Seminari
Kitengo 22: Siku ya 1, 3 Nefi 1


Kitengo 24: Siku ya 1

3 Nefi 1

Utangulizi

Kabla ya kuondoka nje ya nchi, nabii Nefi (mwana wa Helamani) alipitisha rekodi kwa mwanawe mkubwa, Nefi. Wasioamini walipanga kuwaweka waaminifu kwa kifo ikiwa unabii kuhusu kuzaliwa kwa Yesu hazingetimia kwa siku fulani. Wakati Nefi alipokuwa akimlilia Bwana kwa niaba ya waaminio, sauti ya Bwana ilikuja kwake na kutangaza kwamba ishara ya kuzaliwa Kwake itatolewa usiku huo. Katika kutimiza unabii wa Samweli Mlamani, wakati jua lilipotua hapakuwa na giza na nyota mpya ilitokea. Licha ya jitihada za kila mara za Shetani za kuharibu imani ya watu, “sehemu kubwa ya watu iliamini, na wakamgeukia Bwana” (3 Nefi 1:22).

3 Nefi 1:1–26

Unabii kuhusu kuzaliwa kwa Yesu Kristo unatimia, na Wanefi wengi wanaongoka

Kesho Mimi Nitakuja Ulimwenguni

Fikiria juu ya watu wengine katika maandiko au katika historia ya Kanisa ambao wamejitolea maisha yao kwa ajili ya injili ya Yesu Kristo. Kwa nini unadhani walikuwa tayari kufanya toleo hilo?

Kama ilivyoandikwa katika 3 Nefi 1, kundi la Wanefi waaminifu iliwabidi kua kuamua ikiwa walikuwa tayari kutoa maisha yao ili kubakia waaminifu kwa imani yao. Sura inaanza kwa kueleza kwamba Nefi alipeana kumbukumbu takatifu kwa mwanawe, ambaye pia aliitwa Nefi, na kisha akaondoka nje ya nchi (ona 3 Nefi 1:1–3). Kisha kinahusisha majaribio ya imani ambayo Wanefi wengi walipitia.

Soma 3 Nefi 1:4–9, na uangalie hali zenye changamoto ambazo Wanefi waaminifu walipitia. Ungejisikiaje kama ungekuwa Nefi na wakati ulifika ambapo waumini walikuwa karibu kuharibiwa? Tafakari kwa muda kwa nini watu wengine wanaweza kujitahidi ili kubakia waaminifu katika hali hii.

Soma 3 Nefi 1:10–12, na uangalie kile ambacho Nefi alifanya wakati huu muhimu. Soma majibu ya Bwana kwa Nefi katika3 Nefi 1:13–14. Unaweza kutaka kuwekea alama taarifa katika 3 Nefi 1:13 ambayo inaonyeshawkanuni hii: Bwana atatimiza maneno yote ambayo amesababisha kusemwa kupitia kwa manabii Wake.

  1. ikoni ya shajaraJaribu kufikiria vile ilivyokuwa kwa Nefi mara baada ya ishara ya kuzaliwa kwa Mwokozi ilipotolewa. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandikojinsi unafikiri ungeweza kujibu kama ungalikuwa huko wakati huo. Je unafikiri ungejisikiaje kama ungekuwa Nefi na ishara ilikuwa imetokea?

Soma 3 Nefi 1:4, 14–15, 19–21, na uangalie vishazi vya ziada ambavyo vinasisitiza msimamo wa Bwana katika kutimiza maneno ya manabii Wake. Unaweza kutaka kuyawekea alama vishazi hivi katika maandiko yako. Unaposoma 3 Nefi 1:14, inaweza kuwa na manufaa kuelewa kwamba Kiumbe ambaye alizungumza anajaza majukumu mawili na alikuwa akizungumza kutoka mitazamo zote miwili: kama Yehova (ambaye ni Baba kwa maapisho matakatifu ya mamlaka) na kama Yesu Kristo, atakaye kuwa Mwana wa Mungu wa dunia.

Ili kuona jinsi unabii wa kuzaliwa kwa Mwokozi zilivyotimia, andika unabii uliotolewa na Samweli Mlamani katika safu ya kushoto ya chati ifuatayo. Kisha andika mstari kutoka 3 Nefi 1 na maelezo mafupi ya utimilifu wake katika safu ya kulia.

Unabii wa Samweli Mlamani

Utimilifu

Unabii wa 1 (Helamani 14:3–4):

3 Nefi 1:

Unabii wa 2 (Helamani 14:5):

3 Nefi 1:

Unabii wa 3 (Helamani 14:6):

3 Nefi 1:

Unabii wa 4 (Helamani 14:7):

3 Nefi 1:

Unaposoma 3 Nefi 1:16–18, tambua jinsi waovu walivyofanya wakati ishara zilipotokea. Unaweza kutaka kuwekea alama baadhi ya maoni yao. Tunajifunza katika 3 Nefi 1:18 kwamba watu wengine “walianza kuogopa kwa sababu ya uovu wao na kutoamini kwao.” Tafakari swali lifuatalo: Jinsi gani dhambi na kutoamini kunasababisha hofu?

Soma 3 Nefi 1:22–23, na uangalie kile ambacho shetani alijaribu kufanya baada ya ishara ya kuzaliwa kwa Bwana kutolewa. Kamilisha taarifa ifuatayo ili kueleza kanuni inayopata katika mstari 22: Tunapoona uongo wa Shetani, tunaweza kuchagua.

Askofu Richard C. Edgley, aliyehudumu katika Askofu Kiongozi, alitoa ushauri kuhusu jinsi tunaweza kufanya wakati wa majaribu ya imani yetu. Wekea alama maneno yake yoyote au vishazi vinavyokuhimiza kuchagua kuamini licha ya mashaka kwamba Shetani anaweza kukujaribu:

Askofu Richard C. Edgley

“Kwa sababu ya migogoro na changamoto tunayokumbana nayo katika dunia ya leo, napenda kupendekeza chaguo moja—chaguo la amani na ulinzi na chaguo ambalo ni sahihi kwa wote. Chaguo hilo ni imani. Kuwa na ufahamu kwamba imani si zawadi ya bure inayotolewa bila mawazo, juhudi, au tamaa. Mwokozi alisema, ‘Njoni kwangu’(Mathayo 11:28) na ‘Bisheni, nanyi [mtapewa]’ (Mathayo 7:7). Hizi ni vitenzi tendaji —njoo, bisha. Ni chaguzi. Hivyo nasema, chagua imani. Chagua imani badala ya shaka, chagua imani badala ya hofu, chagua imani badala ya kisichojulikana na cha siri, na chagua imani badala ya wasiwasi. 

 Wakati mantiki, sababu, au ujuzi wa binafsi unapogongana na mafundisho matakatifu na mafundisho, au ujumbe tatanishi unaposhambulia imani yako chagua kutoipanda mbegu [ya imani] nje ya moyo wako kwa kutoamini. Kumbuka, hatupati ushahidi wowote mpaka baada ya majaribu ya imani yetu (ona Etheri 12:6)” (“Faith—the Choice Is Yours,” Ensign or Liahona, Nov. 2010, 31–33).

  1. ikoni ya shajaraNini uongo na udanganyifu gani shetani hukuza leo ili kujaribu kukaza mioyo ya watu dhidi ya ukweli? Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kile unaweza kufanya ili kudumisha imani yako katika Yesu Kristo na injili Yake rejesho hata wakati shetani anapojaribu kukufanya kuwa na shaka na imani yako.

Soma 3 Nefi 1:24–25, na utambue changamoto ya ziada ambazo baadhi ya waumini hupitia. Tafakari kile unaweza kujifunza kutoka kwa mwitikio wa watu hawa walipojifunza kuwa walikuwa na makosa.

3 Nefi 1:27–30

Wapinzani Wanefi na baadhi ya vijana Walamani wajiunga na wezi wa Gadiantoni

Miaka michache baada ya ishara ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo kutolewa, wapinzani wengine wa Wanefi walianza kuwa na athari juu ya uwezo wa waamini kusimama imara katika injili. Unawezaje kusimama imara katika injili, hata kukiwa na mashambulizi dhidi ya Kanisa katika siku zetu? Soma 3 Nefi 1:27–30, na uangalie ikiwa “kizazi kinachoinuka” cha Walamani kilikuwa na athari nzuri au hasi juu ya imani ya wengine.

Tambua kwamba Walamani wengi vijana “walijitegemea wenyewe” (3 Nefi 1:29) na kugeuka mbali na injili. Dada Kathleen H. Hughes, aliyehudumu katika Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, alipendekeza maana ya kishazi “walijitegemea wenyewe”: “[Hii] ina maana kwangu kwamba walijipendelea wenyewe kwanza na kujiingiza kwa tamaa ambazo manabii waliwaonya kuepuka. Walikubali vishawishi vya Shetani na vivutio” (“Grow Up unto the Lord,” Ensign, Feb. 2010, 18).

Unaweza kutaka kuandika kanuni ifuatayo katika maandiko yako karibu na 3 Nefi 1:29–30 au katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Tukikubali majaribu, mfano wetu unaweza kuwa na athari hasi juu ya imani na haki za wengine.

  1. ikoni ya shajaraKukusaidia kuelewa jinsi kanuni hii inahusiana na wewe, jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni lini umewahi kushuhudia mfano wa kanuni hapo juu? Unawezaje kubakia mwaminifu hata kama wale walio karibu nawe hawaja amua vile?

    2. Wakati ni muhimu kujua kwamba mfano wetu unaweza kuwa na athari hasi juu ya wengine, ni muhimu pia kukumbuka kwamba mfano wetu unaweza kusaidia kuimarisha mtu mwingine. Ni lini umewahi kuona “kizazi kinachoinuka,” au vijana wa Kanisa leo, wakiwa na athari mema katika imani ya watu wengine?

  2. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, tengeneza orodha ya baadhi ya njia ambazo unaweza kuwa na ushawishi mwema juu ya imani ya watu katika familia yako mwenyewe, kata yako au tawi, au rika zako. Chagua mawazo mawili kutoka kwenye orodha yako, na uandike hasa kile utafanya ili kukamilisha hili.

  3. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo mwisho wa kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza 3 Nefi 1 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: