Seminari
Kitengo 5: Siku ya 1, Nefi 20–22


Kitengo 5: Siku ya 1

1 Nefi 20–22

Utangulizi

Katika 1 Nefi 20–21, Nefi alinukuu unabii wa Isaya nabii wa Agano la Kale, ambaye maandiko yake yalikuwa katika mabamba ya shaba ambayo Nefi na ndugu zake walitumwa Yerusalemu kuchukua kutoka kwa Labani. Isaya alifundisha kwamba hata wakati Israeli ya zamani ilipokosa kutii maagano yao, Bwana bado aliwapenda na kuwaalika kutubu na kuja Kwake. Unapojifunza sura hizi, angazia kwa kile Isaya alifundisha kuhusu Yesu Kristo na mapenzi Yake ya kuwakomboa watu Wake.

Picha
Isaya Anaandika kuhusu Kuzaliwa kwa Kristo

1 Nefi 20

Bwana anamrudi Israeli na kuwaalika wao kurudi Kwake

Unaweza kufikiria wakati ambapo ulifanya kitu ambacho hakilingani na maagano ambayo umefanya au na kanuni ya Kanisa? Ulihisi vipi kuhusu uamuzi wako? Soma 1 Nefi 20:1–2 ( “kukaa” katika mstari wa 2 inamaanisha kutegemea). Isaya alikuwa akiongea na nani? Ni nani “nyumba ya Yakobo”?

Katika Agano la Kale, Yakobo alikuwa mwana wa Isaka na mjukuu wa Ibrahimu. Alipewa jina Israeli na Bwana (ona Mwanzo 32:28). “Nyumba ya Israeli” humaanisha uzao wake na wakati mwengine huitwa “nyumba ya Yakobo.” Pia humaanisha muumini wa kweli yeyote katika Yesu Kristo. (Ona Kamusi ya Biblia, “Israel”; ona pia Bible Dictionary, “Israel, Kingdom of.”) Kama vile nyakati ya zamani, wale wanaofanya maagano (kama vile ubatizo) na Mungu leo wanatambulika kama washiriki waagano wa nyumba ya Israeli.

Tafuta 1 Nefi 20:3–4, 8, 18, na uweke mstari chini ya maneno au vishazi vinavyoeleza nyumba ya Isreali haikuwa aminifu kwa Bwana. Kishazi “shingo yako ni msuli wa chuma, na kichwa chako shaba” (1 Nefi 20:4)Kwa mfano inaonyesha hali ambayo maandiko inaita “ukaidi” kila wakati. Elezeo moja la kishazi hiki ni kuwa wanyama kama vile ng’ombe na punda hukaza shingo zao ili wasiweze kuongozwa au kuelekezwa na mabwana zao. Elezeo lingine ni kuwa watu ambao hawataki kuinamisha vichwa vyao ni wakaidi. Vile vile, nyumba ya Israeli walikaza shingo zao kupitia kwa kiburi na uovu na kukataa kuongozwa na Bwana.

Ili kuelewa mistari hizi vyema na kuifananisha kwa siku yetu, fikiria jinsi maelezo haya ya nyumba ya Israeli yanaeleza matendo ya watu wengine leo.

Unaposoma 1 Nefi 20:9–14, 16, tafakari kile mistari hii inafundisha juu ya Bwana na vile Yeye alivyo.

  1. Andika majibu mafupi kwa maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ingawa watu walikuwa waasi zamani, Bwana aliwafanyia nini? Kwa nini?” (Ona 1 Nefi 20:9–11, 14.)

    2. Bwana alitaka watu Wake wa agano kufanya nini? (Ona1 Nefi 20:12, 16.)

Kutoka kwa mistari hii tunajifunza kwamba Bwana anawaalika wale ambao wamekuwa waasi kutubu na kurudi Kwake.Unaposoma taarifa ifuatayo kutoka kwa Rais Dieter F. Uchtdorf wa Urais wa Kwanza, weka mstari chini ya kishazi kimoja ama zaidi ambacho kinathibitisha ukweli huu:

“[Shetani] anataka sisi tuhisi kwamba tumepita msamaha (Ona Ufunuo12:10). Shetani anataka sisi tufikirie kwamba tumefanya dhambi na tukapita ‘eneo la kutoweza kurudi’ —kwamba tumechelewa sana kubadilisha mwelekeo …

“Kristo alikuja kutuokoa. Kama tumechukua mwelekeo mbaya, Upatanisho wa Yesu Kristo unaweza kutupatia sisi hakikisho kwamba dhambi sio eneo la kutoweza kurudi. Kurudi salama inawezekana kama sisi tutafuata mpango wa Mungu kwa wokovu wetu” (“Point of Safe Return,” Ensign or Liahona, May 2007, 99).

1 Nefi 21:1–17

Isaya anatoa unabii kwamba Yesu Kristo hatawasahau watu Wake wa agano.

Katika 1 Nefi 21:1–13, Nefi aliandika mojawapo wa unabii wa Isaya kuhusu Yesu Kristo, ambaye atakuwa Masiya Kristo (neno la Kigriki) na Masiya (neno la Kiebrania) yote yanamaanisha “mpakwa mafuta” au “Mteule wa Pekee.” Yesu Kristo alichaguliwa kuwa Mkombozi wa Israeli na Wayunani.

Unaposoma 1 Nefi 21:6–13, weka alama katika maadiko yako vishazi vile vinavyoelezea Yesu Kristo na kile Atakachofanya kama Mkombozi wa Israeli.

Kama matokeo ya dhambi zao, watoto wa Israeli walijitenga na Bwana na kuhisi kusahaulika na kuachwa Naye (ona 1 Nefi 21:14). Ingawa alihisi kuachwa na Bwana, pekua 1 Nephi 21:14–16ili kupata ushahidi kwamba Bwana anatupenda, na kamwe hatatusahau.Unaweza kutaka kuweka alama kwa vishazi vyovyote katika mistari hii ambavyo ni muhimu kwako.

Picha
Yesu Anaonyesha Makovu Yake

Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Wale Mitume Kumi na Wawili alielezea jinsi Mwokozi alihifadhi makovu ya kusulubiwa Kwake kama ushahidi kwamba hatawahi kutusahau: “Kristo hatawasahau watoto ambao yeye amekomboa au agano aliloweka na wao kwa wokovu katika Sayuni. Vikumbusho vichungu vya huduma [Yake] na maagano ni alama za misumari ya Warumi ilivyochongwa juu ya vigaja vya mikono yake” (Christ and the New Covenant [1997], 84).

  1. Andika majibu mafupi kwa maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Kwa nini unafikiri watu wakati mwengine huhisi kwamba Bwana amewasahau?

    2. Unafikiri inamaanisha nini kuchongwa juu ya vigaja vya mikono ya Mwokozi? Hii inakusaidiaje kushukuru mateso ya Mwokozi msalabani?

    3. Ni uzoefu gani umekusaidia kujua kwamba Bwana hajakusahau?

  2. Fikiria kwamba una rafiki aliyesema kwamba yeye hajihisi mstahiki kuhudhuria kanisa kwa sababu ya dhambi zake za awali. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika barua fupi ya faraja kwa rafiki huyo, ukitumia kile ulijifunza kutoka 1 Nefi 20–21 na taarifa ya Rais Uchtdorf katika sehemu ya kujifunza kwa 1 Nefi 20.

1 Nefi 21:18–22:22

Nefi anaelezea unabii wa Isaya wa kutawanywa na kukusanywa kwa Israeli.

Nefi alijumuisha mojawapo wa unabii wa Isaya kuhusu kukusanywa kwa Israeli katika kumbukumbu yake. Unapatikana katika 1 Nefi 21:18–26. Katika 1 Nefi 22, Nefi alitoa maelezo na ufafanuzi wake wa unabii wa Isaya. Unaposoma 1 Nefi 22:4–12, angalia maelezo ya Nefi ya jinsi Israeli itakusanywa katika siku za mwisho.

Itasaidia kujua kwamba katika Kitabu cha Mormoni neno “Wayunani” humaanisha kila mara watu wasio wa uzao wa Yuda. Kishazi “kazi ya ajabu” humaanisha urejesho wa injili wa siku za mwisho. Pia tambua jinsi Nefi anataja maagano kila wakati—unaweza kutaka kuweka alama haya katika maandiko yako.

Bwana aliahidi kurejesha injili na kuwakusanya Israeli katika siku za mwisho. Weka alama katika maandiko yako kile kitakachofanyika kwa Shetani kwa sababu ya wema wa watu unapojifunza 1 Nefi 22:17, 19–22, 25–28.

  1. Andika yafuatayo mwisho wa kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza1 Nefi 20–22 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha