Utangulizi wa Omni
Kwa nini Ujifunze Kitabu Hiki?
Katika kujifunza kwako kwa kitabu cha Omni, utajifunza kwamba Bwana aliwalinda Wanefi wema na kuwaelekeza wao hadi nchi ya Zarahemla (ona Omni 1:7, 12–13). Kitabu cha Omni pia kinataja makundi mengine—Waamuleki (au watu wa Zarahemla) na Wayaredi, ambao Bwana aliwaongoza hadi nchi ya ahadi.
Nani Aliandika Kitabu Hiki?
Kitabu cha Omni kiliandikwa na watu watano tofauti: Omni, Amaroni, Kemishi, Abinadomu, na Amaleki. Omni alikuwa mwana wa Yaromu na kilembwe cha Lehi na Saria. Omni alijieleza mwenyewe kama “mtu mwovu” ambaye “hakutii amri za Bwana” (Omni 1:2). Amaroni (mwana wa Omni), Kemishi (kaka ya Amaroni), na Abinadomu (mwana wa Kemishi) kila mmoja aliongeza maingizo mafupi. Amaleki mwana wa Abinadomu aliandika sehemu kubwa ya kitabu cha Omni na alikuwa mtu wa mwisho kuandika kwenye mabamba madogo ya Nefi. Alimkabidhi Mfalme Benyamini mabamba hayo.
Kiliandikwa Lini na Wapi?
Watunzi tofauti wa kitabu cha Omni waliandika wakati fulani kati ya miaka 361 Kabla Kristo na miaka 130 Kabla Kristo Watunzi wa kwanza wanne waliandika katika nchi ya Nefi. Amaleki alitengeneza kumbukumbu yake katika nchi ya Zarahemla.