Seminari
Kitengo 24: Siku ya 4, 3 Nefi 11:1–17


Kitengo 24: Siku ya 4

3 Nefi 11:1–17

Utangulizi

Wakati mwingine kufuatia uharibifu mkubwa na siku tatu za giza, wanaume wapatao 2,500, wanawake na watoto walikusanyika kuzunguka hekalu katika nchi ya Neema (ona 3 Nefi 17:25). Walisikia sauti, ambayo kwa mara ya kwanza hawakuelewa. Walipojaribu kusikiliza, walifahamu kwamba ilikuwa ni sauti ya Baba wa Mbinguni akimjulisha Mwanawe, Yesu Kristo. Mwokozi wa dunia akaonekana. Yesu Kristo aliwaalika watu kushuhudia mmoja mmoja kwamba aliuawa kwa sababu ya dhambi za ulimwengu kwa kugusa jeraha ubavuni mwake na alama za misumari katika mikono Yake na miguu.

3 Nefi 11:1–7

Watu wanasikia sauti ya Baba ikitangaza kutokea kwa Mwanawe

Nenda nje na penseli na mwongozo huu wa masomo, na usikilize kwa sekunde 60. Andika chini sauti nyingi uwezavyo katika nafasi iliyotolewa:

Sasa weka nyota karibu na kila sauti ambayo unadhani itakuwa vigumu kutambua au ambayo hautawezeka kutambua bila kujaribu kusikiliza. Kisha rudi ndani.

Muda mfupi baada ya uharibifu mkubwa na giza ukionyesha kifo cha Yesu Kristo, watu walikusanyika katika hekalu, katika nchi ya Neema. Wakati walipokuwa wakijadili kilichotokea, tukio la ajabu likafanyika ambalo wao kwa mara ya kwanza hawakuweza kuelewa. Soma 3 Nefi 11:1–3, na uangalie kile ambacho watu walikuwa na ugumu kuelewa. Unaweza kutaka kuweka alama jinsi sauti ya Mungu ilivyoelezwa na athari ambayo sauti hiyo ilikuwa nayo juu ya wale ambao waliisikia.

Chukua muda kufikiri jinsi namna ya sauti ambayo watu walisikia ni kama vishawishi tunavyopata kutoka kwa Roho Mtakatifu. Ni kweli gani unaweza kujifunza kutoka 3 Nefi 11:1–3 kuhusu jinsi Bwana na Roho Mtakatifu mara nyingi huzungumza nasi? Fundisho moja tunayoona imeonyeshwa katika mstari hizi ni: Roho Mtakatifu mara nyingi husema nasi kwa sauti tulivu na ndogo ambayo tunahisi katika mioyo yetu.

Rais Boyd K. Packer, Rais wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili, alielezea jinsi sauti ya Bwana, kupitia kwa Roho Mtakatifu, inafanya kazi katika akili na moyo yetu:

Picha
Rais Boyd K. Packer

“Labda jambo moja kubwa niliyojifunza kwa kusoma Kitabu cha Mormoni ni kwamba sauti ya Roho huja kama hisia badala ya sauti. Utajifunza, kama nilivyojifunza, ‘kusikiliza’ ile sauti ambayo inahisika badala ya kusikia. 

“Karama ya Roho Mtakatifu itakuongoza na kukulinda na hata kusahihisha matendo yako. Ni sauti ya kiroho ambayo huja akilini kama mawazo au hisia iliyowekwa katika moyo wako” (“Counsel to Youth,” Ensign or Liahona, Nov. 2011, 17–18).

  1. Fikiria juu ya wakati ulipohisi sauti ya Bwana, au vishawishi vya Roho vikiingia akilini mwako au moyo. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kuhusu uzoefu wako na jinsi ilivyokuwa.

Wanefi walisikia sauti mara mbili na wala hawakuielewa. Soma 3 Nefi 11:4–7, na uangalie kile ambacho Wanefi walifanya tofauti mara tatu ili kuelewa sauti. Unafikiri inamaanisha nini kwamba watu “wakafungua masikio yao kuisikiliza” sauti? (3 Nefi 11:5).

Rais Boyd K. Packer alitoa ushauri ufuatao kuhusu kile tunachohitaji kufanya ili kusikiliza na kuelewa sauti ya Bwana kupitia kwa Roho Mtakatifu. Weka mstari chini ya maneno au vishazi vinavyokukusaidia kujua cha kufanya, au cha kuepuka, ili kusikia vyema sauti ya Bwana kupitia kwa Roho Mtakatifu.

“Roho haipati usikivu wetu kwa kupiga kelele. Kamwe haitutingishi kwa mkono mzito. Roho hunong’oneza. Inashawishi kwa upole, kwa kweli, ambapo tukijawa na mawazo, hatuwezi kuihisi kabisa.

“Mara kwa mara, Roho atavutia vilivyo au mara nyingi kiasi ya kutuwezesha kuwa makini; lakini kutokana na uzoefu wangu, mara nyingi, kama hatuwezi kutii hisia tulivu, kama hatuwezi kusikiliza kwa hisia hizo, Roho atajiondoa na kusubiri hadi tutakapokuja kutafuta na kusikiliza, kwa namna yetu na maelezo yetu” (“How Does the Spirit Speak to Us?” New Era, Feb. 2010, 3).

Unaweza kutaka kuandika kanuni ifuatayo katika maandiko yako karibu na 3 Nefi 11:5–6 na katika shajara yako ya kujifunza maandiko yako: Tunapojifunza jinsi ya kusikiliza sauti ya Bwana kupitia kwa Roho Mtakatifu, tutaweza kuelewa mawasiliano Anayotupa.

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni nini inakusaidia kuandaa akili na moyo wako kusikia na kuelewa sauti ya Bwana?

    2. Ni lini umewahi kuelewa mawasiliano kutoka kwa Bwana ambayo unaweza kuwa ulikosa ikiwa haukuwa ukijitahidi kuisikia?

    3. Ni lini uliwahi kupokea ushawishi wa Roho Mtakatifu zaidi ya mara moja kabla ya kuielewa na kuifuata?

3 Nefi 11:8–17

Yesu Kristo anajitokeza na kuwaalika watu kuja mmoja mmoja ili kugusa majeraha Yake.

Picha
Yesu Kristo Anawatokea watu wa Nefi

Jaribu kupiga taswira matukio ya 3 Nefi 11:8–10 unapoyasoma.

  1. Unapofikiria vile ingekuwa kushuhudia kuonekana kwa Yesu Kristo aliyefufuka kwa watu wa Kitabu cha Mormoni, andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko mawazo na hisia ambazo unaweza kuwa ulipitia ikiwa ungekuwa huko.

Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alizungumza kuhusu umuhimu wa kutokea kwa Mwokozi kwa Wanefi:

“Kutokea kule na tangazo hilo lilijumuisha kitovu kikuu, wakati muhimu, katika historia yote ya Kitabu cha Mormoni. Ilikuwa ni udhihirisho na tangazo ambalo lilikuwa limearifu na kuwashawishi kila nabii wa Nefi kwa miaka mia sita iliopita, kutosema chochote juu ya babu zao Waisraeli na Wayaredi kwa maelfu ya miaka kabla ya hapo.

“Kila mtu alikuwa ameongea juu yake, kuimba juu yake, kuota juu yake, na kuomba kwa ujio wake—lakini hapa alikuwepo. Siku za masiku! Mungu ambaye anabadilisha kila usiku wa giza katika mwanga wa asubuhi alikuwa amefika” (Christ and the New Covenant: The Messianic Message of the Book of Mormon [1997], 250–51).

Kumbuka kwamba manusura wa Nefi na Walamani waliobakia hivi karibuni waliona uharibifu wa kutisha siku tatu za giza nene. Soma 3 Nefi 11:10–12,, na uangalie kile ambacho Yesu Kristo alitaka watu kujua juu Yake na juu ya mambo aliyofanya wakati wa huduma Yake ya dunia. Ni taarifa gani kati ya hizi za zi unafikiri itakufariji zaidi kusikia kama ungalikuwa huko? Tafakari ni kwa nini taarifa hiyo ingekuwa na maana sana kwako. Unaweza kutaka kuwekea alama kishazi ambayo ina maana zaidi kwako katika maandiko yako.

