Seminari
Kitengo cha 30: Siku ya 2, Etheri 6


Kitengo cha 30: Siku ya 2

Etheri 6

Utangulizi

Baada ya kujitayarisha kulingana na amri za Bwana, Wayaredi walipanda mashua na kuamini Bwana kuwapeleka salama kwenye safari yao ngumu kwenda nchi ya ahadi. Bwana alituma pepo ambazo zisukasuka mashua kwenye mawimbi na kuyazamisha katika bahari mara nyingi, lakini pepo hizo hizo ziliwaelekeza kwa nchi ya ahadi. Baada ya kujipanga katika nchi ya ahadi, watu walichagua mfalme licha ya maonyo kutoka kwa kaka ya Yaredi.

Etheri 6:1–12

Bwana aendesha mashua ya Wayaredi kwa upepo hadi kwa nchi ya ahadi

Kuna wakati ambapo tunaweza kuhisi kuwa vigumu kufanya yale ambayo Bwana anauliza, kama vile kushiriki injili na rafiki, kubaki wasafi kimaadili, kuchagua marafiki walio na viwango vya juu, na kuweka vipaumbele sahihi maishani. Je, unaweza kufikiria juu ya mifano mengine ya wakati inaweza kuwa vigumu kufanya yale ambayo Bwana anauliza?

Maelezo ya safari ya Wayaredi kwenda nchi ya ahadi yanafundisha kanuni zinazoweza kukuongoza unapoona kuwa vigumu kufanya yale ambayo Bwana huamuru. Soma Etheri 2:24–25, na utafute kile Bwana alionya Wayaredi kingefanya safari yao kwenda nchi ya ahadi kuwa ngumu.

Ili kushinda matatizo haya, Bwana aliwaamuru Wayaredi watengeneze mashua ili kwamba yawe “yamekazwa sana kama sahani” (Etheri 2:17), na matundu juu na chini ili kwamba waweze kufunua kwa ajili ya hewa. Soma Etheri 6:1–4, na utambue njia zingine Bwana aliwawezesha Wayaredi kujitayarisha kwa ajili ya matatizo ya safari.

Inaweza kusaidia kuelewa kwamba “wakimtegemea Bwana Mungu wao awalinde” (Etheri 6:4) inamaanisha kwamba Wayaredi walijikabithi kwa Mungu kwa ajili ya kuhudumiwa na kuhifadhi kwao.

  1. ikoni ya shajaraJibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Kwa nini ingekuwa vigumu kwa Wayaredi kumwamini Bwana katika hali hii?

    2. Kwa nini unafikiria yote kujitayarisha na kujikabithi kwao kwa Bwana kulikuwa muhimu?

Unaposoma Etheri 6:5–11, jaribu kufikiria vile huenda ilikuwa kusafiri katika mashua ya Wayaredi.

  1. ikoni ya shajaraIli kukusaidia kujitayarisha kutambua kanuni za injili unazoweza kujifunza kutoka kwa maelezo haya, jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya maandiko:

    1. Wayaredi walionyeshaje imani yao katika Bwana wakati wa safari yao ngumu? (ona Etheri 6:7, 9).

    2. Bwana aliwabariki vipi katika safari yao?

Baada ya karibu mwaka kwenye maji, safari ya Wayaredi hatimaye ilikamilika. Soma Etheri 6:12, na utambue jinsi walivyohisi walipofika katika nchi ya ahadi. Fanya muhtasari wa yale uliyojifunza katika somo hili hadi sasa kwa kukamilisha kauli ya msingi ifuatayo: Tunapomtumainia Bwana na kufanya mapenzi Yake, Yeye ata.

Njia moja ya kukamilisha kauli hii ipo katika kishazi “ongoza mwelekeo wa maisha yetu” Ili kudumisha ufahamu wako wa kanuni hii, reje nyuma kwenye hali ambapo huenda tunaweza kuhisi kuwa vigumu kufanya kile ambacho Bwana anauliza, zilizoorodheshwa mwanzoni mwa somo. Kama tu vile alivyofanya na Wayaredi, Bwana hututayarisha kushinda matatizo tutakayokumbana nayo maishani tunapoomba, tunapomfuata nabii, na kutii amri.

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika jinsi mtu anaweza kuonyesha tumaini katika Bwana. Kulingana na mfano wa Wayaredi, tunapaswa kufanya nini tunapokumbana na amri ngumu kutoka kwa Bwana?

  2. ikoni ya shajaraWazia kanuni ifuatayo: Tukitumainia Bwana, dhiki na shida zinaweza kutusaidia kuendelea na kupata baraka zilizoahidiwa. (Unaweza kutaka kuiandika katika maandiko yako karibu na Etheri 6:5–10.) Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, jibu maswali yafuatayo:

    1. Unahisi umeendelea vipi na kupokea baraka kupitia kwa kuvumilia kwa uaminifu shida zilizokukabili ama zinazokukabili kwa sasa katika maisha yako?

    2. Unawezaje kumtumainia Bwana zaidi na kufuata maelekezo yake katika hali ngumu zinazoweza kukukabili?

Etheri 6:13–18

Wayaredi wanafundisha watoto wao kutembea kwa unyenyekevu mbele ya Bwana

Fikiria kwamba wewe, kama Wayaredi, umevuka bahari na kufika katika nchi mpya kabisa kwako. Soma Etheri 6:13–18, na ufikirie kuhusu maswali yafuatayo: Ni ipi baadhi ya mifano ya kile kinachomaanisha kutembea kwa unyenyekevu mbele ya Bwana? Je! Wazazi wako na wengine wamekuhimiza kutembea kwa unyenyekevu mbele ya Bwana? Unafikiria ni nini uhusiano kati ya kutembea kwa unyenyekevu na kufundishwa kutoka mbinguni? Lini umehisi “ulifundishwa kutoka mbinguni?” (Etheri 6:17).

  1. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Etheri 6 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningetaka kushiriki na mwalimu wangu: