Seminari
Kitengo cha 19: Siku ya 1, Alma 33–35


Kitengo cha 19: Siku ya 1

Alma 33–35

Utangulizi

Akitumia mafundisho yapatikanayo katika maandiko, Alma aliwasaidia wengi wa Wazoramu kuelewa kwamba wanaweza kumwabudu Mungu bila ya kujali hali zao. Aliwahimiza kumtazamia Yesu Kristo na kuamini katika Upatanisho Wake. Amuleki alithibitisha mafundisho ya Alma na kutangaza ushuhuda wake mwenyewe wa Yesu Kristo. Amuleki alisisitiza kwamba ni tu kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo ndipo mwanadamu anaweza kuokolewa. Aliahidi kwamba watu wanaweza kupata baraka zote za Upatanisho wa Yesu Kristo wanapotumia imani kwa ajili ya toba. Wazoramu wengi walitii onyo la Amuleki, walitubu, na kujiunga tena na Wanefi.

Alma 33:1–10

Alma anafundisha kundi la Wazoramu kwamba wanaweza kuabudu Mungu nje ya masinagogi yao

Kumbuka kwamba, kama ilivyoandikwa katika Alma 32, Alma aliwafundisha Wazoramu juu ya haja ya kupanda neno la Mungu katika mioyo yao na kwa kutumia imani katika neno la Mungu. Soma Alma 33:1, na utambue maswali Wazoramu walikuwa nayo kuhusu kile Alma aliwafundisha.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika jinsi ungejibu swali la Wazoramu kuhusu jinsi wanapaswa kuanza kutumia imani yao. Kisha, unapojifunza Alma 33–34, linganisha majibu yako kwa kile Alma na Amuleki walifundisha Wazoramu.

Wakati Alma alianza kujibu maswali ya Wazoramu, alisahihisha wazo la uongo kuhusu ibada ambayo ilikuwa ikiwazuia kutekeleza imani yao kikamilifu. Soma Alma 33:2, na utambue wazo hili la uongo. Kumbuka kwamba Wazoramu hawakuruhusu watu maskini kuingia masinagogi yao ili kuabudu (ona Alma 32:1–3). Kulingana na Alma 33:2, ni nini Alma aliwaambia watu wanapaswa kufanya ili kupata jibu la kusahihisha wazo hili la uongo?

Ili kusahihisha mawazo ya uongo ya Wazoramu kuhusu kumuabudu Mungu, Alma alinukuu maandiko yaliyoandikwa na nabii aitwaye Zeno. Zeno aliwafundisha watu wa Israeli katika Agano la Kale, lakini unabii wake uliandikwa tu katika Kitabu cha Mormoni. Soma Alma 33:3, na upate neno ambalo Alma alitumia kuabudu.

Fikiria kuandika kanuni ifuatayo katika maandiko yako karibu na Alma 33:3 au katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Tunaweza kumuabudu Mungu daima kwa njia ya maombi.

Soma Alma 33:4–11, na uweke alama kila moja ya hali ambayo Zeno aliombea. Ni nini Bwana alifanya kila wakati Zeno aliomba? Ili kukusaidia kufananisha mistari hii na maisha yako, chora mstari inaolingana na hali ambayo Zeno aliombea kwa hali sawa kama hiyo katika maisha yako mwenyewe. (Chagua hali ambayo inahusiana vilivyo na maisha yako. Hakuna majibu sahihi au yasio sahihi katika zoezi hili.)

Hali ya Zeno

Hali yako

Katika jangwa

Kazini

Kuhusiana na maadui zake

Kanisani

Katika shamba lake

Maombi ya Familia

Katika nyumba yake

Wakati huwezi kujua cha kufanya au unaogopa

Katika chumba chake

Unapohisi mpekweke

Katika mikusanyiko ya Bwana

Maombi ya kibinafsi

Alipotupwa nje na kudharauliwa

Katika hali zako ngumu zote

Katika taabu zake zote

Wakati una shida na marafiki

  1. Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Ni kwa jinsi gani kuomba katika hali hizi zote kunaweza kubariki maisha yako? Andika lengo la kibinafsi la jinsi unavyoweza kuomba kila mara sana.

Fikiria kuweka alama vishazi katika Alma 33:4–5, 8–9 vinavyotaja huruma ya Mungu, na utafakari jinsi kuomba kila mara zaidi kunaweza kukusaidia kuhisi huruma na upendo wa Mungu. Endelea kuangalia ni kwa nini huruma hii inawezekana unapoendelea kusoma Alma 33.

Alma 33:11–23

Alma anafundisha Wazoramu kuamini katika Yesu Kristo.

Picha
Usulubisho

Moja ya sababu baadhi ya Wazoramu walikuwa wakijitahidi kujua jinsi ya kumuabudu Mungu ilikuwa ni kwa sababu hawakujua kwamba imani yao inapaswa kuwa katika Kristo Yesu. Hawakuelewa au kuamini katika jukumu Lake katika mpango wa wokovu (ona Alma 33:14). Soma Alma 33:12–16, ambapo Alma alijadili mafundisho ya Zeno na kisha kuleta maneno ya Zenoki, nabii mwingine wa Agano la Kale. Angalia baraka ambazo Alma alitambua ambazo huja kwetu kwa sababu ya Yesu Kristo. Unaweza kutaka kuweka alama kishazi “kwa sababu ya Mwana wako” kila wakati kinapoonekana. Kutoka kwa aya hizi tunajifunza ukweli huu: Tunapokea huruma ya Baba wa Mbinguni, ikiwemo msamaha kwa dhambi zetu, kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo. Tafakari rehema ambazo Baba wa Mbinguni ameweka juu yako, ikiwemo uwezo wa kutubu na kusamehewa dhambi zako, kwa sababu ya Upatanisho wa Mwokozi.

Aidha kuwakumbusha Wazoramu juu ya mafundisho ya Zeno na Zenoki, Alma pia aliwakumbusha juu ya wakati Musa alifundisha kuhusu Upatanisho wa Mwokozi. Wakati Musa na wana wa Israeli walipokuwa jangwani, nyoka wenye sumu waliwauma watu wengi. Bwana alimwambia Musa atengeneze nyoka kutokana na shaba, amfunge juu ya mti, na kuwaamuru Waisraeli ambao walikuwa wameumwa kumtazama. Nyoka wa shaba juu ya mti alikuwa mfano au ishara ya Yesu Kristo juu ya msalaba (onaAlma 33:19).

Picha
Musa na Nyoka wa Shaba

Soma Alma 33:19–20, na utambue kile kilichotokea kwa Waisraeli ambao walichagua kuangalia nyoka wa shaba walipokuwa wameumwa na kile kilichotokea kwa wale ambao walichagua kutoangalia.

Tafakari majibu kwa maswali yafuatayo: Ni nini maelezo ya Waisraeli na nyoka wa shaba yanatufundisha juu ya kile tunapaswa kufanya ili kuponywa kiroho? Unaweza kufanya nini ili kuangalia Mwokozi ili Yeye aweze kukusaidia kiroho?

  1. Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Ni baadhi ya njia gani mahususi unaweza kuangalia kwa Yesu Kristo katika maisha yako ya kila siku?

Soma Alma 33:22–23, na uweke alama kile tunahitaji kuamini kuhusu Yesu Kristo ili kuonyesha imani Kwake.

Alma 34:1–14

Amuleki anafundisha Wazoramu kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo

Ushuhuda wa Amuleki kwa Wazoramu, kama ilivyoandikwa katika Alma 34, ulipatiana ushahidi wa pili kwa ushuhuda wa Alma wa Yesu Kristo. Soma sehemu ya ushuhuda wa Amuleki, unayopatikana katika Alma 34:8–9, na ufikirie kuweka alama yale Amuleki alifundisha juu ya haja ya Upatanisho wa Yesu Kristo. Tafakari swali hili: Maisha yangu ingekuaje kama Yesu Kristo hakuja na kutimiza jukumu Lake maalum?

Soma Alma 34:10–14, na utambue vishazi vinavyojumuisha maneno isiyo na mwisho na milele. Andika ukweli ufuatao katika shajara yako ya kujifunza maandiko:. Upatanisho usio na mwisho na wa milele wa Yesu Kristo hupatiana wokovu kwa watu wote.

Ili kutusaidia kuelewa jinsi Upatanisho hauna mwisho na ni wa milele, Askofu Richard C. Edgley wa Uaskofu Kiongozi alifundisha: “Katika kuzungumza juu ya Upatanisho wa Kristo, napenda ufafanuzi wa kamusi ya isiyo na mwisho na milele kwa sababu naamini inaeleza hasa kile Mungu alimaanisha. Isiyo na mwisho: ‘Kuwa bila mipaka au kipimo.’ Na ufafanuzi wa milele: ‘Kuwa bila mwanzo wala mwisho’ (The American Heritage Dictionary of the English Language, 4th ed. [2000], “infinite,” “eternal,” 898, 611)” (“For Thy Good,” Ensign, May 2002, 66).

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni katika njia gani Upatanisho wa Yesu Kristo unaweza kuwa bila mwisho na wa milele?

    2. Ni kwa jinsi gani kujua Upatanisho hauna mwisho na ni wa milele kunaongeza shukrani yako kwa Mwokozi? Ni kwa jinsi gani unaongeza imani yako Kwake?

Alma 34:15–41

Amuleki anafundisha jinsi ya kupokea baraka ya Upatanisho

Soma Alma 34:15–17 ili uone kile Amuleki aliwafundisha Wazoramu walichohitaji kufanya ili kupokea baraka ambazo Mwokozi anataka kutupatia kwa njia ya Upatanisho Wake. Andika ukweli ufuatao katika maandiko yako au shajara yako ya kujifunza maandiko: Ili kupokea baraka kamili ya Upatanisho, ni lazima tufanye imani kwa ajili ya toba.

Soma maelezo yafuatayo kutoka kwa Rais Dieter F. Uchtdorf wa Urais Kwanza:

Picha
Rais Dieter F. Uchtdorf

“Tunahitaji imani ya nguvu katika Kristo ili kuweza kutubu. Tukiamini kwamba Mungu anajua mambo yote, ana upendo, na ni mwenye huruma, tutaweza kuweka imani yetu Kwake kwa ajili ya wokovu wetu bila kuyumbayumba. Imani katika Kristo itabadilisha mawazo, imani, na tabia zetu zisizowiana na mapenzi ya Mungu.

Toba ya kweli inatuletea kufanya kile ambacho ni sahihi. Toba inamaanisha mabadiliko ya akili na moyo —tunaacha kufanya mambo ambayo ni mabaya, na tunaanza kufanya mambo ambayo ni sahihi. Inatuletea mtizamo safi mbele ya Mungu, ya mtu binafsi na maisha kwa ujumla (“Point of Safe Return,” Ensign or Liahona, May 2007, 100).

  1. Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Tunawezaje kufanya imani vipi katika Yesu Kristo tunapotubu?

SomaAlma 34:17–27, na uangalie kile Amuleki alifundisha kuhusu wakati tunatakiwa kuomba na kile tunapaswa kuombea. Unadhani ushauri huu uliwasaidiaje Wazoramu, ambao walidhani wangeweza kuabudu tu mara moja kwa wiki? Chagua mstari moja ambao unadhani unaweza hasa kukusaidia. Fikiria jinsi unaweza kufuata ushauri kuhusu sala katika mstari huu wakati wa wiki ijayo.

Amuleki alifundisha kwamba tunapaswa kuwa tayari kukubali baraka za Upatanisho wa Mwokozi kwa kutubu dhambi zetu sasa, badala ya kusubiri kutubu baadaye. Soma Alma 34:30–35, na uweke mstari chini ya maneno au vishazi vinavyotambua ni kwa nini hatupaswi kuahirisha toba yetu. Katika mstari 31, tafuta baraka ambayo Amuleki alisema itakuja kwa wale ambao wamechagua kutubu sasa. Kwa makini chambua mstari 32, na kisha fikiria: Ni kwa vipi mstari huu unaathiri jinsi ninaishi kila siku?

Chambua Alma 34:33, na ufikirie kile Rais Joseph Fielding Smith alisema: “Uahirishaji, kama inavyotumika kwa kanuni za injili, ni mwizi wa uzima wa milele, ambao ni maisha katika uwepo wa Baba na Mwana. Kuna wengi miongoni mwetu, hata washiriki wa Kanisa, ambao wanaona kuwa hakuna haja ya haraka katika utii wa kanuni za injili na kushika amri” (in Conference Report, April 1969, 121).

Alma 35

Wazoramu waliotubu wanakaa miongoni mwa watu wema

Wazoramu wengi walitii onyo la Amuleki la kutokuahirisha toba yao, na walitubu na kubadili maisha yao. Watawala wa Wazoramu waliwatupa nje ya nchi yao, na watu hawa wakaja katika nchi ya Yershoni, ambapo walikaribishwa na watu wa Amoni —ambao pia waliitwa Waanti-Nefi-Lehi (ona Alma 35:6–7). Wazoramu na Walamani waovu walikasirika kwamba watu wa Amoni waliwakubali Wazoramu waliotubu, wakaanza kufanya maandalizi kwa ajili ya vita dhidi ya Wanefi (ona Alma 35:8–11).

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    NimejifunzaAlma 33–35 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha