Kitengo 25: Siku ya 1
3 Nefi 11:18–12:48
Utangulizi
Baada ya watu ambao walikuwa katika hekalu katika nchi ya Neema kugusa alama za majeraha katika upande wa Yesu Kristo, mikono na miguu, Mwokozi aliwapa Nefi na wengine uwezo wa kubatiza. Mwokozi aliwaonya watu kuepuka ubishi na kuahidi kwamba wale ambao wanaishi injili watarithi ufalme wa Mungu. Pia aliwafundisha jinsi ya kupokea baraka za injili Yake na kuwaamuru kushawishi wengine kwa ajili ya mema. Mwokozi alitangaza kwamba alitimiza sheria ya Musa, na akawapa watu amri ya juu ili kuwaandaa kuwa kama Yeye na Baba yetu wa Mbinguni.
3 Nefi 11:18–30
Yesu Kristo anawapa Nefi na wengine uwezo wa kubatiza na anakataa ubishi
Je, unakumbuka mawazo yako na hisia ulipojitayarisha kwa ubatizo wako, au umewahi kuona rafiki au mwanafamilia akijiandaa kubatizwa? Watu wengi wana maswali kama “Ni nani anaweza kunibatiza mimi?” na “Jinsi gani agizo la ubatizo hufanywa?” Fikiria jinsi ungejibu maswali hayo.
Ulipokuwa ukisoma 3 Nefi 11:1–17, ulijifunza kuhusu kutokea kwa Yesu Kristo kwa “watu wa Nefi, karibu na Hekalu ambalo lilikuwa katika nchi ya Neema” (3 Nefi 11:1). Watu hawa walihisi alama za majeraha Yake na wakawa mashahidi binafsi wa Ufufuo Wake na uungu. Mara baada ya tukio hili, Mwokozi aliwafundisha kuhusu ubatizo, ikiwemo ni pamoja na yule anayeweza kubatiza na jinsi ubatizo unapaswa kufanywa.
Soma 3 Nefi 11:18–22, 24–25, na uandike jibu kwa swali hili “Ni nani anaweza kunibatiza?”
Kama ilivyoandikwa katika 3 Nefi 11, kutokana na kile Mwokozi alisema na kufanya, tunajifunza: Ubatizo lazima ifanywe na mtu ambaye ana mamlaka sahihi.Ufunuo wa kisasa unabainisha kwamba ubatizo unaweza kufanywa tu na mtu ambaye anashikilia afisi ya kuhani katika Ukuhani wa Haruni (ona M&M 20:46) au ambaye ana Ukuhani wa Melkizedeki (ona M&M 20:38–39; 107:10–11). Zaidi ya hayo, ni lazima atende chini ya uongozi wa kiongozi wa ukuhani anayeshikilia funguo za ukuhani ambazo ni muhimu kwa kuidhinisha agizo (kama vile Askofu, rais wa tawi, rais wa misheni, au Kiongozi Mkuu Mwenye Mamlaka).
Soma 3 Nefi 11:23–27, na uandike jibu la swali “Ni kwa njia gani agizo la ubatizo hufanywa?”
-
Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika ni kwa nini unafikiriubatizo ni lazima ifanyike katika namna iliyowekwa na Bwana. Ni nini kitafanyika ikiwa maneno ya agizo la ubatizo hazijasemwa sahihi au ikiwa mtu anayebatizwa hajazamishwa kikamilifu chini ya maji?
-
Jibu moja au zaidi ya makundi ya maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Unakumbuka nini kuhusu sababu ya kubatizwa kwako na juu ya huduma ya ubatizo? Ni nani aliyekubatiza? Una miaka mingapi? Ulikuwa na hisia gani ulipobatizwa? Ina maanisha nini kwako kubatizwa na mtu mwenye mamlaka sahihi na kwa namna iliyowekwa na Bwana?
-
Je, hivi karibuni ulishuhudia mtu akibatizwa? Je, ni hisia gani ulikuwa nazo?
-
Ikiwa unashikilia afisi ya kuhani katika Ukuhani wa Haruni, unajisikiaje ukijua kwamba una mamlaka ya kubatiza? Ikiwa umekuwa na fursa ya kubatiza mtu, ulihisi na kujifunza nini wakati wa tukio hilo?
-
Kama ilivyoandikwa katika 3 Nefi 11:28–30, Bwana aliwashauri watu wasiwe na mgogoro au kushindana (ubishi) na kila mmoja kuhusu ubatizo au mawazo mengine ya mafundisho. Alifundisha kwamba ubishi ni wa shetani na unapaswa kuondolewa mbali.
3 Nefi 11:31–41
Yesu Kristo anatangaza mafundisho Yake
Fikiria juu ya kitu ulichofanya leo (hatua) kilisababisha matokeo mema. Andika hatua na matokeo kwenye pande sahihi wa mchoro ufuatao. Kisha fikiria juu ya kitu ulichofanya leo kilichosababisha matokeo mabaya.
Uhusiano wa hatua na matokeo wakati mwingine huitwa sheria ya mavuno. Ufunuo wa kisasa unaelezea kwa njia hii: “Chochote unachopanda, ndicho pia wewe utakachokivuna; kwa hiyo, kama utapanda mema pia utavuna mema kwa thawabu zenu” (M&M 6:33).
Soma 3 Nefi 11:31, na utambue kile Yesu Kristo alisema Atawatangazia watu.
-
Kama ilivyoandikwa katika 3 Nefi 11:32–39, Yesu Kristo alitangaza mafundisho Yake, “ambayo Baba [alimpa]” (3 Nefi 11:32). Nakili chati ifuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Soma kila marejeo ya maandiko, na utambue matendo na matokeo ambazo Yesu Kristo alifundisha kuwa yalihusiana na mafundisho Yake. Rekodi kile unapata katika chati katika shajara yako ya kujifunza maandiko.
Matendo
Matokeo
Kulingana na chati chako, ni matendo gani muhimu ambazo Yesu Kristo alifundisha kwamba watoto wote wa Baba wa Mbinguni lazima wafanye ili kuingia katika ufalme wa mbinguni?
Unaweza kuwa umetambua kwamba 3 Nefi 11:32 inaeleza Roho Mtakatifu anashuhudia juu ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Tafakari wakati wa hivi karibuni wakati Roho Mtakatifu alipokushuhudia juu ya ukweli na upendo wa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.
3 Nefi 12:1 –16
Yesu Kristo anafundisha umati juu ya baraka tunazopokea tunapoishi injili Yake
Kamilisha zoezi lifuatalo la kweli-si kweli kwa kuweka mviringo majibu hapa chini:
-
Baba wa Mbinguni anataka tuwe wakamilifu.
-
Tunapaswa kuwa wakamilifu katika maisha haya ili kuingia katika ufalme wa mbinguni.
-
Tunaweza kuwa kamilifu.
Ili kusaidia kuangalia majibu yako, soma kwanza3 Nefi 12:48. (Hiki ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza kutaka kuiwekea alama katika njia tofauti ili uweze kuitambua katika siku zijazo.)
Inawezekanaje kuwa mkamilifu? Mzee Russell M. Nelson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisema yafuatayo kuhusu amri ya kuwa mkamilifu: “Hatufai kufadhaika ikiwa jitihada zetu za dhati kuhusiana na ukamilifu sasa zinaonekana kuwa ngumu [vigumu] na isiokuwa na mwisho. Ukamilifu unasubiri. Inaweza kuja kwa ukamilifu tu baada ya Ufufuo na tu kupitia kwa Bwana. Inasubiri wote wampendao, na kushika amri zake” (“Perfection Pending,” Ensign, Nov. 1995, 88).
Tafakari maswali yafuatayo: Unafikiri ina maanisha nini kuwa ukamilifu unaweza kuja “tu kupitia kwa Bwana”?
Tazama nyuma katika zoezi la kweli-sikweli ulichofanya, na ubadilishe yoyote ya majibu yako kulingana na kile ulichojifunza kutoka 3 Nefi 12:48 na taarifa ya Mzee Nelson.
Mafundisho ya Yesu Kristo katika 3 Nefi 12–14 wakati mwingine hujulikana kama “mahubiri ya hekaluni” kwa sababu yanafanana na mara nyingi huongeza uelewa wetu wa Mahubiri ya Mwokozi ijulikanayo vyema ya Mlimani (ona Mathayo 5–7). Rais Harold B. Lee alifundisha, “Katika Mahubiri yake ya Mlimani Bwana ametupa kiasi fulani ya ufunuo wa tabia yake mwenyewe, ambayo ilikuwa kamilifu, au kile kinaweza kusemekana kuwa ‘tawasifu, kila silabi alilokuwa ameadika katika matendo,’ na katika kufanya hivyo ametupa mwongozo kwa ajili ya maisha yetu wenyewe” (Decisions for Successful Living [1973], 56). Unaposoma 3 Nefi 12–14, angalia njia ambayo Mwokozi anataka ujitahidi kwa ukamilifu.
Kama vile katika Mahubiri ya Mlimani, Mwokozi alianza mahubiri yake kwa Wanefi kwa heri kadhaa —matangazo ya hali ya baraka na furaha ya wale ambao ni waaminifu (ona 3 Nefi 12:1–12). Unapoyasoma, tafuta sifa ambazo Mwokozi anatuhimiza kukuza na zile baraka anazoahidi kama matokeo yetu ya kufanya hivyo. Unaposoma, unaweza kutaka kuwekea alama sifa hizi na baraka zilizoahidiwa. Inaweza kusaidia kujua kwamba maskini katika roho (3 Nefi 12:3) ina maanisha kuwa mnyenyekevu na mtegemezi kwa Bwana, kuomboleza (3 Nefi 12:4) inahusu kuhisi huzuni kwa dhambi zetu ambayo inaongoza kwa toba, na kuwa mpole (3 Nefi 12:5)inaweza kumaanisha kuwa mnyenyekevu na mpole, kuwa mtiifu kwa mapenzi ya Mungu, au kuwa na subira katika kuvumilia majeraha bila chuki.
-
Tambua sifa moja ambayo umesoma sasa ambayo unajitahidi au kujitahidi kupata. Rekodi katika shajara yako ya kujifunza maandiko ni baraka gani unazopokea au kutarajia kupokea unapokuza sifa hiyo.
Kutokana na kweli nyingi katika 3 Nefi 12:1–12, tunajifunza kwamba tunapoishi kulingana na mafundisho ya Yesu Kristo, tutabarikiwa na kutayarishwa kuingia katika ufalme wa mbinguni. Tunapofanya hivyo, tutakuwa pia mfano au mwanga kwa ulimwengu (ona 3 Nefi 12:14–16).
3 Nefi 12:17–48
Yesu Kristo anawafundisha umati sheria ya juu ambayo itawasaidia kuwa kama Yeye na Baba wa Mbinguni
Yesu Kristo alifundisha Wanefi jinsi ya kuja Kwake kwa kutubu na kutii amri Zake (ona 3 Nefi 12:19–20). Katika salio ya 3 Nefi 12, alireje sehemu za sheria za Musa na kisha kufundisha sheria ya juu. Alianzisha sehemu za sheria za Musa kwa vishazi kama vile “imesemwa na wale wa kale” au “imeandikwa.” Kisha Akaanzisha sheria mpya na ya juu, ambayo anataka tuishi leo, kwa kishazi “nawaambia …”
-
Soma marejeo ya maandiko yafuatayo, na uandike katika shajara yako ya kujifunza maandiko zile tabia Mwokozi alisema zitaelekeza kwa ukamilifu:
-
2 Nefi 12:21–22. Inaweza kuwa na manufaa kuelewa kwamba neno rakani neno la kushusha hadhi lenye maana kuonyesha dharau, chuki ya wazi, au chuki.
-
3 Nefi 12:23–24. Tumia tanbihi 24 a ili kusaidia kugundua kinachomaanisha kupatanishwa na mtu.
-
3 Nefi 12:25. Inaweza kuwa na manufaa kuelewa kwamba “kubaliana na adui yako haraka” inahusu kutatua migogoro na wengine kwa haraka na kutoziruhusu kukereketa na kukua katika matatizo makubwa. Mzee Daudi E. Sorensen, akiwa anahudumu kama mshiriki wa Sabini, alifundisha, “Hakuna mahali popote ambapo kanuni hii inatumika zaidi kuliko katika familia zetu” (“Forgiveness Will Change Bitterness to Love,” Ensign or Liahona, May 2003, 11).
-
3 Nefi 12:27–30. Inaweza kuwa na manufaa kuelewa kwamba tamaa inamaanisha shauku isiofaa, maovu, na ubinafsi.
-
Kanuni moja tuyonaweza kujifunza katika mistari hizi katika 3 Nefi 12 ni: Tunapokuja kwa Kristo na kushika amri Zake, tunaweza kuwa zaidi kama Yeye na Baba yetu wa Mbinguni, ambao ni wakamilifu.
Ingawa hatutafikia ukamilifu katika maisha haya, Rais James E. Faust wa Urais wa Kwanza alieleza kwamba ni lazima tujitahidi ili kujiendeleza kwenye ukamilifu sasa ili kuweza kuufikia katika maisha yajayo: “Ukamilifu ni lengo la milele. Ingawa hatuwezi kuwa wakamilifu katika maisha, kujitahidi kuipata ni amri, ambayo hatimaye, kupitia kwa Upatanisho, tunaweza kutii” (“This Is Our Day,” Ensign, May 1999, 19).
Umahiri wa Maandiko—2 Nefi 12:48
-
Angalia kama unaweza kukariri3 Nefi 12:48 kikamilifu. Andika kifungu katika shajara yako ya kujifunza maandiko unapofikiri umeikariri.
Kumbuka, Bwana hatarajii tuwe wakamilifu katika mambo yote wakati wa maisha yetu, lakini tunapojitahidi kumfuata na kushiriki baraka ya Upatanisho, hatimaye tunaweza kuwa wakamilifu.
-
Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
Nimejifunza3 Nefi 11:18–12:48 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).
Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: