Utangulizi wa Yakobo
Kwa nini Ujifunze Kitabu Hiki?
Kwa kujifunza kitabu cha Yakobo, unaweza kujifunza masomo muhimu kutoka kwa mtu ambaye alikuwa na imani katika Yesu Kristo isiyotingisika. Yakobo alishuhudia kila mara juu ya Mwokozi na aliwaalika watu wake na wale ambao wangesoma maneno yake na kutubu. Alifunza na kuonyesha umuhimu wa kutimiza miito yetu kutoka wa Bwana kwa bidii. Alionya watu wake dhidi ya hatari za kiburi, utajiri, na ukosefu wa maadili. Yakobo pia alinukuu na kusema juu ya istairi ya Zenu ya miti ya mizeituni, ambayo huonyesha juhudi zisizokoma za Mwokozi za kuleta wokovu wa watoto wote wa Mungu. Katika makabiliano yake na Sheremu, mpinga Kristo, Yakobo alionyesha jinsi ya kujibu kwa haki wale ambao wanatilia shaka au kukashifu imani yetu.
Nani Aliandika Kitabu Hiki?
Yakobo, mwana wa tano wa Sarai na Lehi, ndiye aliandika kitabu hiki. Alizaliwa nyikani wakati familia yake ilikuwa inasafiri kwenda nchi ya ahadi. Katika ujana wake, Yakobo “aliteseka kwa masumbuko, kwa sababu ya ujeuri wa kaka [zake]” (2 Nefi 2:1). Hata hivyo, Lehi alimwahidi kwamba Mungu “ataweka wakfu masumbuko [ya Yakobo] kwa faida [yake]”na kwamba angetumia siku zake “akimutumikia Mungu [wake]” (2 Nefi 2:2–3). Katika ujana wake, Yakobo aliona utukufu wa Mwokozi (ona 2 Nefi 2:3–4). Nefi alimweka wakfu Yakobo kuwa kuhani na mwalimu wa Wanefi (ona 2 Nefi 5:26) na baadaye akamkabidhi yeye mabamba madogo ya Nefi (ona Yakobo 1:1–4). Kama kiongozi wa ukuhani na mwalimu mwaminifu, Yakobo alifanya kazi kwa bidii kuwashawishi watu wake kuamini katika Kristo (ona Yakobo 1:7). Alipokea mafunuo kuhusu Mwokozi, alipata uzoefu wa huduma ya malaika na kusikia sauti ya Bwana (ona Yakobo 7:5), na akamwona Mkombozi wetu (ona 2 Nefi 11:2–3). Yakobo alikuwa baba ya Enoshi, ambaye alimkabidhi mabamba kabla ya kifo chake.
Kiliandikwa Lini na Wapi?
Kitabu cha Yakobo kinaanza takriban miaka 544 Kabla Kristo, wakati Nefi alipomkabidhi Yakobo mabamba madogo. Kinaishia karibu na mwisho wa maisha ya Yakobo, wakati alipompatia mwanawe, Enoshi mabamba hayo. Yakobo aliandika kumbukumbu hii alipokuwa anaishi katika nchi ya Nefi.