Seminari
Kitengo 24: Siku ya 2, 3Nefi 2–5


Kitengo 24:Siku ya 2

3 Nefi 2–5

Utangulizi

Mara baada ya watu kuona ishara ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, walianza kusahau ushahidi waliopokea, na waka kaza mioyo yao. Wanefi Wengi na Walamani walipuuza ishara na maajabu zaidi na kuendelea kwa uovu. Matokeo yake, wezi wa Gadiantoni walikua kwa nguvu na kutishia kuharibu Wanefi. Jaji Mkuu wa Wanefi, Lakoneyo, alikusanya Wanefi na Walamani wote watakatifu pamoja na kuwaita watu kutubu na kujiandaa kwa vita. Kwa sababu ya umoja wao na imani katika Bwana, walipata ushindi dhidi ya maadui zao. Kufuatia ukombozi wao, Wanefi na Walamani watakatifu walikiri uwezo wa Mungu katika uhifadhi wao.

3 Nefi 2

Wanefi na Walamani wenye haki wanaungana ili kujitetea dhidi ya wezi wa Gadiantoni

Fikiri kuhusu matukio machache muhimu ya kiroho ambazo umekuwa nazo katika maisha yako. (Kumbuka kwamba matukio ya kiroho hayahitaji kuwa makubwa au geni ili kuwa na maana.) Kwa nini unafikiri inaweza kuwa muhimu kukumbuka matukio haya ya kiroho?

Soma 3 Nefi 2:1–3, ukiangalia kile kilichotokea kati ya watu walipoanza kusahau ishara zinahusiana na kuzaliwa kwa Mwokozi. Unaweza kujifunza nini kutoka kwa maelezo haya kuhusu hatari ya kusahau matukio ya kiroho?

Moja wapo wa kanuni tunayoweza kujifunza kutokana na kile kilichotokea kwa Wanefi ni kwamba tukisahau matukio ya zamani ya kiroho, tunaathirika kwa urahisi zaidi kwa majaribu ya Shetani na udanganyifu. Unaweza kutaka kuandika kanuni hii katika maandiko yako karibu na3 Nefi 2:1–3. Unapofanya, fikiria ni kwa nini kusahau matukio ya kiroho kunaweza kutufanya kuaathirika kwa urahisi zaidi kwa Shetani.

Tafakari kile unaweza kufanya ili kukusaidia kutambua na kukumbuka matukio ya kiroho. Orodhesha mawazo machache ambazo unafikiri yatakuwa ya kusaidia zaidi:

Rais Henry B. Eyring wa Urais wa Kwanza alieleza jinsi kurekodi matukio yake ya kiroho katika shajara ilivyomsaidia. Unaposoma kuhusu uzoefu wake, piga mstari chini ya baraka kadha ambazo zinaweza kutokea kutokana na kurekodi uzoefu wa kiroho:

Picha
Na Rais Henry B. Eyring

“Niliandika mistari michache kila siku kwa miaka. Kamwe sikukosa hata siku moja bila kujali vile nilivyochoka au jinsi nitakavyoanzisha siku inayofuata. Kabla ya sijaandika, ningetafakari swali hili: ‘Je! Nimeona mkono wa Mungu ukinyooshwa kutugusa sisi au watoto wetu au familia yetu leo?’ Nilivyoendelea hivyo, kitu kikaanza kutendeka. Kama ningeangazia juu ya siku, ningeona ushahidi wa kile Mungu alifanya kwa mmoja wetu ambayo sikuwa nimetambua katika wakati wa kazi nyingi wa siku. Wakati hicho kikitokea, na kilitokea mara nyingi, niligundua kwamba kujaribu kukumbuka kuliruhusu Mungu kunionyesha kile Alichokifanya.

“Zaidi ya shukrani ilianza kukua katika moyo wangu. Ushuhuda ulikua. Nikawa na uhakika zaidi kwamba Baba yetu wa Mbinguni husikia na hujibu maombi. Nilihisi shukrani zaidi kwa ulainishaji na usafishaji unaokuja kwa sababu ya Upatanisho wa Mwokozi Yesu Kristo. Na nilikua na ujasiri zaidi kwamba Roho Mtakatifu anaweza kuleta mambo yote kwa kumkumbuka zetu—hata mambo ambayo hatukujua au kutilia maanani zilipotokea” (“O Remember, Remember,” Ensign or Liahona, Nov. 2007, 67).

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko elezea jinsi kukumbuka uzoefu wa kiroho imekusaidia kubakia mwaminifu licha ya jitihada za Shetani kujaribu au kukudanganya. (Hii inaweza kujumuisha kukumbuka uzoefu wa kiroho kwa kuzirekodi katika shajara.)

Kama ilivyoandikwa katika 3 Nefi 2:4–19, wengi wa Wanefi waliendelea katika uovu na wezi wa Gadiantoni wakaongezeka kwa idadi na kwa nguvu. Walikuwa wakali zaidi, na kuwaongoza Walamani waongofu kuungana pamoja na Wanefi ili kupigana nao. Ingawa walikuwa na mafanikio kadhaa katika kuwaondoa wezi wa Gadiantoni nje ya nchi zao, Wanefi na Walamani walikuwa bado katika hali ya hatari miaka 15 baada ya ishara ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo zilipotolewa.

3 Nefi 3:1–10

Kiongozi wa wezi wa Gadiantoni anadai kwamba Wanefi na Walamani wajisalimishe

Katika 3 Nefi 3:1–10 tunaona mfano wa jinsi shetani wakati mwingine hufanya kazi kupitia kwa wengine ili kujaribu kudhoofisha imani yetu na kutupotosha. Giddianhi, kiongozi wa wezi wa Gadiantoni, aliandika barua kwa Lakoneyo, jaji mkuu na gavana wa kundi la Wanefi na watu wa Walamani, ili kumshawishi kujisalimisha kwa wezi wa Gadiantoni. Soma 3 Nefi 3:2–10, ukiangalia maneno au vishazi vinavyoonyesha mbinu ambazo Gidianhi alitumia ili kujaribu kudhoofisha imani ya Lakoneyo na kumpoteza. Unaweza kutaka kuwekea alama maneno haya au vishazi kadri unavyovipata.

Mistari hizi zinatufundisha kwamba Shetani na wafuasi wake mara nyingi hutumia ubembelezaji, ahadi za uongo, na vitisho ili kupoteza watu. Ni muhimu kutambua kwamba mbinu za Shetani mara nyingi ni janja, na anaweza kutumia marafiki zetu na watu tunaowapenda badala ya maadui wanaojulikana kutujaribu. Bado, kuna ufanano kati ya nia na mbinu ya Giddianhi na jinsi Shetani anavyofanya kazi leo ili kuwapoteza watu.

  1. Chagua moja ya mbinu ya Giddianhi, na ueleze katika shajara yako ya kujifunza maandiko jinsi shetani anaweza kutumia mbinu sawa kwa vijana leo. Pia andika jinsi unaweza kupinga mbinu hii .

3 Nefi 3:11–4:33

Watu wa Lakoneyo wajiandaa kujitetea, na wanawashinda wezi wa Gadiantoni

Picha
Jibu la Lakoneyo

Lakoneyo alishangazwa na barua ya Gidianhi na akaamua kutayarisha watu wake kwa ajili ya mashambulizi yajayo. Soma vifungu vya maandiko vifuatavyo, na utambue angalau njia nne kwa ambazo Lakoneyo aliwatayari watu wake kiroho na kidunia (kimwili) ili kuhimili mashambulizi ya wezi wa Gadiantoni. (Dokezo: unapojifunza mistari hizi, kuwa na uhakika kutofautisha kati ya Giddianhi, kiongozi wa wezi wa Gadiantoni, na Gidgiddoni, nabii mkuu na mkuu wa jeshi miongoni mwa Wanefi.)

  1. Katika ukurasa tupu katika shajara yako ya kujifunza maandiko, chora mstari katikati ya ukurasa. Andika kishazi Maandalizi ya Lakoneyo juu ya upande mmoja na kishazi Mifano ya Kisasa juu ya upande wa pili. Chini ya kichwa “Maandalizi ya Lakoneyo,” andika au chora njia nne ulizotambua ambazo Lakoneyo na Wanefi walijitayarisha kuhimili mashambulizi. Chini ya kichwa “Mifano ya Kisasa,” andika au chora mifano kadhaa ya mifano ya kisasa ya kile Lakoneyo alifanya ili kuandaa watu. Mifano hizi lazima zionyeshe maandalizi ya kiroho na ya kidunia ambazo tumeshauriwa kufanya katika siku za mwisho.

  2. Ili kukusaidia kufikiri kuhusu jinsi unaweza kutumia kile ulichojifunza, jibu mawili au zaidi ya maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Unawezaje kuimarisha nyumba yako dhidi ya mashambulizi ya adui?

    2. Jinsi gani kukusanyika pamoja katika familia, matawi, au kata kunatoa ulinzi kwetu?

    3. Kwa nini masomo ya kila siku ya maandiko ni njia muhimu ya kujiimarisha mwenyewe?

    4. Ni lini ambapo maombi ilikusaidia kupata nguvu ya kiroho dhidi ya shida au hatari?

    5. Jinsi gani toba inaweza kuwa njia ya maandalizi kwa siku zijazo?

    6. Kwa nini unafikiri kuchagua kufuata wale ambao wana roho ya unabii na ufunuo ni muhimu hasa leo?

Ili kuona kile kilichotokea wakati wezi wa Gadiantoni waliposhambulia Lakoneyo na watu wake, soma3 Nefi 4:7–12. Kutoka kwa maelezo haya tunajifunza kwamba tunapojiandaa kiroho na kidunia, tunaweza kushinda changamoto kupitia kwa nguvu ya Bwana.

Lakoneyo na watu wake walikuwa na uwezo wa kuwashinda wezi wa Gadiantoni na kuharibu viongozi wa wezi. Walikuwa washindi kwa sababu ya chaguo lao la viongozi (ona 3 Nefi 3:19; 4:17), utii wao (ona 3 Nefi 3:21; 4:18), na utegemezi wao juu ya Mungu (ona 3 Nefi 4:30–31). Soma 3 Nefi 4:30–33, na uangalie jinsi watu walijibu baada ya ushindi wao juu ya wezi wa Gadiantoni. Ni nini ambacho watu walikiri kama chanzo cha ukombozi wao kutoka kwa wezi wa Gadiantoni? Kanuni moja ambayo mistari hizi zinaoyesha ni: Kutambua wema na huruma ya Mungu katika ukombozi wetu kutoka kwa matatizo inatusaidia kubakia wanyenyekevu.

3 Nefi 5

Amani imerejeshwa miongoni mwa watu; Mormoni anaelezea ufupisho wake wa kumbukumbu

Picha
Mormoni Afupisha Mabamba

Fikiria jinsi uzoefu wa binafsi wa kiroho umeshawishi imani yako, tamaa yako, au jinsi ulivyotenda baada ya uzoefu wa kiroho. Soma 3 Nefi 5:3–4, na uangalie kile ambacho Wanefi walifanya kama matokeo ya msaada na baraka waliopokea kutoka kwa Bwana. Tambua kwamba moja ya njia ambayo watu waliitikia ilikuwa ni kuhubiri injili kwa watu wengine.

Katika 3 Nefi 5:14–26, Mormoni alieleza ni kwa nini alikuwa akitengeneza rekodi yake iliofupishwa. Soma 3 Nefi 5:12–13, na uangalie kile Mormoni alisema kuhusu wajibu wake katika kuandika ufupisho wake wa rekodi za Wanefi.

Kutoka kwa mistari hizi tunajifunza kwamba kama wanafunzi wa Yesu Kristo, tuna wajibu wa kuwafundisha wengine njia ya uzima wa milele. Moja wapo ya njia muhimu zaidi tunayoweza kuonyesha shukrani zetu kwa Bwana kwa kile anatufanyia ni kwa kuwasaidia wengine kuja Kwake na kupokea baraka alizonazo kwao.

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko njia chache ambazo unaweza kuwafundisha wengine njia ya uzima wa milele kama mwanafunzi wa Yesu Kristo. Pia fikiria hali nyingine ambapo ungeweza kufundisha haya kwa wengine.

  2. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza 3 Nefi 2–5 na kukamisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha