Seminari
Kitengo cha 9: Siku ya 3, Yakobo 1–2


Kitengo cha 9: Siku ya 3

Yakobo 1–2

Utangulizi

Baada ya kifo cha Nefi, Wanefi walianza “kujihusisha na matendo maovu” chini ya utawala wa mfalme mpya (Yakobo 1:15). Ndugu wadogo wa Nefi, Yakobo na Yusufu, walikuwa wamewekwa wakfu na Nefi kama makuhani na walimu wa watu, na kwa bidii walifanya kazi kuwashawishi watu watubu na kuja kwa Kristo. Yakobo alitii amri ya Nefi ya kuandika mafundisho matakatifu, mafunuo, na unabii kwenye mabamba madogo. Mkweli kwa jukumu lake takatifu alilopatiwa, Yakobo aliwaita watu wake kwenye toba, akiwaonya juu ya dhambi za kiburi, kupenda utajiri, na dhambi za uashareti. Aliwafunza kuhusu hatari na matokeo ya dhambi hizi tatu zilizokuwa zimekithiri.

Yakobo 1:1–2:11

Yakobo anawaonya watu juu ya uovu wao

Fikiria kile ungesema katika hali ifuatayo: Mmoja wa marafiki zako Kanisani anaonyesha mtizamo hasi kwa viongozi wake wa ukuhani na anasema, “Hawaonekani kuelewa mambo halisi ya ulimwengu. Wanaendelea kutoa maonyo kuhusu chaguo ambazo sio jambo kubwa. Ningependa wasingetumia wakati mwingi kutwambia sisi vitu vyote vibaya tunavyohitaji kuepuka. Wanafaa tu kuongea kuhusu vitu chanya.”

Picha
Yakobo anafundisha

Fikiria kuhusu kwa nini viongozi wa ukuhani wakati mwingine wanaonya dhidi ya dhambi. Yakobo aliandika kwamba baada ya kifo cha Nefi (ona Yakobo 1:9), watu walianza kujihusisha katika tabia fulani ovu. Soma Yakobo 1:15–16, na utambue kile watu walikuwa wanafanya ambacho kilimsumbua Yakobo.

Unaweza kutaka kuweka duara neno walianza katika Yakobo 1:15–16. Kwa nini ni baraka kuwa na viongozi wa ukuhani ambao wanatuonya kuhusu shida wakati au hata kabla hazijaanza?

Soma Yakobo 1:6–8, na utambue kwa nini Yakobo na viongozi wenzake walikuwa wanawashauri watu wa Nefi dhidi ya dhambi. Kwa nini unafikiria viongozi wa ukuhani katika familia yako, vile vile viongozi wa ukuhani na viongozi wakuu wenye mamlaka, wanawaonya ninyi dhidi ya dhambi na kukufundisha injili kwa bidii jinsi hiyo? Unaweza kutaka kuweka alama vishazi katika Yakobo 1:7 ambavyo vinafunza ukweli ufuatao: Viongozi wa ukuhani wanafanya kazi kwa bidii kutusaidia kuja kwa Kristo.

Soma Yakobo 1:17–19, na utafute sababu zozote za ziada za kwa nini Yakobo na ndugu yake Yusufu walikuwa wanafanya kazi kwa bidii jinsi gani kuwafunza watu.

Unafikiria inamaanisha nini kupokea “wito kutoka kwa Bwana” (Yakobo 1:17)?

Unaweza kutaka kuweka alama vishazi vyovyote vingine ambavyo vinasaidia kufundisha kanuni ifuatayo: Viongozi wa ukuhani wana jukumu takatifu walilopewa la kufunza neno la Mungu na kuonya dhidi ya dhambi.

Tafakari kwa muda kuhusu kwa nini ni muhimu kuelewa kwamba viongozi wa Kanisa wanawajibika kwa juhudi zao za kutufundisha kile Bwana anataka sisi tujue.

Unaposoma Yakobo 2:1–3, 6–7, 10–11, tafuta vishazi ambavyo vinaonyesha jinsi Yakobo alihisi kuhusu kazi ngumu ya kuwaita watu wake kwenye toba.

  1. Fikiria kuhusu kile vishazi vifuatavyo vinakufunza kuhusu motisha ya Yakobo ya kukamilisha kazi yake ngumu: “siku ya leo nimelemewa sana kwa hamu na wasiwasi wa ustawi wa nafsi zenu. (Yakobo 2:3) na “Mimi lazima nitende kulingana na amri kali za Mungu” (Yakobo 2:10). Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko mjibizo wa maswali yafuatayo:

    1. Ni wakati gani ulihisi upendo na kujali kwa viongozi wa ukuhani kwako?

    2. Ni wakati gani wewe ulihisi maneno au matendo ya viongozi wa ukuhani yameongozwa na Mungu ili kukusaidia wewe?

Fikiria tena juu ya hali iliyowasilisha hapo mwanzoni mwa somo hili. Fikiria kuhusu jinsi wewe ungemjibu rafiki yako kulingana na kile umejifunza leo.

Yakobo 2:12–21

Yakobo anawarudi watu wake kwa ajili ya kiburi chao

Ili kukusaidia kujitayarisha kujifunza kile Bwana alimwamuru Yakobo afunze, fikiria kuhusu baraka Bwana amekupatia katika maeneo yafuatayo: familia, marafiki, viongozi wa Kanisa na walimu, vipaji vya sanaa na muziki, ujuzi wa riadha, talanta, kisomo, nafasi za kukua, elimu ya injili, na mali. Fikiria njia zingine Bwana amekubariki.

Soma Yakobo 2:12–13, na utambue kile Wanefi walikuwa wanatafuta. Kumbuka kwamba Yakobo alifunza kwamba “mkono wa majaliwa” ulikuwa umewabariki Wanefi kwa utajiri. Kishazi hiki kinalenga Baba yetu aliye Mbinguni.

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kwa nini ni muhimu kwako kukumbuka kwamba Bwana amekupatia baraka na uwezo ulionao.

Ikiwa sisi si makini, tunaweza kujiruhusu wenyewe kuinuliwa juu kwa kiburi baada ya kupokea baraka tunazotafuta, kama walivyofanya Wanefi. Katika nafasi iliyotolewa, andika kile unafikiria inamaanisha “kuinuliwa juu katika kiburi cha mioyo yenu.”

Kama ilivyoandikwa katika Yakobo 2:13, Yakobo alisema nini zilikuwa sababu kadhaa za kiburi chao?

Fikiria mtu wa kisasa au kundi la watu ambao wanawatendea vibaya, kuwapuuza, au kuwatesa wengine kwa sababu “wamepata mengi zaidi” kuliko wale wanaotendea vibaya (Yakobo 2:13). Kwa mfano, kwa sababu watu fulani wana pesa nyingi, marafiki wengi, uwezo zaidi wa riadha, au hata elimu kubwa ya injili kuliko mtu mwingine, wanaweza kimakosa kufikiria wao ni bora kuliko wengine au hata kuwatesa . Tafakari kama kumekuwa na wakati katika maisha yako wakati wewe umetenda katika njia ya kiburi.

Soma Yakobo 2:17–21, na uweke alama vishazi ambavyo vinaweza kukusaidia kushinda kiburi.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika vishazi viwili au zaidi ambavyo umevipata katika Yakobo 2:17–21, na uelezee jinsi vishazi hivyo vinaweza kukusaidia kushinda kiburi. Baadhi ya maswali yafuatayo yanaweza kuwa ya msaada kuyafikiria unapokamilisha kazi hii:Unafikiri inamaanisha nini kutafuta ufalme wa Mungu? Kupata tumaini katika Kristo? Kutafuta ufalme wa Mungu na kupata tumaini katika Kristo kunaweza kuathiri vipi jinsi unavyowaona na kuwafanyia wengine?

Fikiria kwamba mama yako, baba yako, au kiongozi wako alikuuliza kile wewe unajifunza leo. Andika chini kanuni moja kutoka kwa Yakobo 2:17–21 ambayo unaweza kutumia kuwajibu wao.

Kanuni moja katika Yakobo 2:17–21 ni: Tunapaswa kutafuta ufalme wa Mungu badala ya vitu vingine vyote.

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko njia moja unayoweza kutumia baraka na nafasi ambazo Bwana ametoa kwenu ili kusaidia kujenga ufalme wa Mungu na kubariki maisha ya wengine.

Yakobo 2:22–30

Yakobo aliwarudi watu wake kwa dhambi ya uasherati

Kauli ifuatayo ilitolewa na Rais Ezra Taft Benson. Bahatisha ni maneno gani mawili yanayoweza kuingia katika mapengo:

“Dhambi inayopotosha ya kizazi hiki ni ” (“Cleansing the Inner Vessel,” Ensign, May 1986, 4; angalia mwisho wa somo hili kwa majibu sahihi).

Soma Yakobo 2:22–23, 28, na uweke alama vishazi Yakobo alitumia kuelezea uzito wa dhambi ya uasherati. Inaweza kusaidia kuelewa kwamba neno uasherati humaanisha dhambi ya uzinzi.

Picha
Mzee Richard G. Scott

Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili anaelezea baadhi ya matendo ambayo yanavunja sheria ya usafi wa kimwili ya Bwana: “Kujamiiana nje ya kifungo cha ndoa—mimi namaanisha kwa makusudi kushika sehemu takatifu, sehemu za siri za mwili mwingine, akiwa au bila kuwa na nguo—ni dhambi na imekatazwa na Mungu. Pia ni uvunjaji sheria kimakusudi kuamsha hisia hizi katika mwili wako mwenyewe” (“Making the Right Choices,” Ensign, Nov. 1994, 38).

Matendo ya kishoga na kutazama picha za ngono pia inavunja sheria ya Bwana ya usafi wa kimwili.

Kumbuka jinsi Wanefi walivyotafuta kujitetea dhambi zao, kama ilivyoandikwa katika Yakobo 2:23–24. Chukua dakika ufikirie kuhusu jinsi watu wanavyotafuta kujitetea katika uashareti leo.

Mojawapo ya dhambi za Wanefi ilikuwa ni desturi isiyoidhinishwa ya ndoa za mitalaa. Yakobo alifunza amri za Bwana kwamba mwanaume anapaswa kuoa mwanamke mmoja tu (ona Yakobo 2:27). Kuwa na zaidi ya mwanamke mmoja bila idhinisho la Bwana kupitia viongozi Wake wateule wa ukuhani ni mfano wa dhambi ya uasherati. Katika macho ya Mungu, dhambi ya uasherati ni nzito sana (ona Alma 39:5).

Watu wa Bwana wanaidhinishwa kuwa na ndoa ya mitalaa tu wakati Bwana ameamuru (ona Yakobo 2:30). Wakati fulani katika historia ya ulimwengu, Bwana aliamuru watu Wake kuwa na ndoa ya mitalaa. Kwa mfano, ndoa ya mitalaa ilifanyika katika nyakati za Agano la Kale na Ibrahimu na Sera (see Mwanzo 16:1–3; M&M 132:34–35, 37) na mjukuu wao Yakobo (ona M&M 132:37), na pia ilifanyika kwa muda nyakati za siku za mwanzo wa Kanisa lililorejeshwa, kuanzia na Nabii Joseph Smith (ona M&M 132:32–33, 53). Hata hivyo, Mungu alimwamuru nabii Wake Wilford Woodruff kusitisha ndoa ya mitalaa (ona Tamko Rasmi 1 katika Mafundisho na Maagano).

Soma Yakobo 2:31–35, na uweke alama vishazi vinavyoonyesha baadhi ya matokeo hasi ya dhambi ya uzinzi.

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Kulingana na Yakobo, dhambi ya uasherati inathiri familia vipi?

    2. Baadhi ya vijana wanaweza kujitetea kwamba wanaweza kuwa wazinzi kwa sababu wao hawajaoa na, kwa hivyo, wao sio wasiowaaminifu kwa wenzi wao, na wao hawana watoto. Je! Uasherati unaweza kuathiri kijana na familia yake vipi?

    3. Kwa nini unafikiria Bwana anachukulia uasherati kama dhambi nzito?

Rejea mwanzo wa Yakobo 2:28, na uweke alama kile Bwana hufurahishwa nacho. (Kumbuka kwamba Yakobo anataja wanawake hasa katika aya hii, ni kweli kabisa kwamba Bwana hufurahia na usafi wa kimwili wa wanaume.) Aya hii hufunza kanuni hii: Bwana hufurahia katika usafi wa kimwili.

Kulingana na kile ulichojifunza leo, fikiria kwa nini Bwana hufurahia katika usafi wa kimwili wa watoto Wake. Fikiria kuhusu familia yako, vile vile familia unayotumainia katika siku za usoni. Ni kwa jinsi gani kuishi kulingana na sheria ya Bwana ya usafi wa kimwili hukubariki wewe na wao? Tafakari jinsi chaguo unazofanya kuwa msafi kimwili na msafi humfurahisha Bwana.

Unaweza kubakia msafi. Kama tayari umeshatenda dhambi dhidi ya sheria ya usafi wa mwili, unaweza kutubu na kuwa msafi kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo. Tafuta mwongozo wa Roho Mtakatifu unapofikiria njia moja au zaidi unazoweza kujilinda vyema dhidi ya kuvunja sheria ya usafi wa kimwili. Kama umefanya uasherati wowote, fanya chochote kinachohitajika,ikijumuishaa kukutana na askofu wako au rais wa tawi, kukiri kile umefanya katika kuvunja sheria ya Bwana ya usafi wa kimwili.

Picha
Ee Baba Yangu
  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Yakobo 1–2 na kukamisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu:

Jibu la maneno yanayokosekana katika dondoo iliyopo mwanzoni mwa somo hili: Rais Benson alisema, “Dhambi inayopotosha ya kizazi hiki nidhambi ya uasherati.

Chapisha