Kitengo cha 10: Siku ya 4
Yaromu na Omni
Utangulizi
Vitabu vya Yaromu na Omni vina maandishi ya mwisho kutoka kwa mabamba madogo ya Nefi. Yaromu alipokea mabamba haya kutoka kwa baba yake, Enoshi, na akaandika masumbuko ya Wanefi na baraka kwa kipindi cha takriban miaka 60. Kisha yeye akampa mabamba haya kwa mwanawe, Omni. Kitabu cha Omni kina maandishi ya waweka kumbukumbu Wanefi watano tofauti na kinahusika na takriban miaka 230.
Yaromu 1:1–15; Omni 1:5–7
Yaromu anaelezea jinsi Wanefi walivyofanikiwa wakati waliposhika amri za Bwana
Ili kujitayarisha kujifunza kanuni muhimu iliyofunzwa katika Yaromu na Omni, soma uzoefu ufuatao ulioshirikishwa na Rais Dieter F. Uchtdorf wa Urais wa Kwanza:
“Nakumbuka wakati nikijitayarisha kujifunza kama rubani wa ndege ya vita. Tulitumia wakati mwingi wa mfunzo yetu ya msingi ya kijeshi katika mazoezi ya mwili. Mimi bado sina uhakika hasa kwa nini kukimbia bila kukoma kulichukuliwa kuwa muhimu kwa sehemu ya matayarisho ya kuwa rubani. Hata hivyo, tulikimbia na tukakimbia na tukakimbi sana zaidi.
“Nilipokuwa nikikimbia nilianza kuona kitu ambacho, hakika, kilinisumbua. Kila wakati nilikuwa ninapitwa na watu ambao walikuwa wanavuta sigara, wanaokunywa pombe, na kufanya kila aina ya mambo ambayo yalikuwa ni kinyume na injili na, hasa, na Neno la Hekima.
“Nakumbuka nikifikiria, ‘Ngoja kidogo! Si mimi ninapaswa kuweza kukimbia na nisichoke?’ Lakini miminilikuwa nikichoka, na nilipitwa na watu ambao kwa kweli hawakuwa wakifuata Neno la Hakima. Nakiri, ilinisumbua wakati huo. Mimi nikajiuliza mwenyewe, ahadi hii ilikuwa ya kweli au siyo?” (“Continue in Patience,” Ensign or Liahona, May 2010, 58).
Je! Wewe umeshashangaa kama au jinsi Bwana angetimiza ahadi Yake kukubariki wewe kwa kuweka amri Zake?
Nabii Yaromu, ambaye alikuwa mwana wa Enoshi, alielezea jinsi ahadi mahususi ya Bwana kwa baba zake ilithibitishwa, kutambulika ni kweli. Soma Yaromu 1:9, na uweke alama ahadi ambayo Bwana alithibitisha kwa watu.
-
Yaromu alionyesha kwamba tunapotii amri ya Mungu, tutafanikiwa. Ili kuona mifano ya ukweli huu, jifunze kila moja ya marejeo ya maandiko hapo chini, na ujibu maswali yanayoambatishwa katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Yaromu 1:4–5, 8. Ni ipi baadhi ya mifano ya jinsi Wanefi walikuwa watiifu na jinsi walibarikiwa?
-
Yaromu 1:7, 10–12. Je! Manabii na viongozi wengine walichukua nafasi gani katika kuwasaidia Wanefi kuwa watiifu na kufanikiwa?
-
Omni 1:5–7. Ahadi ya Mungu baadaye ilithibitishwa vipi katika njia tofauti?
-
Soma kile Rais Uchtdorf alifunza na kushuhudia kuhusu uzoefu wake wa kushangaza kama Bwana atathibitisha ahadi iliyotolewa katika Neno la Hekima: “Jibu halikuja mara moja. Lakini hatimaye nilijifunza kwamba ahadi za Mungu kila mara hazitimizwi haraka au katika njia tunayoweza kutumainia; zinakuja kulingana na wakati Wake na katika njia Zake. Miaka baadaye niliweza kuona wazi ushahidi wa baraka za kimwili ambazo huja kwa wale ambao wanatii Neno la Hekima— kama ziada ya baraka za kiroho ambazo huja mara moja kutokana na utii wa sheria yoyote ya Mungu. Nikitazama nyuma, mimi ninajua kwa hakika kwamba ahadi za Bwana, kama labda sio za upesi kila mara, daima ni za uhakika” (“Continue in Patience,” 58, mlazo umeongezwa).
-
Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, elezea uzoefu wakati Bwana amekubariki au umefanikiwa kwa kuweka amri Zake. Kutoka kwa uzoefu wako, ni nini unaweza kushuhudia kuhusu Bwana na ahadi Zake?
Omni 1:1–30
Waweka kumbukumbu wanasimulia historia ya Wanefi
Uzao wa Yaromu uliandika kitabu cha Omni, ambacho kinahusisha takriban miaka 230. Weka alama majina ya watu tofauti ambao waliweka mabamba madogo baada ya Yaromu. Unaweza kuyapata haya katika Omni 1:1, 4, 9, 10, 12, na 25.
Kitabu cha Omni kinaelezea matukio kadhaa katika historia ya Kitabu cha Mormoni. Unaweza kukumbuka kwamba katika nyakati za Nefi, Wanefi waliwaacha Walamani na kuhamia katika mahali walipopaita nchi ya Nefi. Uhamiaji huu unawakilishwa kwenye ramani kwa mshale kutoka nchi ya urithi wa kwanza hadi nchi ya Nefi.
Soma Omni 1:12–13, na utambue jinsi Wanefi walikuja kuishi katika nchi ya Zarahemla. Unaweza kutaka kuweka mstari vishazi vyovyote katika aya hizi ambavyo vinaonyesha Wanefi walisafiri kwa maelekezo na uwezo wa Bwana. Katika ramani, mshale kutoka nchi ya Nefi hadi nchi ya Zarahemla unashiria uhamiaji huu.
Soma Omni 1:14–19, na utafute mifanano na tofauti kati ya Wanefi na watu waliowapata katika nchi ya Zarahemla.
-
Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Ni kwa jinsi gani ukosefu wa maandiko uliathiri watu wa Zarahemla?
-
Ni kwa jinsi gani kujua hivi kunakusaidia kuhisi shukrani kubwa sana kwa maandiko na kuwa na biidi katika kujifunza?
-
Kitabu cha Omni pia kinatambulisha makundi mawili mengine ya watu ambao wewe utajifunza baadaye katika Kitabu cha Mormoni. Ili kutambua mojawapo wa makundi haya, soma Omni 1:20–22, na uandike neno Wayaredi katika maandiko yako karibu na aya hizi. Koriantumri alikuwa mmoja wa manusura wawili wa mwisho wa taifa la Wayaredi; yule mwingine alikuwa ni nabii Etheri. Utajifunza kuhusu Wayaredi katika kujifunza kwako kwa kitabu cha Etheri.
Ili kujifunza kuhusu kundi la mwisho la watu waliotajwa katika Omni, angalia mshale kwenye ramani ambao unaendelea kutoka nchi ya Zarahemla karibu na nchi ya Nefi na kisha kurudi hadi Zarahemla na mshale kutoka nchi ya Zarahemla ambao unaendelea kote mpaka nchi ya Nefi. Mishale hii inaashiria uhamiaji wa watu wa Zenifu, ambao walitajwa katika Omni 1:27–30. (Unaweza kutaka kuandika “watu wa Zenifu” karibu na aya hizi.) Utajifunza kuhusu kundi hili la watu unapojifunza kitabu cha Mosia
Kitabu cha Mormoni hakidai kuwa ni kumbukumbu ya watu wote ambao waliishi katika Amerika. Licha ya Wayaredi, watu wa Zarahemla, na uzao wa Lehi, kulikiwa na wengine ambao walikuja katika bara la Amerika pia. Rais Anthony W. Ivins wa Urais wa Kwanza alisema katika mkutano mkuu wa Aprili 1929: “Kitabu cha Mormoni … hakituambii kwamba kulikuwa hakuna mtu yeyote hapa kabla ya [watu wa Kitabu cha Mormoni]. Hakituambii kwamba watu hawakuja baada ya hapo” (in Conference Report, Apr. 1929, 15).
Angalia katika Omni 1:23–24 kwamba sehemu ya mwisho ya kitabu hiki iliandikwa na Amaleki. Aliishi wakati wa Mfalme Benyamini, kufautia uhamiaji wa Wanefi hadi nchi ya Zarahemla. Soma Omni 1:25–26, na uweke alama mwaliko ambao Amaleki unautoa mara tatu.
Angalia vile kila mmoja ya miialiko hiyo mitatu ya kuja kwa Kristo katika Omni 1:25–26 inafuatiwa na neno na, pamoja na maelekezo mahususi ambayo yanatusaidia sisi kujua jinsi ya kuja kwa Kristo. Rejea tena kwa Omni 1:25–26, na uweke alama kile Amaleki anatuhimiza sisi tufanye ili kuja kwa Kristo.
Unapaswa kuwa umepata ushauri ufuatao wa jinsi ya kuja kwa Kristo:
-
Amini
-
Shiriki wokovu Wake (pokea baraka za Upatanisho Wake)
-
Itoe nafsi yako yote Kwake (toa moyo wako, hamu zako, na juhudi zako bora—bila kuzuia chochote)
-
Funga na uombe
-
Vumilia hadi mwisho
Amaleki alitoa ahadi hapo mwishoni mwa Omni 1:26 kwa wale wanaofuata ushauri huu. Tafuta ahadi hiyo, na ukamilishe kanuni ifuatayo : Kama tutakuja kwa Kristo na kuvumilia hadi mwisho, sisi .
-
Chagua mojawapo wa vishazi katika ushauri wa jinsi ya kuja kwa Kristo vilivyoorodheshwa hapo juu, na uandike au ufanya ufupisho katika shajara yako ya kujifunza maandiko hotuba ya dakika moja au mbili ukielezea jinsi tunaweza kuja kwa Kristo kwa kutumia kanuni hiyo.
Kwa mfano, unaweza kuandika hotuba yako juu ya jinsi kufunga na maombi yanaweza kutusaidia kuja kwa Kristo. Hotuba yako inaweza kujumuisha (1) kusoma Omni 1:25–26 na kuelezea kwa maneno yako mwenyewe kishazi unachochagua; (2) maandiko ya ziada ambayo yanafafanua au yanaongeza maana kwa kishazi hicho; (3) na uzoefu kutoka kwa maisha yako au maisha ya mtu unayemjua ambao unaonyesha mfano wa kishazi hicho; na (4) mawazo, hisia, na ushuhuda wako.
Mwalimu wako anaweza kukuuliza ushiriki hotuba yako wakati mwingine mtapokutana. Unaweza pia kutaka kushiriki hotuba yako katika jioni ya familia nyumbani au mazingira mengine.
-
Andika yafuatayo mwisho wa kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
Nimejifunza Yaromu–Omni na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).
Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu: