Kitengo cha 10: Siku ya 1
Yakobo 5–6
Utangulizi
Yakobo 5kina istiara ya miti ya mizeituni shamba na mwitu, ambayo mwanzo ilitolewa na nabii aliyeitwa Zeno. Yakobo alitumia istairi hii kufundisha kwamba Bwana daima anafanya kazi kuuleta wokovu kwa watu wa wake wa agano , hata wakati wanapogeuka kutoka Kwake. Istairi hii inaonyesha kwamba Bwana alitawanya sehemu ya nyumba ya Israeli—watu Wake wa agano—kote ulimwenguni na kwamba Yeye atawakusanya watu Wake katika siku za mwisho. Istairi hii ina matumizi mahususi na ya kibinafsi kwetu leo kama washiriki wa nyumba ya Israeli na watumishi wa Bwana. Katika Yakobo 6, Yakobo alisisitizia rehema ya Mungu na haki alipokuwa akiwahimiza watu wake—na sisi—tutubu.
Yakobo 5:1–12
Yakobo anamnukuu Zeno, ambaye alifananisha nyumba ya Israeli na mti wa mzeituni shamba.
Unamjua rafiki au mtu unayempenda ambaye ametilia shaka upendo wa Mungu kwake, hasa wakati wa majaribio wakati mtu huyu anaweza kuwa amegeuka kutoka Kwake? Fikiria mifano ifuatayo:
-
Kijana wenye ukuhani anaanza tabia ya dhambi. Anaamini kwamba wengine wanaweza kusamehewa, lakini anashaka Bwana atakubali toba yake.
-
Msichana anavunja amri. Anahisi hatia, anajihisi vibaya kuhusu yeye mwenyewe, na anatilia shaka ikiwa Bwana bado anampenda.
Yakobo alitoa unabii kwamba Wayahudi wanangemkataa Yesu Kristo (ona Yakobo 4:15). Pia alitabiri kwamba Yesu Kristo angeendelea kufanya kazi kwa wokovu wa watu Wake hata baada ya wao kumkataa Yeye. Ili kuonyesha ukweli huu, Yakobo alinukuu istairi iliyotolewa na nabii aliyeitwa Zeno (ona Yakobo 5:1). Istiara, kama fumbo, ni hadithi ambayo hutumia wahusika,vyombo, na matendo ya kiishara ili kufunza kweli. Unapojifunza Yakobo 5, fikiria jinsi Bwana daima anakufikia wewe hata wakati umetenda dhambi.
Soma Yakobo 5:2, na uweke alama katika maandiko yako ni kina nani Zeno alielekeza mafundisho haya kwao.
Kwa sababu wewe umeshafanya maagano na Bwana kupitia ubatizo, wewe ni mshiriki wa nyumba ya Israeli. Wewe ni sehemu ya hadithi iliyosimuliwa katika Yakobo 5, Soma Yakobo 5:3, na uweke alama kile Zeno alitumia katika istairi yake kuwakilisha nyumba ya Israeli. Pia weka alama kile kilianza kutendeka kwa mti wa mzeituni shamba.
Kumbuka kwamba tanbihi d katika Yakobo 5:3 inaoyesha kwamba kuoza kwa mti kunaashiria ukengeufu. Ukengeufu hutokea wakati watu au makundi ya watu wanangeuka kutoka kwa Bwana na injili Yake.
Chati ifuatayo inaorodhesha ishara ambazo zinatusaidia sisi kuelewa maana ya istairi ya Zeno. Pia zilizoorodheshwa ni aya ambapo hizi ishara zinatokeza kwanza. Weka alama ishara hizi katika maandiko yako. Unaweza pia kutaka kuandika maana ya baadhi ya hizi ishara pembezoni mwa maandiko yako.
Yakobo 5: Istairi ya Miti ya Mizeituni Shamba na Mwitu | |
---|---|
Ishara |
Maana |
Mti wa mzeituni (aya ya 3) |
Nyumba ya Israeli, watu wa agano wa Mungu |
Shamba la mizabibu (aya ya 3) |
Ulimwengu |
Kuoza (aya ya 3) |
Dhambi na ukengeufu |
Bwana wa shamba la mizabibu (aya ya 4) |
Yesu Kristo |
Kuupogoa, kuupaililia, na kuulisha (aya ya 4) |
Juhudi za Bwana za kutusaidia sisi kuwa wenye haki na kuzaa kazi nzuri |
Matawi (aya ya 6) |
Makundi ya watu |
Mchekele (aya ya 7) |
Watu wa mataifa— wale ambao hawajafanya maagano na Bwana. Baadaye katika istairi hii, miti ya mizeituni asili, inawasilisha sehemu ya nyumba ya Israeli katika ukengeufu , pia inaelezea kama “mchekele” |
Kugoboa na kupandikiza matawi (aya ya 7–8) |
Kutawanywa na kukusanywa kwa watu wa agano wa Bwana. Kwa ziada, kupandikiza matawi ya michekele kwenye mizeituni inaashiria uongofu wa watu wa Mataifa ambao wamekuwa sehemu ya watu wa agano wa Bwana kupitia ubatizo. |
Kuchoma matawi (aya ya 7) |
Hukumu ya Mungu juu ya waovu |
Tunda (aya ya 8) |
Maisha na kazi za watu |
Mizizi ya mzeituni (aya ya 11) |
Maagano ambayo Bwana hufanya na wale wanaomfuata Yeye. Mizizi inaweza pia kuwakilisha watu ambao Bwana alifanya maagano nao hapo kale, kama vile Ibrahimu, Isaka, na Yakobo (ona Yakobo 6:4). |
Soma Yakobo 5:4–6, na uweke alama kile Bwana wa shamba la mizabibu alifanya kwanza kuokoa mzeituni shamba. Angalia chati iliyopo juu, na utambue Bwana wa shamba la mizabibu ni nani na matendo Yake ya kupogoa, kupalilia, na kulisha yanawakilisha nini.
Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alielezea kile istairi ilidhamiriwa kuwa. Unaposoma maelezo yake, weka alama kile yeye anafunza ni cha maana ya kina ya istairi hii.
Istairi hii kama ilivyosimuliwa na Yakobo kutoka mwanzoni inadhamiriwa kuhusu Kristo (Bwana wa shamba la Mizabibu]. …
“Hata kama Bwana wa shamba la mizabibu na watumishi wake wanajitahidi kushikilia, kupogoa, kusafisha, na vingine kuifanya miti yao ipate kuzaa inakuwa sura moja ya kihistoria fupi ya kutawanyika na kukusanywa kwa Israeli, maana ya kina ya Upatanisho unavyohimili na kusaidia kazi zao” (Christ and the New Covenant: The Messianic Message of the Book of Mormon [1997], 165).
Hali Yakobo 5 huonekana kuwa kuhusu miti ya mizeituni, istairi hii ni kuhusu watu ambao waligeuka kutoka kwa Bwana katika dhambi na juhudi za Bwana za kuwasaidia wao kurudi Kwake. Sura hii hufunza kwamba Bwana anatupenda sisi na hufanya kazi kwa bidii kwa ajili wokovu wetu. Unapoendelea kujifunza istiara hii, tafuta ushahidi wa ukweli huu kwa kuzingatia kwa makini hisia za Bwana kwa Israeli—mti wa mzeituni shamba—na juhudi Zake zisizokoma za kuwaokoa. Kwa mfano, soma Yakobo 5:7, na utafakari juu ya kishazi “Inanihuzunisha kwamba nitaupoteza mti huu.” Ni mhemuko gani unafikiria Bwana alionyesha hapa, na kwa nini?
Soma kishazi hiki tena, na wakati huu tia jina lako katika mahali pa “mti huu”: “Inanihuzunisha kwamba nimpoteze [jina lako].” Kwa kutia jina lako kote Yakobo 5 katika sehemu ambazo zina maana na zinazofaa, utaweza kuhusisha istairi hii na wewe mwenyewe na kujifunza zaidi kuhusu Bwana anavyokujali .
Soma Yakobo 5:7–11, na utafute kile Bwana wa shamba la mzabibu alifanya baada ya hapo kuokoa mzeituni.
-
Ukitumia maana ya ishara kwenye chati, andika maelezo katika shajara yako ya kujifunza maandiko juu ya kile Bwana wa shamba la mzabibu na watumishi Wake wanafanya katika Yakobo 5:7–11 kujaribu na kuwaokoa watoto wa Baba wa Mbinguni.
Bwana anachukua watu ambao si wa nyumba ya Israeli na kuwapandikiza wao katika Israeli, kuwafanya wao sehemu ya watu Wake wa agano. Ili kuokoa nyumba ya Israeli, Yeye atapogoa matawi yaliyo maovu sana (watu) na kuwaangamiza wao.
Soma Yakobo 5:13–14, na utafute kile Bwana alifanya na matawi machanga na nyororo kutoka kwa mti wa mzeituni uliotajwa katika aya ya 6. Unaweza kutaka kuandika pembezoni mwako kwamba chini sana humaanisha duni au kisichoonekana vizuri
-
Ukitumia maana ya ishara zilizopo kwenye chati, elezea katika shajara yako ya kujifunza maandiko jinsi familia ya Lehi inaweza kulinganishwa na tawi changa na ororo ambalo lilifichika katika sehemu za chini sana za shamba la mizabibu.
Rais Joseph Fielding Smith alielezea kwamba watumishi wa Bwana “walitwaa baadhi ya matawi na kuyapandikiza katika michekele yote. Ni kina ndiyo michekele? Watu wa mataifa. Na hivyo Bwana alituma watumishi wake katika sehemu zote za shamba la mizabibu, ambayo ni ulimwengu, na kupanda haya matawi ya mti. …
“Sasa katika mithali ile mti wa mzeituni ni Nyumba ya Israeli. Ni katika nchi ya asili ulianza kufa. Kwa hivyo Bwana alichukua matawi kama vile Wanefi, kama vile makabila yaliyopotea, na kama wengine ambao Bwana aliwaongoza ambao hatujui chochote kuwahusu, kwenye sehemu zingine za ulimwengu. Yeye aliwapanda wote kote katika shamba lake la mizabibu, ambalo ni ulimwengu. Hamna shaka alituma baadhi ya matawi haya hadi Japani, Korea, China. Hamna mjadala kuhusu hili, kwa sababu aliwatuma sehemu zote za ulimwengu” (Answers to Gospel Questions, comp. Joseph Fielding Smith Jr., 5 vols. [1957–66], 4:204–5).
Rais Smith pia alifunza kwamba “ufafanuzi wa mithali hii ni hadithi ya kutawanywa kwa Israeli na kuchanganyika kwa damu ya Israeli na miti ya michekele, au watu wa Mataifa, katika sehemu zote ulimwengu. Kwa hivyo tunapata katika China, Japani, India, na katika nchi zingine zote ambazo zilikuwa makazi ya Mataifa ambako damu ya Israeli ilitawanywa, au ‘kupandikizwa,’ miongoni mwao”(Answers to Gospel Questions, 4:40–41).
Yakobo 5:15–77
Bwana wa shamba la mzabibu na watumishi wake wanafanya kazi kusaidia shamba la mzabibu kuzaa tunda nzuri
Nyingi za aya hizi Yakobo 5 zinaeleza vipindi tofauti na matukio kuhusu sehemu tofauti za nyumba ya Israeli kutawanywa kote ulimwenguni na kazi ya Mwokozi ya kuwakusanya wao. Sura inaishia na Milenia na kutakaswa kwa ulimwengu kwa mwisho.
Kusisita kujali kwa Bwana kwa miti ya shamba Lake la mzabibu na juhudi Zake zinazoendelea za kuwaokoa, Zeno alirudia vishazi vichache muhimu kupitia istairi yake. Soma Yakobo 5:20, 23–25, 28, 31, na uweke alama kila wakati Bwana alitaja juhudi Zake za kushamirisha miti ya shamba Lake la mzabibu.
Licha ya juhudi za Bwana na watumishi Wake za kusaidia shamba la mzabibu kuzalisha tunda nzuri, hatimaye matunda yote ya shamba la mzabibu yakaharibika (ona Yakobo 5:39). Soma Yakobo 5:41–42, 46–47, na uweke alama vishazi katika maandiko yako ambavyo vinaonyesha upendo wa Bwana, wasi wasi, au huzuni juu ya shamba Lake la mzabibu.
Kwa sababu miti ilikuwa inazaa matunda mabaya licha ya yote Yeye aliyofanya, Bwana wa shamba la mzabibu alifikiria kuikatia chini miti yote (ona Yakobo 5:49). Soma Yakobo 5:50–51. Salio la Yakobo 5 linawakilisha juhudi za Bwana na watumishi Wake za kuokoa wale wanaoishi katika siku za mwisho. Anawakusanya watu wake na kuwalisha wao kwa mara ya mwisho (ona Yakobo 5:52–77).
Rais Joseph Fielding Smith alifunza kwamba kukusanyika kwa Israeli kulikoelezwa katika Yakobo 5 kunafanyika sasa: “Katika siku hii ya kukusanyika Bwana anatimiza madhumuni yake na kuwaita warudi katika zizi la Mchungaji wa Kweli, watoto wa Ibrahimu” (Answers to Gospel Questions, 4:41).
-
Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kile umejifunza kutoka kwa Yakobo 5 kuhusu upendo wa Bwana kwako. Andika mfano wa jinsi umeona upendo Wake ulivyodhihirishwa katika maisha yako au katika maisha ya mtu unayemjua.
Yakobo 6
Yakobo anafunza juu ya rehema na haki ya Bwana na kutualika sisi tutubu
Yakobo 6 ina muhtasari wa Yakobo wa kweli muhimu kutoka kwa istiara ya miti ya mizeituni. Soma Yakobo 6:4–6, na utafute kile Yakobo alisisitiza kuhusu silka ya Mungu. Ni neno gani unaweza kutumia kufanya muhtasari kile Yakobo alikuwa anataka tujifunze kuhusu Mungu?
Yakobo anahitimisha ujumbe wake katika Yakobo 6:7–13 kwa kushuhudia kwamba tutakuwa wenye hekima kujitayarishia kwa ajili hukumu sasa kwa kutubu na kupokea rehema ya Bwana.
-
Rejelea Yakobo 6:5. Tazama vile Yakobo alituhimiza sisi “mjishikilie kwa Mungu kama vile anavyowashikilia.” Kushikilia humaanisha kugandama au simama imara. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Ulijifunza nini kutoka kwa istairi ya miti ya mizeituni ambacho kinaonyesha jinsi Mungu anavyokushikilia au kusimama imara nawe.
-
Unaweza kufanya nini ili kumshikilia Yeye kwa uthabiti kama Yeye anavyokushikilia wewe?
-
-
Andika yafuatayo mwisho wa kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
NimejifunzaYakobo 5–6 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).
Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu: