Kitengo cha 8: Siku ya 2
2 Nefi 28
Utangulizi
Nefi alitoa unabii kwamba baadhi ya hali zenye changamoto za siku za mwisho, ikijumuisha mafundisho ya uongo na kiburi cha makanisa ya uongo ambayo yangeanzishwa. Anafunza jinsi ya kutambua mafundisho ya uongo na mitazamo ya kilimwengu na hutambua njia ambazo Shetani anajaribu kuwapotosha wanaume na wanawake kutoka kwa maisha ya haki.
2 Nefi 28:1–19
Nefi anaelezea makanisa ya uongo na mawazo ya uongo ya siku zetu
Katika tamaduni nyingi kuna ishara nyingi za kuwaonya wasafiri wakati kuna hatari yoyote mbele barabarani au mapito. Katika nchi na mji ambapo unaishi, ni umbo gani au rangi za alama za barabarani ambazo zina watahadharisha madereva hatari zilizo mbele?. Vivyo hivyo, sumu na vitu vinginevyo vya hatari huwekwa alama kwa ishara na maonyo kwenye pakiti na vyombo. Vitu hivi vimetiwa alama kwa jinsi gani sehemu unapoishi?
Kama vile hizi ishara za kimwili za maonyo, Kitabu cha Mormoni kina maonyo kukusaidia kuepuka shawishi ambazo zinadhuru roho yako. Rais Ezra Taft Benson alitambua jinsi Kitabu cha Mormoni kinaweza kukuonya na kukuimarisha dhidi ya usanifu wa muovu wa Shetani: “Kitabu cha Mormoni huwafichua maadui wa Kristo. Kinayakanganya mafundisho ya uongo na kushinda ubishi. (Ona 2 Ne. 3:12.) Kinaimarisha wafuasi wanyenyekevu wa Kristo dhidi ya mipango ya hila, mikakati, na mafundisho ya ibilisi katika siku zetu. Aina ya ukengeufu katika Kitabu cha Mormoni ni sawa na aina tuliyonayo leo. Mungu, kwa elimuYake ya kujua kimbele isio na mwisho, vivyo alitengeneza Kitabu cha Mormoni kwamba sisi tuweze kuona makosa na kujua jinsi ya kupambana na mawazo ya uongo ya kielimu, kisiasa, kidini, na kifalsafa ya nyakati zetu (“The Book of Mormon Is the Word of God,” Ensign, Jan. 1988, 3).
Kitabu cha Mormoni kinafichua mawazo ya uongo ya ibilisi na kinatuimarisha dhidi ya mipango yake miovu. Kama ilivyoandikwa katika 2 Nefi 28, Nefi alitaja baadhi ya mafundisho ya ibilisi yaliyo ya kawaida katika vizazi vyote. Pekua 2 Nefi 28:3–9, na uweke alama mafundisho ya uongo na ulaghai wa Shetani uliojifunza hapa. (Kumbuka kwamba 2 Nefi 28:7–9ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza kutaka kukiweka alama kwa njia ya kipeeke hili uweze kukipata hapo siku za usoni.)
-
Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kutoka kwa 2 Nefi 28:3–9 mojawapo wa mafundisho ya uongo unayofikiria yana uharibifu mkubwa kwa vijana leo, na uelezee sababu zako. Pia jumuisha mfano wa jinsi vijana wanaweza kuvutiwa na mafundisho hayo ya uongo.
Soma 2 Nefi 28:12–14, na utafute kile Nefi alionya kitatokea kwa makanisa mengi na watu, hata kwa baadhi ya “wafuasi wanyenyekevu wa Kristo” mstari wa 14). Mambo haya yanasababishwa na kiburi na mafundisho ya uongo uliyosoma kuyahusu katika 2 Nefi 28:3–9. Soma 2 Nefi 28:15–16, 19, na utambue baadhi ya matokeo haya ya mafundisho ya uongo. Unaweza kutaka kuweka alama kishazi katika 2 Nefi 28:19 ambacho kinaelezea nini ibilisi atafanya na wale ambao hawatubu.
Umahiri wa Maandiko—2 Nefi 28:7–9
-
Soma kwa sauti 2 Nefi 28:7–9. Tumia wakati fulani kukariri 2 Nefi 28:8. Unaweza kutaka kuandika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kutoka akilini au utongoe kwa mwana familia au rafiki. Katika siku za mwisho, watu wengi watafundisha mafundisho ya uongo, yasiyofaa na ya kipumbavu. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, orodhesha njia chache haya mafundisho ya kipumbavu yanaendelezwa na kwa kifupi elezea jinsi unaweza kutambua mafundisho ya kipumbavu ya ulimwengu na kuepukana nayo.
2 Nefi 28:20–32
Nefi anaonya dhidi ya udanganyifu wa Shetani
Kama matayarisho ya mafunzo yako ya salio la 2 Nefi 28, soma uzoefu ufuatao wa Rais Boyd K. Packer, Rais ya Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, alipokuwa akitembelea hifadhi ya wanyama akiwa katika kazi katika Afrika:
“Tulisimama katika kidimbwi ili kutazama wanyama wakija kunywa maji. Kulikuwa na ukame sana kipindi hicho na hakukuwa na maji ya kutosha, kulikuwa tu vidimbwi vya matope. …
“Swara, haswa, walikuwa na uoga sana. Wangekaribia kidimbwi cha tope, na ghafla kugeuka na kukimbia kwa uoga mwingi. Niliweza kuona hakukuwa na simba wowote karibu na nikamuuliza mwelekezi kwa nini hawakunywa maji. Jibu lake, na hili ndilo somo, ilikuwa ‘mamba.’
“Nilijua ni lazima ilikuwa anatania na nikamwuliza kwa makini, ‘Tatizo ni nini?’ Jibu tena: ‘Mamba.’
“‘Upuuzi’ nikasema. ‘Hakuna mamba yeyote hapo. Mtu yeyote anaweza kuona hivyo.’ …
“Aliweza kuona sikumwamini na akiwa na dhamira, nadhani, kunifundisha somo. Tulielekea kwenye eneo lingine ambapo gari lilikuwa kwenye ukuta juu ya shimo lenye matope ambapo tungeweza kuangalia chini. ‘Pale,’ alisema. ‘Jionee mwenyewe.’
“Singeweza kuona lolote ila matope, maji kidogo, na wanyama waoga kwa umbali. Kisha yote kwa mara moja nikamwona!—mamba mkubwa, amelala katika matope, akisubiri mnyama mwingine hasiyeshuku kupata kiu ya kutosha ili kuja kunywa.
“Mara nikawa muumini! Alipoona ya kuwa nilikuwa tayari kusikiliza, akaendelea na somo. ‘Kuna mamba kote kwenye mbuga,’ alisema, ‘sio tu katika mito. Hatuna maji yoyote yanayokosa mamba mahali karibu nayo, na ni vyema ujue hayo.’ …
“Katika safari nyingine ya Afrika nilijadili uzoefu huu pamoja na mhifadhi wa mbuga katika mbuga nyingine. …
“Kisha akanionyesha mahali ambapo janga lilitokea. Kijana mdogo kutoka Uiingereza alikuwa akifanya kazi katika hoteli kwa msimu. Licha ya tahadhari za mara kwa mara, alipitia ua la kiwanja ili kuangalia kitu katika maji maangavu ambayo hayakufunika viatu vyake vya tenisi.
“Yeye hakuwa hatua mbili ndani,’ mhifadhi alisema, ‘kabla ya kushikwa na mamba, na hatungeweza kufanya chochote kumwokoa”’ (“Spiritual Crocodiles,” Ensign, May 1976, 30–31).
Kuna hatari gani ya kutilia shaka kuwepo kwa mamba wakati huwaoni? Je! Uzoefu wa Rais Packer na kijana unafanana vipi na kile Nefi alielezea katika 2 Nefi 28:22?
Rais Packer alielezea:
“Wale walio mbele yenu katika maisha wamechunguza kifupi juu ya mashimo ya maji na kuongeza sauti ya onyo kuhusu mamba. Si tu mijusi wakubwa, wenye rangi ya kijivu ambao wanaweza kukuuma vipande vipande, bali mamba wa kiroho, ambao ni hatari zaidi, na wenye udanganyifu zaidi na wasioonekana, hata, kuliko wale wanyama watambaao wajifichao vizuri wa Afrika.
“Hawa mamba wa kiroho wanaweza kuua au kulemaza nafsi zenu. Wanaweza kuharibu amani yenu ya akili na amani ya akili ya wale wanaowapenda ninyi. Hao ndio wale wa kuonywa dhidi yao, na hakuna pahali pa maji katika maisha haya yote sasa pasipojaa tele mamba hao” (“Spiritual Crocodiles,” 31).
Katika mistari ifuatayo, jibu swali lifuatalo: Ni kwa njia gani mamba katika Afrika wanaweza kuwa sawa na majaribu na mbinu za Shetani?
Soma 2 Nefi 28:20–21, 24–26, na utafute njia ambazo Shetani hutafuta kutuangamiza. (Inaweza kusaidia kujua kwamba neno patanisha katika 2 Nefi 28:21 humaanisha kutuliza, kuliwaza, au kukufanya ulale kiroho.) Kulingana na aya hizi, ni mbinu gani Shetani hutumia ili kujaribu kutuliwaza sisi na kutuongoza kwenye nguvu zake? .
Kanuni muhimu iliyofunzwa katika mistari hii ni: Shetani hutumia mbinu nyingi ili kujaribu kutushinda, kama vile kutuchochea hata kwenye hasira na kutuliwaza, na kutuhadaa.
-
Jibu moja au zaidi ya maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Shetani anatumia vipi hasira kudanganya na kuangamiza watu, familia, na jamii?
-
Ni baadhi ya mambo gani mazuri ambayo Shetani amevutia watu kuwa na hasira nayo?
-
Elezea angalau mifano miwili ya jinsi watu fulani wameliwazwa na kupofushwa hadi kwenye hatari za Shetani
-
Soma maelezo yafuatayo kutoka kwa Askofu Richard C. Edgley, mshauri katika Uaskofu Kiongozi, kuhusu mchakato wa polepole ambao Shetani hutumia kututega sisi: “Sisi hatuwezi kusema tutapanda shayiri mwitu chache katika vijana wetu au kwamba tutachovyachovya kidogo pembezoni mwa dhambi. Hakuna pembezoni za dhambi. Kila kitendo, kizuri au kibaya, kina matokeo. Kila kitendo kizuri huboresha uwezo wetu wa kufanya vizuri na kusimama imara zaidi dhidi ya dhambi au kushindwa. Kila kosa, bila kujali udogo, hutufanya kuwa rahisi kushambuliwa zaidi na ushawishi wa Shetani wakati mwingine akitujaribu. Shetani hutuchukua kiasi kwa wakati, akitudanganya kwa madhara ya kile kiitwacho dhambi kidogo mpaka atakapotukamata katika makosa makubwa. Nefi anaelezea mbinu hii kama moja ya kutupatanisha, kutuliwaza, na kutudanganya hadi Shetani ‘atashika na minyororo yake miovu, kutoka ambapo hakuna ukombozi’(2 Ne. 28:22; ona pia v. 21)” (“That Thy Confidence Wax Strong,” Ensign, Nov. 1994, 40).
Shetani hutumia mbinu za kisiri ili kutushawishi sisi kufikiri, kusema, na kufanya makosa. Soma 2 Nefi 28:27–29, na utafute maonyo ya ziada.
Bwana alitoa onyo lingine na baraka, ambayo imejumuishwa karibu na mwisho wa sura hii. Soma 2 Nefi 28:30–32, na utafakari maswali yafuatayo: Kwa nini Mungu anawaita baadhi ya watu wabarikiwa? Je! Kuitikia ushauri wa Mungu kunatusaidia vipi kushinda mbinu za ibilisi?
-
Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kuhusu kile umejifunza kutoka kwa somo hili ambacho kitakusaidia kushinda mbinu za Shetani. Ni baadhi ya sehemu, shughuli, au mitazamo gani unataka kuepuka ili usipatikane na ushawishi wa Shetani?
-
Fikiria kuhusu mazungumzo juu ya ishara za maonyo hapo mwanzo wa somo hili. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, chora ishara ya onyo ambalo linaonyesha hatari ya kiroho unafikiria vijana wanahitaji kutahadharishwa nayo leo. Kuwa tayari kushiri haya na mwalimu wako na washiriki wa darasa.
-
Andika yafuatayo katika sehemu ya chini ya kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
Nimejifunza 2 Nefi 28na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).
Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu: