Seminari
Kitengo cha 31: Siku ya 2, Moroni 1–5


Kitengo cha 31: Siku ya 2

Moroni 1–5

Utangulizi

Baada ya kukamilisha ufupisho wa mabamba ya Etheri, Moroni alieleza kwamba “sikudhani kama ningeandika zaidi” (Moroni 1:1). Hata hivyo, alihifadhiwa ili “aandike vitu vichache zaidi, kwamba vingekuwa vya manufaa kwa ndugu zangu” kwa wale katika siku za mwisho (Moroni 1:4). Moroni 1–5 inadhibitisha uaminifu wa Moroni kwake Yesu Kristo. Inatoa pia maelezo ya maagizo muhimu ya injili, ikiwa ni pamoja na uhudumiaji wa sakramenti.

Moroni 1

Moroni anatangatanga kwa ajili ya usalama wa maisha yake na kuendelea na maandishi yake.

Mzee David E. Sorenson, mshiriki mstaafu wa Wale Sabini, alisimulia hadithi ifuatayo kuhusu msichana mdogo aliyekuwa na ujasiri wa kusimama kwa ajili ya imani yake:

“Mjukuu wangu wa kike Jennifer alialikwa kwenda na baadhi ya marafiki zake wa shule kwa chakula cha jioni na sinema. Wasichana wote walikubaliana na sinema ambayo walikuwa wanaenda kutazama, na Jennifer alijisikia sawa kuhudhuria. Hata hivyo, msichana aliyeondoka walipokuwa wanakula ili kununua tikiti za sinema za kundi alirudi na tikiti za sinema tofauti na ile iliyopangiwa! Alisema, “Ni sinema mzuri, na ina kikwazo kwa watu wenye umri mdogo.”

“Jennifer, akiwa amegutushwa, hangeamini hali ilikuwa imebadilika haraka hivyo. Lakini kwa bahati mzuri alikuwa ameamua hapo awali kabla ajipate katika hali hii kwamba hatatazama sinema zilizo na kikwazo kwa watu wenye umri mdogo. Aliweza kusimama imara na kuwaambia marafiki zake, “Siwezi kuenda kutazama sinema yenye kikwazo kwa watu wenye umri mdogo. Wazazi wanagu hawangeidhinisha.” Ambapo wasichana walijibu, “Ah, wacha nawe! Wazazi wako hawatajua kamwe!” Akiwa amekumbana na haya, Jennifer aliendelea na kusema, ‘Vizuri, kwa kweli haijalishi kama wazazi wangu watajua. Huwa tu siendi kwa sinema zilizo na kikwazo kwa watu wa umri mdogo!’

“Marafiki zake walikasirika na kujaribu kumfanya atulie na kukubali. Walimwambia alikuwa ‘anaharibu kila kitu.’ Wakati hakukubali, walitupa tikiti na pesa iliyobaki usoni mwake na kumwacha wakienda kwa sinema ile yenye kikwazo. Ilitimia kuwa usiku wa upweke uliojaa kukataliwa kutoka kwa marafiki zake. Lakini ilikuwa wakati mwema kwa Jennifer na familia yetu. Alipata kujiamini, kujithamini, na nguvu ya kiroho” (“You Can’t Pet a Rattlesnake,” Ensign, Mei 2001, 42).

Soma Moroni 1:1–3, na utafute jinsi Moroni alisimama peke yake kwa ajili ya imani yake. Moroni na mjukuuye Mzee Sorensen wote wanatoa mfano wa njia ambazo watu binafsi wanaweza kuchagua kusimama kwa kile ambacho wanajua ni kweli. Wewe pia unaweza kufanya chaguo zinzoonekana kuwa ndogo kila siku ambazo zinaoonyesha imani, utiifu, na nia ya kumfuata Kristo.

  1. ikoni ya shajaraAndika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kuhusu wakati ambapo ulichagua kusimama kwa ajili ya imani yako ama kuonyesha imani yako kupitia utiifu.

Fikiria kuhusu jinsi unaweza kusimama vyema zaidi kwa ajili ya imani yako katika Yesu Kristo. Soma Moroni 1:4 ili kugundua ni kwa nini Moroni alichagua kuandika zaidi, Tunaweza kujifunza nini kutoka kwa mfano wa Moroni na motisha ya kuandika zaidi kwa vizazi vya wale wanaosaka maisha yake? Nini huenda ukaandikia vizazi vyako mwenyewe ambacho huenda ikawa baraka kwao? Unaposoma Moroni 2–5, zingatia jinsi vitu ambavyo Moroni alichagua kuandika kuhusu “vinamanufaa” kwako (Moroni 1:4).

Moroni 2

Moroni aandika maelekezo juu ya kupewa karama ya Roho Mtakatifu

Fikiria kuhusu yale uliopitia ulipodhibitishwa mshiriki wa Kanisa na mikono kuwekwa kichwani mwako ili uweze kupokea karama ya Roho Mtakatifu. Unakumbuka nini kuhusu agizo hili? Soma Moroni 2:1–3, na uzingatie jinsi karama ya Roho Mtakatifu imekuwa baraka katika maisha yako.

Ukweli moja ya injili uliofundishwa katika mistari hii ni huu: Waumini wastahiki wenye mamlaka ya ukuhani yanayostahili wanaweza kuwapa karama ya Roho Mtakatifu waumini waliobatizwa kwa kuwawekea mikono.

Moroni 3

Moroni anaandika maelekezo juu ya kuwatawaza watu binafsi kwenye ofisi za ukuhani

Je, umewahi kuona kumbukumbu ya mtiririko wa mamlaka ya ukuhani ya mtu? Kumbukumbu hii huonyesha aliyemtawaza mtu kwenye ukuhani na aliyemtawaza mtu yule na vivyo hivyo hadi kwake Yesu Kristo. Pengine unayo nakala yako ya mtiririko wako wa ukuhani ama umeiona ya ndugu ama baba. Fikiria kuhusu umuhimu wa kuweza kufuatilia mtiririko wa ukuhani moja kwa moja hadi kwa Yesu Kristo unaposoma kauli ifuatayo kutoka kwa Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:

Mzee Jeffrey R. Holland

“Hakika, kutenda kwa mamlaka ya kiungu kunahitaji zaidi ya mkataba tu wa kijamii. Hakuwezi kuwezeshwa na mafundisho ya kithiologia ama uteuzi kutoka kwa waumini. Hapana, katika kazi ya Mungu iliyoidhinishwa lazima kuwe na nguvu kuu zaidi kuliko ile ambayo tayari imerithiwa na watu katika viti ama katika mitaa ama katika seminari—ukweli ambao watafutaji wengi wa kidini waaminifu walikuwa wamejua na kukubali wazi kwa vizazi vilivyofuatilia hadi kwa Urejesho. …

“… Sisi katika Kanisa la Yesu Kristo tunaweza kufuatilia mtiririko wa mamlaka ya ukuhani yanayotumiwa na shemasi mpya katika kata, askofu anayemsimamia, na nabii anayetusimamia sisi sote. Mtiririko huo unaenda nyuma katika mfuatano usiovunjika hadi kwa watumishi wakimalaika waliokuja kutoka kwa Mwana wa Mungu Mwenyewe, wakiwa na karama isiyo na kifani kutoka mbinguni” (“Our Most Distinguishing Feature,” Ensign ama Liahona, Mei 2005, 44).

Kila mtu anayepokea ukuhani wa Haruni ama Melkezediki pia anatawazwa kwa ofisi ya ukuhani ambayo inajumuisha majukumu fulani. Soma Moroni 3:1–4, na utafute jinsi watu binafsi wanatawazwa kwa ofisi za ukuhani, ikiwa ni pamoja na ofisi ya mkuhani ama mwalimu.

Unaweza kutaka kuandika ukweli ufuatao katika maandiko yako kando ya mistari hii: Watu binafsi hutawazwa katika ofisi za ukuhani kwa kuwekewa mikono na wale walio na mamlaka.

  1. ikoni ya shajaraJibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Kwa nini unafikiria ni muhimu kwa mtu binafsi kutawazwa kwa ofisi ya ukuhani na mtu ambaye tayari ana ukuhani?

    2. Kuwa na mamlaka ya ukuhani katika Kanisa ama katika familia yako kuna thamani gani kwako?

Moroni 4–5

Moroni anaelezea jinsi sakramenti inapaswa kuhudumiwa

mkate na maji kwenye meza ya sakramenti
  1. ikoni ya shajaraFikiria kuhusu nembo za sakramenti na kuhusu tukio lako la kupokea sakramenti. Kisha fanya yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Kutoka akilini, vyema uwezavyo, andika moja ya sala za sakramenti, ya mkate ama ya maji.

    2. Baada ya kurejelea sala hizi takatifu (ona Moroni 4:3; 5:2) na ukiangalia kile ulichoandika katika sehemu ya kwanza ya zoezi hili, andika kuhusu sehemu ya sala moja ya sakramenti inayokuvutia, na ueleze ni kwa nini sehemu hio ya sala hiyo ina maana kwako.

Moroni alijumuisha sala za kuhudumia sakramenti katika kumbukumbu yake kwa sababu alihisi ingekuwa “ya manufaa” kwa watu “katika siku zijazo” (Moroni 1:4). Soma Moroni 4:1–3 na 5:1–2, na utambue vishazi vinavyoelezea kile ambacho mkate na maji ya sakramenti yanasimamia. Unaposoma, inaweza kusaidia kukumbuka kwamba siku za leo Kanisa hutumia maji katika sakramenti badala ya divai kama matokeo ya ufunuo uliopewa Nabii Joseph Smith (ona M&M 27:2).

Fanya muhtasari madhumuni ya sakramenti kwa kukamilisha kauli hii: Nembo za sakramenti zinatusaidia kukumbuka .

Tafakari ni kwa nini mwili na damu ya Mwokozi ni muhimu kwako.

Mateso ya kimwili, kifo na Ufufuo wa mwili wa Mwokozi na mateso Yake makali ya kiroho, yanayoshuhudiwa kupitia kumwangwa kwa damu Yake, yaliwezesha kusamehewa kwa dhambi kwa watu wote wanaoweka imani Kwake na kutubu. Nembo za sakramenti zinatusaidia kukumbuka Upatanisho wa Yesu Kristo.

  1. ikoni ya shajaraJibu moja ya maswali yafuatayo ama yote katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Kutafakari kwa dhati Upatanisho wa Mwokozi wakati wa sakramenti kumekusaidiaje ama kumekuimarishaje kiroho?

    2. Unaweza kufanya nini ili kuzingatia zaidi kukumbuka Upatanisho wa Mwokozi wakati wa sakramenti?

Ili kukusaidia kuelewa kile ambacho umeahidi kufanya unapopokea sakramenti, rejelea Moroni 4:3 na ukamilishe chati ifuatayo:

Kile ninachoahidi kufanya

Kile nafikiria inamaanisha kuweka sehemu hii ya agano

Kile ninaweza kufanya ili kuweka vyema zaidi sehemu hii ya agano

1.

2.

3.

Tunajifunza pia kutoka Moroni 4:3 kwamba tunapoweka kwa uaminifu sehemu yetu ya agano wa sakramenti, tunaweza daima kuwa na Roho ya Bwana kuwa nasi.

Unaposoma kauli ifuatayo kutoka kwa Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, fikiria kuhusu jinsi umekuwa na karama ya Roho Mtakatifu kwa njia asemazo: “ Roho wa Bwana anaweza kuwa kiongozi wetu na atatubariki na mwongozo, maelekezo, na ulizi wa kiroho wakati wa safari yetu duniani” (“That We May Always Have His Spirit to Be with Us,” Ensign ama Liahona, Mei 2006, 31).

Tafakari Upatanisho wa Mwokozi unapopokea sakramenti Jumapili. Jaribu kuweka sehemu za agano ambazo umetambua katika chati ili kwamba uweze daima kuwa na Roho wa Bwana.

  1. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Moroni 1–5 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningetaka kushiriki na mwalimu wangu: