Seminari
Kitengo cha 12: Siku ya 1 Mosia 7–8


Kitengo cha 12: Siku ya 1

Mosia 7–8

Utangulizi

Picha
Mfalme Benyamini Anaukabidhi Ufalme kwa Mosia

Mfalme Mosia alikuwa mwana wa Mfalme Benyamini, ambaye alikuwa mwana wa Mosia wa kwanza aliyetajwa katika Kitabu cha Mormoni. Takriban miaka 80 kabla Mosia kuwa mfalme, mtu aliyeitwa Zenifu aliongoza kundi la Wanefi kutoka Zarahemla kurudi kuishi katika nchi ya Nefi (ona Omni 1:27–30). Mosia 7 inaelezea kwamba Mfalme Mosia alimuidhinisha “mtu mwenye nguvu na shujaa” aliyeitwa Amoni (Mosia 7:3) na kundi dogo kusafiri hadi nchi ya Nefi (wakati mwingine iliitwa nchi ya Lehi-Nefi) na kujua hatima ya kundi la Zenifu. Amoni aligundua uzao wa watu wa Zenifu, ambao sasa walikuwa wanaongozwa na mjukuu wa Zenifu, Limhi. Kuwasili kwa Amoni kulileta matumaini kwa Limhi na watu wake, ambao uovu wao uliwafanya wawekwe katika utumwa kwa Walamani. Mapema, wakati wanajaribu kupata Zarahemla na kuomba msaada, kundi la watu wa Limhi lilipata mabamba 24 ya dhahabu yenye michoro juu yake. Wakati Limhi alipomwuliza Amoni kama angeweza kutafsiri michoro hii, Amoni alielezea kwamba muonaji, kama Mfalme Mosia, angeweza kutafsiri kumbukumbu za kale.

Muhtasari wa Mosia 7–24

Je! Umeshataka kukombolewa kutoka kwa hisia mbaya, hali ya uchungu, mazingira yenye changamoto au udhalimu, ua hatia kutokana na dhambi? Uzoefu wa watu utakaojifunza kuwahusu katika Mosia 7–24 unaweza kukufunkuhusu ukombozi—mahali pa kuutafuta, jinsi ya kuualika, na hata jinsi ya kuungojea. Angalia njia unazoweza kutumia hadithi za watu wa Zenifu na uzao wao katika maisha yako mwenyewe, ikijumuisha hamu ya ukombozi kutoka kwa kitu kinachokufanyia udhalimu.

Kabla ya kujifunza Mosia 7, itakuwa na usaidizi kwako kuwa unafahamu safari tofauti zilizoandikwa katika Mosia 7–24. Shughuli ifuatayo itakupatia muhtasari wa safari hizi, ambazo zilitokea wakati wa kipindi cha takriban miaka 80 (miaka 200 Kabla Kristo hadi miaka 120 Kabla Kristo). Habari katika masanduku yaliyotiwa kivuli kwenye chati inaelezea kile kilitokea katikati ya safari hizo.

Safari

Nani Walisafiri Wapi

1

Zenifu na Wanefi wengine walisafiri kutoka Zarahemla hadi nchi ya Nefi, ambayo ilikuwa imetekwa na Walamani. Wanefi hawa walipigana miongoni mwao wenyewe, na manusura walirudi Zarahemla (ona Omni 1:27–28; Mosia 9:1–2).

2

Zenifu na wengine waliondoka Zarahemla na kufanya makazi katika nchi ya Nefi (ona Omni 1:29–30; Mosia 9:3–7).

Baada ya Zenifu kufa, mwanawe Nuhu alitawala kwa uovu. Bwana alimtuma nabii Abinadi kuwaonya watu watubu. Alma, mmoja wa makuhani wa Mfalme Nuhu, alitii ujumbe wa Abinadi na kuufunza kwa wengine (ona Mosia 11–18).

3

Alma alitoroka hadi Maji ya Mormoni na baadaye kuongoza kundi la waumini hadi nchi ya Helamu (ona Mosia 18:4–5, 32–35; 23:1–5, 19–20).

Walamani waliwashambulia watu wa Nuhu katika nchi ya Nefi. Nuhu baadaye aliuawa, na mwanawe Limhi akatawala. Watu wa Limhi walikuwa katika utumwa kwa Walamani (ona Mosia 19–20).

4

Limhi alituma kundi la Wanefi wakatafute Zarahemla. Baada ya kupotea katika nyika, kundi hili liligundua magofu ya taifa lililoangamizwa na kumbukumbu zilizoandikwa juu ya mabamba 24 ya dhahabu (ona Mosia 8:7–9; 21:25–27).

5

Amoni na wengine 15 walisafiri kutoka Zarahemla ili kutafuta wale ambao walirudi hadi nchi ya Nefi (ona Mosia 7:1–6; 21:22–24).

6

Limhi na watu wake walitoroka kutoka kwa Walamani na waliogozwa na Amoni na ndugu zake hadi Zarahemla (ona Mosia 22:10–13).

Baada ya watu wa Limhi kutoroka, Walamani walituma jeshi liwafuate. Jeshi lilipotea nyikani wakati walipomgundua Alma na watu wake katika nchi ya Helamu. Walamani waliweka katika utumwa. Watu wa Alma waliomba msaada ili watoroke (ona Mosia 22–24).

7

Bwana alimkomboa Alma na watu wake na kuwaongoza hadi Zarahemla (ona Mosia 24:20–25).

Weka nambari ya kila safari katika mviringo unaofaa kwenye ramani”

Picha
mchoro wa safari

Mosia 7:1–8:4

Amoni anagundua nchi ya Nefi (Lehi–Nefi), na Mfalme Limhi anaelezea jinsi watu wake walivyowekwa katika utumwa

Katika Mosia 7, Amoni na wanaume wengine 15 wenye nguvu walisafiri kutoka Zarahemla ili kujua kile kiliwatokea watu ambao Zenifu alikuwa ameongoza hadi nchi ya Nefi miaka 80 mapema (ona Mosia 7:2; ona pia safari ya 5 kwenye ramani). Baada ya kuwasili kwao katika nchi ya Nefi, Amoni na watatu wa ndugu zake walikamatwa na kutupwa gerezani (see Mosia 7:6–11). Baada ya siku mbili walitolewa gerezani na kuhojiwa na Mfalme Limhi, ambaye alikuwa mjukuu wa Zenifu. Soma Mosia 7:12–15 ili uone jinsi Amoni alielezea uwepo wake katika nchi ya Nefi na jinsi Limhi alijibu.

Fahamu kwamba tanbihi b ya Mosia 7:14 inakurejesha kwa Mosia 21:25–26. Soma aya hizi kwa uelewa zaidi kwa nini Limhi alikuwa na “furaha sana” kujua pale Amoni alitokea.

Ukitumia kile umejifunza katika Mosia 21:25–26, kwa kifupi elezea kwa nini Limhi alikuwa na furaha sana kujua kwamba Amoni alikuwa anatokea Zarahemla:

Kundi ambalo Limhi alilituma likatafute msaada lilipata magofu ya taifa la Wayaredi. Kimakosa waliamini ilikuwa ni Zarahemla na kwamba Wanefi pale walikuwa wameangamizwa (ona safari ya 4 kwenye ramani). Utajifunza kuhusu taifa la Wayaredi katika kitabu cha Etheri.

Mfalme Limhi aliwakusanya watu wake ili kumjulisha Amoni kwao. Limhi alizungumza kwa watu wake kuhusu utumwa wao kwa Walamani na kuonyesha matumaini kwamba Mungu angewakomboa karibuni (ona Mosia 7:17–19). Soma Mosia 7:20, 24–26, na uweke alama sababu za kwa nini watu wa Limhi walikuwa wameweka utumwani. (Nabii aliyetajwa katika Mosia 7:26 ni Abinadi, ambaye watu walikuwa wamemchoma hadi kufa wakati wa enzi za Mfalme Nuhu mwovu, kabla ya Amoni kufika katika nchi hiyo.)

Picha
Mfalme Limhi akiongea

Unaweza kutaka kuweka alama kishazi “sababu za kuomboleza kwetu ni kuu” katika Mosia 7:24 ili kukusaidia kukumbuka kwamba uovu, au dhambi, ina madhara yake. Katika hali hii, wengi waliuawa wakati Walamani walipowashambulia na watu wakawekwa utumwani. Kuomboleza humaanisha kuhisi huzuni au majuto. Tafakari kwa dakika kama umeshaomboleza “kwa sababu ya uovu.”

Ingawa ni bora kutotenda dhambi, kujifunza kutoka kwa makosa yako, kumgeukia Mungu kwa usaidizi, na kutubu kutakuleta karibu zaidi na Mungu. Soma Mosia 7:29–32, na utafute ushahidi zaidi kwamba Limhi alielewa mshikamano kati ya uovu wa watu wake na huzuni waliokuwa inawapata. (“Watavuna makapi” katika aya ya 30 humaanisha kupokea kitu kilicho bure; “kuvuna upepo wa mashariki” katika aya ya 31 humaanisha kuangamizwa.)

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni kwa njia gani matokeo ya dhambi yanaweza kuwa na usaidizi katika maisha yetu? Tunaweza kutumia vipi kujifunza kwetu na tusirudie dhambi?

    2. Kwa nini ni muhimu kutambua na kukubali jinsi dhambi zetu zilivyo nzito? Kwa nini ni muhimu kuhisi huzuni ya kiungu kwa sababu yazo? (ona 2 Wakorintho 7:10; huzuni ya kiungu ni kutambua kwa kina kwamba matendo yetu yamemkasirisha Baba yetu aliye Mbinguni). Kwa nini ni muhimu kutochelewesha kutambua na kuhisi huzuni kwa ajili ya dhambi zetu?

Baada ya Limhi kuwaelezea watu wake uzito wa dhambi zao, aliwahimiza wafanye vitu fulani. Weka alama kile Limhi aliwahimiza watu wake wafanye katika Mosia 7:33.

Kutokana na uzoefu wa watu wa Limhi, tunajifunza kwamba kutambua uovu wetu na kuhisi huzuni ya kiungu kwa ajili yake kunaweza kutuelekeza sisi kumgeukia Bwana kwa ukombozi.

Fikiria kwamba rafiki au mwana familia anahisi majuto kwa ajili ya dhambi zake na ana hamu ya uaminifu kutubu na kumgeukia Bwana lakini hana uhakika wa jinsi ya kufanya hivyo. Pekua Mosia 7:33, na urejelee vishazi ambavyo vinafunza jinsi ya “kumgeukia Bwana” kikweli.

  1. Katika shajara yako ya maandiko, andika barua kwa rafiki huyo au mwana familia ukimfundisha jinsi ya kumgeukia Bwana. Shiriki vishazi vitatu kutoka kwa Mosia 7:33 ulivyogundua, na uelezee maana ya kila kishazi aidha (1) ukitumia maneno yako mwenyewe au (2) ukitoa mfano wa yale matendo au mitazamo unayoweza kuona katika maisha ya mtu ambaye anajitahidi kutumia kishazi hicho.

Fikiria ikiwa una dhambi ambazo haujatubu ambazo zinaweza kukusabishia huzuni na majuto kwako na wale unaowapenda. Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alitoa ushauri ufuatao kuhusu kuanzisha mchakato wa toba: “Jifunze na utafakari ili kutathimini jinsi Bwana anavyoelezea uzito wa dhambi zako utakavyo kuwa. Kwamba utaleta uponyaji wa huzuni na majuto. Pia utaleta hamu ya dhati ya mabadiliko na hiari ya kujitolea kwa kila hitaji la msamaha” (“Finding Forgiveness,” Ensign, May 1995, 76).

Mosia 8:5–21

Amoni anapata kujua kuhusu mabamba 24 ya Wayaredi na kumwambia Limhi juu ya muonaji ambaye anaweza kuyatafsiri.

Kumbuka kutoka kwa safari ya 4 kwenye ramani hapo mwanzo wa somo hili kwamba watu waliojaribu kutafuta njia ya kwenda Zarahemla waligundua magofu ya taifa zima ambalo lilikuwa limeangamizwa. Pia walipata mabamba 24 ya dhahabu ambayo waliyachukua hadi kwa Limhi (onaMosia 8:5–9). Limhi alimuuliza Amoni kama alijua mtu yeyote ambaye alikuwa na uwezo wa kutafsiri mabamba hayo. (ona Mosia 8:12). Amoni anaelezea kwamba watu fulani wanaweza kupewa uwezo kutoka kwa Mungu wa kutafsiri. Soma Mosia 8:13, na uweke alama kile Amoni aliwaita wale ambao wamepewa uwezo huu.

Amoni alielezea kwamba Mosia, mfalme Mnefi katika Zarahemla alikuwa muonaji. Pekua Mosia 8:16–18, na uweke alama uwezo muonaji amepewa kama ziada ya uwezo wa kutafsiri.

Mistari hii inafundisha kwamba Bwana hutoa manabii, waonaji, na wafunuaji kwa manufaa ya wanadamu. Leo, kila mshiriki wa Urais wa Kwanza na Jamii ya Mitume Kumi na Wawili ni nabii, muonaji, na mfunuaji.

Mzee Neil L. Andersen wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifunza: “Hawa wanaume 15 tunaowakubali kama manabii, waonaji, na wafunuaji wamepatiwa uwezo mtakatifu wa kuona kile [wengine] wakati mwingine hawawezi kukiona” (“Beware of the Evil behind the Smiling Eyes,” Ensign or Liahona, May 2005, 47).

Picha
ndani ya Kituo cha Mkutano
  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Kwa nini unafikiria ni hekima kusikiliza wale wanaoweza kuona vitu ambavyo hatuwezi kuviona?

    2. Je! Umeshanufaika vipi kutokana na kusikiliza manabii, waonaji, na wafunuaji wa kisasa?

    3. Ni zipi baadhi ya njia unaweza kujifunza kutoka kwa manabii, waonaji, na wafunuaji wa kisasa?

  2. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Mosia 7–8 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha