Seminari
Kitengo 23: Siku ya 3, Helamani 13–14


Kitengo 23: Siku ya 3

Helamani 13–14

Utangulizi

Miaka michache kabla ya kuzaliwa kwa Mwokozi, Bwana alimtuma nabii Mlamani aitwaye Samweli kuhubiri toba kwa Wanefi huko Zarahemla. Nabii Samweli alikuwa shahidi wa pili wa Yesu Kristo, pamoja na nabii Nefi. Aliwaonya Wanefi mbeleni juu ya uharibifu wao ikiwa hawakutubu. Samweli alikabiliana nao juu ya mwelekeo wao wa kukataa manabii na tabia yao kutafuta furaha katika kufanya maovu. Alitangaza ishara zitakazoashiria kuzaliwa na kifo cha Yesu Kristo. Pia alifundisha kwamba wanadamu wote, kwa njia ya ukombozi wa Yesu Kristo, waletwa tena katika uwepo wa Mungu kwa ajili ya hukumu.

Helamani 13

Samweli awaonya wanefi juu ya kuangamizwa kwao ikiwa hawatatubu

Picha
Samweli Mlamani Ukutani

Wakati umefanya kitu kibaya na ilihitajika kusahihishwa na mzazi au kiongozi mwingine, jinsi ulifanya nini?

Maelezo ya nabii akiwaita watu kutubu yaliyoandikwa katika Helamani 13–16 ni ya kipekee kwa sababu ni mara ya kwanza katika Kitabu cha Mormoni ya nabii Mlamani akiwaita Wanefi kutubu.

Soma Helamani 13:1–8, 11 ili kuelewa ni kwa nini Samweli aliwahubiria Wanefi na kile Bwana alimwongoza kusema. Mistari hizi zinaonyesha kanuni: Manabii hupokea na kusema ujumbe ambao Mungu huweka katika nyoyo zao. Ni ujumbe gani Mungu aliweka ndani ya moyo wa Samweli? Kulingana na Helamani 13:7, ni athari gani Samweli alitumaini ujumbe wake utakuwa nao juu ya Wanefi?

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kuhusu wakati ulipohisi kuwa mzazi au kiongozi wa Kanisa aliongozwa kutoa ujumbe fulani. Ujumbe huo ulikuathiri vipi?

Katika nafasi zilizotolewa, andika majibu ya maswali katika chati vifuatavyo unaposomaHelamani 13:17–23 and Helamani 13:24–30.

Helamani 13:17–23

Kanuni:Wakati hatumkumbuki Bwana, tunaathirika kutokana na kiburi na uovu.

Ni mistari gani ambayo unahisi inafundisha kanuni hapo juu?

Nini laana gani Samweli alisema itakuja juu ya Wanefi?

Kulingana na Samweli, ni nini ambacho Wanefi hawakuwa wakifanya walipoweka mioyo yao juu ya utajiri wao?

Je, ni njia gani vijana wa leo wanaweza kuweka mioyo yao juu ya utajiri—mali, mazoea, na tamaa —ambayo inaweza kusababisha kiburi na uovu?

Kwa nini unafikiri ni muhimu “kumkumbuka Bwana Mungu wako kwa vitu ambavyo amekubariki navyo”? (mstari 22).

Helamani 13:24–30

Kanuni: Tukikataa maneno ya manabii wa Bwana, tutapata majuto na huzuni.

Mistari gani ambayo unahisi inafundisha kanuni hapo juu?

Ni sababu gani Samweli alisema Wanefi walitumia kwa kuwakataa manabii wa Bwana?

Kwa nini unafikiri watu mara nyingi hukubali manabii wa uongo kwa njia ambayo Samweli aliieleza?

Jibu maswali mawili yafuatayo kwa kusoma hotuba za hivi karibuni za mkutano mkuu katikaEnsign au Liahona:

Ni mafundisho gani maalum ya manabii wetu walio hai na mitume?

Ni matatizo gani maalum ambazo manabii na mitume wametuonya tuepuke?

Chambua Helamani 13:26–28, ukiangalia jinsi Wanefi walikuwa wakijibu manabii wa uongo. Rais Ezra Taft Benson alitangaza: “Jinsi tunavyoitika kwa maneno ya nabii aliye hai anapotueleza tunachohitajika kujua, lakini badala yake hatusiki, ni mtihani wa uaminifu wetu”(The Teachings of Ezra Taft Benson [1988], 140).

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Je, ni mfano gani wa ushauri wa kinabii ambao umechagua kutii?

    2. Umebarikiwa vipi kwa kufuata ushauri huu?

    3. Jinsi gani unaweza kujiboresha katika kufuata ushauri wa manabii hai?

Samweli alitabiri kwamba Wanefi wangeangamizwa katika miaka 400 kama hawangetubu (Helamani 13:9–10), na alifundisha kwamba sababu pekee ya kutoangamizwa tayari ilikuwa ni kwa sababu ya wenye haki ambao waliishi miongoni mwao (ona Helamani 13:12–14).

Soma Helamani 13:38 ili kugundua jinsi Wanefi wengi katika siku za Samweli walikuwa waovu sana.

Samweli alitangaza kwamba hatuwezi kupata furaha katika kufanya maovu, ambayo inatusaidia kuelewa kwamba furaha ya kweli huja tu tunaposhika amri za Mungu. Ni kifungu gani ya umahiri wa maandiko unaofundisha pia ukweli huu? (Ona tanbihi c kwa Helamani 13:38.)

Picha
Rais Ezra Taft Benson

Rais Ezra Taft Benson ametusaidia kuelewa kanuni hii aliposema: “Kuna msemo wa zamani unaosema: Ni bora kujiandaa na kuzuia kuliko kukarabati na kutubu. Jinsi ilivyokweli. Mstari wa kwanza wa ulinzi wa kujiweka wasafi kimaadili ni kujiandaa kupinga majaribu na kujizuia kuanguka katika dhambi” (“The Law of Chastity,” in Brigham Young University 1987–88 Devotional and Fireside Speeches [1988], 51;

Samweli alifundishwa kwamba uamuzi wa Wanefi wa kuchelewesha toba utasababisha mateso yao na uharibifu. Maelezo mengine katika Kitabu cha Mormoni yanafundisha kwamba watu wanaweza kuendelea katika uasi na uovu mpaka roho ya toba aweze kuwaacha. Kwa mfano, Lamani na Lemueli, hawangesikiza Mungu na wakawa wenye“hisia ya zamani” (1 Nefi 17:45). Mifano kama hiyo inaonyesha ni kwa nini ni muhimu sana kwetu kutoahirisha toba yetu. Kupitia kwa toba unaweza kufanya mambo kuwa sahihi na kuzuia dhambi na majaribu kushinda tamaa yako ya kumfuata Mungu.

Soma taarifa ifuatayo na Rais Dieter F. Uchtdorf wa Urais wa Kwanza ili kuelewa vyema kwamba unaweza kurejesha njia sahihi katika maisha ikiwa umechukua mwelekeo mbaya:

Picha
Rais Dieter F. Uchtdorf

“Wakati wa mafunzo yangu ya kuwa rubani wa ndege, ilinibidi kujifunza jinsi ya kuendesha ndege juu ya umbali mrefu. Safari juu ya bahari kubwa, kuvuka jangwa, na kuunganisha mabara yanahitaji mipangilio makini ili kuhakikisha kuwasili salama katika eneo lililopangwa. Baadhi ya ndege hizi za moja kwa moja zinaweza kukaa hadi masaa 14 na kutembea karibu maili 9,000.

“Kuna eneo la uamuzi muhimu wakati wa safari ndefu kama lile linalojulikana kwa kawaida kama eneo la kurudi salama. Kufikia eneo hili ndege lina mafuta ya kutosha ya kugeuka na kurudi salama kwenye uwanja wa ndege wa kuondoka. Baada ya kupita eneo la kurudi salama, nahodha amepoteza chaguo hili na lazima aendelee mbele. Hiyo ndio sababu eneo hili mara nyingi hujulikana kama eneo la kutoweza kurudi

“… Shetani anataka tufikirie kwamba tunapofanya dhambi tumepita ‘eneo la kutoweza kurudi’ —kwamba tumechelewa sana kubadilisha mwelekeo wetu. …

“… Ili kutufanya kupoteza matumaini, kujisikia kuhuzunika kama yeye mwenyewe, na kuamini kwamba tumepita zaidi ya msamaha, Shetani anaweza hata kutumia vibaya maneno kutoka maandiko yanayosisitiza haki ya Mungu, ili kuashiria kwamba hakuna huruma. …

“Kristo alikuja kutuokoa. Kama tumechukua mwelekeo mbaya, Upatanisho wa Yesu Kristo unaweza kutupatia sisi hakikisho kwamba dhambi sio eneo la kutoweza kurudi. Kurudi salama inawezekana kama tutafuata mpango wa Mungu kwa wokovu wetu” (“Point of Safe Return,” Ensign or Liahona, May 2007, 99).

Jinsi gani hotuba ya Rais Uchtdorf unatoa matumaini kwa wale wanaohisi kuwa wametenda dhambi sana wamekwenda zaidi ya “eneo la kutoweza kurudi”?

Helamani 14

Samweli anatabiri ishara ya kuzaliwa kwa Mwokozi na kifo

Fikiria juu ya tukio iliotokea hivi karibuni nje ya nchi yako na kutambuliwa na dunia yote. Jinsi gani watu hujifunza kuhusu matukio yanayotokea katika maeneo mengine ya dunia, kama vile majanga ya asili na vita? Kwa nini watu hutaka kujua kuhusu matukio yanayotokea katika maeneo mengine ya dunia?

Samweli alitabiri juu ya kuzaliwa kwa Mwokozi na kifo, matukio ambayo yangetokea mbali na Zarahemla. Soma Helamani 14:3–6, na uwekee alama katika maandiko yako ishara ambazo zitaambatana na kuzaliwa kwa Yesu Kristo. SomaHelamani 14:20–27, na uweke alama ishara ambazo zitaambatana na kifo Chake.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika jinsi unafikiri ungefanya kama ungekuwa huko na kusikia Samweli akitoa unabii huu. Kati ya ishara zote zilizopeanwa, ni gani ambayo unafikiri ingekuvutia zaidi juu ya haja ya kutubu?

Ishara hizi ni za kuelimisha na mfano. Wakati Yesu Kristo alipokuja ulimwenguni, mwanga uliongezeka. Alipokufa, giza likaongezeka. Vile vile hufanyika katika maisha yetu tunapomruhusu kuingia mioyo yetu au kumzuia kuingia.

Soma Helamani 14:11–13, na utambue nia ya Samweli au kusudi katika kuwahubiria Wanefi. Unaweza kutaka kuandika katika maandiko yako kile Samweli alitaka Wanefi kujua na kufanya. (Kishazi “kupitia kwa uzuri wake” katika mstari 13 ina maanisha kupitia kwa Upatanisho wa Yesu Kristo.) Kutoka mistari hizi tunajifunza kwamba imani katika Yesu Kristo inaelekeza kwenye toba na ondoleo la dhambi.

Soma Helamani 14:28–29, na uangalie ni kwa nini Bwana hutoa miujiza na maajabu. Ukweli moja tunayojifunza ni: Bwana hutoa ishara na maajabu ili kuwasaidia watu kumwamini Yeye. Tafakari ishara (ushahidi) ambazo unahisi zinakusaidia kuamini katika Yesu Kristo.

Unapojifunza kuhusu ishara zilizotabiriwa na Samweli, ni muhimu kukumbuka kwamba Bwana hutoa ishara ili kuwasaidia watu wenye haki kuamini na kutubu, wakati waovu wakitafuta au kudai ishara kwa sababu zao za kichoyo (ona M&M 46:9). Wakati ishara za kifo cha Bwana au ishara za Ujio Wake wa Pili ni muhimu kujua, mafundisho ya Samweli kuhusu umuhimu wa kifo na ufufuo wa Yesu Kristo ni muhimu kujua.

Soma kwa makini Helamani 14:15–19, na kisha ujifunze mchoro hapa chini.

Picha
dunia na uwepo wa Mungu

Baada ya kusoma Helamani 14:15–19 na kusoma mchoro, fikiria pointi zifuatazo:

  • Kuzaliwa katika dunia kunaweza kuitwa kama kifo cha kiroho kwa sababu tumetengwa kutoka uwepo wa Baba yetu wa Mbinguni.

  • Kupitia kifo Chake na Ufufuo, Yesu Kristo anawakombowa wanadamu wote kutoka kwa Anguko ili tuweze kurudi katika uwepo wa Mungu.

  • Kupitia kwa Upatanisho wa Kristo Yesu, wanadamu wote wanaletwa katika uwepo wa Mungu kuhukumiwa.

  • Wakati wa Hukumu ya Mwisho, watu ambao wanaendelea kukataa kutubu watapitia kifo kingine cha kiroho —kutolewa katika uwepo wa Mungu milele.

  • Yesu Kristo anatukombowa kutoka kifo cha kiroho kwa masharti ya toba.

Wekea alama vishazi katika Helamani 14:15–19 vinavyohusiana na mafundisho muhimu uliyosoma. Hitimisha kwa kusomaHelamani 14:30–31.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kuhusu jinsi ungetumia Helamani 14:30–31 kuelezea rafiki ni kwa nini chaguzi zetu katika maisha haya ni muhimu sana.

  2. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Helamani 13–14 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha