Seminari
Kitengo 24: Siku ya 3, 3Nefi 6–10


Kitengo 24: Siku ya 3

3 Nefi 6–10

Utangulizi

Kufuatia ukombozi wao wa kimiujiza kutoka kwa wezi wa Gadiantoni, Wanefi na Walamani walifurahia amani kwa miaka mitatu. Kiburi, tofauti za tabaka, na mateso yakatokea na kuongoza kwa uovu mkuu na hatimaye kupinduliwa kwa serikali ya Wanefi. Ishara ya kifo cha Yesu Kristo katika Yerusalemu zilijumuisha uharibifu mkubwa ulioharibu miji mingi ya Wanefi, na kuua wenyeji waovu. Giza ilifunika nchi kwa siku tatu. Katikati ya giza, sauti ya Mwokozi iliwaita watu warejee Kwake. Wakati giza ilipotawanyika, maombolezo ya watu ikageuka na kuwa furaha na sifa ya Yesu Kristo.

3 Nefi 6–7

Wanefi wanakuwa na kiburi, Kanisa linavunjika, makundi ya siri yanaharibu serikali, na watu wanagawanyika katika makabila

Fikiria juu ya wakati ambapo ilikubidi kufanya uamuzi kuhusu kama utafuata nabii au la. Kama ilivyoandikwa katika 3 Nefi 6–7, baadhi ya Wanefi waliona matokeo ya kutisha ya kuwakataa manabii, wakati wengine wakiona baraka zinazopatikana kwa kutubu na kuwasikiliza watumishi wa Bwana waliochaguliwa.

Unaposoma katika 3 Nefi 5, Wanefi walitubu na kumtumikia Mungu kwa bidii na walikombolewa kimungu kutoka kwa wezi wa Gadiantoni. Wanefi kisha wakafanikiwa kwa muda mfupi. Hata hivyo, kiburi kikaingia kwa haraka mioyoni mwa wengi, ambao ulisababisha mgawanyiko ndani ya Kanisa. Manabii walitumwa kuhubiri dhidi ya uovu wa watu, lakini majaji waliwachukua na kuwaua kisiri (ona 3 Nefi 6:4–23). Ndani ya takriban miaka sita, watu walijisalimisha “kwa nguvu ya Shetani” (3 Nefi 7:5) na wakawa waovu sana kiasi kwamba walipigana dhidi ya haki yote. Makundi ya siri yaliharibu serikali ya nchi na kusababisha watu kugawanyika katika makabila.

Licha ya uovu wa watu, Nefi aliendelea kutoa ushahidi dhidi ya dhambi zao na kuwaita kwa toba (ona 3 Nefi 7:15–20). Soma 3 Nefi 7:21–22, na uweke alama mifano michache ya jinsi watu walivyobarikiwa kwa kufuata Nefi. Kutoka mistari hizi tunajifunza kwamba tutakapotubu na kufuata watumishi wa Bwana, tutafurahia ushawishi wa Roho Mtakatifu katika maisha yetu.

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kuhusu wakati ambapo ulichagua kufuata ushauri wa nabii au viongozi wengine wa ukuhani. Ulibarikiwa vipi kwa kufanya hivyo?

3 Nefi 8:1–18

Uharibifu mkuu anatimiza ishara ya kifo cha Yesu Kristo

Fikiria siku ambapo Ujio wa Pili wa Yesu Kristo utakapotimia. Unadhani utajihisi vipi wakati huo utakapofika? Katika njia sawa, Wanefi walikuwa wakisubiri kwa muda mrefu kwa ajili ya ujio wa Yesu Kristo. Samweli Mlamani alikuwa ametabiri juu ya ishara zitakazotokea kwa kifo cha Yesu Kristo (ona Helamani 14:20–27). Soma 3 Nefi 8:3–4, na utambue tofauti kwa jinsi baadhi ya Wanefi walihisi kuhusu ishara.

Soma 3 Nefi 8:5–7, na uangalie kile kilichotokea katika mwaka wa 34 kuanzia tarehe ya ishara ya kuzaliwa kwa Mwokozi. Pitia 3 Nefi 8:8–18, ukiangalia kilichotokea kwa wenyeji wa miji zilizoathirika na dhoruba na matetemeko ya ardhi yaliofuata. Soma 3 Nefi 10:11–12, na uweke alama ni nani aliyekuwa na uwezo wa kunusurika na uharibifu huu. Hata ingawa waathirika walikuwa “sehemu ya walio haki zaidi” ya Wanefi, bado walihitajika kutubu na kuja kwa Yesu Kristo.

  1. Tumia ukurasa katika shajara yako ya kujifunza maandiko ili kuunda makala ya gazeti kuripoti matukio katika3 Nefi 8:5–18. Jumuisha kichwa cha habari, chora picha, na kisha andika ripoti ya uharibifu.

3 Nefi 8:19–25

Giza inafunika nchi kwa siku tatu

Fikiria wakati ambapo ulikuwa katika mahali penye giza kabisa, kama vile pango au chumba lisilo na madirisha wakati mtu akizima taa (au fikiria vile itakavyokuwa). Umejisikiaje kuwa katika giza na kuwa na uwezo wa kuona? Soma 3 Nefi 8:19–23, na uangalie kilichofuata baada ya dhoruba na maangamizo kutulia. (Unaweza kutaka kuwekea alama maneno yoyote au vishazi vinavyoonyesha jinsi giza ilivyokuwa kuu.)

Soma 3 Nefi 8:24–25, ukitafuta kile wanefi walisema ingezuia kifo na maangamizi ya watu wao.

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Jinsi gani madhara ya dhambi ni kama kuwa katika giza?

    2. Jinsi gani toba ni kama kuruhusu mwanga katika chumba chenye giza?

3 Nefi 9:1–14

Katika giza, sauti ya Yesu Kristo inawaalika wale walionusurika uharibifu kutubu na kuja Kwake

Katika siku tatu za giza, sauti ya Mwokozi iliongea na wale walionusurika. Soma 3 Nefi 9:1–2, 7, na uangalie ni kwa nini Mwokozi alisema uharibifu huu ulitokea kati ya watu. Kisha soma 3 Nefi 9:13–14, na uangalie kile Mwokozi alisema ili kuwafariji watu katika mateso yao. Unaweza kutaka kuweka alama sehemu za mistari hizi ambazo zina maana kwako.

Mzee C. Scott Grow wa Sabini alishuhudia kwamba Mwokozi huwaalika wote kuja Kwake na kuponywa:

Picha
Mzee C. Scott Grow

“Yesu Kristo ni Mponyaji Mkuu wa roho zetu. Na bila ya dhambi ya upotevu, hakuna dhambi au kosa, maumivu au huzuni, ambayo ni nje ya uwezo wa uponyaji wa Upatanisho Wake.

“Tunapotenda dhambi, Shetani hutuambia tumepotea. Kwa kulinganisha, Mkombozi wetu anatoa ukombozi kwa wote—bila kujali tulichokosea —hata kwako na mimi” (“The Miracle of the Atonement,” Ensign or Liahona, May 2011, 109).

Mwaliko wa Mwokozi katika 3 Nefi 9:13 wa kuja Kwake na kupokea uwezo wa uponyaji Wake unahusu kila mmoja wetu. Ili Mwokozi kutuponya, ni lazima tukubali mwaliko Wake na kuja Kwake, na kutubu dhambi zetu, na kuongoka.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kuhusu nyanja ya maisha yako ambayo inaweza kunufaika kutokana na uwezo wa uponyaji wa Mwokozi. Unahitaji kufanya nini ili kumkaribisha kukuponya?

3 Nefi 9:15–22

Sauti ya Mwokozi inatangaza kwamba kupitia kwa toleo Lake sheria ya Musa imetimizwa imetimizwa

Kama sehemu ya sheria ya Musa, ambayo Wanefi walikuwa wanaishi mpaka wakati huu, Bwana aliwaagiza watu Wake kutoa dhabihu ya wanyama kama aina na kivuli ya sadaka ya mwisho ambayo hatimaye Angetoa kupitia kwa Upatanisho Wake. Tumia maneno ya Mwokozi katika 3 Nefi 9:17 ili kukamilisha sentensi ifuatayo: “Kupitia kwangu, ukombozi huja, na ndani yangu .”

Mwokozi alitangaza kwamba maagizo yote, sheria, ibada, na ishara za sheria za Musa, ambazo zilikuwa zilitolewa ili kuekeleza watu Kwake, zilitimizwa Alipokamalisha toleo Lake la upatanisho. Soma 3 Nefi 9:19, na utambue kile ambacho Mwokozi alitangaza ambacho Wanefi hawangetoa tena. Kisha tafuta 3 Nefi 9:20, na uweke alama kile ambacho walistahili kutoa kama dhabihu badala yake.

Unafikiri inamaanisha nini kutoa dhabihu ya “moyo uliopondeka na roho iliyovunjika”? Roho iliyovunjika ni moja ambayo ni nyenyekevu, ya kufundishika, na yenye toba. Ili kuzidisha uelewa wako wa maana ya kuwa na moyo uliopondeka na roho iliyovunjika, soma taarifa ifuatayo na Mzee D. Todd Christofferson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, na uweke alama maneno aliyotumia kufafanua “moyo uliopondeka” na “roho iliyovunjika”:

Picha
Mzee D. Todd Christofferson

“Katika nyakati za zamani wakati watu walitaka kuabudu Bwana na kutafuta baraka Zake, mara nyingi walileta zawadi. Unapotafuta baraka ya uongofu, unaweza kumtolea Bwana zawadi ya moyo wako uliopondeka, au wenye toba, na roho yako iliyovunjika, au mtiifu. Kwa kweli, ni zawadi ya wewe mwenyewe—kile ulicho na kile unakuwa.

“Je, kuna kitu ndani yako au katika maisha yako ambayo ni chafu au isiofaa? Unapoiondoa, hiyo ni zawadi kwa Mwokozi. Je, kuna tabia nzuri au ubora ambayo inakosekana katika maisha yako? Unapoichukua na kuufanya kuwa sehemu ya tabia yako, unatoa zawadi kwa Bwana” (“When Thou Art Converted,” Ensign or Liahona, May 2004, 12).

Soma 3 Nefi 9:21–22, na uangalie kile Mwokozi alifundisha tunahitaji kuwa kama ili kuja Kwake.

  1. Fikiria juu ya watoto wengine wadogo ambao unajua. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko elezea tabia ambayo watoto wadogo wanayo ambayo tunahitaji ili kuja kwa Mwokozi.

Picha
Alijua Lini

Kamilisha kanuni ifuatayo kwa maneno sahihi au vishazi unavyoona katika 3 Nefi 9:13–14, 20–22: Tukija kwa Yesu Kristo kwa moyo uliopondeka na roho iliyovunjika, Yeye ata. (Kuna majibu mengi sahihi.)

  1. Ili kukusaidia kutumia ukweli huu, jibu maswali yafuatayo:

    1. Nini mitazamo gani zinazoweza kutuzuia kutoa moyo uliopondeka na roho iliyovunjika kwa Bwana?

    2. Jinsi gani umeona Bwana akikubariki ulipokuja Kwake kwa moyo wenye toba na roho tiifu?

    3. Unawezaje kutoa vyema moyo uliovunjika na roho iliyopondeka kwa Bwana?

3 Nefi 10

Bwana ameahidi kuwakusanya watu Wake kama vile kuku anavyokusanya vifaranga vyake

Picha
Ni Mara Ngapi

Baada ya kusikia sauti ya Mwokozi, watu walishangaa sana kwamba kulikuwa na kimya katika nchi kwa masaa mengi. Kisha sauti ikazungumza tena kwa watu (ona 3 Nefi 10:1–3). Soma 3 Nefi 10:4–6, na utambue kile Mwokozi alisema alijaribu kufanya ili kulinda na kuboresha watu. Wekea alama ahadi Mwokozi alipeana katika mstari 6 kwa wale wanaotubu na kuja Kwake kwa kusudi kamili ya moyo.

Mwokozi alitumia mfano wa kuku akiwakusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake ili kuwalinda kutokana na hatari. Fikiria kuhusu njia ambazo Mwokozi ni kama kuku anayetaka kuwalinda vifaranga vyake kutoka kwa hatari. Aidha, kulingana na 3 Nefi 10:4–6, ni kwa nini nyumba nzima ya Israeli haikukusanywa?

Soma 3 Nefi 10:8–10, na uangalie kilichotokea baada ya watu kusikia sauti ya Mwokozi.

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza 3 Nefi 6–10 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha