Seminari
Kitengo cha 30: Siku ya 4, Etheri 12


Kitengo cha 30: Siku ya 4

Etheri 12

Utangulizi

Baada ya kueleza historia ya miaka mingi ya Wayaredi, Moroni alitanguliza huduma ya nabii Etheri. Moroni kisha alitua katika usimulizi wake wa kihistoria na kuandika baadhi ya baraka zilizokuja kwa wale ambao waliweka imani katika Yesu Kristo. Pia alikiri tatizo. Alikuwa na wasiwasi kwamba wale ambao wangesoma Kitabu cha Mormoni katika siku za mwisho hawangekikubali kwa sababu ya udhaifu wake na wa waandishi wengine katika kuandika. Bwana alimwahidi Moroni kwamba Yeye huimarisha udhaifu wa wote ambao hujinyenyekeza mbele Yake na kuwa na imani.

Etheri 12:1–4

Etheri anahubiri toba kwa Wayaredi

Picha
mashua iliyotiwa nanga pwani

Kwa nini ni muhimu kwa mashua kuwa na nanga? Ni hatari gani ama shida ambazo mashua huenda ikakumbana nazo ikiwa haina nanga? Weka alama mashua katika picha Maisha yangu.Fikiria kuhusu maswali yafuatayo:

  • Ikiwa mashua inawakilisha maisha yako, mawimbi yanaweza kufananishwa na nini?

  • Tukilinganisha mawimbi na shida na uovu, maisha ya mtu yanaweza kuwa vipi asipokuwa na nanga? (Ona Mormoni 5:18.)

  • Bwana amekupa nini ili kusaidia kukushikilia mahali salama kama nanga?

Unaposoma Etheri 12, tafuta kile ambacho lazima ufanye ili kuwa kama mashua iliyo na nanga —imara na salama licha ya mawimbi na shinikizo unazokumbana anazo. Etheri 12 inaanza na Mormoni akimtambulisha nabii Etheri, ambaye aliishi katika wakati ambapo watu waliwakataa manabii na kuishi katika uovu. Soma Etheri 12:1–3, na utafute chochote ambacho kinakuvutia kuhusu vitendo vya Etheri wakati wa hali hizi ugumu.

Alipokuwa anatembea akiwahimiza watu watubu, Etheri alifundisha kile mtu anayeamini katika Mungu anaweza kutumainia licha ya kuzingirwa na shida na uovu. Soma Etheri 12:4, na ualamishe kile ambacho ni tumaini hiyo. (Unaposoma, inaweza kusaidia kujua kwamba kuwa na “mahali katika mkono wa kulia wa Mungu” kunamaanisha kurudi kwenye uwepo wa Mungu na kupokea uzima wa milele.)

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Unafikiria kuwa na tumaini “kwa hakika” kunatofautianaje na kutamani tu kwa ajili ya kitu?

    2. Imani katika Yesu Kristo inaturuhusu vipi kutumaini “kwa hakika” kwa ajili ya nafasi katika mkono wa kulia wa Mungu?

    3. Ni vishazi gani katika Etheri 12:4 vinavyoelezea vitendo vya mtu ambaye ana tumaini na imani katika Yesu Kristo?

Kwenye picha ya mashua mwanzoni mwa somo hili, weka alama nanga na maneno imani na tumaini.

Etheri 12:4 anafundisha kanuni kwamba tunapokuwa na tumaini na imani katika Yesu Kristo, tutapokea nguvu kuwa imara na thabiti kuzidi sana kutenda kazi njema.

Tafakari wakati ambapo huenda kuwa vigumu kwako kuwa imara (kutoyumbayumba) na kuzidi kutenda kazi njema. Ili kukusaidia katika hali hizi na maishani mwako mwote, tafuta njia unaweza kuongeza imani yako katika Bwana Yesu Kristo unapoendelea kusoma Etheri 12.

Etheri 12:5–22

Moroni aelezea miujiza na vitendo vikuu vilivyotendeka kwa imani

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, kamilisha sentensi zifuatazo na kweli zozote za injili ambazo unatafuta ushahidi wa kiroho:Ningependa kupata ushahidi wa kiroho wa …

Watu wengine huhisi kwamba lazima kwanza waone ushahidi wa ukweli fulani na kuudhibitisha kwao kabla wauishi. Etheri alizungumza kuhusu mtazamo huo katika Etheri 12:5–6. Soma mistari hii na ualamishe sehemu hizo za ushauri wake ambazo zinakuvutia. (Etheri 12:6 ni kifungu cha umahiri wa maandiko.)

Kulingana na Etheri 12:6, ni lazima tuwe na nini kabla ya kupokea ushahidi kutoka kwa Bwana? Nini kinakuja akilini unapofikiria kuhusu “majaribu ya imani yenu”?

Picha
Mzee Richard G. Scott

Baadhi ya watu hutafsiri kimakosa “majaribu ya imani yenu” kurejelea kila mara kwa shida. Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alitoa ufahamu ya kile “majaribu ya imani yenu” humaanisha: “Unaweza kujifunza kutumia imani vyema zaidi kwa kutumia kanuni hii iliyofundishwa na Mornoni: ‘hamtapata ushahidi wowote mpaka baada ya majaribu ya imani yenu’ [Etheri 12:6; himizo kuongezwa]. Hivyo basi, kila wakati unapojaribu imani yako, yaani, kutenda kwa ustahiki kwenye mvutio, utapokea ushahidi wa kudhibitisha wa Roho. Hisia hizo zitadhibiti imani yako. Unaporudia mpangilio huo, imani yako itaimarika” (“The Sustaining Power of Faith in Times of Uncertainty and Testing,” Ensign ama Liahona, Mei 2003, 76).

Soma vifungu vya maandiko vifuatavyo, na utafute baraka ambazo huja baada ya watu kutumia imani:

Huenda ikasaidia kubaini matumizi ya neno baada katika Etheri 12:7, 12, 17, 18, na 31.

  1. Kulingana na kile umejifunza katika Etheri 12, kwa maneno yako mwenyewe, andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kile unahisi Moroni alifundisha kuhusu kupokea shahidi za kiroho kutoka kwa Bwana.

Moja ya kanuni Moroni alifundisha ilikuwa: Ikiwa tunatamani ushahidi, basi lazima kwanza tuweke imani katika Yesu Kristo.

  1. Soma mipangilio ya matukio yafuatayo, na kisha andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko jinsi mtu katika hali hizo mbili ama zaidi angeweza kuonyesha imani katika Bwana:

    1. Msichana anataka kupokea ushahidi wa ukweli wa Kitabu cha Mormoni.

    2. Mvulana ana nia kuu kuwasaidia wapendwa wake kukubali injili.

    3. Msichana anamtazamia Bwana kumbariki babake aliye mgonjwa.

  2. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kuhusu wakati ambapo wewe ama mtu unayemjua alipokea ushahidi ama muujiza baada ya kuonyesha imani.

Rejelea kimawazo juu ya kanuni ama fundisho ambalo kwalo ungetaka kupokea ushahidi wa kiroho (ona zoezi la 2 katika somo hili). Unaweza kufanya nini ili kuonyesha imani yako kabla ya kupokea ushahidi?

Picha
ikoni ya umahiri wa maandiko
Umahiri wa Maandiko—Etheri 12:6

  1. Ili kukusaidia kukariri Etheri 12:6, isome mara kadhaa, kisha andika chini kiasi chote ambacho unaweza kukumbuka katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Baadaye, linganisha kile ulichoandika na mstari yenyewe. Soma mstari huo tena, na uuandike chini mara ya pili katika shajara yako ya kujifunza maandiko.

Etheri 12:23–41

Moroni aeleza wasiwasi kuhusu jinsi Wayunani watakavyopokea Kitabu cha Mormoni

Kama ilivyoandikwa katika Etheri 12:23–41, Moroni alieleza wasiwasi kwamba wale ambao wangepokea Kitabu cha Mormoni katika siku za mwisho hawangekikubali kwa sababu ya udhaifu wake na wa waandishi wengine katika kuandika. Unaposoma jibu la Bwana kwa wasiwasi ya Moroni katika Etheri 12:26–27, tafuta jinsi Bwana alisema kwamba vitu dhaifu vinaweza kuwa vya nguvu. (Etheri 12:27 Ni fungu la umahiri wa maandiko.)

Maandiko wakati mwingine huonyesha kanuni ya injili kwa kutumia maneno kwani na basi. Nenokwani linaelezea kile ambacho lazima tufanye, na basi linaeleza kile kitakachotendeka kwa ajili ya vitendo vyetu. Soma Etheri 12:27, utambue kanuni ya kwani–basi, na uiandike chini.

Kwani tuki , basi Bwana ata.

Utajadili mistari hii kwa kina zaidi katika somo pamoja na mwalimu wako wiki hii. Utasoma pia na kujifunza zaidi kuhusu mjadala wa Moroni kuhusu imani, tumaini, na hisani katika Etheri 12:28–41.

Picha
ikoni ya umahiri wa maandiko
Umahiri wa Maandiko —Etheri 12:27

Ili kukusaidia kukumbuka mawazo katika Etheri 12:27, nakili yafuatayo kwenye kipande cha karatasi: Ikiwa kuja onyesha udhaifu. Kupeana udhaifu unyenyekevu neema watu wote nyenyekea ikiwa nyenyekea imani dhaifu nguvu.

Soma tena Etheri 12:27, ukitambua maneno haya. Nena upya kiasi uwezacho cha mstari huu, ukitazama tu maneno kwenye karatasi yako. Weka kipande cha karatasi mahali ambapo utakiona baadaye leo ama kesho (kwa mfano, mfukoni mwako ama katika maandiko yako). Rejelea Etheri 12:27 wakati wowote unapoona kipande cha karatasi hicho hadi ukariri fungu hilo.

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Etheri 12 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningetaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha