Seminari
Kitengo 25: Siku ya 3, 1 Nefi 14


Kitengo 25: Siku ya 3

3 Nefi 14

Utangulizi

Mahubiri ya Yesu Kristo katika hekalu yanaendelea katika3 Nefi 14. Aliwafundisha watu kuhusu kuhukumu wengine na kuwaagiza kutafuta baraka kutoka kwa Baba wa Mbinguni kwa njia ya maombi. Mwokozi pia alionya dhidi ya manabii wa uongo na kusisitiza umuhimu wa kufanya mapenzi ya Mungu.

3 Nefi 14:1–6

Mwokozi anafundisha kuhusu kuhukumu wengine

Soma maneno ya mstari wa pili wa wimbo “Lord, I Would Follow Thee” (Wimbo, nambari. 220)—au iimbe mwenyewe ukijisikia vizuri kufanya hivyo:

Mimi ni nani kuhukumu mwingine

Ninapotembea visivyo?

Katika moyo tulivu kumefichwa

Huzuni ambayo jicho haliwezi kuona.

Mimi ni nani kuhukumu mwingine?

Bwana, mimi nitakufuata wewe.

Kama ilivyoandikwa katika 3 Nefi 14, Mwokozi aliendelea kufundisha Wanefi katika hekalu. Soma 3 Nefi 14:1–2, na ufikiri jinsi mwelekeo huu kutoka kwa Mwokozi inahusiana na mstari wa pili wa wimbo uliosoma. (Inaweza kukusaidia kuelewa kwamba kishazi “kwa hukumu mnayo hukumia” inahusiana na kiwango ambacho mtu anapima au anahukumu mtu.)

  1. Andika majibu kwa maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Jinsi gani ushauri wa Mwokozi katika 3 Nefi 14:1–2 inahusiana na mstari wa pili wa wimbo “Lord, I Would Follow Thee”?

    2. Unawezaje kueleza ukweli muhimu Mwokozi alifundisha katika 3 Nefi 14:2 kwa maneno yako mwenyewe? (Unaweza pia kuandika ukweli huu au kanuni katika ukingo wa maandiko yako.)

Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alitoa ufahamu ambao unatusaidia kuelewa amri ya Mwokozi ya “msihukumu” katika3 Nefi 14:1. `Unapoisoma, weka mstari chini ya aina ya hukumu aliosema tunapaswa kuepuka na kwa nini.

Picha
Mzee Dallin H. Oaks

“Kuna aina mbili ya hukumu: hukumu ya mwisho, ambayo hatupaswi kufanya, na hukumu wastani, ambayo tunaongozwa kufanya, lakini juu ya kanuni ya haki. …

“Hukumu ya mwisho ni tukio la baadaye ambayo sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo ili kuhukumiwa kulingana na matendo yetu. Naamini kwamba amri ya maandiko ‘msihukumu’ inahusu wazi zaidi hukumu hii ya mwisho. …

 Kwa nini Mwokozi aliamuru kwamba tusihukumu hukumu ya mwisho? Naamini amri hii ilitolewa kwa sababu tunakisia kutoa hukumu ya mwisho kila tunapotangaza kwamba mtu fulani anaenda jehanamu (au mbinguni) kwa kitendo fulani au kwa wakati fulani. Tunapofanya hivi — na kuna majaribu makubwa ya kufanya hivyo —tunajiumiza wenyewe na yule tunayejifanya kuhumu. …

 Hukumu ya haki lazima, kwa ufafanuzi, liwe wastani. Itajiepusha na kutangaza kwamba mtu ameahidiwa wokovu au kupuuza mtu kama kuwa amekemewa kwa moto wa jehanamu. Itajiepusha na kutangaza kwamba mtu amepoteza kila fursa ya wokovu au hata fursa zote kwa ajili ya jukumu muhimu katika kazi ya Bwana. Injili ni Injili ya matumaini, na hakuna mmoja wetu anayeruhusiwa kukana uwezo wa Upatanisho ili kuleta utakaso wa dhambi ya mtu binafsi, msamaha, na marekebisho ya maisha kwa hali sahihi (“‘Judge Not’ and Judging,” Ensign, Aug. 1999, 7, 9).

Tafakari jinsi taarifa ya Mzee Oaks inakusaidia kuelewa amri ya Mwokozi ya “msihukumu.”

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Ni jinsi gani kanuni kutoka 3 Nefi 14:2 kwamba tutahukumiwa kulingana na jinsi tunavyo hukumu unabadilisha jinsi tunavyotazama makosa ya wengine au udhaifu? Soma 3 Nefi 14:12. Jinsi gani mstari hii inahusiana na kanuni hii?

Umewahi kuwa na kitu kidogo katika jicho lako, kama vile ukope au doa ya udongo? Maandiko yanaelezea doa katika jicho la mtu kama kibanzi. Kipande ndefu, cha kuni nene kinajulikana kama boriti. Mwokozi alitumia picha hizi ili kutusaidia kuelewa matatizo yanayotokea tunapohukumu wengine kwa dhuluma au kuwapata na kosa visivyo. Soma 3 Nefi 14:3–5, na ufikiri kile kibanzi na boriti vinawakilisha.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, chora picha ya kile Mwokozi alieleza katika3 Nefi 14:4. Kisha uliza maswali yafuatayo:

    1. Unafikiri kibanzi kinawakilisha nini?

    2. Unafikiri boriti inawakilisha nini?

    3. Kwa nini unafikiri boriti badala ya kibanzi hutumika kuwakilisha makosa ya wale ambao huhukumu kwa dhuluma?

Tambua kuwa mlinganisho wa Mwokozi hulenga vitu vilivyokaa katika jicho na hivyo, kuathiri maono ya mtu. Tafakari maswali yafuatayo kuhusu wewe mwenyewe: Jinsi gani makosa yangu inaweza kuathiri jinsi ninavyotazama watu wengine? Jinsi gani naweza kutumia ushauri wa Yesu Kristo katika3 Nefi 14:5?

Unafikiri ni sahihi daima au muhimu kutoa maamuzi kuhusu tabia ya watu wengine? Nabii Joseph Smith alifafanua kwamba wakati hatupaswi kuhukumu wengine kwa dhuluma, tunaelezwa kutumia hukumu ya haki (ona Tafsiri la Joseph Smith, Mathayo 7:1 [katika Mathayo 7:1, tanbihi a]).

Maelezo yafuatayo yanatoa ufahamu zaidi katika suala la kuhukumu wengine: “Wakati mwingine watu huhisi kwamba ni makosa kuhukumu wengine kwa njia yoyote. Wakati ni kweli kwamba hupaswi kuwalaumu watu wengine au kuwahukumu kwa dhuluma, utahitaji kufanya hukumu ya mawazo, hali, na watu katika maisha yako yote. Bwana ametoa amri nyingi ambazo huwezi kutii bila kutoa hukumu” (True to the Faith: A Gospel Reference [2004], 90).

Ili kukusaidia kuelewa umuhimu wa kutoa maamuzi ya haki, soma 3 Nefi 14:6 na utambue baadhi ya hukumu ambazo Yesu Kristo alituamuru tufanye. Kabla ya kusoma, inaweza kuwa na manufaa kuelewa kwamba “kutoa kilicho kitakatifu kwa mbwa” na “kutupa lulu mbele ya nguruwe” inamaanisha kushiriki kitu kitakatifu na wale ambao hawatafahamu au kuelewa utakatifu wake .

Jinsi gani 3 Nefi 14:6 inakusaidia kuelewa haja ya kufanya maamuzi ya haki? Mzee Dallin H. Oaks alielezea baadhi ya hali nyingine ambapo tunapaswa kufanya maamuzi ya haki:

Picha
Mzee Dallin H. Oaks

“Sisi sote tunafanya maamuzi katika kuchagua marafiki zetu, katika kuchagua jinsi sisi kutumia muda wetu na fedha zetu, na, bila shaka, katika kuchagua rafiki wa milele. …

 Maamuzi ya haki itaongozwa na Roho wa Bwana, na si kwa hasira, kisasi, wivu, au maslahi binafsi” (“‘Judge Not’ and Judging,” 9).

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Kwa nini ni muhimu kufanya maamuzi ya haki katika maeneo kama vile kuchagua marafiki, kuamua jinsi ya kutumia muda wetu na fedha, au kuchagua rafiki wa milele? Inaweza kuwa ni katika matukio gani ambapo itakuwa muhimu au sahihi kutoa hukumu juu ya wengine?

    2. Unawezaje kuhukumu kwa haki zaidi? Tafakari kama kuna mtu yeyote unayeweza kuwa mkarimu kwake zaidi au kuhitaji kujiepusha kumhukumu visivyo.

3 Nefi 14:7–12

Mwokozi anafundisha kuhusu kutafuta baraka kutoka kwa Baba wa Mbinguni

Fikiria juu ya nyakati ambapo Baba wa Mbinguni amesikia maombi yako. Soma {3 Nefi 14:7–11, na uangalie kile Yesu Kristo alifundisha kuhusu utayari wa Baba wa Mbinguni wa kujibu maombi yetu.

Kanuni moja tunayoweza kujifunza kutoka 3 Nefi 14:7–11 ni kwamba Baba wa Mbinguni atatubariki ikiwa tutamwomba na kumtafuta katika sala. Jinsi gani kujua kwamba Baba wa Mbinguni ana hamu kujibu maombi yako kutabadilisha jinsi unavyoomba?

  1. Uliza mtu mzima anayeaminika swali lifuatalo: Ni lini ulihisi upendo wa Baba wa Mbinguni kwako kupitia jinsi alivyojibu maombi yako? Fupisha jibu lake na yale uliyojifunza kutoka kwa jibu hilo katika shajara yako ya kujifunza maandiko.

3 Nefi 14:13–27

Mwokozi anafundisha umuhimu wa kufanya mapenzi ya Baba wa Mbinguni

Kama vile Mwokozi alivyoendelea kufundisha Wanefi walikusanyika katika hekalu, alitoa mifanano kadhaa ili kutusaidia kuelewa umuhimu wa kutii mafundisho Yake. Kila mfanano kina mfano mzuri na mfano mbaya.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, chora mchoro rahisi wa mfano mzuri na mfano mbaya unaopatikana katika kila moja ya vifungu vitatu vya maandiko. Pia andika chini kile unafikiri Mwokozi anataka tujifunze kwa kulinganisha mifano nzuri na mbaya. Kuwa tayari kuonyesha picha zako kwa darasa lako, na kueleza kile ulichojifunza kutoka kwa mifanano hizi.

    1. 3 Nefi 14:13–14

    2. 3 Nefi 14:15–20

    3. 3 Nefi 14:24–27

Soma 3 Nefi 14:21–23, na ufikiri kuhusu kile unaweza kusema kwa mtu ambaye alikuambia yote unayohitaji kufanya ili kuokolewa katika ufalme wa Mungu ni kusema kwamba unaamini katika Yesu Kristo.

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza 3 Nefi 14 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha