Kitengo 27: Siku ya 4
3 Nefi 28–30
Utangulizi
Kabla ya kuondoka Kwake, Yesu Kristo aliuliza kila mmoja wa wanafunzi Wake kumi na wawili kile walitaka Kwake. Tisa kati yao waliomba waweze kurudi Kwake haraka wakati huduma yao hapa duniani itakapokamilika. Watatu waliuliza kubakia duniani ili kuendelea kufanya kazi ya kuleta nafsi kwa Kristo mpaka Atakaporudi. Bwana Alikubali tamaa hizi zote za haki. Mormoni alitoa maelezo kadha kuhusu huduma za Wanefi Watatu duniani.
Mormoni alipohitimisha maelezo yake ya ziara ya Mwokozi miongoni mwa Wanefi, alielezea kwamba kutokea kwa Kitabu cha Mormoni kitakuwa ishara kwamba Bwana Alikuwa akitimiza ahadi Yake na nyumba ya Israeli. Kuhitimisha 3 Nefi, Mormoni aliandika maneno ya Yesu Kristo, akiwakaribisha watu wote kutubu na kuhesabiwa pamoja na nyumba ya Israeli.
3 Nefi 28:1–11
Yesu Kristo Anakubali tamaa ya wanafunzi Wake kumi na wawili
Tafakari jinsi unaweza kujibu ikiwa Yesu Kristo alikutokea na kuuliza, “Ni kitu gani ambacho mnahitaji Kwangu?”
Kwa ufupi andika ni gani kati ya tamaa zako za haki ungependa kushiriki Naye.
Soma 3 Nefi 28:1–3, na uangalie jinsi tisa ya wanafunzi Wanefi walijibu wakati Bwana alipouliza, Ni kitu gani ambacho mnahitaji Kwangu? Tambua jinsi Mwokozi alihisi kuhusu matakwa yao.
Soma 3 Nefi 28:4–7, na uangalie kile ambacho wanafunzi watatu walihitaji kutoka kwa Mwokozi. Tambua jinsi Yesu Kristo alihisi kuhusu matakwa ya wanafunzi hawa watatu. Tafakari ni kwa nini unafikiri Bwana alisema “heri zaidi” kwa sababu ya matakwa yao.
Soma3 Nefi 28:8–10 ili kuona jinsi Mwokozi alivyoelezea baraka ambazo Wanefi Watatu wangepokea kwa sababu ya tamaa yao ya kufanya kazi miongoni mwa watu wa dunia. Fikiria kuandika ukweli ufuatao ukiongoni mwa maandiko yako au katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Bwana hutubariki kulingana na tamaa yetu ya haki. Soma taarifa ifuatayo kutoka kwa Mzee Neal A. Maxwell wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili ili kuona umuhimu wa tamaa ya haki:
“Kile tunachotamani kwa lazima, kwa wakati, ndicho kile tutakachokuwa na ndicho tutakachopokea katika milele. …
Tamaa ya Haki yapaswa kuwa thabiti, kwa hiyo, kwa sababu, alisema Rais Brigham Young, wanaume na wanawake, wanaotamani kupata viti katika ufalme wa selestia, watapata kwamba ni lazima wapambane kila siku (in Journal of Discourses, 11:14) (According to the Desire of [Our] Hearts,” Ensign, Nov. 1996, 21–22).
-
Jibu moja ya maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Nilini uliwahi kuhisi kubarikiwa na Bwana ulipotenda kwa tamaa zako za haki?
-
Ni nini utaanza kufanya leo ili kukuza tamaa za haki katika maisha yako mwenyewe ili uweze kuhitimu kwa baraka ya Bwana?
-
3 Nefi 28:12–35
Mormoni anaelezea utume wa Wanefi Watatu
Watu wengi wamesikia hadithi, kisasili, na uvumi kuhusu ziara ya Wanefi hawa Watatu. Badala ya kutegemea hadithi, tambua kile maandiko inasema kuhusu lengo lao na jinsi wanaweza kuhudumu kwa nguvu “kama malaika wa Mungu” (3 Nefi 28:30).
Soma 3 Nefi 28:12–17 ili kujifunza kile kilichotokea kwa Wanefi Watatu. Kwa mujibu wa 3 Nefi 28:15, ilikuwa ni sababu gani moja ya wanafunzi kutaka kupitia mabadiliko haya?
Soma 3 Nefi 28:18–23, ukiangalia jinsi Bwana aliwabariki Wanefi Watatu ili waweze kutimiza tamaa zao zenye haki. Fikiria kile mistari hizi zinatufundisha kuhusu utayari wa Bwana wa kutubariki tunapoishi kulingana na tamaa zetu za haki.
Jifunze3 Nefi 28:25–31, na utambue yule aliyefaidika na yule atakayefaidika kutokana na huduma ya wale Wanefi Watatu. Unaweza kutaka kuwekea alama kile unachopata.
3 Nefi 28:36–40
Mormoni anajifunza kuhusu asili ya viumbe waliotafsiriwa
Fikiria kuhusu wakati ulipokuwa na swali kuhusu injili au changamoto iliyokukabili. Soma 3 Nefi 28:36, na uangalie kile Mormoni hakuelewa kuhusu hali ya kimwili ya Wanefi Watatu baada ya mabadiliko waliopitia. Tafakari jibu lako kwa swali lifuatalo: Ni nani ambaye unamgeukia kila wakati unapokuwa na swali kuhusu Injili? Soma 3 Nefi 28:36–37 ili kujifunza kile Mormoni alifanya ili kupata jibu la swali lake.
Jifunze 3 Nefi 28:37–40, na uangalie kile Mormoni alijifunza kuhusu mabadiliko yaliyotokea kwa miili ya Wanefi Watatu. Hali au uhai uliofurahiwa na Wanefi Watatu unaitwa “mgeuzo,” ambayo ni kama mabadiliko (ona 3 Nefi 28:17) ambayo ni ndefu kwa muda. Viumbe vilivyogeuzwa bado ni vya dunia, lakini, kama vile Nabii Joseph Smith alivyofundisha, miili yao ya kimwili imebadilishwa kutoka hali ya telestia kwa hali ya terestia; wamewekwa huru kutoka kwa mateso ya kimwili ya miili yao ya dunia (ona History of the Church, 4:210). Viumbe vilivyogeuzwa vinaweza kuonekana na kutoweka wanavyotaka na kulingana na mapenzi ya Mungu (ona 3 Nefi 28:27–30). Wanasaidia katika kuleta nafsi kwa wokovu, na wanabakia katika hali ya kugeuzwa mpaka Ujio wa Pili wa Yesu Kristo, wakati watakapopitia mabadiliko mengine ili wawe viumbe vilivyofufuliwa na kutukuzwa (ona 3 Nefi 28:7–8, 39–40).
Kutokana na uzoefu wa Mormoni, tunajifunza kwamba tunapoulizia kutoka kwa Bwana kwa ajili ya uelewa, tutapata ufunuo. Unaweza kutaka kuandika kanuni hii katika maandiko yako au shajara yako ya kujifunza maandiko.
-
Katika shajara yako kujifunza maandiko, andika uzoefu ambayo wewe au mtu unayemjua alitafuta Bwana kwa majibu kupitia kwa maombi ya moyoni.
3 Nefi 29
Mormoni anashuhudia kwamba Bwana atatimiza ahadi Yake na nyumba ya Israeli katika siku za mwisho
Baada ya Mormoni kuandika juu ya ziara ya Mwokozi kwa watu wa Kitabu cha Mormoni, alitabiri kuhusu utimizaji wa ahadi za Bwana katika siku za mwisho. Tafakari jibu lako kwa swali lifuatalo: Ni lini uliwahi kujifunza juu ya au kushuhudia utimizaji wa moja ya ahadi za Mungu?
Fikiria kuwekea alama manenowakati na ndipo unapojifunza 3 Nefi 29:1–3. Maneno haya yatakusaidia kutambua tukio ambalo linaaashiria kuwa Bwana anatii ahadi Zake kwa nyumba ya Israeli katika siku za mwisho. (Kishazi “haya maneno” katika 3 Nefi 29:1 inahusu maandiko ya Kitabu cha Mormoni.)
Tunajifunza kutoka 3 Nefi 29:1–3 kwamba ujio wa Kitabu cha Mormoni ni ishara kwamba Bwana anatimiza maagano Yake na nyumba ya Israeli.
Kitabu cha Mormoni kinatuhakikishia kwamba Bwana anaandaa watu Wake kwa ajili ya ujio Wake (ona 3 Nefi 29:2). Unaposoma taarifa ifuatayo kutoka kwa Mzee Russell M. Nelson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, wekea alama jinsi Kitabu cha Mormoni kinatusaidia kujiandaa kwa ujio wa Mwokozi:
“Kitabu cha Mormoni ni ishara dhahiri kwamba Bwana Ameanza kuwakusanya watoto Wake wa agano la Israeli. …
“Hakika, Bwana hajasahau! Ametubariki pamoja na wengine duniani kote na Kitabu cha Mormoni. Kinatusaidia kufanya maagano na Mungu. Kinatualika kumkumbuka Yeye na kujua Mwanawe Mpendwa. Ni agano nyingine la Yesu Kristo” (“Covenants,” Ensign or Liahona, Nov. 2011, 88).
-
Soma 3 Nefi 29:4–6, na ufanye moja au yote ya shughuli zifuatazo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Tambua vifungu vitatu maalum vya Kitabu cha Mormoni ambavyo unafikiri vinaweza kusaidia mtu mwingine kuja kwa Yesu Kristo. Kwa kila fungu, andika sentensi moja au mbili vinavyoeleza ni kwa nini alichagua kifungu hicho.
-
Andika aya kuhusu jinsi unafikiri Kitabu cha Mormoni kinaweza kusaidia mtu kuelewa na kukubali karama ya ufunuo, unabii, na lugha au uwezo wa Roho Mtakatifu.
-
3 Nefi 30
Bwana anawahimiza Wayunani kutubu na kuja Kwake
Mormoni alihitimisha rekodi yake ya huduma ya Mwokozi kwa kuandika baadhi ya maelekezo maalum alizopokea kutoka kwa Yesu Kristo kuhusu Wayunani. Soma 3 Nefi 30:1–2, na ufikirie kuweka alama mengi ya maelekezo ya Mwokozi kwa Wayunani unavyoweza kupata. Fikiria pia kuwekea alama baraka zinazopatikana kwa Wayunani kama watakuja kwa Kristo. Ingawa 3 Nefi 30:2 imeandikwa kwa wale walio nje ya Kanisa, tunaweza kutumia mwaliko wa Yesu Kristo kupima utayari wetu wenyewe wa kuishi kulingana na mahitaji ya agano Lake.
-
Andika kanuni ifuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:Tunapokuja kwa Kristo, tunaweza kuhesabiwa miongoni mwa watu Wake. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kwa nini ni baraka ya Bwana “kuhesabiwa na watu [wake] ambao ni wa nyumba ya Israeli” (3 Nefi 30:2).
-
Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
Nimejifunza3 Nefi 28–30 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).
Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: