Seminari
Mormoni


Utangulizi wa Mormoni

Kwa nini Ujifunze Kitabu Hiki?

Unaposoma kitabu cha Mormoni, utajifunza masomo ya thamani kutoka kwa Mormoni, aliyeishi kwa imani kama mfuasi wa Yesu Kristo hata ingawa alizingirwa maishani mwake na “mfululizo wa kuonekana kwa uovu na machukizo” (Mormoni 2:18). Utafaidika pia kutoka kwa kujifunza maneno ya Moroni, mwana wa Mormoni, aliyewashuhudia watakatifu wa siku za mwisho, “Yesu Kristo amenionyesha nyinyi kwangu, na ninajua yale mnayofanya” (Mormoni 8:35). Kwa kujifundisha maandiko haya unaweza kujifunza umuhimu wa kuchagua kuishi kulingana na amri na maagano ya injili ya Yesu Kristo.

Nani Aliandika Kitabu Hiki?

Mormoni aliandika sura saba za kwanza kama maelezo mafupi ya uovu na vita kati ya Wanefi na Walamani katika siku zake. Pia aliandika “nakili kamili” ya matukio kutoka kwa maisha yake yote kwenye bamba kubwa za Nefi. (Ona Mormoni 2:18; 5:9.) Wakati Mormoni alikuwa “takriban umri wa miaka kumi,” mweka rekodi aliyeitwa Amoroni alimjulisha kwamba hatimaye atakuwa na jukumu la kurekodi “vitu vyote ambavyo utakuwa umeviona kuhusu hawa watu” (Mormoni 1:2, 4). Alipokuwa takriban umri wa miaka 24, alipata umiliki wa bamba za Nefi na aliandika “rekodi kulingana na maneno ya Amaroni” (Mormoni 2:17). Baadaye, Mormoni alianza kufanya ufupisho wa mabamba makubwa ya Nefi, yaliyojumuisha maandiko kutoka kwa manabii na wawekaji rekodi kutoka kwa Lehi hadi Amaroni. Akikaribia mwisho wa maisha yake, Mormoni “alizificha katika kilima cha Kumora kumbukumbu zote ambazo zilikuwa zimekabidhiwa [kwake] na mkono wa Bwana,” ila tu mabamba machache ambayo alimpa mwanae Mormoni (Mormoni 6:6). Kisha aliwaongoza Wanefi katika vita vyao vya mwisho dhidi ya Walamani. Kabla Mormoni kufa, alimshauri Moroni akamilishe rekodi yake. Moroni aliongeza maandiko yanayojumuisha milango ya 8–9 ya kitabu hiki.

Kiliandikwa Lini na Kiliandikiwa Wapi?

Mormoni huenda aliandika Mormoni 1–7 kati ya miaka 345 Baada ya Kristo na miaka 401 Baada ya Kristo (ona Mormoni 2:15–17; 8:5–6). Alikamilisha maandishi yake baada ya vita vikuu vya mwisho kati ya Wanefi na Walamani katika Kumora (ona Mormoni 6:10–11). Moroni huenda aliandika Mormoni 8–9 kati ya miaka 401 Baada ya Kristo na miaka 421Baada ya Kristo alipotembea kwa ajili ya usalama wa maisha yake (ona Mormoni 8:4–6; Moroni 1:1–3).

Chapisha