Seminari
Kitengo 27: Siku 2, 3 Nefi 24–26


Kitengo cha 27: Siku ya 2

3 Nefi 24–26

Utangulizi

Katika 3 Nefi 24–25, Yesu Kristo alitimiza amri ya Baba wa Mbinguni ya kuwapa watu baadhi ya unabii wa Malaki. Malaki alikuwa ametangaza haja ya nyumba ya Israeli kutubu na kurudi kwa Bwana kwa maandalizi ya ujio wa Mwokozi. Kama ilivyoandikwa katika 3 Nefi 26:3, Yesu Kristo aliwaeleza watu “vitu vyote, hata kutoka mwanzo mpaka wakati ambao angekuja katika utukufu wake.” Mormoni kisha akafundishwa kwamba wale ambao wanaamini Kitabu cha Mormoni watapata kudhihirishiwa vitu vikubwa zaidi(ona 3 Nefi 26:9).

3 Nefi 24:1–6

Yesu Kristo ananukuu maneno yaliyotolewa na Malaki kuhusu Ujio wa Pili

Ujio wa Pili

Alipokariri baadhi ya unabii wa Malaki kwa Wanefi, Yesu Kristo alirejea mifano ya moto na sabuni. Fikiria moto unaon’gaa na kipande cha sabuni. Fikiria juu ya jinsi vitu hivi viwili vinavyofanana kama vyombo vya kutakasa au kusafisha.

Soma 3 Nefi 24:2–3. Katika 3 Nefi 24:2, Yesu Kristo Analinganishwa na moto wa msafishaji na sabuni ya dobi kwa sababu ya kile Atakachofanya wakati wa Ujio Wake wa Pili. Katika 3 Nefi 24:3, Analinganishwa na mfua fedha, anayetakasa fedha. Ili kuelewa mistari hizi, ni muhimu kujua kwamba utaratibu wa kusafisha fedha unahitaji mfua fedha kushikilia kipande cha fedha juu ya sehemu kali ya moto ili kuchoma uchafu. Mfua fedha ni lazima atazame fedha kwa karibu, kwa maana kama fedha itakaa kwa muda mrefu mno katika moto, itaharibiwa. dobi ni mtu anayesafisha mavazi au kuyang’arisha kwa kutumia sabuni. “Wana wa Lawi” walikuwa wale ambao walioshikilia ukuhani katika Israeli ya kale; neno hili linaweza kutumika kwa watu wote wa Bwana leo.

Tafakari kile picha hiki kinaonyesha kitafanyika katika Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Katika maandiko yako karibu na 3 Nefi 24:2–3, unaweza kutaka kuandika: Wakati wa Ujio Wake wa Pili, Yesu Kristo atawatakasa watu Wake.

Soma 3 Nefi 24:5–6, na utambue ni nani atachomwa na ni nani hatachomwa au kuharibiwa wakati wa ujio wa Mwokozi. (Kumbuka kwamba katika kifungu hiki “wana wa Yakobo” ni watu wa agano wa Bwana katika nyumba ya Israeli.) Mistari hizi zinafundisha kanuni:Yesu Kristo atawahukumu waovu wakati wa ujio Wake.

  1. ikoni ya shajaraAndika vichwa vifuatavyo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Kile lazima nifanye ili kujiandaa kwa Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Unapoendelea kujifunza 3 Nefi 24–26, orodhesha chini ya kichwa hiki kile unachojifunza ambacho kitakusaidia kujiandaa kwa Ujio wa Pili wa Yesu Kristo.

3 Nefi 24:7–18

Malaki anafundisha nyumba ya Israeli jinsi ya kurudi kwa Bwana

Fikiria kwamba rafiki wa karibu au mwanafamilia haionekani kujali jinsi matendo ya mtu yanaweza kumwathiri wakati wa Hukumu, Ujio wa Pili, au katika umilele. Fikiri kuhusu kile unaweza kusema ili kujaribu na kumsaidia huyu mtu. Soma 3 Nefi 24:7, na ubaini kile Bwana aliwaambia wana wa Yakobo waliokuwa wameanza kupotea kutoka Kwake. Unafikiri ina maanisha nini kwamba watu walikuwa “wamegeuka upande” kutoka kwa maagizo ya Bwana?

Katika Kanisa, ibada ni kitendo kitakatifu, rasmi, kinachofanywa na mamlaka ya ukuhani. Ibada nyingine ni muhimu kwa kuadhimishwa kwetu. Maagizo hizi zinaitwa “ibada za kuokoa.” Zinajumuisha ubatizo, uthibitisho, uteuzi kwa Ukuhani wa Melkizedeki (kwa wanaume), endaomenti ya hekalu, na ufungaji wa ndoa. Kwa kila moja ya maagizo hizi, tunaingia katika maagano ya dhati na Bwana. Unaweza kutaka kuorodhesha maagizo ya kuokoa chini ya kichwa katika zoezi la shajara 1. Fikiria jinsi maagizo hizi zinaweza kutusaidia kujiandaa kwa Ujio wa Pili.

Ingawa watu wa Bwana walikuwa wamepotea kutoka kwa ibada na maagano ya injili, tambua ahadi katika 3 Nefi 24:7, ambayo Bwana aliwapa kama wangeweza kurudi Kwake. Unaweza kutaka kuweka alama kwenye ahadi hii katika maandiko yako ili kukusaidia kukumbuka kwamba tukirudi kwa Bwana, Atarudi kwetu.

Soma3 Nefi 24:8–10, na uangalie njia moja ambayo kwayo Bwana alieleza kwamba wana wa Yakobo wanaweza kurudi Kwake na hivyo kujiandaa kwa Ujio Wake wa Pili. Unaweza kutaka kujumuisha kulipa zaka na sadaka katika orodha chini ya kichwa katika zoezi la 1 la shajara.

Soma shauri lifuatalo kutoka kwa Rais Gordon B. Hinckley kuhusu kulipa zaka: “Tunaweza kulipa zaka zetu. Hii si sana suala la fedha kwani ni suala la imani”(“Let Us Move This Work Forward,” Ensign, Nov. 1985, 85).

Tafakari kwa muda jinsi nia yako ya kutoa zaka na sadaka kwa Bwana ni ishara ya imani yako Kwake. Soma 3 Nefi 24:10–12, na ulenge juu ya baraka kwa wale wanaolipa zaka kamili na aaminifu.

  1. ikoni ya shajaraJibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni baraka gani umepokea kutoka kwa utii kwa sheria ya kutoa zaka?

    2. Unafikiri kutunza amri ya kulipa zaka yako na sadaka imekusaidiaje kujiandaa kiroho kwa Ujio wa Pili?

Watu wengine katika Israeli ya kale walinung’unika kwamba kushika amri za Bwana hazikuwafanyia yoyote mazuri. Walihisi kwamba juhudi zao zilikuwa bure, au bila maana(ona 3 Nefi 24:14). Kwa upande mwingine, walisema kwamba wenye kiburi na waovu walikuwa na “heri”, “kunufaika,” na “wanaookolewa”(3 Nefi 24:15). Kwa maneno mengine, watu hawa walidai kwamba waovu walikuwa bora zaidi kuliko wenye haki. Bwana alijibu malalamishi haya kwa kusema kwamba wale wanaomcha Bwana na kulitafakari jina Lake, na wanaokutana pamoja kila mara ili kusemezana wao kwa wao, watapata majina yao yameandikwa katika “kitabu cha ukumbusho”(3 Nefi 24:16). Watakuwa ndio wale waliotayarishwa kwa Ujio wa Pili wa Bwana na kuwaachiliwa kama “vito” vyake vyenye thamani (ona 3 Nefi 24:16–17). Bwana aliwarai waliokuwa wakilalamika kusubiri na kuona matokeo ya mwisho “watakaporudi na kupambanua miongoni mwa yule amtumikiaye Mungu na yule asiyemtumikia” (3 Nefi 24:18). Wataona kwamba wenye haki ni bora zaidi mwishowe.

3 Nefi 25

Yesu Kristo ananukuu unabii wa Malaki kwamba Eliya atarudi kabla ya Ujio wa Pili

Eliya Anarejesha Funguo za Uwezo wa Kuunganisha za Ukuhani

Soma 3 Nefi 25:1–3, na uangalie ni kwa nini Ujio wa Pili utakuwa baraka kwa wale ambao ni waaminifu kwa Yesu Kristo. Neno shina katik amstari 1 inahusu mababu, na tawi inahusu vizazi. Hivyo, katika maisha ijayo waovu hawatafurahia baraka za kufungwa kwa mababu zao au vizazi vyao. Ndama “zinazokua … zizini” ni ishara ya watoto waliolindwa, kutunzwa, na wenye vitu vyote muhimu kwa ajili yao wanapokua.

Mwokozi alishiriki pamoja na Wanefi kile Malaki aliandika juu ya tukio ambalo lingetokea kabla ya Ujio wa Pili na litahusisha nabii Eliya wa Agano la Kale. Soma 3 Nefi 25:5–6, na uangalie kile Malaki alifundisha kwamba Eliya atafanya ili kusaidia kuandaa ulimwengu kwa ujio wa Bwana.

Kurudi kwa Eliya duniani lilikuwa sehemu muhimu ya Urejesho wa injili. Mnamo Aprili 3, 1836, Eliya alimtokea Joseph Smith na Oliver Cowdery katika Hekalu jipya la Kirtland lililowekwa wakfu(onaM&M 110). Aliwatunukia uwezo wa kuunganisha wa ukuhani, na kuziwezesha familia kuungana katika vizazi vyote. Unafikiri taarifa kwamba “Na atageuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao”(3 Nefi 25:6) ina maana?

Mistari hii inafundisha kwamba jinsi mioyo yetu inavyogeuzwa kwa baba zetu, tunasaidia kuandaa ardhi kwa Ujio wa Pili wa Yesu Kristo.

  1. ikoni ya shajaraAndika katika shajara yako ya kujifunza maandiko uzoefu ambayo wewe au wanafamilia yako wamepata ambayo imekusaidia kugeuza moyo wako kuelekea kwa mababu zako. Hii inaweza kujumuisha kufungwa katika hekalu takatifu, kutafiti historia ya familia yako, au kushiriki katika ubatizo kwa ajili ya wafu. Kama huwezi kufikiria juu ya uzoefu, andika aya fupi kuhusu hamu yako ya kushiriki katika kazi hii. (Chini ya zoezi la shajara 1, unaweza kutaka kuandika: kupokea maagizo ya hekalu kwa ajili yako na familia yako, kuhudhuria hekalu, na kukusanya habari ya historia ya familia.)

3 Nefi 26

Kile lazima kifanyike ili kupokea vitu vikubwa ambavyo Yesu Kristo alifunua

Tunajifunza kutoka 3 Nefi 26:3 kwamba Mwokozi aliwafundisha Wanefi “vitu vyote ambavyo vingekuja juu ya uso wa dunia.” Soma 3 Nefi 26:6–8, ukiangalia ni kiasi gani ya mahubiri ya Mwokozi iliandikwa katika Kitabu cha Mormoni. Jifunze 3 Nefi 26:9–11ili ujue ni kwa nini Mormoni hawakujumuisha kila kitu.

Bwana ameamuru Mormoni kujumuisha sehemu kidogo tu ya mafundisho hayo ili kujaribu imani yetu. Kutoka kwa 3 Nefi 26:1–21tunajifunza kwamba tunapoamini kile Mungu amefunua, tunajiandaa kupokea ufunuo zaidi. Kwa nini unafikiri kuamini kweli ambazo tayari tumepokea ni muhimu kabla ya kupokea ukweli zaidi? (Ona Alma 12:9–11.) Tunawezaje kuonyesha kwamba tunaamini kile Bwana amefunua?

  1. ikoni ya shajaraIli kutumia kanuni muhimu hapo juu, jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Unafanya nini katika maisha yako ili kuonyesha imani yako katika Kitabu cha Mormoni?

Kama ilivyoandikwa katika salio la 3 Nefi 26, Mormoni alifupisha huduma ya Mwokozi na athari zake kwa Wanefi. Soma 3 Nefi 26:13–21, na ufikirie kuwekea alama jinsi watu walivyoweka maneno ya Yesu Kristo kwa matendo.

  1. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza3 Nefi 24–26 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: