Kitengo ya 1: Siku ya 2
Mpango wa Wokovu
Utangulizi
Baba yetu wa Mbinguni ametupa sisi, watoto Wake, mpango unaolenga kutuongoza sote katika furaha ya milele na utukufu. Katika kiini cha mpango wake ni Upatanisho wa Yesu Kristo. Upatanisho hushinda madhara ya Kuanguka na unatuwezesha kutubu na kutakaswa kutokana na dhambi zetu ili tuweze kuwa na furaha katika maisha haya na milele.
Somo hili litakupa maelezo ya jumla fupi ya mpango wa wokovu wa Baba wa Mbinguni. Linaweza kukusaidia kuona jinsi ukweli wa injili utakao jifunza mwaka huu zinahusiana moja kwa nyingine na kwa lengo lako duniani. Ufahamu wako wa mpango wa wokovu unapozidi kukua, imani yako katika Mungu na Mwana Wake, Yesu Kristo itaongezeka, kama pia uwezo wako wa kutimiza sehemu yako katika mpango. Mpango wa wokovu ni “utimilifu wa injili ya Yesu Kristo, uliopangiwa kuleta kutokufa kwa binadamu na uzima wa milele. Unajumuisha Uumbaji, Anguko, na Upatanisho, pamoja na sheria, ibada, na kanuni zote zilizotolewa na Mungu. Mpango huu unawezesha watu wote kuinuliwa na kuishi milele na Mungu” (Guide to the Scriptures, “Plan of Redemption,” scriptures.lds.org).
Mpango Unatusaidia Kuelewa Lengo Letu Duniani
Mpango wa Baba Yetu wa Mbinguni unajibu maswali mengi ambayo watu wengi wamefikiria katika wakati fulani maishani mwao. Je, umewahi kutafakari maswali kama : “ Nilitoka wapi?” Kwa nini niko hapa?” “Nitaenda wapi baada ya maisha haya?”
Kabla tuzaliwe duniani, tuliishi katika uwepo wa Baba yetu wa Mbinguni kama watoto Wake wa kiroho Sisi ni watoto Wake halisi, na Yeye anatupenda. Mpango Wake wa wokovu ndio njia ya kila moja wetu kuwa kama Yeye na kufuraia baraka Zake zote. Tulielewa na kukubali mpango Wake kabla ya duniani.
Kitabu cha Mormoni kinatekeleza wajibu muhimu katika kuelewa kwetu mpango wa wokovu. Manabii wa Kitabu cha Mormoni walitumia maneno mengi tofauti walipokuwa wakirejea mpango huo.
-
Soma maandiko yaliyoorodheshwa chini, na tambua jina “lililotumiwa” kwa mpango wa Baba wa Mbinguni katika kila mstari. Katika jarida lako la masomo ya maandiko, andika jina kando ya rejeleo ya maandiko. La kwanza limetambulishwa
-
2 Nefi 9:6—Mpango wa nehema wa Muumba mkuu
-
Maneno kama vile rehema, ukombozi, wokovu, furaha na fidia yanasisitiza funzo kuwa mpango wa Baba wa Mbinguni umeundwa kuwaletea watoto Wake wokovu wa milele na furaha
-
Jibu maswali yafuatayo katika jarida lako la masomo ya maandiko: Ni tofauti gani katika maisha yako inaletwa na kujua kuwa Baba wa Mbingunu yuko na mpango wa furaha yako na wokovu ?
Wajibu wa Haki ya Kujiamulia na Kuanguka kwa Adamu na Hawa katika Mpango wa Wokovu
Adamu na Hawa ndio walikuwa watoto wa kwanza wa Mungu kuja duniani. Aliwaweka katika Bustani ya Edeni na kuwapa haki yao ya kujiamulia — “uwezo na uhuru wa kuchagua na kutenda kwa ajili yao wenyewe (Guide to the Scriptures, “Agency,” scriptures.lds.org). Aliwaamuru wasile tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Kutii amri hii kulimaanisha kuwa wangeweza kubaki katika bustani, lakini hawangeweza kuendelea kwa kupitia upinzani katika maisha ya muda. Hawangeweza kujua furaha kwa sababu hawangeweza kupitia huzuni na uchungu.
Soma 2 Nefi 2:17–20 na tafuta kile kilichowatendekea Adamu na Hawa baada ya wao kuchagua kutotii amri ya Mungu. Katika nafasi iliyotolewa, elezea kile Adamu na Hawa walichagua kufanya na matokeo mawili ya uchaguzi huo— unaojulikana kwa kawaida kama Kuanguka — ulikuwa nao kwao:
Soma 2 Nefi 2:22–26 na utambue matokeo zaidi ya chaguo Adamu na Hawa walifanya. Weka alama kwenye maandiko yako katika ukweli zaidi unajifunza kuhusu athari ya Kuanguka.
-
Katika jarida lako la masomo ya maandiko, kamilisha aya ifuatayo kwa kuelezea athari ya Kuanguka kwa Adamu na Hawa kwako binafsi. Jumuisha mawazo kuhusu chaguo, wakala, mili ya kidunia, kifo, watoto, na dhambi.
“Kwa sababu ya kosa la Adamu na Hawa, Mimi pia niko katika hali ya kuanguka na …”
Wajibu wa Upatanisho wa Yesu Kristo katika Mpango wa Wokovu
Dhambi na kifo hututenga kutoka kwa uwepo wa Baba yetu wa Mbinguni. Hatuwezi kurudi katika uwepo wa Mungu bila usaidizi wa kiungu. Lazima tuelewe wajibu wa Yesu Kristo na Upatanisho Wake katika mpango wa wokovu ili tuweze kuwa na imani Kwake na mpango wa Baba wa Mbinguni. Soma Mosia 3:17–19, ukitafuta vishazi vinavyoelezea jinsi Upatanisho wa Yesu Kristo unashinda madhara ya Kuanguka na unatusaidia kupata furaha na kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni. Fupisha mistari hii kwa maneno yako mwenyewe.
Kanuni tunayojifunza ni Yesu Kristo ni mtu muhimu katika mpango wa wokovu, na Upatanisho Wake ndio unaofanya mpango utendeke kwa watoto wote wa Mungu.
-
Soma vifungu vifuatavyo vya maandiko: 2 Nefi 2:8; Mosia 3:7–11; 16:4–8; Alma 34:9, 15–16; Mormoni 9:13–14. Katika jarida lako la masomo ya maandiko, andika aya ukielezea kile vinafundisha kuhusu wajibu muhimu wa Upatanisho wa Yesu Kristo katika mpango wa wokovu. Unaweza kutaka kupiga mstari vishazi ambavyo vinamaana kwako.
Jukumu letu katika Mpango wa Wokovu.
Baba wa Mbinguni ametupa mpango Wake kamili wa kuleta furaha yetu ya milele na utukufu pamoja Naye na wapendwa wetu. Yesu Kristo ametimiza wajibu Wake katika mpango, akishinda kifo na kutuwezesha kushinda dhambi na kurudi kuishi tena pamoja na Baba yetu wa Mbinguni. Hata hivyo, hii haiondoi wajibu wetu katika mpango.
-
Katika jarida lako la masomo ya maandiko, andika Baadhi ya majukumu yangu katika mpango wa wokovu,na uorodheshe kile kila maandiko yafuatayo yanafunza kuhusu jukumu letu la kibinafsi la kualika uwezo wa Upatanisho katika maisha yetu na kupokea kikamilifu baraka za mpango wa wokovu:
Maandiko haya yanaweza kutusaidia kuelewa kuwa tunapochagua kuishi injili ya Yesu Kristo na kufuata mpango wa Mungu, tunajitayarisha kupokea uzima wa milele kupitia Upatanisho wa Mwokozi
-
Tuseme umeulizwa kutoa hotuba kanisani kuhusu mpango wa wokovu. Ukitumia kile umejifunza kutoka kwa maandiko katika kazi ya hapo awali, andika katika jarida lako la masomo ya maandiko kile ungesema kuhusu jukumu letu la kibinafsi katika mpango wa Baba wa Mbinguni.
Tafakari kile unaweza kufanya ili kutimiza jukumu lako zaidi katika mpango wa Baba wa Mbinguni na kualika uwezo wa Mwokozi maishani mwako. Zingatia kushiriki mawazo yako na mmoja wa wazazi wako, ndugu, ama rafiki wa karibu.
Mpango wa Wokovu Unatoa Majibu na Mwongozo.
Ufahamu wa mpango wa wokovu unaweza kukuongoza unapofanya uamuzi na kupata majibu ya maswali ambayo wewe na wengine mnakabiliana nayo.
-
Katika jarida lako la masomo ya maandiko, jibu swali moja ya maswali yafuatayo kwa kueleza jinsi ufahamu wa mpango wa wokovu unatoa mwongozo na majibu.
-
Kujua kuwa wewe ni bin au binti halisi wa Mungu kunaathiri vipi hisia zako za kujithamini?
-
Ni jinsi gani ungemjibu mtu ambaye anasema, “ Ni maisha yangu — Nitafanya kile ninachotaka kufanya”?
-
Kuelewa mpango wa wokovu kungewezaje kumsaidia mtu kushinda hisia kuwa maisha inahusisha kuwa na furaha tu na kutosheleza matakwa yetu wenyewe ya anasa?
-
Unawezaje kutumia maarifa yako ya mpango wa wokovu kusaidia mtu ambaye anapitia shida na anahisi ni kwasababu Mungu hampendi yeye?
-
Kuelewa mpango wa wokovu kunaweza kukusaidia kutii amri za Mungu kwa sababu kunaeleza kwa nini tunapaswa kuzitii (ona Alma 12:32).
-
Soma 2 Nefi 2:25, na fupisha lengo la mpango wa wokovu kwa kujibu maswali yafuatayo katika jarida lako la masomo ya maandiko: Ni kwa njia gani mpango wa wokovu umeleta furaha kwako na kwa familia yako ?
-
Andika yafuatayo chini ya kazi ya leo katika jarida lako la masomo ya maandiko:
Nimejifunza somo la “Mpango wa Wokovu” na kulikamilisha (siku).
Maswali, fikra na mawazo ya ziada ningetaka kushiriki na mwalimu wangu: