Seminari
Kitengo cha 5: Siku ya 2, 2 Nefi 1


Kitengo cha 5: Siku ya 2

2 Nefi 1

Utangulizi

Unapojifunza 2 Nefi 1, kumbuka kwamba kina maneno ya mzazi na kiongozi wa ukuhani mwenye upendo ambaye alikuwa karibu na kufa. Baba Lehi aliisihi familia yake itii amri za Mungu (ona 2 Nefi 1:16). Alitoa unabii kwamba kama wangetii amri za Mungu, wangestawi katika nchi ya ahadi. Pia aliwahimiza watoto wake na wale ambao walikuja pamoja nao kutoka Yerusalemu wafuate uongozi wa kinabii wa Nefi. Unapojifunza sura hii, tathimini utiifu wako wa kibinafsi kwa amri za Bwana. Je! Unafuata vipi ushauri wa viongozi wa Kanisa?

2 Nefi 1:1–23

Lehi anawashawishi watu wake kuishi kwa haki

Fikiria kwamba ghafula inakubidi uwache familia yako na hautaiona tena. Una fursa moja ya mwisho ya kuongea nao. Je! Unaweza kuwaambia nini katika hali hii?

Katika 2 Nefi 1–4, Nefi aliandika kumbukumbu ya ushauri wa mwisho wa baba yake kwa familia yake. Unapojifunza sura hizi, fikiria njia ambazo kumbukumbu ya mafundisho ya mwisho ya Lehi yanavyohusiana nawe.

Soma 2 Nefi 1:1–4, na utambue yale “mambo makuu Bwana aliyowafanyia” familia ya Lehi.

  1. ikoni ya shajaraAndika majibu mafupi kwa maswali yafuatayo katika shajara yako ya maandiko:

    1. Ni kwa njia gani Bwana alionyesha huruma kwa familia ya Lehi?

    2. Ni “mambo makuu” gani Bwana amekufanyia wewe na familia yako? Ni hisia gani ulizonazo kwa Bwana unapofikiria kuhusu jinsi Yeye amekuwa na huruma kwako na familia yako?

Lehi alifunza familia yake kwamba kuchagua kushika amri za Mungu kungeamua kama wangeendelea kupokea “mambo makuu” na “neema za Mungu katika maisha yao au la.

  1. ikoni ya shajaraIli kukusaidia kuona kwamba Bwana hutubariki wakati tunashika amri Zake, na Yeye huzuia baraka tusiposhika amri Zake, chora mchoro kama huu uliopo hapa katika shajara yako ya maandiko. Soma 2 Nefi 1:7–11, na utambue vitendo (“kama”) ambavyo Lehi alisema vingeleta matokeo fulani (“basi”). Andika kile unagundua chini ya safu ifaayo ya mchoro katika shajara yako ya kujifunza.

Kama (matendo)

Basi (matokeo)

Lehi akifundisha

Lehi alijali hasa kuhusu hali za kiroho za Lamani na Lemueli na akafahamu kwamba walihitaji kutubu. Alipokuwa anawasihi, alitumia ishara kadhaa kuwasaidia kuelewa dhambi na toba. Pekua 2 Nefi 1:13–14 ishara ambazo Lehi alitumia ili kuwatia moyo wanawe watubu, na uandike majibu yako katika mapengo hapo chini:

kutoka mzito

mjifungue

kutoka

  1. ikoni ya shajaraJibu swali lifutalo katika shajara yako ya maandiko: Je! toba inafanana vipi na kila moja ya vishazi katika zoezi hili?

Soma 2 Nefi 1:15, na uweke alama katika maandiko yako vishazi vitatu ambavyo Lehi alitumia kuelezea baraka ambazo alipokea kwa sababu ya utiifu wake wa amri za Mungu. Linganisha hizi baraka na matokeo hasa katika 2 Nefi 1:17–18, 22 ambayo Lehi alisema yatawapata wale ambao hawashiki amri za Mungu.

Weka alama ushauri wa Lehi katika 2 Nefi 1:23, na utafakari kile unahitaji kufanya katika maisha yako ili “uzinduke” au “ufunguke” au “uinuke” ili uweze kupokea baraka ambazo Lehi alizungumzia katika sura hii.

2 Nefi 1:24–32

Lehi anawashawishi wanawe kufuata uongozi wa kinabii wa Nefi.

Lehi kisha alikumbusha familia yake na wengine juu ya asili ingine ya maelekezo na maongozi waliyokuwa wamebarikiwa nayo ili kuwasaidia kufanya maamuzi ya haki katika maisha yao. Soma 2 Nefi 1:24, na utambue asili hii.

Unaposoma 2 Nefi 1:24–27, tafuta jinsi Lehi alivyowatia moyo watu wake ili wamfuate Nefi. Fikiria kuhusu majibu yako kwa maswali yafuatayo:

  • Ni sifa gani Lehi alisisitiza ambazo zingekusaidia wewe kuwa na imani na Nefi kama kiongozi?

  • Kwa nini wewe ungemwamini kiongozi mwenye sifa hizi?

  • Je! Unawaonaje viongozi wa Kanisa siku hizi wakionyesha sifa kama hizi?

Soma 2 Nefi 1:28–32, na uweke alama katika maandiko yako ahadi ambazo Lehi alitoa kwa wale ambao wangefuata uongozi wa Nefi. Hizi ahadi zinaonyesha kwamba tunapowafuata wale ambao Mungu amewaita kutuongoza, tunabarikiwa na mafanikio ya kiroho na usalama. Tafakari kile viongozi wa Kanisa wamekufundisha hivi majuzi kuhusu jinsi utiifu kwa ushauri wenye maongozi unaweza kukuongoza kwenye mafanikio yako ya kiroho na usalama.

Rais Wilford Woodruff

Soma dondoo ifuatayo ya Rais Wilford Woodruff, na upige mstari chini ya ahadi ambazo yeye alitoa kama sisi tutafuata ushauri wa watumishi wa Bwana: “Mimi natumaini sote tutafuata mkondo uliowekwa chini kwa ajili yetu na watumishi wa Bwana, kwani kama tutafanya hivyo mimi najua kwamba tutakuwa salama katika ulimwengu huu, na tutapata furaha na kuinuliwa katika ulimwengu ujao. Kama sisi ni waaminifu watatuongoza katika njia ya maisha, na kadri tulivyo na imani ya kuamini katika maelekezo yao, katika mafundisho ya Roho Mtakatifu kupitia kwao, tuko daima katika njia salama, na tutakuwa na uhakika wa zawadi yetu” (Teachings of Presidents of the Church: Wilford Woodruff [2004], 199).

  1. ikoni ya shajaraAndika katika shajara yako ya maandiko kwa nini unafikiria kuwa mtiifu kwa amri za Bwana na ushauri wa watumishi Wake ni muhimu kufanya katika maisha yetu yote.

  2. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya chini ya kazi za leo katika shajara yako ya maandiko:

    Nimejifunza 2 Nefi 1 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu: