Seminari
Kitengo cha 30: Siku ya 3, Etheri 7–11


Kitengo cha 30: Siku ya 3

Etheri 7–11

Utangulizi

Ingawa kaka ya Yaredi alitoa unabii kwamba kuweka mfalme Myaredi kungewaelekeza kwenye utumwa, maneno yake hayakutimia mara moja. Mfalme wa kwanza Myaredi, Oriha, aliongoza kwa haki. Hata hivyo, mtu aliyeitwa Yaredi alikuwa mfalme vizazi viwili baadaye kwa kuunda genge la siri. Wakati wa uongozi wa wafalme wao, Wayaredi walipitia misimu kadhaa ya kuwasikiliza manabii na kuishi katika haki, na kuwakataa manabii na kuishi katika uovu.

Etheri 7

Korihori ateka ufalme wa babake, kakake Shule auchukua tena, na manabii waushutumu uovu wa watu.

Unafikiria mtu huenda akahisi vipi akiwa anaishi katika utumwa? Je, umewahi kuwa na hisia kama hizo za kutekwa kwa sababu ya chaguo zisozosahihi ambazo umefanya? Tafuta umaizi ya jinsi unaweza kuepuka utumwa wa kimwili na kiroho unapojifunza Etheri 7–11.

Picha
mtu jelani

Wakati Yaredi na nduguye walipokuwa wazee, Wayaredi waliomba kuwa na Mfalme. Kaka ya Yaredi aliwaonya watu kwamba kuwa na mfalme kungewaelekeza katika utumwa (ona Etheri 6:19–23). Manabii daima wametoa unabii dhidi ya vitendo vitakavyoelekeza katika ufungwa wa kimwili ama kiroho.

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko mfano mmoja ama miwili ya vitendo ambavyo manabii wa kisasa wanaonya dhidi na jinsi vitendo hivyo vinaweza kuelekeza kwa ufungwa wa kimwili na kiroho.

Licha ya onyo la kaka ya Yaredi, watu walichagua kuwa na mfalme. Soma Etheri 7:1–2 ili kujifunza kama unabii wa kaka ya Yaredi ulitimia katika siku za Oriha, ambaye alikuwa ni mwana wa Yaredi. Fikiria kuhusu kile ungemwambia mtu aliyeishi katika siku za Mfalme Oriha na hakuamini kwamba unabii wa kaka ya Yaredi ungetimia.

Katika vizazi viwili onyo la kinabii la kaka ya Yaredi lilitimia. Soma Etheri 7:3–7, na utambue jinsi Kibu na watu wake waliishi katika ufungwa chini ya Korihori, ambaye matakwa yake ya kibinafsi kuwa mfalme yalimleta kuasi dhidi ya baba yake. Ufungwa huu ulitokana na ubinafsi na uasi.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kile ungewaambia watu leo ambao wanakosa kutii ushauri wa manabii lakini hawahisi kama wako katika ufungwa wa kiroho. (Katika jibu lako, unaweza kutaka kujumuisha wazo kwamba wale wanaonaswa katika ufungwa wa kiroho huwa mara nyingi wa mwisho kutambua. Toa hali ya kisasa ya kitu ambacho kinaweza kumweka mtu katika ufungwa wa kiroho.)

Sehemu hii ya historia ya Wayaredi inaonyesha kanuni kwamba kukataa maneno ya manabii kunaelekeza kwenye ufungwa.Tafakari njia ambazo huenda umepitia ufungwa wa kiroho kwa sababu ya kutokutii amri ama ushauri wa kinabii.

Uasi wa Korihori dhidi ya babake, Kibu, kulielekeza kwa upinzani na vita kuendelea. Akiwa katika siku zake za uzee, Kibu alikuwa na mwana mwingine — Shule. Shule alipokuwa, alipigana dhidi ya kakake mwasi, Korihori.

  1. Fikiria wewe ni mwanahabari aliyetumwa kuripoti hadithi ya Shule. Soma Etheri 7:8–13, na uandike aya fupi katika shajara yako ya kujifunza maandiko ukiripoti kile ungetilia mkazo katika kuripoti kwako maisha ya Shule.

Wakati wa utawala wa Shule, manabii wengi walikuja miongoni mwa watu na kuwaonya juu ya uovu wao. Soma Etheri 7:23–25, na utambue kile manabii walitoa unabii kuhusu na jinsi watu waliuchukulia. Shule aliuchukulia vipi? Ni jinsi gani ulinzi wa Shule wa manabii ulibariki watu wake?

Soma Etheri 7:26–27, na utafute kile kilichotendeka wakati watu walitii maneno ya manabii. Shule “alikumbuka vitu vikubwa ambavyo Bwana alikuwa amewafanyia babu zake” (Etheri 7:27). Unapokumbuka vitu vikubwa ambavyo Bwana amekufanyia, basi unaweza kwa urahisi zaidi kuwa na shukrani Kwake na kuishi kwa haki.

Matukio haya yanashuhudia kanuni muhimu: Tunapotubu dhambi zetu, tunaanza kufanikiwa. Neno fanikiwa linamaanisha “tumaini” na pia “faulu,” na mara nyingine hutumika katika dhana ya kufaulu kimali, [lakini] halimaanishi hasa uhaba wa mali —ama maisha yasiokuwa na shida. …

“Wale ambao kwa kweli ni wema wamefanikiwa , kwa dhana kwamba wana imani, ambayo inavutia imani hata katika kutenda na husababisha hali za kufaidi kutoka kwa yale yasiyo ya kufaidi Huwa hawangoji Bwana atoe ama azuuie zawadi, lakini badala yake humwita kwa ajili ya mwongozo kuhusu kile ambacho kitawafaidi zaidi, kimwili pamoja na kiroho. Mwongozo kama huo unaweza kuelekeza kwa kubadilisha ajira, kuhama kwenda kwa wilaya zingine, kupokea mafunzo ama vipaji vipya, ama kukubali vitu kama vile vilivyo lakini kufanya kazi kati ya vikwazo vya kibinafsi na kufuata maelekezo ya Roho katika njia zingine” (Alan Webster, “I Have a Question,” Ensign, Apr. 1990, 52–53).

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Umebarikiwa vipi kwa kutii maneno ya manabi?

    2. Nini kitu kimoja unachoweza kufanya ili kutii vyema zaidi maneno ya manabii na kustahili baraka za Bwana?

Etheri 8:1–9:12

Yaredi na kisha Akishi walikuwa wafalme wa Wayaredi kupitia makundi ya siri

Soma orodha ifuatalo: mziki unaosikiliza, fikra unazoruhusu, jinsi unavyotenda shuleni, sinema unazotazama, tabia yako ya miadi, shughuli unazofanya na marafiki zako, kile unachofanya wakati hakuna yeyote mwingine aliyekaribu. Ni kwa nini mtu aliyehusika katika tabia ovu angetaka kuficha jinsi walivyoshiriki katika moja ama nyingi ya shughuli hizi kutoka kwa marafiki, wazazi na viongozi wao? Ni nini hatari ya kujihusisha katika shughuli za kisiri zisozo za haki ?

Kulingana na Etheri 8, Omeri alikuwa mfalme baada ya Shule kufa, lakini mwanawe Omeri aliyeitwa Yaredi “aliasi dhidi ya babake” (Etheri 8:2) na “alikuwa ameweka moyo wake kwa ufalme na utukufu wa ulimwengu”(Etheri 8:7). Bintiye Yaredi aliunda njama na babaye ambayo ingempa ufalme. Alikuwa mwanamke mrembo, na alipocheza mbele ya mwanume aliyeitwa Akishi, alitaka kumoa. Yaredi alimwambia Akishi kwamba angeweza tu kuoa bintiye “ikiwa utaniletea kichwa cha baba yangu, mfalme” (Etheri 8:12). Akishi aliingia katika kundi la siri na marafiki zake kumuuwa Mfalme Omeri. Kundi la siri ni mahali watu wawili ama zaidi huchukua kiapo kuweka vitendo vyao visivyo vya haki siri ili kuepuka matokeo ya vitendo vyao.

Soma Etheri 8:15–18, na utambue maneno na vishazi ambavyo vinaeleza baadhi ya nia na njia zilizomo nyuma ya wale wanaokubaliana na vikundi vya siri.

  1. Jibu moja ama zaidi ya maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni kwa nini watu wengine hushiriki katika vikundi vya siri?

    2. Kwa nini unafikiria inadhuru kiroho kuamini unaweza kufanya “aina yote ya maovu” (Etheri 8:16) ama “kitu chochote” unachotaka (Etheri 8:17) bila kukabiliana ana matokeo?

    3. Kishazi kipi katika Etheri 8:18 kinaonyesha jinsi Bwana anavyohisi kuhusu vikundi vya siri? Ni kwa nini unafikiria vikundi kama hivyo vinazingatiwa kuwa “ovu kushinda yote”?

Soma Etheri 8:20–22, 25 na Etheri 9:5–6, 11–12, ukitafuta matokeo ya kusaidia vikundi vya siri. Fanya muhtasari wa kile ulichojifunza:

Moja ya kweli uliyotambua katika mistari hii ni:Kusaidia vikundi vya siri hutupeleka kwenye maangamizo ya mtu i binafsi na jamii.

Moroni alitua katika kuandika kuhusu vita vya Wayaredi ili kutuzungumzia. Soma Etheri 8:23–24, 26, na utambue jinsi Moroni alihimiza watu wa siku zetu kutumia maonyo yake kuhusu vikundi vya siri.

Fikiria kuhusu majibu ya maswali yafuatayo: Kwa nini unafikiria taifa, jamii, ama kikundi kingine kiko katika “hali ya kutisha” (Etheri 8:24) wakati kuna vikundi vya siri miongoni mwake? Ni jinsi gani usiri unavipatia nguvu vikundi hivi? Kujua ukweli kuhusu vikundi vya siri kunawezaje kuwasaidia watu kuachana na uovu huu?

  1. Reje orodha ya shughuli iliyotolewa hapo mwanzoni mwa sehemu hii ya somo. Ingawa kufanya chaguo zisizo za haki katika maeneo haya ya maisha yako hakutajumuishwa hasa kama kikundi cha siri, andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko hatari inayokuja kutoka kwa kuchagua na kushiriki katika shughuli ambazo mtu atahisi haja ya kuziweka siri kutoka kwa wengine.

Etheri 9:13–11:23

Mfalme mmoja amfuata mwingine — wengine ni wema, wengine ni waovu.

Kama ilivyoandikwa katika Etheri 9–11, wafalme wengi waliwatawala Wayaredi, wengine katika haki na wengine katika uovu. Soma Etheri 9:26–35 (wakati wa utawala wa Hethi) na Etheri 11:1–8 (wakati wa utawala wa Komu na Shiblomu), ukitafuta ushahidi wa ukweli wa kanuni kwamba kukataa maneno ya manabii hutupeleka kwenye ufungwa, ambayo ilijadiliwa hapo awali katika somo hili.

Picha
taji ya vito vya dhamani

Kumbuka jinsi ulivyofikiria juu ya kufuata vyema zaidi maneno ya manabii. Katika siku zijazo, fuatilia lengo hili na tafuta fursa za kushiriki ushuhuda wako kuhusu umuhimu wa kutii maneno ya manabii.

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Etheri 7–11 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningetaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha