Seminari
Kitengo cha 28: Siku ya 4, Mormoni 7:1–8:11


Kitengo cha 28: Siku ya 4

Mormoni 7:1–8:11

Utangulizi

Baada ya pigano la mwisho kati ya Wanefi na Walamani, Mormoni aliwaandikia uzao ujao wa watu wa Kitabu cha Mormoni kuhusu umuhimu wa kujua wao ni akina nani na kile wanapaswa kufanya ili kuokolewa. Akiwa na upendo mkuu kwa ajili ya uzao ujao wa maadui zake, Mormoni alifundisha umuhimu wa kufuata injili ya Yesu Kristo, kwamba iweze “kuwa vyema nanyi katika siku ya hukumu” (Mormoni 7:10). Baada ya Mormoni kuaga, Moroni aliwachwa pekee yake kuandika juu ya maangamizo ya watu wake.

Mormoni 7

Katika ushuhuda wa Mormoni wa mwisho, aliwashauri Walamani waliobaki kuamini katika Yesu Kristo na kufuata injili Yake.

Picha
Mormoni Aiaga Nchi Iliyokuwa Kuu Hapo Awali

Katika Mormoni 6 ulijifunza kwamba kulikuwa na majeruhi 230,000 wa Wanefi katika pigano la mwisho na Walamani. Wazia kwamba ulinusurika kwenye pigano kuu kama hili, lakini marafiki zako na familia hawakunusurika. Ungehisi vipi juu ya kizazi cha watu waliouwa wapendwa wako na kuteka taifa lako? SomaMormoni 7:1–4, na utafute kile ambacho Mormoni aliwaandikia uzao wa Walamani.

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni nini Mormoni alitaka Walamani na vizazi vyao vijue?

    2. Hii inalinganika vipi na vile ulifikiria ungehisi kuhusu vizazi vya watu ambao waliwaua marafiki zako na familia yako katika hali iliowaziwa?

    3. Ni sifa gani ya Mwokozi unaona katika jibu la Mormoni kwa maadui zake?

Mormoni aliendelea kuwaandikia uzao wa Walamani. Soma Mormoni 7:5–7, na utie alama angalau kweli tatu ambazo Mormoni aliwashauri uzao wa Walamani waamini kuhusu Mwokozi, Yesi Kristo

  1. Chagua mmoja ya kweli kuhusu Yesu Kristo ambazo umetambua, na uandike katika shajara yako ya kujifunza maandiko jinsi kuamini fundisho hilo kumeadhiri maisha yako.

Mormoni angehisi kuwa na haki katika kuandika maneno ya hukumu kwa Walamani ambao walikuwa wameuwa wengi wa watu wake, lakini kwa sababu ya ufahamu wake wa ukweli, aliandika ili kuwafundisha kile wao (na sisi) lazima wafanye ili wawe bila hatia mbele ya Mungu kwenye baraza la haki. Soma Mormoni 7:8–10, na utambue kile ambacho Mormoni alishuhudia mtu sharti afanye. Unaweza kuamua kutia alama kile ambacho umekitambua katika maandiko yako.

Mistari hii inatufunza kwamba Bwana hutoa uokovu kwa kila mtu na atakomboa wale ambao wanakubali kanuni na maagizo ya injili Yake.Unaweza kuamua kuandika kanuni hii katika maandiko yako. Tazama kwamba Mormoni alifundisha kwamba jinsi tunavyokuja kujua njia ya kuishi kanuni hizi ni kupitia kujifunza kwetu maandiko (ona Mormoni 7:8). Inaweza kusaidia kuelewa kwamba kishazi “maandishi haya” kinarejelea Kitabu cha Mormoni, na “maandishi ambayo yatawajia Wayunani kutoka kwa Wayahudi” kinarejelea Bibilia. Vile vile, “haya” katika Mormoni 7:9 linarejelea Kitabu cha Mormoni, na “hiyo” linarejelea Bibilia. Unaweza kuamua kuyaweka alama hizi tofauti katika maandiko yako.

Unapokamilisha Mormoni 7, chukua muda kutafakari mfano wa Mormoni wa hisani na upendo kama wa Kristo katika kuandika ujumbe kama huo wa tumaini na himizo kwa uzao wa wale waliokuwa maadui wao kabisa.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika mawazo yako juu ya swali lifuatalo: Je! Ninawezaje kufuata mfano wa Mormoni na kutendea wengine, ikiwa ni pamoja na wale ambao wangenitendea vibaya, kwa njia inayoonyesha thamani yao ya milele?

Mormoni 8:1–11

Moroni anaandika juu ya kifo ya babake, maangamizo ya watu wake, na kubaki kwake pekee yake.

Fikiria wakati ulikuwa pekee yako. Ulihisi vipi kuhusu kuwa pekee yako? Wazia kuwa pekee yako kwa miaka mingi.

Ona tarehe katika miuhtasari ya sura ama chini ya kurasa katikaMormoni 7 na 8. Miaka mingapi ilipita kati ya wakati Mormoni alipoandika maneno yake ya mwisho katika mlango wa 7 na wakati Mormoni alipoanza kuandika kwenye mabamba katika mlango wa 8

Picha
Moroni akiomboleza juu ya Mormoni

Soma Mormoni 8:1–2, na utafute kile kilichotokea baada ya pigano kuu kule Kumora. Kisha soma Mormoni 8:3–9 na uweke alama vishazi vinavyoelezea hali za Moroni baada ya maangamizo ya watu wake. Tafakari jinsi ungehisi ikiwa ungekuwa katika hali kama hizo.

Fikiria juu ya wakati ulipohisi kuwa pekee yako katika imani yako ama viwango. Je, uamuzi wako kumfuata Mwokozi na kutii amri Zake wakati huo uliongezeka, ulibaki sawa, ama ulipungua? Kwa nini?

Angalia tena Mormoni 8:1, 3 ili kupata kile Moroni alikuwa ameamua kufanya licha ya hali zake. Mfano wa Moroni unaonyehsa kwamba hata ukiwa pekee yako, unaweza kuchagua kubaki mwaminifu.Unaweza kuamua kuandika ukweli huu katika maandiko yako.

Kuna wengine katika Kitabu cha Mormoni ambao, kama Moroni, walibaki kuwa waaminifu hata walipokuwa pekee yao. Abinadi alisimama na kushuhudia pekee yake mbele ya Mfalme Nuhu na makuhani wake (ona Mosia 12–17). Alma alikuwa kuhani pekee aliyeamini maneno ya Abinadi na kujaribu kumtetea (onaMosia 17:1–4).

Mzee Richard G. Scott alishiriki hadithi ifuatayo kuhusu mvulana aliyechagua kuwa mwaminifu hata aliposimama pekee yake:

Picha
Mzee Richard G. Scott

“Zingatia mfano wa [huyu] mvulana. Kwa miaka iliyopita nimetazama jinsi wazazi wake wamemfunza kuanzia alipokuwa mchanga kuishi amri za Mungu bila kusita. Kwa mfano na maadili, walimkuza, pamoja na watoto wao wengine, katika ukweli. Walihimiza ukuzi wa nidhamu na kujitolea ili kufikia malengo ya kustahili. Mvulana huyu alichagua kuogelea kama mbinu ya kukuza ndani yake sifa hizo. Mazoezi ya asubuhi mapema yalihitaji nidhamu na kujitolea. Baada ya muda alipata umahiri katika mchezo huo.

“Kisha changamoto zikaja— kwa mfano, shindano la kuogelea lilikuwa Jumapili. Je, angeshiriki? Je, angesingizia marekebisho ya kanuni yake ya kutoogelea Jumapili ili kusaidia timu yake kushinda shindano? Hapana, hangethubutu, hata katika ushawishi mzito wa rika lake. Alitukanwa, hata kuumizwa kimwili. Lakini hangethubutu. Kukataliwa na marafiki, upweke, na ushawishi mzito ulileta nyakati za huzuni na majonzi. Lakini hangethubutu. Alikuwa anajifunza yeye mwenyewe kile sisi sote ni lazima tuje kujua, ukweli wa ushauri wa Paulo kwake Timotheo, “wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa” (2 Tim. 3:12). Kwa miaka iliyopita mpangilio huu thabiti wa maisha ya haki —ukiambatana na mamia ya maamuzi sahihi, baadhi katika uso wa changamoto kubwa — umekuza tabia ya nguvu na uwezo. Sasa, kama mmisionari, anaheshimiwa na rika lake kwa uwezo wake wa kufanya kazi, ufahamu wake wa ukweli, kujitolea kwake kusikosita, na bidii yake ya kushiriki injili. Mmoja ambaye awali alikataliwa na rika lake sasa amekuwa kiongozi anayeheshimiwa na rika lake” (“First Things First,” Ensign, Mei 2001, 8).

Soma Mormoni 8:10–11, na ubainishe njia moja Bwana alimhimili Moroni na Mormoni (kabla ya kifo chake) wakati wa hali ngumu walizopitia. Himizo lifuatalo la Rais Thomas S. Monson linaweza kukusaidia katika uamuzi wako kubaki mwaminifu hata ukiwa pekee yako.

Picha
Rais Thomas S. Monson

“Tunapoendelea kuishi siku baada ya siku, ni dhahiri kwamba imani yetu itapingwa. Tunaweza saa zingine kujipata tumezungukwa na watu wengine na bado tukiwa tumesimama katika wale wachache ama hata kusimama pekee yetu kuhusu kile ambacho kinakubalika na kile ambacho hakikubaliki. Je, tuna ujasiri wa kimaadili kusimama imara kwa imani yetu, hata ikiwa kwa kufanya hivyo ni lazima tusimame pekee yetu? …

“… Na tuweze daima kuwa wajasiri na tayari kusimama kwa ajili ya yale tunayoamini, na ikiwa lazima tusimame pekee yetu katika kufanya hivyo, tuweze kufanya hivyo kwa ujasiri, tukiwa tumeimarishwa na ufahamu kwamba kwa ukweli kamwe hatuko pekee yetu tunaposimama na Baba yetu aliye Mbinguni”(“Dare to Stand Alone,” Ensign na Liahona, Nov. 2011, 60, 67).

  1. Katika shajara yako ya maandiko, andika majibu ya maswali yafuatayo:

    1. Unajua nani mwingine ambaye ni mfano wa kusimama mwaminifu hata unaposimama pekee yako?

    2. Kauli ya Rais Monson inakusaidiaje kuamua kubaki mwaminifu hata wakati uko pekee yako?

  2. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Mormoni 7:1–8:11 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningetaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha