Kitengo 4: Siku ya 2
1 Nefi 16
Utangulizi
Kuhisi uwezo wa maneno ya Nefi, ndugu zake walijinyenyekeza mbele za Bwana. Familia ilipokuwa ikisafiri nyikani, Bwana aliwapatia Liahona ili kuwaongoza katika safari yao. Familia ilipatwa na shida nyingi walipokuwa wakisafiri, ikijumuisha kulegea kwa upinde na kuvunjika kwa upinde wa Nefi, ambayo ilipunguza upatikanaji wa chakula. Wakati wengi wa familia wakinung’unika kwa ajili ya upungufu huu, Nefi alitengeneza upinde mwengine na kutafuta ushauri wa Bwana kwa pahali pa kuwinda. Kujifunza 1 Nefi 16 kunatoa fursa kwako kutathmini jinsi utakavyofanya kwa ukosoaji na mateso. Kama vile Bwana alivyoongoza familia ya Lehi kupitia shida zao, Yeye atakuongoza kupitia changamoto katika maisha yako ikiwa utamtafuta kwa unyenyekevu na kufuata ushauri Wake.
1 Nefi 16:1–6}
Nefi alijibu kunung’unika kwa ndugu zake
Umewahi kuona mtu mwengine akikosolewa au kukemewa kwa makosa? Huyo mtu alifanyaje?
Lamani na Lemueli walihisi kukemewa na Nefi alipowafundisha kwamba waovu watakataliwa na hawatakubaliwa kushiriki mti wa uzima (ona 1 Nefi 15:36–16:1). Soma 1 Nefi 16:1–2, na upige mstari jinsi Nefi alivyosema watu fulani wanafanya baada ya kusikia kweli wakati wao hawaiishi.
Kishazi “huwakata hadi sehemu zao za ndani” inamaanisha kwamba inaanika wazi uovu wao. Unafikiria “wenye hatia huchukua ukweli kuwa mgumu” inamaanisha nini? a
-
Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, orodhesha vitu vichache unavyoweza kufanya ili kuwa mtiifu hata kama ukweli ni mgumu kusikia na “inakukata hadi sehemu za ndani” (1 Nefi 16:2). Kwa nini unafikiri vijana wengine huipata kuwa vigumu kuwa mtiifu kwa kweli fulani? Linganisha orodha yako kwa kile Nefi alimweleza Lamani na Lemueli katika 1 Nefi 16:3–4.
Kulingana na 1 Nefi 16:5, Lamani na Lemueli walijibu vipi maelekezo ya Nefi? Ni neno au kishazi gani katika mstari huu inaeleza kile tunapaswa kufanya wakati ukweli unatukata hadi sehemu za ndani? Weka alama kwenye swali hizi katika maadiko yako.
1 Nefi 16:7–33
Familia ya Lehi inaongozwa kupitia kwa Liahona
Jibu taarifa zifuatazo kama ni kweli (K) au sikweli (S) katika zoezi hili kwa kuweka mviringo majibu yako:
-
Nefi alioa binti mkuu wa Ishmaeli
-
Lehi alipewa mpira unaofanana kama dira iitwayo Liahona
-
Mpira wa duara ulikuwa na vipini vinne vilivyopeana maelekezo kwa Lehi na familia yake.
-
Baada ya familia ya Lehi kupokea mpira, safari ya nyikani ikawa rahisi.
Unapojifunza 1 Nefi 16:7–10 na muhtasari wa kifungu, rejea majibu yako kwa maswali matatu ya kwanza (ona pia Alma 37:38). Soma 1 Nefi 16:17–19 ili kutambua ikiwa umejibu swali la nne ipasavyo. (Maswalisahihi yanapatikana mwisho mwa somo hili.)
Hata kama sisi ni watiifu, bado tunapitia majaribio. Mengi ya majaribio tunayopitia sio matokeo ya kufanya chaguzi mbaya. Bali, zinatujia kama matokeo asili ya maisha ya dunia, lakini zinatupatia fursa ya kujifunza na kukua wakati wa maisha yetu ya dunia, kama vile Mwokozi alivyofanya (ona M&M 122:7–8). Mojawapo wa majaribio yetu ni jinsi tunavyojibu kwa majaribio haya.
Kulingana na maelezo ya Nefi ya mpira katika 1 Nefi 16:10, ni kwa njia gani zawadi kama hiyo ingekuwa usaidizi kwa Lehi na familia yake waliposafiri katika nchi ya ahadi? Tafuta na uweke alama jinsi Liahona ilivyo isaidia familia ya Lehi katika 1 Nefi 16:16.
Tafuta1 Nefi 16:20–22, na utambue jinsi baadhi ya familia ya Lehi walifanya kuhusu kuvunjika kwa upinde wa Nefi. Soma 1 Nefi 16:23–25, 30–32, ukitafuta majibu ya Nefi kwa haya majaribu. Jinsi gani majibu yake yaliathiri familia yake?
-
Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Umejifunza nini kwa kulinganisha majibu tofauti ya Nefi na familia yake kwa majaribu sawa?
Badala ya kulalamika, Nefi alitengeneza upinde mpya na kisha kutafuta mwongozo ili kujua mahali pa kupata chakula. Mfano wa Nefi unadhihirisha kwamba kama tutafanya yote tuwezayo na kutafuta maelekezo ya Bwana, basi Yeye atatusaidia sisi kupitia shida zetu.
Katika matukio haya, Bwana alielezea Lehi jinsi Liahona inavyofanya kazi. Katika 1 Nefi 16:26–29, tafuta kile kilichohitajika ili Bwana aweze kuongoza familia ya Lehi kupitia kwa Liahona.
-
Fikiria kuwa unafundisha mtoto mdogo kuhusu Liahona. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, elezea kwa maneno rahisi jinsi Liahona ilivyoongoza familia ya Lehi na kile iliwabidi kufanya ili iweze kuendelea kuwaongoza.
-
Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maadiko: Ni kwa njia gani Liahona inatuonyesha kwamba “kwa vitu vidogo, Bwana anaweza kuleta mambo makubwa.” ? {(1 Nefi 16:29).
Kama watu wa Lehi, Bwana amewapatia ninyi vipawa vingi vya kuwasaidia ninyi kuokea usaidizi wa kibinafsi. Soma taarifa tatu zifuatazo kuhusu baadhi ya vipawa hivi, na utafakari jinsi kila moja ya vipawa hivi kutoka kwa Bwana vinafanana na Liahona.
Baraka za Patriaki
Rais Thomas S. Monson alieleza baraka za kipatriaki kama Liahona ya kibinafsi:
“Bwana yule yule ambaye alitoa Liahona kwa Lehi hutoa kwako na kwangu kipawa nadra na cha thamani kutupatia maelekezo ya maisha yetu, na kuweka alama hatari kwa usalama wetu, na kupanga njia, hata mapito salama—sio tu hadi nchi ya ahadi, lakini hadi kwenye nyumba yetu ya mbinguni. Kipawa ambacho nimesema kinajulikana kama baraka yako ya baba mkuu. Kila mshiriki mstahiki wa Kanisa ana haki ya kupokea hazina ya thamani kuu na tunu. …
Baraka zako hazifai kukunjwa kimaridadi na kuwekwa kando. Hazifai kuwekwa kwenye fremu au kuchapishwa. Bali, inafaa kusomwa. Inafaa kupendwa. Inafaa kufuatwa. Baraka zako za baba mkuu zitakuwezesha kupitia katika usiku wa giza. Zitakuelekeza wewe kupitia hatari za maisha. … Baraka zako za kipatriaki ni Liahona ya kibinafsi kwako ya kupanga njia yako na kuongoza njia yako” (“Your Patriarchal Blessing: A Liahona of Light,” Ensign, Nov. 1986, 65–66).
Maandiko na Maneno ya Manabii wa Siku za Mwisho
Mzee W. Rolfe Kerr, ambaye alikuwa akihudumu kama mshiriki wa Wale Sabini, alithibitisha kuwa maneno ya Kristo na watumishi Wake ni Liahona ya kibinafsi: “Maneno ya Kristo yanaweza kuwa Liahona ya kibinafsi kwa kila mmoja wenu, yakituonyesha njia. Acha tusiwe wazembe kwa sababu ya urahisi wa njia Acha sisi kwa imani tuchukue maneno ya Kristo katika akili zetu na katika mioyo yetu kama yalivyoandikwa katika maandiko matakatifu na yanavyotamkwa na manabii hai, waonaji, na wafunuaji. Acha sisi kwa imani na bidii kusherekea juu ya maneno ya Kristo, kwani maneno ya Kristo yatakuwa Liahona ya kiroho kutueleza sisi vitu vyote ambavyo tunapaswa kufanya” (“The Words of Christ—Our Spiritual Liahona,” Ensign or Liahona, May 2004, 37).
Roho Mtakatifu
Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alilinganisha Roho Mtakatifu na Liahona: “Tunapojaribu kuwianisha mitazamo yao na matendo katika utakatifu, basi Roho Mtakatifu hufanyika kwetu leo kile Liahona ilikuwa kwa Lehi na familia yake katika siku yao. Mambo hayo hayo ambayo yalisababisha Liahona kufanya kazi kwa Lehi vile vile hualika Roho Mtakatifu katika maisha yetu. Na mambo hayo hayo ambayo yalisababisha Liahona isifanye kazi wakati wa kale vivyo hivyo yatatufanya sisi kujiondoa wenyewe kutoka kwa Roho Mtakatifu leo” (“That We May Always Have His Spirit to Be with Us,” Ensign or Liahona, May 2006, 30).
-
Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko njia moja au tatu ambayo kwayo baraka za baba, maandiko na maneno ya manabii, au Roho Mtakatifu ni kama Liahona.
-
Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, elezea wakati ambapo kufuata mwongozo kutoka kwa vyanzo vilivyoorodheshwa hapo juu viliongoza kupokea kwako mwongozo kutoka kwa Bwana?
1 Nefi 16:34–39
Mabinti wa Ishmaeli wanahuzunika kwa kifo chake, na Lamani anapanga kuwaua Lehi na Nefi
Katika 1 Nefi 16:34–38 tunajifunza kwamba Ishmaeli alikufa baada ya kusafiri siku nyingi nyikani. Mabinti zake walihuzunika kwa kifo cha baba yao kupita kiasi, na wengine wa familia yake walinung’unika dhidi ya Lehi na Nefi na walitaka kurudi Yerusalemu. Lamani pia alipanga njama ya kuwaua Nefi na Lehi. Mara nyingine tena ndugu za Nefi walionyesha udhaifu wao na ukosaji wa imani kwa sababu hawakutafuta mapenzi ya Bwana. Walikataa Roho Mtakatifu na usaidizi ambao Yeye angewapatia.
Soma 1 Nefi 16:39, na utambue kile Bwana alifanya katika hali hii. Kutoka kwa kile ulijifunza katika kifungu hiki, kwa nini Bwana huturudi?
Bwana hutuongoza na kuturudi kwa manufaa yetu wenyewe. Tukitenda kulingana na mwongozo au kukemewa tunakopokea kutoka kwa Bwana, Yeye atatubariki.
-
Andika yafuatayo mwisho wa kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
Nimejifunza 1 Nefi 16 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).
Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: