Seminari
Kitengo 27: Siku 1, 3 Nefi 23


Kitengo 27: Siku ya 1

3 Nefi 23

Utangulizi

Baada ya kunukuu maneno ya Isaya, Yesu Kristo aliamuru Wanefi kutafuta maneno ya manabii. Mwokozi pia alisahihisha Wanefi kwa kutokuwa na bidii katika utunzaji wa rekodi zao.

3 Nefi 23:1–5

Yesu Kristo anaamuru watu kutafuta maneno ya manabii

Tafakari uzoefu wako kwa kusoma maandiko katika mwaka huu uliopita. Andika maneno machache au vishazi vifupi vinavyoelezea Baraka ambazo zimekuja katika maisha yako kwa sababu ya masomo yako ya maandiko.

Unapoangalia katika orodha yako, fikiria yale baraka hizi zinaweza kukufundisha juu ya umuhimu wa masomo ya maandiko.

Baada ya kunukuu baadhi ya mafundisho ya Isaya (ona 3 Nefi 22), Mwokozi aliwaamuru watu kutafuta maneno ya Isaya na manabii kwa bidii. Soma 3 Nefi 23:1–5, na utambue ni kwa nini Mwokozi alisema tunapaswa kutafuta maneno ya Isaya na manabii. Fikiria kuwekea alama maneno na vishazi vitakavyokusaidia kukumbuka yale uliyojifunza.

Sababu moja tunaamuriwa kujifunza maneno ya Isaya ni kwa sababu “alizungumza akitaja vitu vyote kuhusu [watu wa agano wa Bwana] watu ambao ni wa nyumba ya Israeli”(3 Nefi 23:2). Kwa sababu umefanya maagano na Bwana, wewe ni sehemu ya nyumba ya Israeli. Maandiko ya Isaya yanahusu wewe. Sababu nyingine tunapaswa kujifunza maneno ya Isaya ni kwa sababu yatatimizwa yote(ona 3 Nefi 23:3).

Tambua katika 3 Nefi 23:1 kwamba Yesu Kristo haswa aliamuru Wanefi “mpekue[maneno ya Isaya] kwa bidii.”

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Unafikiri kuna tofauti gani kati ya kusoma maneno ya manabii na kuyapekua kwa bidii?

    2. Ni mbinu gani ya masomo ya maandiko inaweza kukusaidia kutafuta maneno ya Isaya na manabii kwa ufanisi na kwa maana? (Unaweza kutaka kuchambua Kitengo cha masomo 1: Siku 1, “Kusoma maandiko,” ili kukumbuka baadhi ya visaidizi muhimu vya masomo ya maandiko.)

Mzee Merrill J. Bateman, mshiriki mstaafu wa Sabini, alitambua baadhi ya baraka zinazokuja katika maisha yetu tunapotafuta maneno ya manabii: “Kuna baadhi ya baraka zinazopatikana wakati mtu anapopekua maandiko. Mtu anaposoma maneno ya Bwana na kuzishika, yeye husogea karibu na Mwokozi na kupata hamu kubwa ya kuishi maisha ya haki. Uwezo wa kupinga majaribu huongezeka, na udhaifu wa kiroho kushindwa. Majeraha ya kiroho yameponywa” (“Coming unto Christ by Searching the Scriptures,” Ensign, Nov. 1992, 28).

Soma3 Nefi 23:5, na uangalie ahadi ambazo Mwokozi alitoa kwetu sote kama tutajifunza na kutenda kwa mialiko katika maandiko.

  1. Fikiria kuwa una rafiki au mwanafamilia ambaye anajitahidi kusoma maandiko mara kwa mara. Ukitumia kile ulichojifunza katika 3 Nefi 23:1–5, andika kile unaweza kusema ili kuhimiza mtu huyu kujifunza maneno ya manabii kwa bidii na kupata uzoefu wa maana na maandiko.

3 Nefi 23:6–14

Yesu Kristo anawarudi wanafunzi Wake kwa kushindwa kurekodi matukio muhimu

Soma taarifa ifuatayo kutoka kwa Rais Spencer W. Kimball:

Picha
Rais Spencer W. Kimball:

“Bwana Yesu Kristo Mwenyewe alisisitiza umuhimu mkubwa wa kuweka rekodi kwa Wanefi na Walamani[ona 3 Nefi 23:6–13]. …

“Nafurahi kwamba si mimi niliyepewa onyo, hata ingawa kwa upole na huruma, kwa kukosa kutimiza wajibu wa kuweka kumbukumbu yangu kisasa. …

“… Kumbuka, Mwokozi aliwakemea wale ambao walishindwa kurekodi matukio muhimu”(“The Angels May Quote from It,” New Era, Feb. 2003, 32, 34–35).

Salio ya 3 Nefi 23 ina habari ilivyoelezwa na Rais Kimball, wakati Mwokozi alipowakemea Wanefi kwa kutojumuisha baadhi ya matukio muhimu katika kumbukumbu zao. Soma 3 Nefi 23:6–11, na utambue kile Wanefi walishindwa kurekodi. Kwa nini unafikiri ilikuwa muhimu kwa Wanefi kurekodi utimizaji wa unabii huu uliotolewa na Samweli Mlamani? Jinsi gani kupata rekodi hio katika Kitabu cha Mormoni kunatusaidia katika siku zetu?

  1. Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Kwa nini kinaweza kuwa muhimu kwako kuandika chini matukio ya kiroho na ushawishi unatokea katika maisha yako?

Kama kumekuwa na tukio la kiroho la hivi karibuni katika maisha yako ambalo umeshindwa kurekodi, fikiria kuiandika katika shajara yako binafsi sasa. Daftari la kawaida au daftari la kumbukumbu inatosha kwa kuweka shajara binafsi. Soma 3 Nefi 23:12–14, na uangalie kile Mwokozi alifanya baada ya Wanefi kutii amri ya kuandika kutimia kwa unabii wa Samweli Mlamani.

Mwokozi “alieleza maandiko yote pamoja,” kumaanisha kwamba alielezea maana ya maandiko.

Soma 3 Nefi 24:1, na utambue mifanano kati ya sehemu ya kwanza ya mstari huu na kile kilitokea katika3 Nefi 23:12–14. Tambua kwamba baada ya Wanefi kuandika kile Yesu Kristo aliwafundisha, Aliwapa maarifa zaidi na ufunuo kwa kufafanua juu ya mambo hayo.

Kulingana na kile ulichojifunza kutoka 3 Nefi 23:6–14,kamilisha kanuni ifuatayo: Ninapoandika ushawishi mtakatifu na matukio, Naalika.

Miongoni mwa uwezekano mwingine, ungeweza kukamilisha kanuni hiyo kwa njia hii: Ninapoandika ushawishi takatifu na matukio, Nakaribisha Bwana kunipa ufunuo zaidi.

Ili kuelewa kikamilifu zaidi ukweli uliojifunza, soma taarifa mbili zifuatazo kutoka kwa Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili:

Picha
Mzee Richard G. Scott

“Maarifa yanay orekodiwa kwa uangalifu ni maarifa yanayopatikana katika wakati wa mahitaji. Habari nyeti ya kiroho inapaswa kuhifadhiwa katika mahali patakatifu ambapo panamuonyesha Bwana jinsi unavyoithamini. Zoezi hilo huongeza uwezekano wako wa kupokea mwanga zaidi,” (“Acquiring Spiritual Knowledge,” Ensign, Nov. 1993, 88).

“Andika chini katika mahali salama vitu muhimu ulivyojifunza kutoka kwa Roho. Utakuta kwamba unapoandika chini hisia zenye thamani kubwa, nyingi zitazidi kuja. Pia, maarifa unayopata itapatikana katika maisha yako yote”(“To Acquire Knowledge and the Strength to Use It Wisely,” Ensign, June 2002, 32).

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Kwa nini unafikiri kuandika chini ufunuo tulizopokea kutoka kwa Bwana inaweza kutusaidia kupokea ufunuo zaidi?

    2. Jinsi gani kuchukua muda wa kuandika juu ya ushawishi wa Bwana katika maisha yetu kunatusaidia kushukuru kwa baraka zetu na kutoa shukrani zetu Kwake?

Unaweza kuwa na wasiwasi kwamba hujawahi kupata uzoefu maalum au takatifu ambazo zitakuwa na manufaa ya kutosha kurekodi. Mzee John H. Groberg, mshiriki mstaafu wa Sabini, aligusia suala hili: “Watu wengine husema, ‘Sina chochote cha kurekodi. Hakuna kitu cha kiroho kinachonitokea.’ Nasema, ‘Anza kurekodi, na mambo ya kiroho yatatokea. Zinapatikana kila wakati, lakini tunazitambua zaidi tunapoziandika’” (“Writing Your Personal and Family History,” Ensign, May 1980, 48).

Unaweza kuanza kutumia yale ambayo umejifunza kuhusu kurekodi uzoefu wa kiroho kwa kubeba kipande cha karatasi, daftari, au shajara kwa wiki ijayo. Rekodi ushawishi wowote, maono, uzoefu, au hisia ulizo nazo wiki nzima. Pia rekodi jinsi unavutiwa kutenda kwa zile ushawishi ulizopokea. Baada ya kupitia vitendo hivyo, andika kuhusu uzoefu wako.

Ambia mtu mwingine (mwanafamilia, rafik,au Kiongozi wa Kanisa) kuhusu mpango wako wa kuweka rekodi ya uzoefu wako wa kiroho. Fikiria kukaribisha mtu huyu kujiunga na wewe katika juhudi hili kwa kurekodi baadhi ya uzoefu wake mwenyewe wa kiroho. Kwa kualika mtu mwingine kufanya mradi huu na wewe, unaweza kuhimiza na kuripoti maendeleo yako kwa kila mmoja. Hata hivyo, unapaswa kukumbuka kwamba siyo lazima—na inaweza kuwa sio sahihi—kushirikisha uzoefu wako takatifu na mtu mwingine.

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza 3 Nefi 23 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha