Seminari
Kitengo cha 32: Siku ya 1, Moroni 7:20–48


Kitengo cha 32: Siku ya 1

Moroni 7:20–48

Utangulizi

Kama ilivyoandikwa katika Moroni 7:20–48, Mormoni aliendelea mahubiri yake katika sinagogi kwa kufundisha wasikilizaji wake jinsi ya “kushikilia kila kitu kizuri” (Moroni 7:20–21, 25). Alieleza umuhimu wa imani, tumaini, na hisani. Alikamilisha mahubiri yake na ombi kwamba wasikilizaji wake wangeomba kwake Baba na nguvu zote za mioyo yao kwa ajili ya karama ya hisani ambao Mormoni alielezea kama “upendo msafi wa Kristo” (Mormoni 7:47).

Moroni 7:20–39

Mormoni anafundisha kuhusu imani katika Yesu Kristo

Reje Moroni 7:12–13, na uzingatie kile ulichojifunza katika somo la awali kuhusu jinsi ya kubainisha vitu vizuri kutoka kwa vitu viovu. Katika nafasi iliyotolewa, orodhesha mifano ya vitu vizuri (vitu ambavyo huja kutoka kwa Mungu na kutushawishi kuamini katika Kristo) na vitu vibaya (vitu ambavyo hutushawishi tusiamini katika Kristo na tusimtumikie Mungu):

Vitu Vizuri

Vitu Viovu

Tambua kwamba Mormoni alituhimiza “tushikilie kila kitu kizuri” (Moroni 7:19). Tafakari kile unafikiria inamaanisha kushikilia kila kitu kizuri.

Mormoni aliwauliza wasikilizaji wake swali muhimu, ambalo aliendelea mbele na kulijibu. Soma Moroni 7:20 , na upate swali Mormoni alipanga kujibu. Kisha soma Moroni 7:21–26 , ukitafuta jibu la swali hili.

Unapotazama Moroni 7:21, 25, alamisha maneno na vishazi vinavyofundisha kanuni hii : Tunapoweka imani katika Yesu Kristo, tunaweza kushikilia kila kitu kizuri.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, jibu maswali yafuatayo:

    1. Kulingana na Moroni 7:22–26, ni kwa njia gani Baba wa Mbinguni hutaka kutusaidia kujenga imani katika Yesu Kristo?

    2. Lini imani yako katika Yesu Kristo imekusaidia kushikilia kila kitu kizuri ama kukusaidia kuondosha kitu kiovu?

Mormoni aliendelea kueleza baadhi ya vitu vizuri ambavyo huja kwa wale ambao wanaweka imani katika Yesu Kristo. Soma Moroni 7:32–34, na ualamishe angalau baraka moja katika kila mmoja wa mistari hii ambayo huja kutokana na kuwa na imani katika Yesu Kristo.

  1. Fikiria juu ya na uombe juu ya kitu ambacho unaweza kufanya ili kuwa na imani kuu zaidi katika Yesu Kristo. Unapokuwa na lengo akilini, liandike chini katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Lengo linaweza kuwa kufanya kitu fulani ambacho kitakusaidia kufuata maneno ya manabii (ona Moroni 7:23), kuomba na imani kuu zaidi (ona Moroni 7:26), ama kutubu dhambi fulani (ona Moroni 7:34). Unapoandika lengo lako, jumuisha maelezo maalum kuhusu jinsi utalikamilisha. Pia andika jinsi lengo hili litaleta vitu vizuri katika maisha lako.

Moroni 7:40–43

Mormoni anafundisha kuhusu tumaini

Katika mahubiri yaliyoandikwa katika Moroni 7, Mormoni alitambua kanuni tatu tukufu ambazo ni muhimu kwa ajili ya maisha ya milele. Mzee M. Russell Ballard wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha kwamba “kanuni hizi tatu tukufu zinaunda msingi ambapo tunaweza kujenga jengo la maisha yetu.” Alisema kwamba kanuni hizi tatu “pamoja zinatupa msingi wa kutegemea kama miguu ya kiti cha miguu mitatu” (“The Joy of Hope Fulfilled,” Ensign, Nov. 1992, 33).

Picha
kiti cha miguu mitatu

Nyenzo zifuatazo zitakusaidia kupata kanuni zile tatu ambazo Mormoni alitambua. Kanuni ya kwanza ni imani, ambayo umejifunza katika Mormon 7:20–39. Ita mguu mmoja wa kiti hapo juu Imani katika Yesu Kristo.Pata kile mguu wa pili unasimamia kwa kusoma Moroni 7:40. Andika kanuni hiyo kando ya mguu mwingine wa kiti.

Soma Moroni 7:41–42, na utambue kile Mormoni alifundisha tunapaswa tutumainie. (Moroni 7:41ni kifungu cha umahiri wa maandiko.) Huenda ukataka kuongeza “kwa ajili ya maisha ya milele” kwa jina uliloweka kwa mguu wa pili wa kiti ili kwamba lisome “Tumaini kwa ajili ya maisha ya milele.”

Rais Dieter F. Uchtdorf wa Urais wa Kwanza alizungumzia tumaini ambao Mormoni alikuwa anarejelea:

Picha
Rais Dieter F. Uchtdorf

“Tumaini ni karama ya Roho. Ni tumaini kwamba kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo na nguvu ya Ufufuo Wake, tutafufuliwa kwa maisha ya milele na hii kwa ajili ya imani yetu katika Mwokozi. …

“Tumaini si ufahamu, lakini badala yake imani ya kudumu kwamba Bwana atatimiza ahadi Zake kwetu. Ni imani kwamba tukiishi kulingana na sheria za Mungu na maneno ya manabii Wake sasa, tutapokea baraka tunazotamani katika siku zijazo. Ni kuamini na kutarajia kwamba maombi yetu yatajibiwa. Huonekana katika imani, matumaini, shauku, na uvumilivu” (“The Infinite Power of Hope,” Ensign ama Liahona, Nov. 2008, 21–22).

Kanuni moja tunayojifunza kutoka Moroni 7:40–42 ni: Tukiweka imani katika Yesu Kristo, tunaweza kupokea tumaini kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo kufufuliwa kwa maisha ya milele.

Soma Moroni 7:43 na utambue sifa zinazohitajika ili mtu awe na imani na tumaini ambalo Mormoni alizungumzia.

Kuwa “mnyenyekevu, na mpole katika moyo” inamaanisha kuwa mnyenyekevu kabisa, mpole na mtiifu kwa matakwa ya Bwana. Kwa nini unafikiria unyenyekevu na upole wa moyo ni muhimu ili kuwa na imani na tumaini katika Upatanisho wa Yesu Kristo?

  1. Katika shajara yako ya maandiko, eleza vile imani yako na upatanisho wa Yesu Christo imekupatia imani.

Moroni 7:44–48

Mormoni afundisha kuhusu hisani

Rejea picha ya kiti mwanzoni mwa somo hili. Soma Moroni 7:44, na utambue kanuni ya tatu iliyofundishwa na Mormoni. Weka kitambulisho chenye maelezo kwenye mguu wa mwisho wa kiti na kanuni hii ya mwisho.

Kama ilivyoandikwa katika Moroni 7:44–48, Mormoni alitoa maelezo ya nguvu sana ya hisani. Soma Moroni 7:45–47, na weka alama maneno na vishazi ambavyo Mormoni alitumia kueleza hisani. (Moroni 7:45, 47–48 ni kifungu cha umahiri wa maandiko.) Ili kukusaidia kuelewa vyema zaidi kile Mormoni alikuwa anafundisha, unaweza kutaka kuandika baadhi ya maelezo haya katika maandiko yako: “huvumilia” inamaanisha kustihimili kwa subira, “haina wivu” inamaanisha kutokuwa na husuda, “haijivuni” inamaanisha kuwa mnyenyekevu na mpole, “haitafuti mambo yake” inamaanisha kumweka Mungu na wengine mbele, “haifutuki upesi” inamaanisha kutokukasirika virahisi, na “huamini vitu vyote” inamaanisha kukubali ukweli wote.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, jibu moja ama zaidi ya maswali haya:

    1. Kulingana na maelezo katika Moroni 7:45–47, kwa nini unafikiria hisani ni karama kuu zaidi ya kiroho tunyoweza kupata?

    2. Unafikiria inamaanisha nini kwamba hisani haikosi kufaulu kamwe?

    3. Kwa nini unafikiria sisi si kitu ikiwa hatuna hisani?

Baada ya kutaja mafunzo ya Mtume Paulo juu ya hisani katika 1 Wakorintho 13, Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alieleza: Sababu ya hisani kutokosa kufaulu kamwe na sababu hisani ni kuu zaidi ya hata vitendo vya maana kabisa vya wema alivyotaja ni kwamba hisani, ‘upendo msafi wa Kristo’ (Moro. 7:47), si kitendo lakini ni hali ama hali ya kuwa. Hisani hufikiwa kupitia mfululizo wa vitendo vinavyosababisha uongofu. Hisani ni kitu mtu anakuwa. Hivyo basi, kama Mormoni alivyotangaza, ‘isipokuwa watu wawe na hisani hawawezi kurithi pale mahali ambapo wametayarishiwa nyumbani kwa Baba (Etheri 12:34; himizo kuongezwa)” (“The Challenge to Become,” Ensign, Nov. 2000, 34.)

Soma hali zifuatazo na uzingatie jinsi huenda ukachukulia mambo ikiwa ungekosa karama ya hisani na jinsi huenda ukawa ikiwa ungejawa na hisani:

  • Wanafunzi wengine wanakukejeli wewe ama mtu mwingine shuleni.

  • Unaye ndugu ama dada ambaye mara nyingi hukuuthi.

  • Haumpendi mmoja wa mshauri wako wa jamii ama darasa kama vile ulivyompenda kiongozi wa awali.

Baada ya kueleza jinsi ni muhimu kukuza hisani katika maisha yetu, Mormoni alieleza jinsi tunaweza kupokea sifa hii kuu bainifu. Soma Moroni 7:48, na ualamishe maneno na vishazi vinavyofundisha kanuni hii Tukiomba kwake Baba kwa nguvu zote za moyo na kuishi kama wafuasi wa kweli wa Yesu Kristo, tunaweza kujazwa na hisani.Tafakari kwa nini ni muhimu kuomba kwa ajili ya karama ya hisani kwa nguvu zote za moyo wako badala ya kuomba kwa uzembe kwa ajili ya karama hii.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kuhusu wakati ulihisi kwamba Bwana alikusaidia kuwa na hisani. Ama andika kuhusu wakati ambapo ulimwona mtu mwingine akiwa na hisani. Zaidi ya hayo, weka lengo maalum la jinsi utajiimarisha zaidi katika sifa moja ya hisani iliyoorodheshwa katika Moroni 7:45. Omba kwa ajili ya karama ya ukuhani unapojitahidi kutimiza lengo lako.

Picha
ikoni ya umahiri wa maandiko
Umahiri wa maandiko —Moroni 7:41

Andika mstarii mzima kwenye kipande cha karatasi. Kariri mstari huo mara nyingi. Futa (ama ondoa kwa kuchorea mstari juu ) maneno ama vishazi hadi uweze kukariri mstari mzima kutoka akilini.

Picha
ikoni ya umahiri wa maandiko
Umahiri wa Maandiko—Moroni 7:45, 47–48

Andika herufi ya kwanza ya kila neno katika mistari hii mitatu kwenye kipande cha karatasi. Rejea karatasi ili kukusaidia kukariri mistari hiyo. Baada ya kukariri mistari mara kadhaa, futa ama ondoa herufi kwa kutia mstari juu hadi uweze kukariri mistari kutoka akilini. Kisha chagua kikundi kimoja kifuatacho cha watu ambao kutoka kwao ungependa kuwa na hisani zaidi: familia, jamii ya Kanisa ama wana darasa, wanafunzi wenzako shuleni, marafiki, ama majirani. Fikiria kuhusu watu unaowachagua unaposoma Moroni 7:45, na uzingatie njia utawaonyesha watu hawa upendo zaidi kama wa Kristo.

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko njia moja ama mbili utaonyesha hisani kuu kwa watu hawa. Katika wiki, omba kwa ajili ya usaidizi wa Bwana katika kukuza hisani zaidi kwao. Mwishoni mwa wiki, shiriki kile ulichopitia na rafiki ama mwana familia.

  2. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Moroni 7:20–48na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningetaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha