Seminari
Kitengo cha 30: Siku ya 1, Etheri 4–5


Kitengo cha 30, Siku ya 1

Etheri 4–5

Utangulizi

Bwana alimuamuru Moroni aandike na afunge kumbukumbu yake ya ono la kaka ya Yaredi. Moroni alieleza kwamba maandiko haya yangefunuliwa wakati binadamu wana imani kama vile kaka ya Yaredi. Pamoja na hayo, Moroni alitoa unabii kwamba mashahidi watatu wangetoa ushuhuda wa ukweli wa Kitabu cha Mormoni katika siku za mwisho.

Etheri 4:1–7

Moroni anaandika na kufunga maelezo kamili ya ono la kaka ya Yaredi.

Fikiria kuhusu chombo ambacho ni cha thamani kabisa kwako ama kwa familia yako ambacho ungetaka kuweka mbali na mahali watoto wadogo wanawezakufika. Mtoto angehitaji kujifunza nini ama kufanya nini kabla ungemwamini na chombo hicho?

Vile vile, Bwana ana ukweli za thamani anataka kushiriki nasi, lakini Yeye hungoja hadi tunapokuwa tayari kuzipokea. Unaposoma Etheri 4, tafuta kile Moroni alifundisha kwamba kinaweza kukusaidia kujitayarisha kupokea ukweli mkuu zaidi na mwongozo kutoka kwa Bwana.

Unaposoma katika Etheri 3, Bwana alimuonyesha kaka ya Yaredi ono la kila mmiliki wa dunia—waliopita, wa sasa, na wa siku zijazo—na kila kitu kinachohusiana na dunia. Kaka ya Yaredi kisha aliamuriwa aandike kile alichokuwa ameona na afunge maandiko yake. SomaEtheri 4:4–5, na utafute maelezo ya Moroni ya kile kaka ya Yaredi alionyeshwa. Moroni aliandika kuhusu kile kaka ya Yaredi aliona na aliamuriwa pia na Bwana afunge ono ili lije katika wakati Bwana atakapo kusudia. Ono ambalo mistari hii inarejelea limejumuishwa katika kile ambacho kwa kawaida kuitwa sehemu iliyofichwa ya Kitabu cha Mormoni.

Moroni alitoa unabii wa hali ambazo zilihitaji kuwepo kabla ya ufunuo uliopewa kaka ya Yaredi ujulikane. Unaweza kutaka kualamisha hali hizi katika Etheri 4:6–7.

  1. ikoni ya shajaraIli kukusaidia kutafakari kile kinachomaanisha “kuonyesha imani katika [Bwana], hata kama kaka ya Yaredi” (Etheri 4:7), rejea Etheri 1–3 na uorodheshe katika shajara yako ya kujifunza maandiko njia ambayo kaka ya Yaredi alionyesha imani na tumaini katika Bwana. Pia chagua na ueleze mfano moja uliokufurahisha zaidi na ueleze ni kwa nini.

Kama vile ungeamini mtoto na chombo cha thamani ila tu katika hali fulani, Bwana hushiriki kweli za ziada na watoto Wake ila tu tunapoonyesha utayari wetu wa kiroho, tunapoamini katika kweli za thamani ambazo tayari ametufunulia, na kuonyesha imani Kwake.

Etheri 4:8–19

Moroni anatufundisha kile ambacho lazima tufanye ili kupokea ufunuo zaidi.

Angalia pazia zozote za dirisha katika chumba ulipo. Fikiria kuhusu jinsi pazia hupunguza kile unachoweza kuona.

Moroni alitumia ishara ya pazia, ambayo ni sawa na pazia la dirisha, kufundisha kanuni ambazo zinatawala jinsi kila mmoja wetu anaweza kupokea ufunuo. Soma Etheri 4:15, na utafute kishazi kinachojumuisha neno pazia. Fahamu kwamba Moroni alilinganisha kutoamini na pazia. Ni kwa njia gani kutoamini ni kama pazia?

Inaweza kusaidia kuelewa kwamba neno pasua katika Etheri 4:15 linamaanisha kurarua. Fikiria vile ingekuwa ikiwa ungeweza kupasua pazia kati yako na ufahamu wa Bwana.

pazia limepasuka katikati

Moroni alielezea vile vitu vinavyosaidia “kupasua hilo pazia la kutoamini” na kutukubalisha kupokea ufunuo zaidi. Alianza kwa kuonya dhidi ya mtazamo unaotuzuia kutoka kwa kupokea ufunuo zaidi. Soma Etheri 4:8, na weka alama kile kingesababisha Bwana kuzuia ufunuo na “kutoonyesha vitu vikubwa zaidi”

  1. ikoni ya shajaraJibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Unafikiria inamaanisha nini “kupingana na neno la Bwana”? (Etheri 4:8).

    2. Ni zipi baadhi ya njia kijana siku hizi anaweza “kupingana na neno la Bwana”?

Moroni alijumuisha maneno ya Bwana mwenyewe ili kuelezea jinsi ya kupokea ufunuo zaidi kutoka Kwake. Soma Etheri 4:11, 13–15, na weka alama vishazi vinavyofundisha vitu ambavyo ni lazima tufanye ili kualika ufunuo wa Bwana na jinsi Yeye atajibu tukifanya vitu hivi.

Ni kanuni gani kuhusu ufunuo na jinsi ya kuualika katika maisha yako unajifunza kutoka kwa mistari hii? Unaweza kutaka kuandika kanuni moja umejifunza kutoka kwa mistari hii katika maandiko yako karibu na Etheri 4:11.

Kanuni moja muhimu tunayoweza kujifunza kutoka kwa ushauri wa Bwana ni kwamba tunapoonyesha imani kuu katika neno la Bwana, Yeye, katika wakati wake na njia yake, atatubariki na ufunuo zaidi.

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, eleza kwa nini unafikiria ni lazima uonyeshe imani katika neno la Mungu ambalo tayari umepokea kabla Bwana akufunulie zaidi. Kisha jipime kwenye kipimo cha 1 hadi 10 (10 ikiwa “vizuri sana”) kwa jinsi unahisi unaonyesha imani katika Bwana kwa kutafuta na kufuata neno Lake katika kila moja ya sehemu zifuatazo:

    1. Maombi ya kila siku

    2. Kufuata ushawishi unaopokea kupitia Roho Mtakatifu

    3. Kudumisha na kufuata viongozi katika tawi lako, kata, wilaya, au kigingi

    4. Kujifunza neno la Mungu katika kanisa au seminari

    5. Masomo ya kibinafsi ya maandiko

    6. Kufuata maneno ya manabii na kuishi amri

  2. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, eleza jinsi kutii Mungu katika mojawapo wa sehemu zilizotajwa hapo juu kumekusaidia kupokea ufunuo zaidi kutoka kwa Bwana.

Tafakari jinsi unaweza kujumuisha kanuni hii ya kuonyesha imani katika neno la Bwana katika juhudi zako kualika ufunuo ziada na mwongozo kutoka kwa Bwana.

Etheri 5

Moroni atangaza kwamba mashahidi watatu wataona na kutoa ushuhuda wa mabamba

malaika akionyesha mabamba ya dhahabu kwa Joseph Smith, Oliver Cowdery, David Whitmer

Soma Etheri 5:1–3. Ni nini Moroni alikiandika katika mistari hii ambacho kinaelekezwa kwa Nabii Joseph Smith mtu ambaye siku moja angetafsiri kumbukumbu kwenye mabamba? Fikiria jinsi ingekuwa kwa Joseph Smith kupata mistari hii alipokuwa anatafsiri Kitabu cha Mormoni.

Rais Henry B. Eyring

Soma kauli ifuatayo kutoka kwa Rais Henry B. Eyring wa Urais wa Kwanza, na utafute kishazi kinachokuvutia kuhusu ushuhuda wa Mashahidi Watatu: “ Mashahidi Watatu kamwe hawakukataa ushuhuda wao wa Kitabu cha Mormoni. Hawangeweza kwa sababu walijua kilikuwa cha kweli. Walijitolea na kukumbana na shida zaidi ya yale watu wengi wakiyajua. Oliver Cowdery alitoa ushuhuda ule ule kuhusu chanzo kitukufu cha Kitabu cha Mormoni alipolala akiwa anakufa. Kwamba waliendelea kudhihirisha kile walichoona na kusikia katika tukio hilo zuri, walipokuwa wamejitenga kutoka kwa Kanisa na kwa Joseph kwa muda mrefu, hufanya ushuhuda wao kuwa na nguvu zaidi” (“An Enduring Testimony of the Mission of the Prophet Joseph,” Ensign ama Liahona, Nov. 2003, 90).

Kulingana naEtheri 5:2–3, ni nini Nabii Joseph Smith angepata fursa ya kufanya na mabamba?

  1. ikoni ya shajaraKama tu vile wale wanaume watatu walivyokuwa na fursa ya kushuhudia ukweli wa mabamba ya dhahabu, wewe pia unaweza kuwa shahidi wa ukweli wa Kitabu cha Mormoni. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika njia chache unaweza pia kuwa shahidi wa Kitabu cha Mormoni. Pamoja na hayo, andika vile ushahidi wako wa Kitabi cha Mormoni unaweza kuwashawishi watu wengine.

Kwa maombi tafuta nafasi za kushiriki ushahidi wako wa Kitabu cha Mormoni na mtu wiki hii.

  1. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Etheri 4–5 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningetaka kushiriki na mwalimu wangu: