Seminari
Kitengo 25: Siku ya 4, 3 Nefi 15–16


Kitengo 25: Siku ya 4

3 Nefi 15–16

Utangulizi

Wakati Mwokozi alipoendelea kuwafundisha watu hekaluni, katika nchi ya Neema, alitangaza kwamba amri ya Musa ilitimizwa Kwake, na kwamba Yeye ndiye mwanga na sheria ambayo watu wanapaswa kuangalia. Mwokozi kisha alielezea wanafunzi kumi na wawili Wanefi kwamba watu katika Marekani walikuwa baadhi ya “kondoo wengine” ambao alizungumzia kwa watu katika Yerusalemu (ona Yohana 10:14–16). Pia aliahidi kwamba wale wanaotubu na kurudi Kwake watahesabiwa miongoni mwa watu Wake wa agano.

Picha
Kristo katika Ardhi ya Neema

3 Nefi 15:1–10

Mwokozi anatangaza kwamba ameitimiza sheria ya Musa

Umewahi kujiuliza ni kwa nini Bwana anatutaka tutii sheria fulani na amri, kama vile kulipa fungu la kumi, kuheshimu siku ya Sabato, au kuwaheshimu wazazi wetu? Yesu Kristo alipoendelea kuwafundisha Wanefi, Aliwafundisha kusudi kuu ya sheria Zake na amri. Angalia kusudi hili unapojifunza3 Nefi 15.

Mwokozi alipomaliza kuzungumza na umati wa watu, Aliona kwamba wengine miongoni mwao walikuwa na swali. Soma 3 Nefi 15:1–2, na uandike kile watu walikuwa wakistajaabu na kushangaa:

Ili kuelewa ni kwa nini Wanefi walikuwa wanastajaabu na kushangaa kwa tangazo la Mwokozi kwamba “vitu vya kale” vya sheria ya Musa vilikuwa vimepita na “vitu vyote vilikuwa vimekuwa vipya,” inatusaidia kuelewa kwamba kwa karne Wanefi walijua na kuishi chini ya sheria ya Musa. Sheria zao, ibada, na mfumo wa kanisa ililingana na sheria ya Musa, sheria ambayo ilipeanwa zamani na Yesu Kristo wa kale kuwatayarisha watu kwa ajili ya ujio Wake na kuwaelekeza kwa dhabihu Yake ya upatanisho. Sasa Mtoaji sheria Mtukufu alikuwa amesimama mbele yao akitangaza kwamba Upatanisho ulikuwa umetimia (ona 3 Nefi 11:10–14) na kwamba ndani Yake sheria ya Musa ilitimizwa (ona 3 Nefi 9:16–20; 12:46–47). Tangazo lake kwamba vitu vya kale vya sheria ya Musa vilikuwa “vimepita” na vitu vipya vya kuchukua nafasi ya sheria viligeuza kwa ghafla namna wangemwabudu Mungu.

Mwokozi alijibu shauku zao kwa kusisitiza mafundisho muhimu sana. Soma 3 Nefi 15:3–5, 9, na uonyeshe vishazi katika majibu ya Mwokozi ambavyo vingeweza kuwahakikishia Wanefi kwamba chanzo cha sheria haikuwa ikibadilika

  1. Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Ni nini unafikiri Yesu alikuwa akifundisha Wanefi wakati aliposema, “Mimi ndiye sheria”? (3 Nefi 15:9).

Kutoka kwa mafundisho ya Mwokozi katika mistari hizi, tunaweza kujifunza kwamba Yesu Kristo ndiye kusudi la sheria zote na amri za injili. Tafakari ni kwa nini ukweli huu ungekuwa muhimu kwa Wanefi walipojifunza kwamba sheria ya zamani ya Musa ilibadilishwa na sheria ya juu na kuona mabadiliko katika namna yao ya ibada.

Soma 3 Nefi 15:9–10, na uwekee alama kile Bwana anataka tufanye kama matokeo ya mafundisho haya. Tumia kile ulichojifunza katika mistari hizi ili kukamilisha kanuni ifuatayo:Lakini ikiwa kwa Yesu Kristo kwa kutii Atatupa .

  1. Fikiria juu ya amri kama vile kulipa fungu la kumi, kutii siku ya Sabato, na kuheshimu wazazi wetu, na ujibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Jinsi gani mtu anaweza kufuata sheria na bado asimtazamie Kristo?

    2. Ni katika njia gani utii wetu kwa amri unaweza kubadilika ikiwa mtazamo wetu ulikuwa juu ya kumtazamia Yesu Kristo na wala sio tu kwa kutii sheria?

Njia moja ambayo utii wetu kwa amri unaweza kubadilika ikiwa tutamtazamia Kristo ni kwamba motisha yetu ya kutii utabadilika kutoka kwa wajibu, au hata upendo wa utawala, hadi kwa upendo wa Bwana.

Picha
Mzee Marvin J. Ashton

Soma taarifa ifuatayo na Mzee Marvin J. Ashton wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili: “Ni faraja ya kiroho na baraka kiasi gani kujua kwamba, tukimtazamia Mwokozi wetu Yesu Kristo na kuvumilia hadi mwisho, uzima wa milele na wokovu unaweza kuwa wetu. Mungu anapatikana zaidi tunapomtazamia. Kumtazamia Mungu kunatufundisha kutumikia na kuishi bila kulazimishwa [bila kulazimishwa au kushinikizwa kufanya kitu] (“There Are Many Gifts,” Ensign, Nov. 1987, 21).

  1. Chagua amri ambayo uliwahi kushangaa ni kwa nini unahitaji kuitii, na ufikirie jinsi kutii amri hiyo kunaweza kukuongoza kwa Yesu Kristo. Unaweza kutaka kuweka lengo la kuwa mtiifu zaidi kwa amri uliochagua na uandike maoni machache kuhusu jinsi ya kuikamilisha. Andika mawazo yako katika shajara yako ya kujifunza maandiko.

3 Nefi 15:11–16:5

Yesu Kristo anaongea na wanafunzi Wake kuhusu kondoo Wake wengine

Picha
Biblia Inashuhudia juu ya Yesu Kristo
Picha
Kitabu cha Mormoni Kinashuhudia juu ya Yesu Kristo

Je, umewahi kujihisi kusahaulika au peke yako na kujiuliza kama Baba wa Mbinguni alijua wewe ni nani? Ingawa tunaweza kujihisi tukiwa peke yetu au wakati mwingine kujihisi wanyonge kuliko wengine, Mungu anajali watu Wake na hujionyesha Kwao. Tazama ushahidi wa ukweli huu unapojifunza salio la 3 Nefi 15 na mwanzo wa 3 Nefi 16.

Kama ilivyoandikwa katika Agano Jipya na Kitabu cha Mormoni, Yesu Kristo alihudumu miongoni mwa watu katika Dunia ya Kale na katika Marekani. Soma 3 Nefi 15:11–17 ukiangalia kile Bwana alisema Aliwaambia wale waliokuwa katika Yerusalemu juu ya watu wake huko Marekani.

“Kondoo wengine” inamaanisha wafuasi wengine wa Mchungaji, Yesu Kristo. Zizi ni kizizi cha kondoo, lakini neno zizi kinatumika katika mfano huu kumaanisha kundi la watu wenye imani moja katika Yesu Kristo. Kulingana na 3 Nefi 15:17, jinsi gani Bwana alisema atajionyesha kwa kondoo Wake mwingine?

Yesu alieleza ni kwa nini Baba wa Mbinguni alimuamuru asitoe maarifa zaidi juu ya kondoo Wake wengine kwa wale walikuwa Yerusalemu. Kagua 3 Nefi 15:18–20, na uwekee alama maelezo ya Mwokozi. Kwa kuona kwamba Baba alificha maarifa zaidi ya Wanefi kutoka kwa Wayahudi kwa sababu ya uovu ya Wayahudi, tunaweza kujifunza kanuni muhimu kuhusu jinsi tunavyopokea maarifa na ukweli kutoka kwa Bwana. Kulingana na mistari hizi, unawezaje kukamilisha kanuni zifuatazo? Mungu anatupa maarifa na ukweli kulingana na .

Bwana aliwaambia Wanefi kwamba walikuwa sehemu ya kondoo wengine ambao aliongea kuhusu katika Yerusalemu. Wayahudi walifikiri Alikuwa akizungumza juu ya Wayunani (wasio Waisraeli). Hawakuelewa kwamba Wayunani “hawatasikia” sauti ya Mwokozi (ona 3 Nefi 15:21–23).

Soma 3 Nefi 15:24, na uangalie jinsi Bwana hasa alivyowa hakikishia Wanefi juu ya utunzaji Wake kwao.

Soma 3 Nefi 16:1–3, na ujue ni nani mwingine atasikia sauti ya Mwokozi. Hatuna rekodi ya maandiko ya yeyote ambaye Mwokozi alimtembelea tena, lakini ni wazi kwamba Alitembelea vikundi vingine na kuwaingiza katika “zizi” Lake.

Jinsi gani Yesu Kristo anaonyesha kwamba Anajali wale watu ambao hawapati kusikia sauti Yake? Soma 3 Nefi 15:22–23 na 3 Nefi 16:4, na uangalie jinsi Bwana alisema atajidhihirisha mwenyewe kwa Wayunani.

Kutokana na kile ulisoma hadi sasa katika 3 Nefi 15 and , ni ushahidi gani umeona kwamba Mungu anawajali watu Wake na Hujionyesha kwao?

Soma 3 Nefi 16:5, na uangalie kile kitatokea katika siku za mwisho baada ya Wayunani kupata ujuzi wa Yesu Kristo na injili Yake.

Yesu aliahidi kubariki watoto Wake wote —nyumba ya Israeli na Wayunani—kwa kuwapa maneno Yake kama ilivyoandikwa na Wanefi. Maandiko ya Wanefi ingesaidia kubadilisha Wayunani, ambao kisha wangesaidia kukusanya nyumba ya Israeli katika siku za mwisho (ona 3 Nefi 16:4–5).

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, jibu swali lifuatalo: Ni ushahidi gani kutoka kwa maisha yako mwenyewe umepata ambayo inaonyesha kuwa Yesu Kristo anatujali sote?

3 Nefi 16:6–20

Yesu Kristo anatangaza baraka na anatoa onyo kwa watu wa mataifa mengine ambao wanaishi katika siku za mwisho

Je, umewahi kutaka kuwa sehemu ya kundi, klabu, au timu? Fikiria juu ya mfano maalum. Ni nini kinachotakiwa ili kuwa mshiriki wa kundi hilo? Kundi kubwa ambacho unaweza kuwa mshiriki wake ni Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, watu wa agano wa Bwana.

Soma 3 Nefi 16:6–7, na uangalie kile kitatokea kwa sababu ya imani ya Wayunani na kutoamini kwa nyumba ya Israeli katika siku za mwisho. Inaweza kusaidia kuelewa kwamba kutakuwa pia na Wayunani wasioamini katika siku za mwisho ambao watawatawanya na kuwanyanyasa watu wa nyumba ya Israeli (ona 3 Nefi 16:8–9). Bwana ataondoa injili Yake kutoka kwa waovu na kuifunua kwa wenye haki, Waisraeli na Wayunani, katika siku za mwisho (ona 3 Nefi 16:10–12).

Soma 3 Nefi 16:13, na uangalie kinachohitajika ili kukuwa mmoja wa watu wa Bwana wa agano. Kwa kutumia kile ulichojifunza katika 3 Nefi 16:13, kamilisha kanuni ifuatayo: Lakini ikiwa , basi tutahesabiwa miongoni mwa watu Wake.

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Utajuaje kuwa wewe ni sehemu ya watu wa Bwana wa agano?

    2. Imebariki maisha yako kivipi kwa kuhesabiwa miongoni mwa watu Wake?

  2. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza 3 Nefi 15–16 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha