Seminari
Kitengo cha 29: Siku ya 1, Mormoni 8:12–41


Kitengo cha 29: Siku ya 1

Mormoni 8:12–41

Utangulizi

Baada ya kuandika juu ya uangamizi wa watu wake na kifo cha babake, Moroni alitoa unabii juu ya kuja kwa Kitabu cha Mormoni na kuonya wale ambao wangekihukumu. Moroni aliona kwamba rekodi ya Wanefi ingekuja katika siku ya uovu mkubwa, ambapo wengi wangependa mali za kidunia kuliko Mungu. Alishuhudia kwamba Kitabu cha Mormoni kingekuwa “cha thamani kubwa” (Mormoni 8:14) wakati wa hali hatari za kiroho za siku za mwisho.

Mormoni 8:12–32

Moroni anatoa unabii juu ya kuja kwa Kitabu cha Mormoni

Andika zile unaamini ni baadhi za karama kuu umewahi kupewa:

Chukua muda kufikiria kuhusu sababu karama hizi zimekuwa baraka kwako.

Soma kauli ifuatao kutoka kwa Rais Ezra Taft Benson: “ Ningependa kuzungumzia moja ya karama muhimu iliotolewa kwa dunia katika nyakati za sasa. Karama ninayofikiria kuhusu ni muhimu zaidi kuliko uvumbuzi wowote mwengine ambao umekuja kutokana na mapinduzi ya viwanda na teknolojia. Hii ni karama ya thamani zaidi kwa binadamu kuliko hata maendeleo mengi ya ajabu ambayo tumeyaona katika utibabu wa kisasa. Ni ya thamani zaidi kwa binadamu kuliko maendeleo ya kupaa na ndege ama usafiri angani. Ninazungumzia karama ya .”

Unafikiria karama Rais Benson alikuwa anairejea inaweza kuwa ni ipi?

Moroni alifundisha kuhusu karama hii katika Mormoni 8. Soma Mormoni 8:12–14 ili kujua karama ni gani. Kishazi “maandiko haya” kinaturejesha kwenye Kitabu cha Mormoni. Kitabu cha Mormoni ndicho karama ambayo Rais Benson alizungumuzia (ona “The Book of Mormon—Keystone of our Religion,” Ensign, Nov. 1986, 4). Andika Kitabu cha Mormoni katika pengo mwishoni mwa kauli ya Rais Benson.

Picha
mabamba ya dhahabu

Soma tena Mormoni 8:12–14 ili kutambua kile Mormoni alifundisha kuhusu thamani ya Kitabu cha Mormoni. Alifundisha nini kuhusu thamani ya kifedha ya mabamba? Moroni alieleza kwamba ijapokuwa Bwana hataruhusu mabamba yatumiwe kwa ajili ya faida ya kifedha, maandiko kwenye mabamba ni ya thamani kuu.

Jinsi Kitabu cha Mormoni kilikuja inaweza kutusaidia kuelewa umuhimu wa kitabu hiki. Soma Mormoni 8:15–16, na utambue kile Moroni alifundisha kuhusu jinsi Kitabu cha Mormoni kingekuja.

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Unafikiria inamaanisha nini kwamba Kitabu cha Mormoni kingeletwa tu na mtu aliye na “lengo katika utukufu wa Mungu”? (Mormoni 8:15).

    2. Inamaanisha nini kwako kwamba Kitabu cha Mormoni kingeletwe “na uwezo wa Mungu”? (Mormoni 8:16). Unahisi vipi juu ya Kitabu cha Mormoni unaposoma maneno ya Moroni katika Mormoni 8:16?

Moroni aliwaonya wale ambao wangehukumu ama kukana Kitabu cha Mormoni. Tafuta maonyo yake unaposoma Mormoni 8:17–22. Kwa nini ni muhimu kwako kujua kwamba “kusudi la milele la Bwana litaendelea, mpaka ahadi zake zote zitakapotimizwa”? (Mormoni 8:22).

Moroni alieleza kwamba Bwana alikuwa amefanya agano na “watakatifu ambao wameenda kabla yangu” (Mormoni 8:23)—ikiwa ni pamoja na manabii kama Nefi, Yakobo, Enoshi, na Alma. Bwana alikuwa ameagana kwamba angeleta maneno ya manabii hawa katika siku za mwisho. Unapojifunza Mormoni 8:23–25, tambua yule ambaye manabii hawa waliombea.

Manabii hawa waliwaombea “ndugu ndugu zao” (Mormoni 8:24), kumaanisha Walamani na uzao wao. Waliombea pia mtu ambaye “ataleta mambo haya” katika siku za mwisho (Mormoni 8:25; ona pia Mormoni 8:16), ikimaanisha Nabii Joseph Smith, aliyechaguliwa kuleta Kitabu cha Mormoni kwa ulimwengu katika hizi siku za mwisho (ona M&M 3:5–10). Wengi wa manabii wa kale walikuwa na ufahamu wa Joseph Smith na waliombea ufanisi wake kutafsiri na kuchapisha Kitabu cha Mormoni, hivyo basi kutimiza malengo ya Mungu (ona Mormoni 8:22, 24–25; M&M 10:46).

Rais Boyd K. Packer, Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, alizungumzia jukumu ambalo Joseph Smith alikuwa nalo katika kuleta Kitabu cha Mormoni:

Picha
Rais Boyd K. Packer

“Kudhania kwamba [Joseph Smith] alitoa [Kitabu cha Mormoni] bila usaidizi na bila maongozi kiroho ni upuuzi.

“Ukweli ni, kwa urahisi, kwamba alikuwa nabii wa Mungu— hakuna zaidi ama hata tone ndogo pungufu!

“Maandiko hayakuja kutoka kwa Joseph Smith ila kama yalivyokuja kupitia kwake. Alikuwa ni njia kupitia ambapo mafunuo yalitolewa. Alikuwa kwa maneno mengine ni mtu wa kawaida, kama tu vile manabii wa kale na kama vile manabii katika siku zetu. …

“Nabii Joseph Smith alikuwa kijana wa mashambani asiye na elimu. Kusoma baadhi ya barua zake za kwanza katika hali halisi kunamuonyesha kuwa hana maarifa katika kuandika majina na sarufi na katika kujieleza.

“Kuwa mafunuo yalikuja kupitia kwake katika hali yoyote ya ustaarabu wa kifasihi kwa kweli ni miujiza” (“We Believe All That God Has Revealed,” Ensign, Mei 1974, 94).

Wazia kuwa wewe ni Moroni, aliyeishi takribani miaka 1,600 iliyopita na kupitia uwezo wa Mungu ulikubaliwa kuona siku zetu. Soma Mormoni 8:35, na uzingatie kile ungefikiria kuhusu hali ya kiroho ya siku zetu. Kisha somaMormoni 8:26–32, inayojumuisha maelezo ya kinabii ya Moroni juu ya wakati ambapo Kitabu cha Mormoni kingekuja— siku zetu.

  1. Katika shajara yako ya maandiko, andika maelezo mawili ama zaidi ya Moroni ya siku zetu. Pia andika ni kwa nini unafikiria maelezo haya ni ya kuvutia na kustahili katika siku zetu.

Kuhusu Kitabu cha Mormoni, Rais Ezra Taft Benson alifundisha:

Picha
RaisEzra Taft Benson

“Ni lazima tufanye Kitabu cha Mormoni kiwe msingi wa kujifunza [kwa sababu] kiliandikwa kwa ajili ya siku zetu. Wanefi hawakuwahi kuwa na kitabu hiki; wala hata Walamani wa kale. Kilikusudiwa kiwe chetu. …

“Kila mmoja wa waandishi wakuu wa Kitabu cha Mormoni alishuhudia kwamba aliandika kwa ajili ya uzao wa siku za usoni. …

“Kama waliona siku yetu, na wakachagua mambo yale ambayo yangekuwa ya thamani kuu kwetu, je, hivyo sivyo tunavyopaswa tujifunze Kitabu cha Mormoni? Tunapaswa tujiulize wenyewe kila mara, Kwa nini Bwana alimshawishi Mormoni (au Moroni au Alma) ajumuishe hayo katika kumbukumbu zake? Ni somo gani ninaweza kujifunza kutoka kwa haya litakalonisaidia kuishi katika siku hii na nyakati hizi?’” (“The Book of Mormon—Keystone of Our Religion,” 6).

  1. Ili kutafakari umuhimu wa Kitabu cha Mormoni kwako binafsi, jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko.

    1. Fikiria kuhusu jinsi unabii wa Moroni ni sahihi kuhusu hali za siku zetu (ona Mormoni 8:26–32). Unabii huu unakufundisha nini kuhusu thamani ya Kitabu cha Mormoni kwa siku zetu?

    2. Kwa nini unafikiria Kitabu cha Mormoni kiko, kama Rais Ezra Taft Benson alivyofundisha, “ mojawapo wa karama ya maana kabisa iliopewa ulimwengu katika siku za kisasa”? (“The Book of Mormon—Keystone of our Religion,” 4).

    3. Rafiki akikuuliza ni kwa nini Kitabu cha Mormoni kilikuwa muhimu kwako, utajibu vipi?

Mormoni 8:33–41

Moroni anaona siku za mwisho na alaani uovu wa kiroho wa siku zetu.

Fikiria juu ya wakati ulipogundua mtu aliyekuwa na mahitaji—mtu aliyekuwa na mahitaji ya muda, kihisia, kijamii, ama kiroho. Zingatia kile ulichofanya ama ungefanya ili kumsaidia mtu huyo. Tafakari ni kwa nini ulichagua kumsaidia ama kutomsaidia mtu huyo. Kwa nini unafikiri watu wakati mwingine huwa hawasaidi wale walio na mahitaji?

Soma Mormoni 8:36–41, na utafute sababu Moroni alizitoa za kwa nini baadhi ya watu katika siku za mwisho hawatawasaidia wale walio na mahitaji. Zingatia kutia alama sababu hizi katika maandiko yako. Huenda ukasaidia kuelewa kwamba neno pamba linamaanisha “kurembesha” ama “nakshi.”

Ni ipi baadhi ya mifano ya jinsi vijana siku hizi huenda wakapenda vitu ambavyo pesa inaweza kununua na kufuata malengo ya kidunia kuliko kuwa wafuasi wa kweli wa Yesu Kristo? Soma Mormoni 8:38, 41, na utambue matokeo ambayo watu watakumbana nayo kwa ajili ya kiburi chao, uovu, na kuwatelekeza maskini na walio na shida.

  1. Andika kanuni katika shajara yako ya kujifunza maandiko inayofanya muhtasari yale umejifunza kutoka Mormoni 8:36–41.

Mfano moja wa kanuni iliyofundishwa katika mistari hii ni: Mungu atatuwajibisha kwa jinsi tunavyowatendea maskini na walio na shida.

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Ni yapi baadhi ya mahitaji ya kawaida—ya muda, kijamii, kihisia, na kiroho—miongoni mwa vijana katika shule yako ama jamii? Kisha fikiria juu ya kitu unachoweza kufanya katika wiki ijayo ili kumfariji mtu aliye na mahitaji. Andika lengo hili katika shajara yako ya kujifunza maandiko.

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimesoma Mormoni 8:12–41 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningetaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha