabishano haya bado yanatumika na wapinzani wa dini leo.

Rais Henry B. Eyring wa Urais wa Kwanza alifundisha kwamba imani yetu katika Mungu hutupa uhuru: “Korihori alisema, kama vile wanaume na wanawake wamebishana visivyo tangu mwanzo wa nyakati, kwamba kuchukua ushauri kutoka kwa watumishi wa Mungu ni kusalimisha haki za uhuru zilizopeanwa na Mungu. Lakini ubishi huo ni wa uongo kwa sababu hauwakilishi ukweli. Tunapokataa ushauri utokao kwa Mungu, hatuchagui kuwa huru kutokana na ushawishi wa nje. Tunachagua ushawishi mwingine. Tunakataa ulinzi wa Baba wa Mbinguni mwenye upendo mkamilifu, mwenye nguvu zote, Mjuzi wa yote, ambaye kusudi lake lote, kama lile la Mwanawe mpendwa, ni kutupatia uzima wa milele, na kutupatia yote aliyonayo, na kutuleta nyumbani tena katika familia kwa mikono ya upendo Wake. Katika kukataa ushauri Wake, tunachagua ushawishi wa nguvu nyingine, ambao lengo lake ni kutuletea huzuni na nia yake ni chuki. Tuna wakala wa kimaadili kama zawadi ya Mungu. Badala ya haki ya kuchagua kuwa huru kwa ushawishi, ni haki isiobadilika kujiwasilisha wenyewe kwa namna yoyote ya zile nguvu tunazochagua (“Finding Safety in Counsel,” Ensign, May 1997, 25).

  1. ikoni ya shajaraAndika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kile ungependekeza mtu afanye ili kujilinda dhidi ya kuamini mafundisho ya uongo kama yale yaliofundishwa na Korihori.

Alma 30:30–60

Korihori anadai ishara kutoka kwa Alma na akawa bubu kwa nguvu ya Mungu.

Hatimaye, Korihori aliletwa mbele ya Alma. Soma Alma 30:30–31, na uangalie shutuma ambazo Korihori alitoa dhidi ya Alma na viongozi wengine wa Kanisa. “Kujishibisha kwa kazi ya watu” ina maana kuwa Alma na wengine walitajirika kwa sababu ya huduma yao ya Kanisa. Fikiria kuhusu majibu ya maswali yafuatayo:

  • Kutokana na uzoefu wako na viongozi wako wa Kanisa, kwa nini shutuma hizi ni za uongo?

  • Unafikiri ungejibu vipi kwa shutuma za Korihori kama ungekuwa Alma?

Soma Alma 30:32–35, na ugundue majibu ya Alma kwa Korihori. Fikiria jinsi umeona ukweli wa majibu ya Alma katika maisha ya wale wanaoongoza kata au tawi lako au ya washiriki wengine wa Kanisa wakupendezao.

Kama inawezekana, alika rafiki au mwanafamilia asome Alma 30:37–45 pamoja nawe. Mmoja wenu asome maneno ya Alma, na mwengine maneno ya Korihori. Wakati wawili wenu mnaposoma, angalia kile Alma alisema kama ushahidi wa uwepo wa Mungu. (Kama haiwezekani kuwa na mtu kusoma na wewe, fikiria mabadilishano yanayoendelea kati ya watu wawili unaposoma.)

  1. ikoni ya shajaraKamilisha kazi zifuatazo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Andika ni gani kati ya uhahidi ambao Alma alitoa ni hasa ushahidi wa maana kwako wa uwepo wa Mungu na ni kwa nini ni ushahidi wenye nguvu vile wa uwepo Wake.

    2. Andika angalau ishara tatu zingine ambazo umeona katika maisha yako ambazo “zinaonyesha kwamba kuna Mungu” (Alma 30:44), na ueleze kwa ufupi jinsi kila moja imeimarisha imani yako katika Mungu.

Fundisho moja linalopatikana katika mistari uliyosoma ni: Vitu vyote vinashuhudia Mungu kama Muumbaji Mkuu. Fikiria kinachofanyika kwa imani yako unapochagua kuangalia kwa na kukumbuka ushahidi na shuhuda hizi.

Tambua yale nabii Alma alifanya alipozungumza na Korihori: alikosoa mafundisho ya uongo (ona Alma 30:32–35), alishuhudia ukweli (ona Alma 30:37–39), alibadilisha jukumu la ushahidi kwa Korihori (ona Alma 30:40–42), na alitoa ushahidi wa uwepo wa Mungu (ona Alma 30:44). Unaweza kujifunza nini kutoka kwa mfano wa Alma kuhusu jinsi ya kukabiliana na wale wanaobishana dhidi ya ukweli?

Mzee Jeffrey R. Holland

Wakati mwingine ulinzi tulionao tu dhidi ya wale wanaoshambulia imani yetu ni kushiriki ushuhuda wetu wa ukweli. Hakuna aibu katika kutumia mbinu hii —Alma, nabii wa Mungu, alitumia mbinu hii kwa Korihori. Kama vile Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alieleza: “Mabishano ya Korihori yanasikika ya kisasa kwa msomaji wa siku hizi, lakini Alma kwa kujibu alitumia silaha ya milele na isiokanika mwishowe —uwezo wa ushuhuda binafsi” (Christ and the New Covenant [1997], 121).

Alma na Korihori

Licha ya ushahidi mwingi, au ishara, ambazo Alma alishiriki pamoja na Korihori ili kuthibitisha kuwepo kwa Mungu, Korihori aliuliza ishara nyingine na alipigwa kuwa bubu (kumaanisha hangeweza kuongea; ona Alma 30:45–50). Soma Alma 30:51–53, angalia ni kwa nini Korihori alisema alifundisha yale aliyoyafanya.

Wakati Korihori hangeweza tena kufundisha mafundisho ya uongo, alikubali kwamba alikuwa akifundisha mafundisho ya uongo “kwa sababu yalikuwa yanapendeza kwa akili ya kimwili” (Alma 30:53). Kuwa na “akili ya kimwili” inamaanisha kuwa na umakini katika raha ya kidunia au kutosheleza tamaa za mwili. Wale ambao walioamini mafundisho ya Korihori walidhani wangeweza kujiingiza katika anasa za kimwili na vitu vya dunia na hakungekuwa na madhara. Mawazo haya yalielekeza kwa maisha ya dhambi (ona Alma 30:18).

Alma 30:54 – 59 inaeleza kwamba Korihori alitupwa nje, akaenda nyumba kwa nyumba akiomba chakula, na hatimaye akakanyagwa chini hadi kufa. Soma Alma 30:60, na uangalie kweli muhimu kuhusu kile hatimaye hutokea kwa wale wanaochagua kufuata Shetani. Weka alama maneno yafuatayo katika maandiko yako: “Ibilisi hatasaidia watoto wake [wafuasi wake] siku ya mwisho.” (Katika mstari huu, watoto humaanisha wafuasi.)

  1. ikoni ya shajaraJibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni kwa jinsi gani ukweli uliyoweka alama katika Alma 30:60ulidhihirishwa katika maisha ya Korihori?

    2. LinganishaAlma 30:60 na Alma 36:3. Ni ushahidi gani umeona katika maisha yako au katika maisha ya wengine ambao unaonyesha kwamba Mungu ataendelea kuunga mkono wale wanaojitahidi kufuata amri Zake?

Reje kanuni na mafundisho ya kweli uliyojifunza leo. Fikiria njia unaweza kuepuka kudanganywa na mafundisho ya uongo, kama vile yale ya Korihori.

  1. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Alma 30 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

  • Majibu ya shughuli ya kuoanisha: (1) D, (2) A, (3) E, (4) C, (5) B, (6) F.