Soma 3 Nefi 11:13–15, na uweke alama kile ambacho Yesu Kristo aliwaalika watu kufanya ili kupokea maarifa ya binafsi Aliowataka kupata juu Yake. Fikiria kuhusu majibu ya maswali yafuatayo: Kulingana na 3 Nefi 11:14, ni nini ambacho Mwokozi alitaka watu kujua kutokana na uzoefu huu? Kuzingatia kwamba kulikuwa na watu 2,500 waliokuwepo wakati huo (3 Nefi 17:25), hii ingechukua muda gani? Je, hii inakufundisha nini juu ya Mwokozi?

Picha
Mmoja mmoja
  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, jibu maswali yafuatayo:

    1. Kwa nini unafikiri Bwana alitaka watu kumwona na kumgusa “mmoja mmoja”? (3 Nefi 11:15).

    2. Utaathirika vipi kwa kugusa majeraha ambayo Mwokozi alipata alipokuwa akilipia dhambi zako?

Fikiria kuandika ukweli ufuatao katika maandiko yako karibu na 3 Nefi 11:11–15 au katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Yesu Kristo ananialika kupokea ushuhuda binafsi kwamba Yeye ni Mwokozi wangu.

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni kivipi unahisi ushuhuda wako binafsi wa Mwokozi ni wima? Je, imekua kivipi na kuimarika zaidi kwa siku zilizopita?

    2. Ni matukio gani yamekuongoza kupata ushuhuda wako binafsi wa Mwokozi, au nini unaweza kufanya ili kupata ushuhuda wima?

    3. Unawezaje kujua kwamba Mwokozi anakufahamu binafsi?

Soma 3 Nefi 11:16–17, na uangalie kile ambacho watu walifanya baada ya tukio lao la kibinafsi na Mwokozi. Inaweza kuwa muhimu kuelewa kwamba “Hosana” ni tamko la sifa kwa Bwana.

Angalia kwa karibu 3 Nefi 11:15, na utambue kile watu walifanya baada ya kuhisi binafsi majeraha ya Mwokozi. Kwa kuwa haukuwa huko binafsi kuhisi majeraha ya Mwokozi, kama vile walivyofanya watu walioandikwa katika 3 Nefi, unawezaje kujua kwamba Yesu ni Kristo? (Ona Yohana 20:30–31; Moroni 10:3–7; M&M 46:13–14 kwa uwezekano wa majibu mengine.)

Ili kulinganisha 3 Nefi 11:15 na wewe mwenyewe, kamilisha taarifa ifuatayo: Ninapokea ushuhuda binafsi wa Yesu Kristo, nina wajibu wa.

Fikiria kuhusu njia ambazo mtu mwenye ushuhuda wa Yesu Kristo anaweza “kutoa ushuhuda” Wake.

Rais Boyd K. Packer alifundisha yafuatayo kuhusu ushuhuda: “Huwezi kulazimisha mambo ya kiroho. Ushuhuda haulazimishwi juu yako; inakua. Na ushuhuda ni ushuhuda, na ni lazima iheshimiwe, iwe ni ndogo au kubwa. Tunakuwa wima katika ushuhuda wetu kama vile tunavyokua katika kimo cha kimwili na kutojua kuwa kinatendeka, kwa sababu kinatokana na ukuaji” (“How Does the Spirit Speak to Us?” 3).

  1. Hitimisha somo hili kwa kuandika ushuhuda wako wa Yesu Kristo katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Unaweza kutaka kujumuisha kile ambacho umefanya ili kupata ushuhuda wako au kile ambacho unapanga kufanya ili kuimarisha. Ikiwa umeshawishiwa na Roho, isome kwa mtu mwingine au mwalike mtu kuisoma.

  2. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza3 Nefi 11:1–17 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe)

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha