Seminari
Kitengo cha 32: Siku ya 4, Moroni 10:8–26, 30–34


Kitengo cha 32: Siku ya 4

Moroni 10:8–26, 30–34

Utangulizi

Baada ya kufundisha jinsi ya kupata ushahidi wa ukweli wa vitu vyote kupitia Roho Mtakatifu, Moroni aliwahimiza wale ambao wangesoma maneno yake watambue na kupokea karama za roho. Moroni alihitimisha kumbukumbu ya Kitabu cha Mormoni kwa kuwahimiza watu wote wamjie Yesu Kristo, washikilie kila karama nzuri anatoa, na kukamilishwa kupitia jina Lake.

Moroni 10:8–26

Moroni afundisha kuhusu karama za Roho na malengo yao katika kazi ya Bwana

Fikiria juu ya wakati Baba wa Mbinguni alikubariki kuweza kufanya jambo fulani ambalo haungeweza kulifanya peke yako. Katika mlango wake wa mwisho, Moroni alishuhudia msaada na nguvu Bwana anaweza kutupatia. Soma Moroni 10:8, na utafute kishazi kinachoeleza uwezo wa kiroho ama baraka ambazo Baba wa Mbinguni huwapa watoto Wake waaminifu.

“Karama za Mungu” Moroni anazungumzia katika Moroni 10:8 zinajulikana pia kama “karama za Roho” ama “karama za kiroho.” Huenda ukataka kualamisha kishazi “karama za Mungu” katika maandiko yako. Andika ukweli ufuatao katika maandiko yako kando ya Moroni 10:8: Mungu hutoa karama za Roho kwa faida ya watoto Wake.Kishazi “kwa faida ya watoto Wake” kinamaanisha kuwa na manufaa ama kusaidia watoto Wake.

Soma Moroni 10:9–16, na ualamishe kila karama ya kiroho Moroni alitaja. Ni muhimu kujua kwamba karama za kiroho Moroni alijadili ni mifano michache tu ya karama nyingi za kiroho ambazo zipo. Mzee Marvin J. Ashton wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha kwamba “Mungu ametupa kila mmoja wetu kipaji kimoja ama zaidi cha kipekee”:

Mzee Marvin J. Ashton

“Mmojawapo wa majanga ya maisha, linaonekana kwangu, ni wakati mtu anajiainisha kama mtu ambaye hana kipaji ama karama. Kwetu sisi kuamua kwamba hatuna karama tunapojihukumu kwa kimo, akili, viwango vya kufuzu mitihani, mali, mamlaka , cheo, au muonekano wa nje si tu kukosa haki lakini kukosa maana. …

 Ikichukuliwa bila mpango maalumu, wacheni nitaje karama chache ambazo huwa hazionekani kila mara kwa uwazi ama kutambuliwa lakini ambazo ni muhimu sana. Miongoni mwa hizi huenda kuwa ni karama zako—karama ambazo hazionekani kwa uwazi lakini hata hivyo zipo na zina thamani.

“Acheni tupitie baadhi ya hizi karama zisizowazi kuonekana: karama ya kuuliza; karama ya kusikiliza; karama ya kusikia na kutumia sauti tulivu, ndogo; karama ya kuweza kulia; karama ya kuepuka ubishi; karama ya kuweza kuelewana; karama ya kuepuka marudio ya bure; karama ya kutafuta yale ambayo ni ya haki; karama ya kutokupitisha hukumu; karama ya kuangalia kwake Mungu kwa ajili ya uongozi; karama ya kuwa mfuasi; karama ya kuwajali wengine; karama ya kuwa na uwezo wa kutafakari; karama ya kuomba; karama ya kutoa ushuhuda wa nguvu; na karama ya kupokea Roho Mtakatifu.

“Lazima tukumbuke kwamba kila mtu amepewa karama na Roho wa Mungu [ona M&M 46:11–12]. Ni haki yetu na jukumu kukubali karama zetu na kuzishiriki. Nguvu za Mungu na karama zinapatikana kwetu sote (“There Are Many Gifts,” Ensign, Nov. 1987, 20).

Soma Moroni 10:17, na ufahamu fundisho la Moroni kwamba kila muumini mwaminifu wa Kanisa ana angalau karama moja ya kiroho (ona pia M&M 46:11). Mzee Robert D. Hales wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha kwamba “karama za Roho zitasadia kila mmoja wetu kufikia lengo letu la uzima wa milele.

Mzee Robert D. Hales

“Karama hizi za Roho zimezungukwa na karama ya Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ni mshirika wa tatu wa Uungu wa milele na anatambulika kama Roho Mtakatifu. Huyu Roho Mtakatifu ni karama kutoka kwa Mungu ili kutusaidia kufanya maamuzi ambayo yataturuhusu kupata na kutimiza dhamira yetu. …

“Katika hizi siku za mwisho, ufahamu wa karama za Roho umetupa kwa ufunuo kama ilivyoandikwa katika sehemu ya 46 ya Mafundisho na Maagano . Sehemu ya 46 inabainisha karama maalum za Roho kama ifuatavyo:

“Kwani wote hawapokei vipawa vyote; kwani kuna vipawa vingi, na kwa kila mtu kipawa kimetolewa na Roho wa Mungu’ (v. 11).

“Tunaelezwa wazi kwamba kila mmoja wetu amepewa kipawa ama vipawa. Je, tunajua ni kipawa kipi tumepewa? Je, tunajitahidi kupata karama zetu?” (“Gifts of the Spirit,” Ensign, Feb. 2002, 12).

  1. ikoni ya shajaraFikiria juu ya karama za kiroho umepokea kutoka kwa Mungu, na kisha jibu maswali mawili ama yote ya maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Je, umefaidika kutokana na karama za Roho ambazo umepokea?

    2. Ni mifano ipi ya karama za kiroho umeona Kanisani leo?

    3. Unawezaje kutumia karama za kiroho kubariki maisha ya wengine? Maisha yako yamebarikiwa kwa njia gani na karama za wengine?

Zingatia jinsi karama za kiroho ziko dhahiri katika kuja kwa Kitabu cha Mormoni. Katika nafasi zilizotolewa, tambua karama za kiroho ambazo ziliweza kuonekana katika maisha ya Joseph Smith, kama ilivyoonyeshwa katika kila picha:

Ono la Kwanza

Moroni 10:11

Moroni Anamtokea Joseph Smith katika Chumba Chake

Moroni 10:14

Joseph Smith Apokea Mabamba ya Dhahabu

Moroni 10:16

Mormoni ashuhudia kwamba lazima tuwe na imani ili kupokea karama za kiroho. Alifundisha kwamba Mungu “hufanya kazi kwa uwezo, kulingnana na imani ya binadamu, sawa leo na kesho na milele. (Moroni 10:7). Soma Moroni 10:19, 24, na utambue kile kinachowazuia watu kutopokea na kutambua karama za kiroho.

  1. ikoni ya shajaraAndika katika shajara yako ya kujifunza maandiko ni kwa nini watu katika hali ya kutoamini hawawezi kutambua ama kupokea nguvu na karama za Mungu.

Soma Moroni 10:20–23. Tafuta kile Mormoni alifundisha kuhusu umuhimu wa karama za kiroho za imani, tumaini na hisani. Alishuhudia kwamba karama ya kiroho ya imani huelekeza kwa baraka ya ajabu. Tazama mstari wa 23 ili kupata baraka hii. Kumbuka kwamba neno kutakiwa lina maana ya “kutamanika,” na kishazi “vitu vyote ambavyo vinatakikana kwangu” kinaweza kuwa na maana “vitu vyote ninavyotamani ufanye.” Huenda ukataka kualamisha sentensi katika Moroni 10:23 inayofundisha kanuni hii: Tukiwa na imani, tutaweza kufanya kile Baba wa Mbinguni anataka tufanye.

  1. ikoni ya shajaraIli kukusaidia kutambua jinsi kanuni hii imetimizwa ama inaweza kutimizwa maishani mwako, andika sentensi chache katika shajara yako ya kujifunza maandiko kwa kujibu kauli moja ama zote mbili zifuatazo:

    1. Nilipata ahadi katika Moroni 10:23 nilipo …

    2. Ahadi inayopatikana katika Moroni 10:23 inaweza kunisaidia na …

  2. ikoni ya shajaraFikiria juu ya kanuni mbili umejifunza katika Moroni 10:8–26: Mungu hutoa karama za Roho ili kuwafaidi watoto Wake. Tukiwa na imani, tutaweza kufanya kile nufaisha wa Mbinguni anataka tufanye.Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, jibu maswali yafuatayo:

    1. Kujua kanuni hizi mbili kunawezaje kukusaidia hivi sasa maishani mwako?

    2. Kanuni hizi zinawezaje kukusaidia na fursa ambazo huenda zikaja katika siku za usoni?

Moroni 10:30–34

Moroni ahitimisha kumbukumbu Yake kwa kuwaalika watu wote kumjia Kristo na kukamilishwa Kwake.

Rais James E. Faust

Je, unadhani kuna uwezo wa kuwa mkamilifu katika maisha haya? Rais James E. Faust wa Urais wa Kwanza alielezea amri ya kuwa mkamilifu: “Ukamilifu ni lengo la milele. Wakati hatuwezi kuwa wakamilifu katika maisha duniani, kujitahidi kwa ajili yake ni amri, ambayo hatimaye, kupitia Upatanisho, tunaweza kutii” (“This Is Our Day,” Ensign, Mei 1999, 19).

Kama Rais Faust alivyofundisha, ukamilifu ni lengo tunaloweza kufanyia bidii sasa na kufikia katika maisha yajayo, na usaidizi wa Mwokozi. Moroni alihitimisha ushuhuda wake kwa kufundisha kile tunaweza kufanya ili kualika nguvu ya kusafisha ya Mwokozi katika maisha yetu sasa na hatimaye kuwa wakamilifu kupitia Upatanisho Wake.

  1. ikoni ya shajaraTengeneza chati ifuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Kile ninachoweza kufanya

    Kile Mungu anaahidi

    Soma Moroni 10:30–33, ukitafuta (a) kile sharti tufanye ili kuwa wasafi na hatimaye wakamilifu na (b) kile Mungu anaahidi kufanya ili kutusaidia. Andika kile umepata katika safu sahihi ya chati yako.

Andika kauli ifuatayo chini ya chati katika shajara yako ya kujifunza maandiko ama katika maandiko yako kando ya Moroni 10:32–33: Tunapomjia Yesu Kristo, tunaweza kusafishwa na kukamilishwa kupitia Upatanisho Wake.

Kumjia Kristo ni mchakato wa maishani ambao huanza kwa kumwamini na kisha kwa unyenyekevu kutafuta ushawishi Wake katika maisha yako. Mchakato unaendelea na kukubali injili Yake, kumkubali kama Mwokozi, kutubu, kuagana Naye kupitia maagizo ya injili, na kuvumilia kwa uaminifu katika utiifu kwa amri Zake maishani mwetu mwote. Hatimaye tutakuwa tumemjia Kristo wakati tutakuwa tumekuwa kama Yeye; kisha tutaweza kuishi Naye katika milele.

Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifanya muhtasari wa mwaliko wa mwisho wa Moroni wa kumjia Kristo, unaopatikana katika Moroni 10:30–33:

Mzee Jeffrey R. Holland

“[Ushuhuda wa mwisho wa Moroni unahimiza] imani katika Kristo, tumaini katika Kristo, hisani ya Kristo, na ombi kwamba hizi sifa tatu kuu za Kikristo, hizi kanuni tatu timilifu za Kikristo, zitatuelekeza kwa usafi. …

“Lile ombi la mwisho, la tamati, la upweke la jiwe la katikati la dini yetu na kitabu kilicho sahihi kuliko chochote kilichowahi kuandikwa ni kutokushika chochote kilicho kichafu; ni kuwa watakatifu na bila doa; ni kuwa wasafi. Na usafi huo unaweza kuja tu kupitia damu ya Mwanakondoo aliyechukua ghamu zetu na kubeba huzuni yetu, Kondoo aliyejeruhiwa kwa ajili ya makosa yetu na kuchubuliwa kwa ajili ya maovu yetu, Kondoo aliyechukiwa na kudhulumiwa, lakini yule hatukumheshimu (ona Mosia 14). …

“Usafi — kupitia damu ya Mwanakondoo. Hilo ndilo [Kitabu cha Mormoni] kinasihi juu yake” (“A Standard unto My People” [CES symposium on the Book of Mormon, Aug. 9, 1994], 15, si.lds.org).

Rejelea Moroni 10:32–33, na ualamishe vishazi vinavyohimiza kwamba njia ya pekee tunaweza kukamilika ni kuwa wakamilifu “katika Kristo.” Hii inamaanisha kwamba hatuwezi kufikia ukamilifu peke yetu; lazima tutegemee nguvu na neema ya Upatanisho wa Mwokozi. Tafakari ni kwa nini tunahitaji Upatanisho wa Yesu Kristo ili kuwa wasafi na wakamilifu. Huenda ukataka kualamisha vishazi katika Moroni 10:32–33 unavyopata vinakutia moyo unapojitahidi kwa ajili ya usafi na lengo la milele la ukamilifu.

Angalia nyuma kwa kile ulichoandika chini ya “Ninaweza kufanya nini” katika chati ndani ya shajara yako ya kujifunza maandiko. Chagua kitendo kimoja kilichoandikwa hapo na utafakari jinsi unaweza kujitahidi zaidi katika sehemu hiyo maishani mwako.

Soma Moroni 10:34, na utafute ushahidi wa imani ya Moroni katika Yesu Kristo na tumaini la kupokea uzima wa milele. Sisi pia tunaweza kuwa na imani na tumaini tunapofanya kujifunza Kitabu cha Mormoni jitihada ya kimaisha na kutumia kweli zilizofundishwa katika kurasa zake.

  1. ikoni ya shajaraKatika kuhitimisha kozi hii ya masomo juu ya Kitabu cha Mormoni, jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko, na jitayarishe kushiriki majibu yako na mwalimu wako:

    1. Ni tofauti gani kujifunza Kitabu cha Mormoni mwaka huu kumefanya katika maisha yako?

    2. Ni masomo ama kanuni gani zimekusaidia “kuja kwa Kristo” na kuimarisha imani yako katika Mwokozi?

    3. Una ushuhuda gani wa Kitabu cha Mormoni?

  2. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Moroni 10:8–26, 30–34 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningetaka kushiriki na mwalimu wangu:

Moroni Aficha Bamba katika Kilima Kumora