Kitengo 22: Siku ya 1
Helamani 1–2
Utangulizi
Baada ya jaji mkuu Pahorani kufa, kulikuwa na ubishi mkali miongoni mwa Wanefi kuhusu ni nani kati ya wanawe —Pahorani, Paanchi, na Pacumeni —anayepaswa kuwa jaji mkuu mpya. Pahorani aliteuliwa na watu kama jaji mkuu mpya. Mmoja wa wafuasi wa Paanchi, mtu aliyeitwa Kishkumeni aliyetumika kwa bendi ya siri, alimuua Pahorani, na Pacumeni kisha akateuliwa kama jaji mkuu. Wakichukua fursa ya ubishi na mgawanyiko huu, Walamani waliweza kushinda mji mkuu wa Zarahemla na kuua Pacumeni. Moronihah Jenerali wa Wanefi alimiliki tena mji wa Zarahemla , na Helamani akateuliwa kama, jaji mkuu. Kishkumeni aliuliwa wakati akijaribu kumuua Helamani, na Gadiantoni akawa kiongozi wa bendi ya siri.
Helamani 1
Ubishi juu ya ni nani anayepaswa kuwa jaji mkuu unaruhusu Walamani kushinda Zarahemla, mji mkuu wa Wanefi.
Fikiria mara ya mwisho ulipokuwa na mabishano na mtu au kushuhudia wengine wakiwa na mabishano. Ni matatizo gani yanayosababishwa na ubishi kama huo? Unapojifunza Helamani 1, tafuta matatizo yaliyoletwa na ubishi juu ya Wanefi na utafakari kile unachoweza kujifunza kutokana na uzoefu wao.
Soma vishazi vifuatavyo vya maandiko, na uandike majibu yako kwa maswali katika nafasi zilizopeanwa:
-
Helamani 1:1–4. Ni nini kilichosababisha ubishi na migawanyiko miongoni mwa watu wa Nefi?
-
Helamani 1:5–8. Ni nani aliyeteuliwa jaji mkuu? Nduguze wawili wa jaji mkuu mpya walikumbana vipi?
-
Helamani 1:9–12. Kishkumeni alifanya nini, na ni agano gani Kishkumeni na bendi lake la siri walifanya baina yao?
Wakati huu wa ubishi kati ya Wanefi, mtu aitwaye Koriantumuri aliwaongoza Walamani dhidi ya mji wa Zarahemla katika vita. Soma Helamani 1:18–22, na ubaini kile Walamani waliweza kufanya kama matokeo ya ubishi ya Wanefi.
Moja wapo wa kweli tunazoweza kujifunza kutoka kwa maelezo haya ni: Ubishi hugawanya na hutuhatarisha kwa ushawishi wa adui. Unaweza kutaka kuandika kanuni hii katika maandiko yako karibu na Helamani 1:18.
-
Ili kukusaidia kuelewa kanuni hii vyema, jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Msichana amekuwa akibishana na wazazi wake kuhusu marafiki zake. Jinsi gani ubishi huu unaweza kuathiri tabia yake dhidi ya kusikiliza ushauri wa wazazi wake kuhusu maeneo mengine ya maisha yake?
-
Kijana ana hisia za hasira dhidi ya mtu katika jamii yake ya ukuhani. Jinsi gani ubishi huu unaweza kuathiri jinsi anavyotenda katika kanisa?
-
Fikiria juu ya sehemu katika maisha yako ambapo unahisi kuna ubishi kati yako na watu wengine. Je, ni jambo gani moja maalum unaweza kufanya ili kuondoa ubishi huu kutoka kwa maisha yako? Unawezaje kukamilisha haya?
-
Helamani 1:22 –30 inaeleza kuwa baada ya Walamani kushinda Zarahemla, walianza mara moja kuaandamana kuelekea mji wa Neema ili kuukamata hilo pia. Majeshi ya Wanefi waliweza kuwazingira Walamani na kuwashinda. Walamani wengi waliuawa, na wale waliojisalimisha waliruhusiwa kurudi kwa nchi zao wenyewe.
Helamani 2
Helamani anakuwa jaji mkuu, na wafanyikazi wake wanazuia bendi ya siri kuchukua maisha yake.
Kabla ya kusoma Helamani 2, fikiri jinsi msichana mwaminifu au kijana anaweza kujitahidi kutatua kosa au dhambi. Je, anaweza kujaribu kuuficha au kutafuta msamaha kutoka kwa Bwana na kutoka kwa wale walioathirika?
Baada ya Kishkumeni kumuua Pahorani, yeye na washiriki wa bendi lake la siri waliahidiana kila mmoja kwamba kamwe hawatashtaki mtu yeyote aliyetenda mauaji. Soma Helamani 2:3–4, na uweke maanani kwa kishazi “wameingia katika agano kwamba uovu wake usijulikane na yeyote.” Kisha somaMafundisho na Maagano 58:43, na uangalie jinsi Bwana anataka tutende wakati tumefanya kitu kibaya.
-
Kulingana na masomo yako ya Helamani 2:3–4 na Mafundisho na Maagano 58:43, andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko tofauti kati ya jinsi Bwana anavyotaka tutende tunapotenda dhambi na jinsi Kishkumeni na wafuasi wake walivyotenda.
Helamani akawa jaji mkuu mpya baada ya kifo cha Pacumeni nduguye Pahorani, na kisha Kishkumeni na kundi lake la siri wakaamua kuua Helamani pia. Mtu aitwaye Gadiantoni akawa kiongozi wa kundi la siri kwa wakati huu. Soma Helamani 2:2–9, na uandike katika nafasi hapo chini jinsi Kishkumeni aliuawa:
Soma Helamani 2:10–14, na uangalie kile kilichotokea bendi la Gadiantoni la wezi. Mormoni alionya kuwa makundi ya siri kama wezi wa Gadiantoni, ambao waliitwa “makundi ya siri” (ona, kwa mfano, Helamani 3:23), hatimaye wangesababisha uharibifu wa watu wa Nefi. Manabii wa kale wa Kitabu cha Mormoni pia walionya dhidi ya kuunga mkono makundi ya siri (ona 2 Nefi 26:22; Alma 1:12). Kitabu cha Mormoni kinafunza kanuni hii: Makundi ya siri yanaweza kusababisha uharibifu wa jamii.
Mzee M. Russell Ballard wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alionya kuhusu hatari ya makundi ya siri leo. Unaposoma onyo lake, wekea alama kile tunachoweza kufanya ili kusimama dhidi ya makundi ya siri.
“Kitabu cha Mormoni kinafundisha kuwa makundi ya siri yanayoshiriki katika uhalifu yanatoa changamoto kuu, si tu kwa watu binafsi na familia lakini kwa ustaarabu mzima. Miongoni mwa makundi ya siri ya leo ni magenge, muungano wa wakiritimba wa madawa ya kulevya, na familia za uhalifu zilizopangwa. Makundi ya siri ya siku zetu zinafanya kama vile wezi wa Gadiantoni wa nyakati za Kitabu cha Mormoni. Miongoni mwa madhumuni yao ni ‘mauaji, na kuteka nyara, na kuiba, na kufanya ukahaba na namna yote ya uovu, dhidi ya sheria za nchi yao na pia sheria za Mungu’[Helamani 6:23].
Tusipokuwa waangalifu, makundi ya siri ya leo yanaweza kupata nguvu na uvutio haraka tu na kwa ukamilifu kama vile walivyofanya katika Kitabu cha Mormoni. …
“Kitabu cha Mormoni kinafunza kuwa shetani ndiye ‘mwanzilishi wa dhambi zote’ na mwanzilishi wa makundi hizi za siri[Helamani 6:30]. Kusudi lake ni kuharibu watu binafsi, familia, jamii na mataifa[ona 2 Nefi 9:9]. Kwa kiwango fulani, alifaulu wakati wa Kitabu cha Mormoni. Na anapata ufanisi mwingi sana leo. Hiyo ndio sababu ni muhimu sana kwetu kuchukua msimamo thabiti kwa ukweli na haki kwa kufanya kile tunachoweza ili kusaidia kuweka jamii zetu salama.
[Tunaweza] ‘kusimama kama mashahidi wa Mungu’ kwa kuweka mfano, kuweka viwango vya Kanisa, na kushirikisha ushuhuda wetu na walio karibu nasi [ona Mosia 18:9]” (”Standing for Truth and Right,” Ensign, Nov. 1997, 38).
Fikiria juu ya njia moja au zaidi unaweza kutumia mafundisho ya Mzee Ballard ya kusimama kwa ukweli na haki katika jamii yako na katika nchi yako.
-
Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
Nimejifunza Helamani 1–2na kukamisha somo hili mnamo (tarehe).
Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: