Seminari
Kitengo cha 20: Siku ya 3, Alma 42


Kitengo cha 20: Siku ya 3

Alma 42

Utangulizi

Alma alihitimisha ushauri wake kwa mwanawe Koriantoni anayekuwa anasumbuka kwa kueleza kwamba Baba wa Mbinguni hutoa njia kwa wale wanaotenda dhambi ili kupata huruma. Alimfundisha mwanawe juu ya adhabu ambayo sheria ya haki inadai kwa ajili ya dhambi. Kisha alishuhudia kwamba Yesu Kristo “atawezesha mahitaji ya haki” (Alma 42:15) kwa kuteseka kwa wote waliofanya dhambi na waliotayari kutubu. Bwana hutoa huruma kwa anayetubu (mwenye toba).

Alma 42:1–14

Alma anamfundisha Koriantoni kuhusu sheria ya haki

Funga macho yako kwa dakika moja na utafakari jinsi itakavyokuwa wakati ukifika kwa Hukumu ya Mwisho yako. Unapokagua maisha yako, unataka Hukumu ya Mwisho iwe ya haki? Kwa nini unataka hukumu yako iwe ya haki?

Sasa, fikiria kile neno haki humaanisha. Moja ya ufafanuzi wa haki inajumuisha kupata kile unastahili; wazo la haki linahusiana na neno la maandiko haki.

Picha
sawazisha mizani
  1. Chora seti za mizani rahisi katika shajara yako ya kujifunza maandiko kama vile inavyoonekana hapa. Kisha andika neno Haki chini ya mchoro wako. Acha nafasi katika shajara yako ili kujumuisha vitambulisho vingine kwenye mchoro wako unapoendeleza somo.

Ili kukusaidia kuelewa dhana ya haki vyema, soma maelezo yafuatayo kutoka kwa Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:

Picha
Mzee Dallin H. Oaks

Haki ina maana nyingi. Moja ni usawa. Ishara maarufu ya haki ni mizani katika usawa. …

“… Wazo la haki kama vile mtu anavyostahili ni nguzo ya msingi ya maandiko yote ambayo inazungumza juu ya wanadamu kuhukumiwa kulingana na matendo yao” (“Sins, Crimes, and Atonement” [address to CES religious educators, Feb. 7, 1992], 1).

Koriantoni mwanawe Alma alikuwa na wasiwasi kuhusu haki ya Hukumu ya Mwisho. Soma Alma 42:1, na uweke alama kile Koriantoni alidhani kitakuwa si haki au dhuluma kuhusu Hukumu ya Mwisho.

Kumbuka kwamba Koriantoni alitenda dhambi mbalimbali, nyingine ambazo zilikuwa mbaya sana (angalia Alma 39:2–3); kwa hiyo, Koriantoni huenda alitaka au alitumaini kwamba haikuwa haki kwa wale waliofanya dhambi kuadhibiwa.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika ni kwa nini unafikiri wale ambao hawajatubu dhambi zao watakuwa na wasiwasi ya kupokea “kile mtu anastahili” wakati wa hukumu.

Katika Alma 42:2–11, Alma alishughulikia wasiwasi wa Koriantoni kwa kueleza kwamba Kuanguka kwa Adamu kulileta kifo cha kimwili (utengano wa mwili na roho wakati wa kifo cha mwili) na kifo cha kiroho ( kutengwa na Mungu kwa sababu ya dhambi). Hivyo ilikuwa muhimu kwamba mpango uundwe ili kumkomboa mwanadamu kutoka kwa hali yao ya kuanguka. Vinginevyo watu wote wangebakia katika hali ya dhambi na kuhuzunika milele kulingana na mahitaji ya haki.

Soma Alma 42:12, na utambue kilichosababisha watu kuingia katika hali yao ya kuanguka. Sasa soma Alma 42:14, na uweke alama matokeo ya kutokutii kwetu ambako kunahitajika na haki. Kwenye picha ya mizani ambayo ulichora katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika Ukiukaji— ukaidi au dhambi chini ya mizani ya kushoto Adhabu — kutengwa kutoka uwepo wa Mungu chini ya mizani ya wa kulia.

  1. SomaAlma 42:18. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, jibu maswali yafuatayo:

    1. Unafikiri inamaanisha nini kuwa na “majuto ya dhamiri” (Alma 42:18)?

    2. Majuto ya dhamiri inaweza kutuongoza kufanya nini?

Kutokana na kile Alma alifundisha, sheria ya haki inahitaji nini wakati mtu ni mkaidi? (Kwa sababu ya kutokutii kwetu, sheria ya haki inahitaji kwamba tupitie majuto na kutupwa mbali na uwepo wa Mungu.) Tafakari kwa muda ulipoona majuto na huzuni au kujiondoa kwa Roho Mtakatifu kwa sababu ya kitu ulichokosea. Fikiria hisia hiyo ikijazwa na kila kitu umewahi kufanya vibaya, na kisha fikiria hisia hiyo ikibakia na wewe milele.

Kulingana na kile Alma alifundisha, unataka Hukumu ya Mwisho iwekwe tu juu ya haki? Je, unataka kupata kile “unastahili” kwa mambo uliyokosea?

Alma 42:15–31

Alma anamfundisha Koriantoni juu ya mpango wa huruma

Moja ya sifa takatifu za Mungu ni kwamba Yeye ni mwenye haki. Mahitaji ya haki yanalaani kila mtoto wa Baba wa Mbinguni na hayawezi kuruhusu mmoja wetu kukaa pamoja Naye katika hali yetu ya dhambi. Fikiria swali lifuatalo: Je, kuna njia yoyote kwa mahitaji haya ya haki kufutwa au kuondolewa?

Watu wengi wanaweza kujibu swali hili kwa kupendekeza kwamba tukitubu, hatutalazimika kuteseka madhara ya dhambi zetu. Ingawa jibu hili hatimaye ni sahihi, ni muhimu kuelewa kwamba kufuta au kusamehe madhara itakuwa si haki kwa sababu ya mahitaji ya haki hayatatimizwa. Alma alifundisha kwamba kufutilia mbali adhabu bila kutosheleza mahitaji ya haki haiwezekani. Soma Alma 42:25, na uangalie kile ambacho kingetokea kama Mungu angeondoa madhara ya dhambi na kuacha haki bila kuridhishwa.

Tafakari swali lifuatalo kabla ya kusoma Alma 42:15 ili kupata jibu: Kama adhabu ya dhambi zetu haiwezi kuondolewa mbali, tunawezaje kupata amani ya dhamiri na kurejeshwa kwenye uwepo wa Mungu?

Inaweza kusaidia kuelewa kwamba kishazi “atawezesha mahitaji ya haki” inamaanisha kuridhisha au kulipia adhabu inayohitajika kwa haki.

Kutoka Alma 42:15 tunajifunza: Upatanisho wa Yesu Kristo uliridhisha mahitaji ya haki ili kwamba huruma iweze kuenezwa kwa wanaotubu. Kamilisha picha ya mizani uliochora katika shajara yako ya kujifunza maandiko kwa kuandika Kuridhishwa na huruma —Upatanisho wa Yesu Kristo chini ya kishazi “Adhabu …”.

  1. Fikiria kuwa una rafiki ambaye amekuwa akitaabika chini ya mzigo ulioletwa na dhambi zake. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika jinsi ungeelezea rafiki yako jinsi Upatanisho wa Yesu Kristo unavyoruhusu huruma kuenezwa kwa kila mmoja wetu.

Tafakari kinachomaanisha kwako kujua kuwa Mwokozi aliteseka kwa hiari adhabu zinazohitajika na haki badala yako ili kwamba uweze kupewa huruma?

Soma Alma 42:22–24, na uweke alama kile ambacho Kristo anahitaji ili tuweze kupata huruma. Kishazi “waliotubu kwa ukweli” katika mstari 24 ina maana anayetubu kwa dhati. Kulingana na kile ulichokisoma, kamilisha kanuni ifuatayo: Tukitubu, tutapata kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo.

Rais Boyd K. Packer, Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, amtaja Yesu Kristo kama mpatanishi. Mpatanishi ni mtu anayesimama kati ya pande mbili ili kusaidia kutatua mgogoro. Unaposoma maneno yake, angalia jinsi Mwokozi anahitajika ili rehema kuonyeshwa kwa mwenye dhambi.

Picha
Rais Boyd K. Packer

“Kulingana na sheria ya milele, rehema haiwezi kuonyeshwa ila kuwe na mtu ambaye ana nia na uwezo wa kuchukua madeni yetu na kulipa dhamana na kupanga masharti ya ukombozi wetu.

“Isipokuwa kuwe na mpatanishi, isipokuwa tuwe na rafiki, uzito kamili wa haki isiyopunguzwa, bila huruma, lazima, hakika lazima ianguke juu yetu. Fidia kamili ya kila kosa ijapokuwa dogo namna gani au zito namna gani, itahitajika kutoka kwetu hata hadi senti ya mwisho.

“Lakini kumbukeni jambo hili: Ukweli, ukweli mtukufu, hutangaza kuna Mpatanishi vile. …

“Kupitia Kwake, rehema inaweza kuonyeshwa kikamilifu kwa kila mmoja wetu bila kuvunja sheria ya milele ya haki. …

“Kuonyeshwa huruma hakutakuwa moja kwa moja. Itakuwa ni kupitia kwa agano na Yeye. Itakuwa ni kwa masharti Yake, masharti Yake yenye ukarimu” (“The Mediator,” Ensign, May 1977, 55–56).

Picha
Ee Baba Yangu

Alma alipohitimisha majadiliano yake pamoja na Koriantoni, alifanya muhtasari kila kitu alichokuwa akijaribu kufundisha mwanawe. Soma Alma 42:26–31, na uweke alama kile Alma alitamani kwa ajili ya Koriantoni alipokuja kuelewa mafundisho na kanuni ambayo Alma alimfundisha katika sura hii. Angalia hamu ya Alma kwake Koriantoni ya kutokujiondolea lawama mwenyewe kwa dhambi zake, lakini badala yake kuruhusu mafundisho na kanuni zinazohusiana na haki, rehema na Upatanisho “kuvuma ndani ya moyo [wake]” (Alma 42:30). Unawezaje kuruhusu mafundisho haya na kanuni kuvuma ndani ya moyo wako?

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko yako, andika mawazo yako kuhusu swali lifuatalo: Kama ungedhihirisha shukrani yako binafsi kwa Mwokozi kwa dhabihu yake kwa niaba yako, ungemwambia nini?

Ni muhimu kujua kwamba Koriantoni alitubu na hatimaye alikuwa na athari kubwa katika ukuaji wa Kanisa (ona Alma 49:30).

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Alma 42 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha